< Ezekieli 3 >

1 Naye akaniambia, “Mwanadamu, kula kile kilichoko mbele yako, kula huu ukurasa wa kitabu, kisha uende ukaseme na nyumba ya Israeli.”
Akanambia, “Mwanadamu, kile ulichokikuta, kula. Kula hili gombo, kisha nenda kaongee na nyumba ya Israeli.”
2 Ndipo nikafungua kinywa changu, naye akanilisha ule ukurasa wa kitabu.
Basi nikafungua kinywa changu, na akanilisha hilo gombo.
3 Ndipo akaniambia, “Mwanadamu, kula ukurasa huu wa kitabu ninaokupa ujaze tumbo lako.” Kwa hiyo nikaula, ulikuwa mtamu kama asali kinywani mwangu.
Akanambia, “Mwana wa adamu, lisha tumbo lako na jaza tumbo lako kwa hili gombo ambalo nimekupa!” Basi nikalila, na lilikuwa tamu kama asali kwenye mdomo wangu.
4 Kisha akaniambia, “Mwanadamu, sasa nenda katika nyumba ya Israeli ukaseme nao maneno yangu.
Kisha akanambia, “Mwana wa adamu, nenda kwenye nyumba ya Israeli na ongea maneno yangu kwao.
5 Hukutumwa kwa taifa lenye maneno ya kutatiza na lugha ngumu, bali kwa nyumba ya Israeli.
Kwa kuwa hujatumwa kwa watu wenye maneno ya kushangaza au lugha ngumu, lakini kwa nyumba ya Israeli-
6 Sikukutuma kwa mataifa mengi yenye maneno ya kutatiza na lugha ngumu ambao maneno yao hutayaelewa. Hakika ningekutuma kwa watu hao, wangekusikiliza.
sio kwa taifa lenye nguvu ya maneno ya ajabu au lugha ngumu ambao maneno yao hutaweza kuyaelewa! Kama nikikutuma kwao, watakusikiliza.
7 Lakini nyumba ya Israeli haitakusikiliza kwa kuwa hawako radhi kunisikiliza mimi, kwa kuwa nyumba yote ya Israeli ni wenye vipaji vya nyuso vigumu na mioyo ya ukaidi.
Lakini nyumba ya Israeli haitakuwa tayari kukusikiliza, kwa kuwa hawako tayari kunisikiliza mimi. Hivyo nyumba yote ya Israeli ni paji gumu na moyo mgumu.
8 Tazama nimefanya uso wako mgumu dhidi ya nyuso zao na kipaji cha uso wako kigumu dhidi ya vipaji vya nyuso zao.
Kumbe nimeufanya uso wako kama kaidi kama nyuso zao na paji lako kuwa gumu kama mapaji yao.
9 Kama vile almasi ilivyo ngumu kuliko gumegume, ndivyo nilivyokifanya kipaji cha uso wako. Usiwaogope wala usiwahofu, ijapokuwa ni nyumba ya kuasi.”
Nimekufanya paji lako kama almasi, gumu kuliko jiwe la kiberiti! Usiwaogope wala kufadhaika kwa nyuso zao, kwa kuwa ni nyumba ya uasi.”
10 Naye akaniambia, “Mwanadamu, sikiliza kwa makini na uyatie moyoni mwako maneno yote nitakayosema nawe.
Kisha akanambia, “Mwana wa adamu, maneno yote niliyokutangazia-yachukue kwenye moyo wako na wasikize kwa sikio lako!
11 Kisha nenda kwa watu wa taifa lako walio uhamishoni, ukaseme nao. Waambie, ‘Hivi ndivyo Bwana Mwenyezi asemavyo,’ kwamba watasikiliza au hawatasikiliza.”
Kisha nenda kwa watumwa, kwa watu wako, na uzungumze nao. Waambie, 'Hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo; iwapo watasikia au hapana.”
12 Ndipo Roho akaniinua, nikasikia sauti kubwa nyuma yangu ya ngurumo. (Utukufu wa Bwana na utukuzwe katika mahali pa makao yake!)
Kisha Roho akaniinua juu, na nikasikia nyuma yangu sauti yenye tetemeko la aridhi: “Ubarikiwe utukufu wa Yahwe kutoka mahali pake!”
13 Ilikuwa ni sauti ya mabawa ya wale viumbe hai yakisuguana moja kwa jingine, sauti kama ya ngurumo.
Ilikuwa sauti ya mabawa ya viumbe hai vilipokuwa vikigusana kila kimoja, na sauti ya magurudumu ambayo yalikuwa pamoja na hivyo viumbe, na sauti ya tetemeko kubwa arithi.
14 Ndipo Roho aliponiinua na kunipeleka mbali. Nikaenda nikiwa na uchungu na hasira moyoni mwangu, nao mkono wa Bwana ukiwa juu yangu.
Roho akaniinua juu na kunichukua, Nikaenda kwa uchungu katika hasira kali rohoni mwangu, kwa kuwa mkono wa Yahwe ulikuwa na nguvu ukigandamiza juu yangu!
15 Nikafika kwa wale watu waliokuwa uhamishoni huko Tel-Abibu karibu na Mto Kebari. Nikakaa miongoni mwao kwa muda wa siku saba, nikiwa nimejawa na mshangao.
Hivyo nikaenda kwa watumwa huko Tel Abibu waliokuwa wakiishi karibu na Kebari Kanali, na niliishi miongoni mwao huko kwa mda wa miaka saba, kushinda kabisa katika mshangao.
16 Mwishoni mwa hizo siku saba neno la Bwana likanijia kusema:
Kisha ikatokea baada ya siku saba kwamba neno la Yahwe likanijia, likisema,
17 “Mwanadamu, nimekufanya uwe mlinzi wa nyumba ya Israeli, kwa hiyo sikia neno nisemalo, ukawape onyo litokalo kwangu.
“Mwana wa adamu, nimekufanya uwe mwangalizi kwa ajili ya nyumba ya Israeli, hivyo sikiliza neno kutoka kinywani mwangu, na uwapatie onyo langu.
18 Nimwambiapo mtu mwovu, ‘Hakika utakufa,’ na wewe usipomwonya mtu huyo au kumshauri aache njia zake mbaya ili kuokoa maisha yake, huyo mtu mwovu atakufa katika dhambi yake na damu yake nitaidai mkononi mwako.
Nitakaposema kwa waovu, 'Utakufa hakika' na usimuonye au kuzungumza onyo kwa waovu kuhusu matendo yao maovu hivyo anaweza kuishi-yule muovu atakufa kwa ajili ya dhambi yake, lakini nitaitaka damu yake kutoka kwenye mkono wako.
19 Lakini ukimwonya mtu mwovu naye akakataa kuacha uovu wake na njia zake mbaya, atakufa katika dhambi yake, lakini wewe utakuwa umejiokoa nafsi yako.
Lakini kama ukimuonya muovo, na asiuache uovu wake au kutoka matendo yake maovu, kisha atakufa kwa dhambi yake, lakini utaokoa maisha yako mwenyewe.
20 “Tena, mtu mwenye haki akiacha haki yake na kutenda maovu, nami nikaweka kikwazo mbele yake mtu huyo atakufa. Kwa kuwa hukumwonya, atakufa katika dhambi yake. Mambo ya haki aliyotenda, hayatakumbukwa, damu yake nitaidai mkononi mwako.
Kama mwenye haki ataicha haki yake na kutenda yasiyohaki, na nikaweka kizuizi mbele yake, atakufa. Kwasababu hukumuonya, atakufa katika dhambi yake, na sintokumbuka matendo ya haki aliyoyafanya, lakini nitaitaka damu yake kutoka kwenye mkono wako.
21 Lakini ukimwonya mwenye haki asitende dhambi na akaacha kutenda dhambi, hakika ataishi kwa sababu alipokea maonyo na utakuwa umejiokoa nafsi yako.”
Lakini kama ukimuonya mwenye mtu mwenye haki kuacha kufanya dhambi halafu akaacha kutenda dhambi, ataishi hakika tangu alipo unywa; na utakuwa umeokoa maisha yako mwenyewe.”
22 Mkono wa Bwana ulikuwa juu yangu huko, naye akaniambia, “Simama uende mpaka sehemu tambarare, nami nitasema nawe huko.”
Hivyo mkono wa Yahwe ulikuwa juu yangu huko, akanambia, “Inuka! nenda uwandani, na nitaongea na wewe huko!”
23 Kwa hiyo niliinuka nikaenda mpaka mahali pa tambarare. Utukufu wa Bwana ulikuwa umesimama huko, kama utukufu ule niliouona kando ya Mto Kebari, nami nikaanguka kifudifudi.
Nikainuka na kwenda uwandani, na huko utukufu wa Yahwe ulisimama, kama utukufu ambao niliokuwa nimeuona karibu na Kebari Kanali; hivyo nikaanguka kifudifudi.
24 Ndipo Roho akaja ndani yangu akanisimamisha kwa miguu yangu. Akasema nami akaniambia: “Nenda ukajifungie ndani ya nyumba yako.
Roho akaja kwangu na kusimama juu ya miguu yangu; akaongea na mimi, na kunambia, “Nenda na jifungie mwenyewe kwenye nyumba yako,
25 Nawe, ee mwanadamu, watakufunga kwa kamba, watakufunga ili usiweze kutoka na kuwaendea watu.
kwa sasa, mwana wa adamu, wataweka kamba juu yako na kukufunga ili usiweze kutoka nje miongoni mwao.
26 Nitaufanya ulimi wako ushikamane kwenye kaa la kinywa chako, ili uwe kimya usiweze kuwakemea, wajapokuwa ni nyumba ya kuasi.
Nitaufanya ulimi wako ugandamane na paa ya mdomo wako, ili kwamba uwe kimya, na hutaweza kuwakemea, kwa kuwa ni nyumba ya waasi.
27 Lakini nitakaposema nawe, nitafungua kinywa chako nawe utawaambia, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo.’ Yeyote atakayesikiliza na asikilize, na yeyote atakayekataa na akatae; kwa kuwa wao ni nyumba ya kuasi.
Lakini nitakapozungumza na wewe, nitafungua mdomo wako hivyo utawaambia, 'Hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.' Yeye asikiaye na asikie; yeye asiyesikia na asisikie, kwa kuwa wao ni nyumba ya kuasi!”

< Ezekieli 3 >