< Ezekieli 15 >

1 Neno la Bwana likanijia kusema:
Kisha neno la Yahwe likanijia, liksema,
2 “Mwanadamu, je, ni vipi mti wa mzabibu unaweza kuwa bora zaidi kuliko tawi la mti mwingine wowote ndani ya msitu?
“Mwanadamu, je ni jisni gani mzabibu ulivo bora kuliko mti na matawi yaliyomo kwenye miti katika msitu?
3 Je, mti wake kamwe huchukuliwa na kutengeneza chochote cha manufaa? Je, watu hutengeneza vigingi vya kuningʼinizia vitu kutokana na huo mti wake?
Je watu huwa wanachukua mbao kutoka kwenye mzabbibu kufanyia chochote? au huwa wanatengenezea vitu kutokana na huo kuning'iniza chochote juu ya huo?
4 Nao baada ya kutiwa motoni kama nishati na moto ukateketeza ncha zote mbili na kuunguza sehemu ya kati, je, unafaa kwa lolote?
Tazama! Kama umetupwa kwenye moto kama kuni, na kama moto umezichoma ncha zake zote na katikati pia, je unafaa kwa chochote?
5 Kama haukufaa kitu chochote ulipokuwa mzima, je, si zaidi sana sasa ambapo hauwezekani kufanyishwa chochote cha kufaa baada ya moto kuuchoma na kuuunguza?
Tazama! Wakati ulipokuwa umekamilika, haukuweza kufanya chochote; kisha hakika, wakati moto ulipouchoma, lakini bado haukuweza kutengeneza kitu chochote kwa ajili ya matumizi yoyote.
6 “Kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Kama nilivyoutoa mti wa mzabibu miongoni mwa miti ya msituni kuwa nishati kwa ajili ya moto, hivyo ndivyo nitakavyowatendea watu waishio Yerusalemu.
Kwa hiyo Bwana Yahwe asema hivi: haufanani na miti katika misitu, niliyoitoa mzabibu kama kuni kwa moto; nitatenda vivyo hivyo mbele ya wakaao Yerusalemu.
7 Nitaukaza uso wangu dhidi yao. Ingawa watakuwa wameokoka kwenye moto, bado moto utawateketeza. Nami nitakapoukaza uso wangu dhidi yao, ninyi mtajua kwamba Mimi ndimi Bwana.
Kwa kuwa nitauweka uso wangu juu yao. Ingawa watatoka kutoka kwenye moto, bado moto utawala; hivyo mtajua kwamba mimi ni Yahwe, wakati nitakapoona uso wangu juu yenu.
8 Nitaifanya nchi kuwa ukiwa kwa sababu wamekuwa si waaminifu, asema Bwana Mwenyezi.”
Kisha nitaifanya nchi kuwa ukiwa kwa sababu wamefanya dhambi-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.”

< Ezekieli 15 >