< Ezekieli 22 >
1 Neno la Bwana likanijia kusema:
Kisha neno la Yahwe likanijia, kusema,
2 “Mwanadamu, je, wewe utauhukumu? Je, utauhukumu huu mji umwagao damu? Basi uujulishe juu ya matendo yake yote ya machukizo
“Sasa wewe, mwanadamu, Je! Utanihukumu? Utauhukumu mji kwa damu? Mfanye ajue machukizo yake yote.
3 uuambie: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Ee mji ule ujileteao maangamizi wenyewe kwa kumwaga damu ndani yake na kujinajisi wenyewe kwa kutengeneza sanamu,
Utasema, 'Bwana Yahwe asema hivi: Huu ndiyo mji umbao umwagao damu kati yake ili kwamba mda wake ufike; mji ufanyao sanamu ili ujitie unajisi.
4 umekuwa na hatia kwa sababu ya damu uliyomwaga na umetiwa unajisi kwa sanamu ulizotengeneza. Umejiletea mwisho wa siku zako na mwisho wa miaka yako umewadia. Kwa hiyo nitakufanya kitu cha kudharauliwa kwa mataifa na kitu cha mzaha kwa nchi zote.
Umekuwa na hatia kwa damu uliyoimwaga, na kufanya unajisi kwa sanamu ulizozitengeneza. Kwa kuwa umezileta karibu siku zako na kuzikaribia siku zako za mwisho. Kwa hiyo nitakufanya lawama kwa mataifa na kejeli katika uso wa kila nchi.
5 Wale walio karibu na wale walio mbali watakudhihaki, Ewe mji wenye sifa mbaya, uliyejaa ghasia.
Wote walio karibu na wale walio mbali nawe watakudhihaki, wewe mji mchafu, ujulikanao kila mahali kwa sifa mbaya kama kujaa machafuko.
6 “‘Ona jinsi kila mkuu wa Israeli aliyeko ndani yako anavyotumia nguvu zake kumwaga damu.
Tazama! Wakuu wa Israeli, kila mmoja kwa nguvu yake, wamekuja kwako kumwaga damu.
7 Ndani yako wamewadharau baba na mama, ndani yako wamewatendea wageni udhalimu na kuwaonea yatima na wajane.
Wamefanya udanganyifu kwa baba na mama ndani yako, na wametenda yaliyo kinyume juu ya wageni kati yako. Wamewatenda vibaya yatima na wajane ndani mwako.
8 Mmedharau vitu vyangu vitakatifu na kuzinajisi Sabato zangu.
Umevidharau vitu vyangu vitakatifu na kuinajisi Sabato yangu.
9 Ndani yako wako watu wasingiziaji, watu walio tayari kumwaga damu, ndani yako wako wale wanaokula vyakula vilivyotolewa mahali pa ibada za miungu kwenye milima, na kutenda matendo ya uasherati.
Watu wasingiziaji wamekuja kati yako ili kumwaga damu, na hula juu ya milima. Hufanya uovu kati yako.
10 Ndani yako wako wale wanaovunjia heshima vitanda vya baba zao, ndani yako wamo wale wanaowatendea wanawake jeuri wakiwa katika hedhi, wakati wakiwa si safi.
Uchi wa baba umefunuliwa ndani yako. Wamemtukana mwanamke mchafu ndani yako wakati wa uchafu wake.
11 Ndani yako mtu hufanya mambo ya machukizo na mke wa jirani yake, mwingine kwa aibu kubwa hukutana kimwili na mke wa mwanawe, mwingine humtenda jeuri dada yake, binti wa baba yake hasa.
Watu waliofanya machukizo pamoja na wake za majirani zao, na watu wafanyao uchafu wa aibu kwa mke wa mwanao mwenyewe; watu wawatukanao dada zao wenyewe-binti za baba zao wenyewe-haya yote yapo miongoni mwanu.
12 Ndani yako watu hupokea rushwa ili kumwaga damu, mnapokea riba na faida ya ziada na kupata faida isiyokuwa halali kutoka kwa jirani ili kupata faida kubwa kupita kiasi. Nawe umenisahau mimi, asema Bwana Mwenyezi.
Hawa watu huchukua rushwa kati yenu ili kumwaga damu. Umechukua faida na kuongeza riba nyingi sana, na umenisahau-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.
13 “‘Hakika nitapiga makofi kwa ajili ya faida isiyo halali uliyojipatia na kwa damu uliyoimwaga ndani yako.
Tazama! Kwa mkono wangu nimeipiga faida ambayo uliyoitengeneza kwa njia isiyo halali, na damu iliyo kati yako.
14 Je, ujasiri wako utadumu au mikono yako itakuwa na nguvu siku hiyo nitakapokushughulikia? Mimi Bwana nimesema na nitalifanya.
Je! Moyo wako utasimama, mikono yako itakuwa hodari katika siku wakati mimi mwenyewe nitakapo kushughulikia? Mimi, Yahwe, nasema hivi, na nitalifanya.
15 Nitakutawanya miongoni mwa mataifa na kukutapanya katika nchi mbalimbali nami nitakomesha unajisi wako.
Hivyo nitakutawanya kati ya mataifa na kukutawanya kati ya nchi mbali mbali. Katika njia hii, nitausafisha uchafu kutoka kwako.
16 Ukiisha kunajisika mbele ya mataifa, utajua kuwa Mimi ndimi Bwana.’”
Hivyo utakuwa mchafu machoni mwa mataifa. Kisha utajua kwamba mimi ni Yahwe.”'
17 Ndipo neno la Bwana likanijia kusema:
Kisha neno la Yahwe likanijia, kusema,
18 “Mwanadamu, nyumba ya Israeli imekuwa kwangu takataka ya chuma, wote kwangu wamekuwa shaba, bati, chuma na risasi iliyoachwa kalibuni. Wao ni taka ya madini ya fedha tu.
“Mwanadamu, nyumba ya Israeli imekuwa takataka kwangu. Wote wamekuwa masazo ya shaba na bati, na chuma na risasi kati yenu. Watakuwa kama takataka ya fedha katika tanuu.
19 Kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: ‘Kwa kuwa wote mmekuwa takataka ya chuma, nitawakusanya Yerusalemu.
Kwa hiyo Bwana Yahwe asema hivi, 'Kwa sababu mmekuwa kama takataka, kwa hiyo, tazama! Nataka kuwakusanya katikakati ya mji wa Yerusalemu.
20 Kama vile watu wakusanyavyo fedha, shaba, chuma, risasi na bati kalibuni ili kuyeyusha kwa moto mkali, ndivyo nitakavyowakusanya katika hasira yangu na ghadhabu yangu kuwaweka ndani ya mji na kuwayeyusha.
Kama kukusanya fedha na shaba, chuma, risasi na chuma kati ya tanuu ili kuvifukutia moto na kuviyeyusha juu yake, nitawayeyusha. Hivyo nitawakusanya katika hasira yangu na ghadhabu. Nitawaweka hapo na kufukutisha moto juu yake ili kuiyeyusha; hivyo nitawakusanya katika hasira yangu na ghadhabu yangu, na nitawaweka hapo na kuwayeyusha.
21 Nitawakusanya na kupuliza juu yenu moto wa hasira yangu na ghadhabu yangu nanyi mtayeyushwa ndani ya huo mji.
Basi nitawakusanya na kuwafukutia kwa moto wa hasira yangu juu yenu hivyo basi mtamwagwa kati yake.
22 Kama fedha iyeyukavyo kalibuni, ndivyo mtakavyoyeyuka ndani ya huo mji, nanyi mtajua kuwa Mimi Bwana nimemwaga ghadhabu yangu juu yenu.’”
Kama kuyeyusha fedha kati ya tanuu, mtayeyushwa chini kati yake, na mtajua yakwamba mimi, Yahwe, nimemwaga ghdhabu yangu juu yenu!”'
23 Neno la Bwana likanijia tena kusema:
Neno la Yahwe likanijia, kusema,
24 “Mwanadamu, iambie nchi, ‘Wewe ni nchi ambayo haijapata mvua wala manyunyu katika siku ya ghadhabu.’
“Mwanadamu, mwambie, 'Wewe ni nchi ambayo haijasafishwa. Hakuna mvua siku ya hasira!
25 Kuna hila mbaya ya wakuu ndani yake kama simba angurumaye akirarua mawindo yake, wanakula watu, wanachukua hazina na vitu vya thamani na kuongeza idadi ya wajane ndani yake.
Kuna njama ya manabii wake kati yake, kama simba angurumaye akirarua mawindo. Wamekula uhai na kuchukua utajiri wa thamani; wamewafanya wajane wengi ndani yake!
26 Makuhani wake wameihalifu sheria yangu na kunajisi vitu vyangu vitakatifu, hawatofautishi kati ya vitu vitakatifu na vitu vya kawaida. Wanafundisha kuwa hakuna tofauti kati ya vitu vilivyo najisi na visivyo najisi, nao wanafumba macho yao katika kutunza Sabato zangu, hivyo katikati yao nimetiwa unajisi.
Makuhani wake hufanya kinyume na sheria yangu, na wamevinajisi vitu vyangu vitakatifu. Hawawezi kutofautisha kati ya vitu vitakatifu na vitu vya najisi. Wanaficha macho yao kutoka Sabato zangu hivyo basi nimetiwa unajisi kati yao.
27 Maafisa wake walioko ndani yake ni kama mbwa mwitu wararuao mawindo yao, wanamwaga damu na kuua watu ili kupata faida ya udhalimu.
Wakuu wake ndani mwake wamekuwa kama mbwa mwitu wakirarua mawindo yao. Wamemwaga damu na kuharibu maisha, ili kupata faida kwa njia ya udanganyifu.
28 Manabii wake wanapaka chokaa matendo haya kwa maono ya uongo na utabiri wa udanganyifu. Wanasema, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo,’ wakati Bwana hajasema.
Manabii wake wamepakwa chokaa; wanaona maono ya uongo na kutabiri uongo kwao. Wanasema “Bwana Yahwe asema hivi”' wakati Yahwe hajanena.
29 Watu wa nchi wanatoza kwa nguvu na kufanya unyangʼanyi, wanawatenda jeuri maskini na wahitaji na kuwaonea wageni, wakiwanyima haki.
Watu wa nchi wamewakandamiza kwa kutaka kwa nguvu na kuwanyang'anya kwa nguvu, na wamewatesa maskini na wahitaji, na kuwakandamiza wageni bila haki.
30 “Nami nikatafuta mtu miongoni mwao, ambaye angejenga ukuta na kusimama mbele zangu mahali palipobomoka kwa ajili ya watu wa nchi ili nisije nikaiangamiza, lakini sikumwona mtu yeyote.
Hivyo nimetafuta mtu kutoka kwao ambaye ataweza kujenga ukuta na ambaye atakayeweza kusimama mbele yangu katika uvunjaji wake kwa ajili ya nchi basi sitaweza kuiharibu, lakini sikuona mtu.
31 Hivyo nitaimwaga ghadhabu yangu juu yao na kuwateketeza kwa moto wa hasira yangu, nikiyaleta juu ya vichwa vyao yale yote waliyotenda, asema Bwana Mwenyezi.”
Hivyo nitaimwaga ghadhabu yangu juu yao. Nitawamaliza kwa moto wa ghadhabu yangu na kuweka njia yao juu ya vichwa vyao wenyewe-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.”'