< Ezekieli 30 >

1 Neno la Bwana likanijia kusema:
Neno la Yahwe likanijia, kusema,
2 “Mwanadamu, toa unabii na useme: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: “‘Ombolezeni ninyi na mseme, “Ole wa siku ile!”
“Mwanadamu, toa unabii na sema, 'Bwana Yahwe asema hivi: Maombolezo. “Ole unakuja siku hiyo.”
3 Kwa kuwa siku ile imekaribia, siku ya Bwana imekaribia, siku ya mawingu, siku ya maangamizi kwa mataifa.
siku ikaribu. Siku ikaribu kwa ajili ya Yahwe. Itakuwa siku ya mawingu, mda wa hukumu kwa ajili ya mataifa.
4 Upanga utakuja dhidi ya Misri, nayo maumivu makuu yataijia Ethiopia. Mauaji yatakapoangukia Misri, utajiri wake utachukuliwa na misingi yake itabomolewa.
Kisha upanga utakuja dhidi ya Misri, na huko kutakuwa na maumivu makali katika Kushi wakati wauaji wa watu watakapoanguka katika Misri-wakati watakapochukua utajiri, na wakati misingi yake itakapoharibiwa.
5 Kushi na Putu, Ludi na Arabia yote, Libya na watu wa nchi ya Agano watauawa kwa upanga pamoja na Misri.
Kushi, Putu, na Ludi, na wageni wote, pamoja na watu wa nyumba ya agano-wote wataanguka chini kwa upanga.
6 “‘Hili ndilo Bwana asemalo: “‘Wale walioungana na Misri wataanguka na kiburi cha nguvu zake kitashindwa. Kutoka Migdoli hadi Aswani, watauawa ndani yake kwa upanga, asema Bwana Mwenyezi.
Yahwe asema hivi: Basi wale wanaoisaidia Misri wataanguka, na kiburi cha uweza wake kitashuka chini. Kutoka Migdoli hata Sewene maaskari wao wataanguka kwa upanga-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.
7 “‘Hizo nchi zitakua ukiwa miongoni mwa nchi zilizo ukiwa, nayo miji yao itakuwa magofu miongoni mwa miji iliyo magofu.
Wataogofya kati ya nchi zilizotupwa, na miji yao itakuwa miongoni mwa miji yote iliharibika.
8 Ndipo watakapojua kwamba mimi ndimi Bwana, nitakapoiwasha Misri moto na wote wamsaidiao watapondwa.
Kisha watajua kwamba mimi ni Yahwe, nitakapouweka moto katika Misri, na wakati wasaidizi wake wote watakapoharibiwa.
9 “‘Siku hiyo wajumbe watatoka kwangu kwa merikebu, ili kuwatia hofu Ethiopia, wakiwa katika hali yao ya kuridhika. Maumivu makali yatawapata siku ya maangamizi ya Misri, kwa kuwa hakika itakuja.
Katika siku hiyo wajumbe watatoka mbele yangu katika meli ili kuitia hofu Kushi iliyo salama, na kutakuwa na maumivu makali miongoni mwao katika siku ya kuangamizwa Misri. Kwa kuwa tazama! inakuja.
10 “‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: “‘Nitakomesha makundi ya wajeuri ya Misri kwa mkono wa Nebukadneza mfalme wa Babeli.
Bwana Yahwe asema hivi: Nitaufanya mwisho wa watu wa Misri kwa mkono wa Nebukadreza, mfalme wa Babeli.
11 Yeye na jeshi lake, taifa lililo katili kuliko mataifa yote, litaletwa ili kuangamiza nchi. Watafuta panga zao dhidi ya Misri na kuijaza nchi kwa waliouawa.
Yeye na jeshi lake pamoja naye, hofu ya mataifa, italetwa kuiharibu nchi; watafuta panga zao juu ya Misri na kuijaza nchi pamoja na watu waliokufa.
12 Nitakausha vijito vya Naili na nitaiuza nchi kwa watu waovu, kwa mkono wa wageni, nitaifanya nchi ukiwa na kila kitu kilichomo ndani yake. Mimi Bwana nimenena haya.
Nitaifanya mito kuwa nchi kavu, na nitaiuza nchi kwenye mkono wa watu waovu. Nitaifanya nchi na viijazavyo ukiwa kwa mkono wa wageni-mimi, Yahwe, nimesema.
13 “‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: “‘Nitaangamiza sanamu na kukomesha vinyago katika Memfisi Hapatakuwepo tena na mkuu katika nchi ya Misri, nami nitaeneza hofu katika nchi nzima.
Bwana Yahwe asema hivi: Nitaziharibu sanamu, na nitaleta mwisho wa sanamu za ubatili za Nofu. Hakutakuwa na mkuu katika Misri, na nitaweka hofu katika nchi ya Misri.
14 Nitaifanya Pathrosi kuwa ukiwa na kuitia moto Soani, nami nitaipiga kwa adhabu Thebesi
Kisha nitaifanya Pathrosi ukiwa na kuweka moto katika Soani, nitatekeleza matendo ya hukumu katika No.
15 Nitaimwaga ghadhabu yangu juu ya Pelusiumu, ngome ya Misri, nami nitakatilia mbali makundi ya wajeuri wa Thebesi.
Kwa kuwa nitamwaga ghadhabu yangu juu Sini, ngome ya Misri, na kuwakatilia mbali watu wa mataifa.
16 Nitaitia moto nchi ya Misri; Pelusiumu itagaagaa kwa maumivu makuu. Thebesi itachukuliwa na tufani, Memfisi itakuwa katika taabu daima.
Kisha nitaweka moto katika Misri; Sini itakuwa katika dhiki kuu, No itavunjika, na Nofu itakabiliana na maadui kila siku.
17 Wanaume vijana wa Oni na wa Pi-Besethi wataanguka kwa upanga nayo hiyo miji itatekwa.
Vijana katika Oni na Pi-besethi wataanguka kwa upanga, na miji yao itaenda utumwani.
18 Huko Tahpanhesi mchana utatiwa giza nitakapovunja kongwa la Misri; hapo kiburi cha nguvu zake kitakoma. Atafunikwa na mawingu na vijiji vyake vitatekwa.
Huko Tapanesi, siku itabadilika kuwa usiku nitakapo ivunja nira ya Misri huko, na kiburi cha uwezo wake kitaisha. Kutakuwa na wingu likimfunika, na binti zake wataenda utumwani.
19 Kwa hiyo nitaipiga Misri kwa adhabu, nao watajua kuwa Mimi ndimi Bwana.’”
Nitatekeleza matendo ya hukumu katika Misri, hivyo watajua kwamba mimi ni Yahwe.”'
20 Katika mwaka wa kumi na moja, mwezi wa kwanza, siku ya saba, neno la Bwana likanijia kusema:
Kisha ikawa katika mwaka wa kumi na moja, katika mwezi wa kwanza, katika siku ya saba ya mwezi, lile neno la Yahwe likanijia, kusema,
21 “Mwanadamu, nimevunja mkono wa Farao mfalme wa Misri. Haukufungwa ili upone au kuwekewa kipande cha ubao ili upate nguvu za kuweza kuchukua upanga.
“Mwanadamu, nimeuvunja mkono wa Farao, mfalme wa Misri. Tazama! Haukufungwa, au kufungwa kwa kitambaa cha bendeji ili upone, hivyo basi uweze kuwa imara kushika upanga.
22 Kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Mimi ni kinyume na Farao mfalme wa Misri. Nitavunja mikono yake yote miwili, ule mkono ulio mzima pia na ule uliovunjika na kuufanya upanga uanguke toka mkononi mwake.
Kwa hiyo Bwana Yahwe asema hivi, 'Tazama, mimi niko juu ya Farao, mfalme wa Misri. Kwa kuwa nitauvunja mkono wake, wote yule aliye hodari na yule aliyevunjika, nitaufanya upanga wangu kuanguka kutoka kwenye mkono wake.
23 Nitawatawanya Wamisri miongoni mwa mataifa na kuwafukuza huku na huko katika nchi zote.
Kisha nitaitawanya Misri miongoni mwa mataifa na kuwatawanya katika nchi mbali mbali.
24 Nitaitia nguvu mikono ya mfalme wa Babeli na kuutia upanga wangu mkononi mwake, lakini nitavunja mikono ya Farao, naye atalia kwa huzuni mbele yake kama mtu aliyetiwa jeraha la kumfisha.
Nitaunyoosha mikono kwa mfalme wa Babeli na kuweka upanga wangu katika mkono wake ili kwamba niweze kuiharibu mikono ya Farao. Atagugumia mbele ya mfalme wa Babeli kwa mgumio wa mtu anayekufa.
25 Nitaitia nguvu mikono ya mfalme wa Babeli, lakini mikono ya Farao italegea. Ndipo watakapojua kwamba Mimi ndimi Bwana, nitakapoutia upanga wangu mkononi mwa mfalme wa Babeli, naye ataunyoosha dhidi ya Misri.
Kwa kuwa nitainyoosha mikono ya mfalme wa Babeli, wakati mkono wa Farao utakapoanguka. Kisha watajua yakwamba mimi ni Yahwe, nitakapoweka upanga wangu kwenye mkono wa mfalme wa Babeli; kwa kuwa ataishambulia nchi ya Misri kwa huo.
26 Nitawatawanya Wamisri miongoni mwa mataifa na kuwafukuza huku na huko katika nchi mbalimbali. Ndipo watakapojua kwamba Mimi ndimi Bwana.”
Hivyo nitaitawanya miongoni mwa mataifa na kuyatawanya kwenye nchi tofauti tofauti. Kisha watajua yakwamba mimi ni Yahwe.”'

< Ezekieli 30 >