< Ezekieli 20 >
1 Katika mwaka wa saba, mwezi wa tano siku ya kumi, baadhi ya wazee wa Israeli wakaja ili kutaka ushauri kwa Bwana, wakaketi mbele yangu.
Ikawa ikaja katika mwaka wa saba, siku ya kumi ya mwezi wa tano, wazee wa Israeli wakaja kumuuliza Yahwe na kuketi mbele yangu.
2 Ndipo neno la Bwana likanijia kusema:
Kisha neno la Yahwe likanijia, kusema,
3 “Mwanadamu, sema na wazee wa Israeli uwaambie, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Kwa nini mmekuja? Je, ni kutaka ushauri kwangu? Hakika kama niishivyo, sitawaruhusu mtake ushauri toka kwangu, asema Bwana Mwenyezi.’
“mwanadamu, tangaza kwa wazee wa Israeli na uwaambie, 'Bwana Yahwe asema hivi: Je! Mmekuja kuniuliza swali? Kama niishivyo, sitaulizwa swali na ninyi! -hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.'
4 “Je, utawahukumu? Je, mwanadamu, utawahukumu? Basi uwakabili kwa ajili ya machukizo ya baba zao
Je! Utawahukumu? Utamuhukumu, mwanadamu? Wajulishe kuhusu machukizo ya baba zao.
5 na uwaambie: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Siku ile nilipochagua Israeli, niliwaapia wazao wa nyumba ya Yakobo kwa mkono ulioinuliwa nami nikajidhihirisha kwao huko Misri. Kwa mkono ulioinuliwa niliwaambia, “Mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.”
Waambie, 'Bwana Yahwe asema hivi: Katika siku niliyoichagua Israeli na kuinua mkono wangu kuapa kiapo kwa uzao wa nyumba ya Yakobo, na kufanya kujulikana mimi mwenyewe kwao katika nchi ya Misri, wakati nilipoinua mkono wangu kuapa kiapo kwao. Nalisema, “Mimi ni Yahwe Mungu wenu”-
6 Siku ile niliwaapia wao kwamba nitawatoa katika nchi ya Misri na kuwaleta katika nchi niliyowachagulia, nchi itiririkayo maziwa na asali, nchi nzuri kupita zote.
siku hiyo niliinua mkono wangu kuapa kiapo kwa ajili yao kwamba nitawatoa kutoka nchi ya Misri kwenye nchi ambayo niliyokuwa nimeichagua kwa umakini kwa ajili yao. Ilikuwa ikitiririka maziwa na asali; ilikuwa nzuri sana utukufu miongoni mwa nchi mbali mbali.
7 Nami nikawaambia, “Kila mmoja wenu aondolee mbali sanamu za chukizo ambazo mmekazia macho, nanyi msijitie unajisi kwa sanamu za Misri. Mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.”
Nikawaambia, “Kila mtu atupilie mabli mambo ya machukizo kutoka mbele ya macho yake na sanamu za Misri. Msijitie unajisi; mimi ni Yahwe Mungu wenu.”
8 “‘Lakini waliniasi na hawakunisikiliza, hawakuondolea mbali sanamu za machukizo ambazo walikuwa wamezikazia macho, wala kuondolea mbali sanamu za Misri. Ndipo nikasema, nitawamwagia ghadhabu yangu na kutimiza hasira yangu dhidi yao huko Misri.
Lakini wameasi juu yangu hawakuwa tayari kunisikiliza. Kila mtu hakutupilia mbali mambo ya machukizo kutoka mbele ya macho yake wala kwa ajili ya sanamu za Misri, hivyo nikaona nimwage ghadhabu yangu juu yao kukamilisha hasira yangu miongoni mwao katikati ya nchi ya Misri.
9 Lakini kwa ajili ya Jina langu nilifanya kile ambacho kingelifanya lisitiwe unajisi machoni mwa mataifa waliyoishi miongoni mwao na ambao machoni pao nilikuwa nimejifunua kwa Waisraeli kwa kuwatoa katika nchi ya Misri.
Nilifanya kwa ajili ya jina langu ili lisinajisiwe katika macho ya mataifa ambao walikaa pamoja nao. Nilijifanya mwenyewe kujulikana kwao, katika macho yao, kwa kuwatoa katika nchi ya Misri.
10 Kwa hiyo nikawaongoza watoke Misri na kuwaleta jangwani.
Basi nikawatoa katika nchi ya Misri na kuwaleta kwenye jangwa.
11 Nikawapa amri zangu na kuwajulisha sheria zangu, kwa kuwa mtu anayezitii ataishi kwa hizo.
Kisha nikawapa amri zangu na kufanya maagizo yangu kujulikana kwao, kwa kila mwanadamu atakayezishika ataishi.
12 Pia niliwapa Sabato zangu kama ishara kati yangu nao, ili wapate kujua kuwa Mimi Bwana niliwafanya kuwa watakatifu.
Pia nikawapatia Sabato zangu kama ishara kati yangu na wao, ili wajue kwamba mimi ni Yahwe niwafanyao wawe watakatifu.
13 “‘Lakini watu wa Israeli waliniasi Mimi jangwani. Hawakufuata amri zangu, bali walikataa sheria zangu, ingawa mtu yule anayezitii ataishi kwa hizo sheria, nao walizinajisi Sabato zangu kabisa. Hivyo nilisema ningemwaga ghadhabu yangu juu yao na kuwaangamiza huko jangwani.
Lakini nyumba ya Israeli imeasi dhidi yangu jangwani. Hawakuenenda katika amri zangu; badala yake, wameyakataa maagizo yangu, ambayo mwanadamu ataishi kama akiyatii. Wamezinajisi Sabato zangu sana, basi nikasema nitamwaga hasira yangu juu yao jangwani ili kuwamalliza.
14 Lakini kwa ajili ya Jina langu nikafanya kile ambacho kitalifanya Jina langu lisitiwe unajisi machoni mwa mataifa ambao mbele yao nilikuwa nimewatoa Waisraeli.
Lakini nilifanya kwa ajili ya jina langu hivyo lisinajisiwe katika macho ya mataifa, ambao niliwatoa mbele ya macho yao kutoka Misri.
15 Tena kwa mkono ulioinuliwa nikawaapia huko jangwani kwamba nisingewaingiza katika nchi niliyokuwa nimewapa, yaani, nchi itiririkayo maziwa na asali, nchi nzuri kuliko zote,
Basi mimi mwenyewe pia nimeinua mkono wangu kuapa kiapo kwao jangwani sitawarudisha kwenye nchi ile niliyokuwa naenda kuwapatia, nchi inayotiririkayo maziwa na asali, ambayo ilikuwa nzuri sana ambayo ni nzuri kati ya nchi zote.
16 kwa sababu walikataa sheria zangu na hawakufuata amri zangu na wakazinajisi Sabato zangu. Kwa kuwa mioyo yao iliandama sanamu zao.
Nimeapa hivi kwa sababu walikataa maagizo yangu na kutotembea katika amri zangu, na wazikufuru Sabato zangu.
17 Lakini niliwahurumia wala sikuwaangamiza wala hakuwafuta kabisa jangwani.
Lakini jicho langu likawahurumia kutokana na uharibifu na sikuwaangamiza jangwani.
18 Niliwaambia watoto wao kule jangwani, “Msifuate amri za baba zenu wala kushika sheria zao au kujinajisi kwa sanamu zao.
Nikawaambia watoto wao jangwani, “Msitembee kutokana na amri za wazazi wenu; msiweke maagizo yao au kujinajisi wenyewe kwa sanamu.
19 Mimi ndimi Bwana, Mungu wenu, fuateni amri zangu tena kuweni waangalifu kushika sheria zangu.
Mimi ni Yahwe Mungu wenu, tembeeni katika amri zangu; tunzeni maagizo yangu na kuyatii.
20 Zitakaseni Sabato zangu ili ziwe ishara kati yangu nanyi. Ndipo mtakapojua kuwa Mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.”
Zitunzeni Sabato zangu takatifu ili kwamba zitakuwa ishara kati yangu na ninyi, hivyo basi mtajua yakwamba mimi ni Yahwe Mungu wenu.”
21 “‘Lakini watoto hao wakaniasi: Hawakufuata amri zangu, wala hawakuwa waangalifu kushika sheria zangu, ingawa mtu anayezitii anaishi kwa hizo sheria, nao wakazinajisi Sabato zangu. Hivyo nikasema ningemwaga ghadhabu yangu juu yao na kutimiza hasira yangu dhidi yao huko jangwani.
Lakini watoto wao waliniasi. Hawakutembea kwenye sheria zangu au kushika maagizo yangu, ambazo mwanadamu ataishi kama akizitii. Wamezinajisi Sabato zangu, hivyo nimeamua kumwaga ghadhabu yangu juu yao kutimiza ghadhabu yangu dhidi yao katika jangwa.
22 Lakini nikauzuia mkono wangu na kwa ajili ya Jina langu nikafanya kile ambacho kingelifanya Jina langu lisitiwe unajisi machoni mwa mataifa ambao mbele yao nilikuwa nimewatoa Waisraeli.
Lakini niliurudisha mkono wangu na kutenda kwa ajili ya jina langu, hivyo lisitiwe unajisi katika macho ya mataifa ambao mbele ya macho yao niliwatoa Waisraeli.
23 Tena kwa mkono ulioinuliwa nikawaapia huko jangwani kwamba ningewatawanya miongoni mwa mataifa na kuwatawanya katika nchi mbalimbali,
Mimi mwenyewe pia nimeuinua mkono wangu kuapa juu yao jangwani, kwamba nitawatawanya kati ya maifa na kuwatawanya miongoni mwa nchi mabali mbali.
24 kwa sababu hawakutii sheria zangu lakini walikuwa wamekataa amri zangu na kuzinajisi Sabato zangu, nayo macho yao yakatamani sanamu za baba zao.
Nimeamua kufanya hivi kwa kuwa hawakuzitii amri zangu, na tangu walipo zikataa sheria zangu na kuzinajisi Sabato zangu. Macho yao yalizitamani sanamu za baba zao.
25 Pia niliwaacha wafuate amri ambazo hazikuwa nzuri na sheria ambazo mtu hawezi kuishi kwa hizo sheria.
Kisha niliwapa amri ambazo hazikuwa nzuri, na maagizo ambayo hawakuweza kuishi kwayo.
26 Nikawaacha wanajisiwe kwa matoleo yao, kuwatoa wazaliwa wao wa kwanza kafara kwa sanamu, yaani, kule kuwapitisha wazaliwa wao wa kwanza kwenye moto, nipate kuwajaza na hofu ili wajue kwamba Mimi ndimi Bwana.’
Nikawafanya unajisi kwa zawadi zao wakati walipofanya dhabihu za kila limbuko la tumbo la uzazi na kutupa kwenye moto. Nalifanya hivi ili kuwaogofya hivyo wangeweza kujua kwamba mimi ni Yahwe!'
27 “Kwa hiyo, mwanadamu, sema na watu wa Israeli na uwaambie, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Katika hili pia, baba zenu walinikufuru kwa kuniacha mimi:
Kwa hiyo, mwanadamu, waambie nyumba ya Israeli na waambie, 'Bwana Yahwe asema hivi: Katika hili pia baba zenu walinikufuru wakati walipokuwa sio waaminifu kwangu.
28 Nilipowaleta katika nchi ile ambayo nilikuwa nimeapa kuwapa na kuona kilima chochote kirefu au mti wowote wenye majani mengi, huko walitoa dhabihu zao, wakatoa sadaka ambazo zilichochea hasira yangu, wakafukiza uvumba wenye harufu nzuri na kumimina sadaka zao za kinywaji.
Wakati nilipowaleta kwenye nchi ambayo niliyokuwa nimewaapia kuwapatia, na kisha popote walipoona jiwe lolote refu na mti wenye majani, walitoa sadaka zao, walinikasirisha kwa sadaka zao, na huko pia walichoma ubani wao wa kunukia na kumwaga sadaka zao za kinywaji.
29 Ndipo nikawaambia: Ni nini maana yake hapa mahali pa juu pa kuabudia miungu mnapopaendea?’” (Basi jina la mahali pale panaitwa Bama hata hivi leo.)
Kisha nikawaambia, “Nini maana ya mahali palipoinuka ambapo mmeleta sadaka huko?” Hivyo jina lake linaitwa Bana hata leo.'
30 “Kwa hiyo iambie nyumba ya Israeli: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Je, mtajinajisi kama vile baba zenu walivyofanya na kutamani vinyago vyao vya machukizo?
Kwa hiyo waambie nyumba ya Israeli, 'Bwana Yahwe asema hivi: Je! Kwa nini unajinajisi mwenyewe kwa njia za baba zako? Kwahiyo kwa nini unatenda kama makahaba, kutafuta kwa ajili ya mambo ya machukizo?
31 Mnapotoa matoleo yenu, yaani, wana wenu kafara katika moto, mnaendelea kujinajisi na sanamu zenu zote hadi siku hii ya leo. Je, niulizwe neno na ninyi, ee nyumba ya Israeli? Hakika kama niishivyo, asema Bwana Mwenyezi, mimi sitaulizwa neno na ninyi.
Kwa kuwa wakati mtoapo zawadi zenu na kuwaweka watoto wenu kwenye moto, siku hii mnajitia unajisi pamoja na sanamu zenu zote. Kwa hiyo kwa nini niwaache mniulize mimi, nyumba ya Israeli? Kama niishivyo-Hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-Sitawaacha mniulize swali.
32 “‘Lile lililoko mioyoni mwenu kamwe halitatokea, mnaposema, “Tunataka tuwe kama mataifa mengine, kama watu wengine wa dunia, wanaotumikia miti na mawe.”
Mawazo yanayoumbika kwenye moyo wako hayatatokea kamwe. Mmesema, “Ngoja tuwe kama mataifa mengine, kama koo za nchi nyingine waabuduo mti na jiwe.”
33 Hakika kama niishivyo asema Bwana Mwenyezi, nitatawala juu yenu kwa mkono wa nguvu na kwa mkono ulionyooshwa na kwa ghadhabu iliyomwagwa.
Kama niishivyo-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-Nitatawala hakika juu yenu kwa mkono wenye nguvu, mkono ulionyooshwa, na ghadhabu itakayomwagwa juu yenu.
34 Nitawatoa toka katika mataifa na kuwakusanya kutoka nchi mlikotawanywa, kwa mkono wa nguvu na kwa mkono ulionyooshwa na kwa ghadhabu iliyomwagwa.
Nitawatoa kutoka kwa watu wengine na kuwakusanya kutoka kwenye nchi mlizotawanyika ndani mwao. Nitafanya hivi kwa mkono hodari na kwa ghadhabu iliyomwagika.
35 Nitawaleta katika jangwa la mataifa na huko nitatekeleza hukumu juu yenu uso kwa uso.
Kisha nitawaleta kwenye jangwa la watu, na huko nitawahukumu uso kwa uso.
36 Kama nilivyowahukumu baba zenu katika jangwa la nchi ya Misri, ndivyo nitakavyowahukumu ninyi, asema Bwana Mwenyezi.
Kama nilivyo wahukumu baba zenu katika jangwa la nchi ya Misri, hivyo pia nitawahukumu-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.
37 Nitawafanya mpite chini ya fimbo yangu, nami nitawaleta katika mkataba wa Agano.
Nitawafanya mpite chini ya fimbo yangu, na nitawafanya kutii maagizo yangu ya agano.
38 Nitawaondoa miongoni mwenu wale wanaohalifu na wale wanaoasi dhidi yangu. Ingawa nitawatoa katika nchi wanazoishi, hawataingia katika nchi ya Israeli. Ndipo mtakapojua kuwa Mimi ndimi Bwana.
Nitawasafisha kutoka miongoni mwenu maasi na wale ambao walionichukiza. Nitawatoa kutoka nchi ambayo wanayoishi kama wageni, lakini hawataingia kwenye nchi ya Israeli. Kisha mtajua yakwamba mimi ni Yahwe.
39 “‘Kwa habari zenu ninyi, ee nyumba ya Israeli, hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Nendeni mkatumikie sanamu zenu, kila mmoja wenu! Lakini baadaye hakika mtanisikiliza mimi nanyi hamtalinajisi tena Jina langu takatifu, kwa matoleo yenu na sanamu zenu.
Basi kwenu, nyumba ya Israeli, Bwana Yahwe asema hivi: Kila mmoja wenu ataenda kwa sanamu zake mwenyewe. Muwaabudu kama mtakataa kunisikiliza, lakini hamtalikufuru tena jina langu takatifu kwa zawadi zenu na sanamu zenu.
40 Kwa kuwa katika mlima wangu mtakatifu, mlima mrefu wa Israeli, asema Bwana Mwenyezi, hapo katika nchi nyumba yote ya Israeli itanitumikia mimi, nami huko nitawakubali. Huko nitataka sadaka zenu na matoleo ya malimbuko yenu, pamoja na dhabihu zenu takatifu zote.
Kwa kuwa juu ya mlima wangu mtakatifu, juu ya kilele cha mlima wa Israeli-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-wote wa nyumba ya Israeli mtaniabudu huko katika nchi. Nitabarikiwa kwa kutaka sadaka zenu huko, na pia malimbuko yenu ya shukrani pamoja na vitu vyenu vyote vitakatifu.
41 Nitawakubali ninyi kama uvumba wenye harufu nzuri wakati nitakapowatoa katika mataifa na kuwakusanya kutoka nchi mlipokuwa mmetawanyika, nami nitajionyesha kuwa mtakatifu miongoni mwenu na machoni mwa mataifa.
Nitawapokea kama harufu nzuri ya ubani wakati nitakapowatoa kutoka wale watu na kuwakusanya toka nchi ambazo mlizotawanyika. Nitajifunua mimi mwenyewe kama mtakatifu ndani yenu kwa ajili ya mataifa waone.
42 Ndipo mtakapojua kuwa Mimi ndimi Bwana, nitakapowaleta katika nchi ya Israeli, nchi niliyokuwa nimeapa kwa mkono ulioinuliwa kuwapa baba zenu.
Kisha, wakati nitakapowaleta katika nchi ya Israeli, kwenye nchi ambayo niliuinulia mkono wangu kuapa kuwapatia baba zenu, mtajua yakwamba mimi ni Yahwe.
43 Hapo ndipo nitakapokumbuka mwenendo wenu na matendo yenu yote ambayo kwayo mlijitia unajisi, nanyi mtajichukia wenyewe kwa ajili ya maovu yote mliyokuwa mmetenda.
Kisha mtazikumbuka njia zenu mbaya huko, na matendo yenu yote machafu mliyoyafanya wenyewe, na mtajichukia wenyewe katika macho yenu kwa matendo yenu yote maovu mliyoyafanya.
44 Nanyi mtajua kuwa mimi ndimi Bwana, nitakaposhughulika nanyi kwa ajili ya Jina langu na wala si sawasawa na njia zenu mbaya na matendo yenu maovu, ee nyumba ya Israeli, asema Bwana Mwenyezi.’”
Hivyo mtajua kwamba mimi ni Yahwe nifanyapo haya kwenu kwa ajili ya jina langu, sio kwa njia zenu mbaya au matendo yenu mabovu, nyumba ya Israeli-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.”'
45 Neno la Bwana likanijia kusema:
Kisha neno la Yahwe likanijia, kusema,
46 “Mwanadamu, uelekeze uso wako upande wa kusini, hubiri juu ya upande wa kusini na utoe unabii juu ya msitu wa Negebu.
“Mwanadamu, weka uso wako kuelekea nchi za kusini, na kuongea juu ya kusini; tabiri juu ya msitu wa Negebu.
47 Waambie watu wa Negebu: ‘Sikieni neno la Bwana. Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Ninakaribia kukutia moto, nao utateketeza miti yako yote, mibichi na iliyokauka. Miali ya moto haitaweza kuzimwa na kila uso kutoka kusini mpaka kaskazini utakaushwa kwa moto huo.
Uuambie msitu wa Negebu, 'Hivi ndivyo Yahwe asemavyo-Bwana Yahwe asema hivi: Tazama, nitaweka moto ndani yako. Utakula kila mti mbichi na kila mti mkavu ndani yako. Miali ya moto haitazimika; na kila uso utokao kusini hata kaskazini utateketezwa kwa moto.
48 Kila mmoja ataona kuwa mimi Bwana ndiye niliyeuwasha huo moto, nao hautazimwa.’”
Kisha watu wote wenye mwili watajua yakwamba mimi ni Yahwe nimeuwasha moto, na hautazimika.”'
49 Ndipo niliposema, “Aa, Bwana Mwenyezi! Wao hunisema, ‘Huyu si huzungumza mafumbo tu?’”
Kisha nimesema, Ee! Bwana Yahwe, Wananisema mimi, 'Je! yeye sio mwenye kusema mafumbo?”'