< Ezekieli 13 >
1 Neno la Bwana likanijia kusema:
Tena, neno la Yahwe likanijia, kusema,
2 “Mwanadamu, tabiri dhidi ya manabii wa Israeli wanaotabiri sasa. Waambie hao ambao hutabiri kutokana na mawazo yao wenyewe: ‘Sikia neno la Bwana!
“Mwanadamu, tabiri dhidi ya manabii wanaotabiri katika Israeli, na uwaambie wale wanotabiri nje ya fikra zao wenyewe, 'Lisikilizeni neno la Yahwe.
3 Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Ole wao manabii wapumbavu wafuatao roho yao wenyewe na wala hawajaona chochote!
Bwana Yahwe asema hivi: Ole wao manbii wajinga ambao wafwatao roho zao wenyewe, lakini wale wasioona kitu!
4 Manabii wako, ee Israeli, ni kama mbweha katikati ya magofu.
Israeli, manabii zako wamekuwa kama mbeha kwenye aridhi iliyoharibiwa na vita.
5 Hamjakwea kwenda kuziba mahali palipobomoka katika ukuta ili kuukarabati kwa ajili ya nyumba ya Israeli, ili kwamba isimame imara kwenye vita katika siku ya Bwana.
Hamkwenda kwenye nyufa katika ukuta uliozunguka nyumba ya Israeli kwa ajili ya kuukarabati, ili kupigana katika vita katika siku ya Yahwe.
6 Maono yao ni ya uongo na ubashiri wao ni wa udanganyifu. Wao husema, “Bwana amesema,” wakati Bwana hakuwatuma, bado wakitarajia maneno yao kutimizwa.
Watu wameona uongo na kufanya utabiri wa uongo, wale wasemao, “Hivi na hivi ndvyo Yahwe asemavyo.” Yahwe hajawatuma, lakini hata hivyo wamewafanya watu kutumaini kwamba ujumbe wao utakuwa kweli.
7 Je, hamjaona maono ya uongo na kusema ubashiri wa udanganyifu hapo msemapo, “Bwana asema,” lakini Mimi sijasema?
Je hamkusikia maono ya uongo na kufanya utabiri wa uongo, ninyi msemao, “Hivi na hivi ndivyo Yahwe asemavyo” Wakati mimi mwenyewe sikuongea?'
8 “‘Kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Kwa sababu ya uongo wa maneno yenu na kwa madanganyo ya maono yenu, Mimi ni kinyume na ninyi, asema Bwana Mwenyezi.
Kwa hiyo Bwana Yahwe asema hivi, 'Kwa sababu mmesikia maono ya uongo na kuwaambia uongo-kwa hiyo hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo dhidi yenu:
9 Mkono wangu utakuwa dhidi ya manabii ambao huona maono ya uongo na kusema ubashiri wa udanganyifu. Hawatakuwa katika baraza la watu wangu au kuandikwa katika kumbukumbu ya nyumba ya Israeli wala hawataingia katika nchi ya Israeli. Ndipo mtajua kuwa Mimi ndimi Bwana Mwenyezi.
Mkono wangu utakuwa juu yenu ninyi manabii mliodanganya maono na wale waliofanya unabii wa uongo. Hawatakuwepo kwenye kusanyiko la watu wangu, au kuandikishwa katika kumbukumbu ya nyumba ya Israeli; hawataenda kwenye nchi ya Israeli. Kwa kuwa mtajua yakwamba mimi ni Bwana Yahwe!
10 “‘Kwa sababu ni kweli wanapotosha watu wangu, wakisema, “Amani,” wakati ambapo hakuna amani, pia kwa sababu, wakati ukuta dhaifu unapojengwa, wanaufunika kwa kupaka chokaa,
Kwa sababu hiyo, na kwa sababu wamewaongoza watu wangu kuwapotosha na kusema, “Amani!” wakati hakuna amani, wanajenga ukuta ambao wataupaka rangi ya chokaa.'
11 kwa hiyo waambie hao wanaoupaka chokaa isiyokorogwa vyema kwamba ukuta huo utaanguka. Mvua kubwa ya mafuriko itanyesha, nami nitaleta mvua ya mawe inyeshe kwa nguvu, nao upepo wa dhoruba utavuma juu yake.
Waambie wale wanaopaka chokaa ukuta, 'Utaanguka chini; kutakuwa na mvua ya kufurika, na nitaleta mvua ya mawe kuufanya uanguke chini, na upepo wa dhoruba kupuliza hata kuuvunja chini.
12 Wakati ukuta utakapoanguka, je, watu hawatawauliza, “Iko wapi chokaa mliyopaka ukuta?”
Tazama, ukuta utaanguka chini. Je wengine hawakuwaambia, “Iko wapi chokaa mliyoipaka juu yake?”
13 “‘Kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Katika ghadhabu yangu nitauachia upepo wa dhoruba, pia katika hasira yangu mvua ya mawe na mvua ya mafuriko itanyesha ikiwa na ghadhabu ya kuangamiza.
Kwa hiyo Bwana Yahwe asema hivi: Nitaleta upepo wa dhoruba katika ghadhabu yangu, na kutakuwa na mafuriko ya mvua kwenye ghadhabu yangu! Mvua ya mawe katika ghadhabu yangu itauharibu kabisa.
14 Nitaubomoa ukuta mlioupaka chokaa na kuuangusha chini ili msingi wake uachwe wazi. Utakapoanguka, mtaangamizwa ndani yake, nanyi mtajua kuwa Mimi ndimi Bwana.
Kwa kuwa nitaurarua chini ukuta ambao mlioufunika kwa chokaa, na nitaubomoa hata kwenye nchi na kuifunua misingi yake. Hivyo utaanguka, nanyi nyote mtaangamizwa katikati ya huo.
15 Hivyo ndivyo nitakavyoitimiza ghadhabu yangu dhidi ya huo ukuta na dhidi yao walioupaka chokaa. Nitawaambia ninyi, “Ukuta umebomoka na vivyo hivyo wale walioupaka chokaa,
Ndivyo nitakavouangamiza kwa ghadhabu yangu ukuta na wale walioupaka chokaa. Nitawaambia, “Ukuta hautaonekana tena, wala watu wanaoupaka chokaa-
16 wale manabii wa Israeli waliotabiri juu ya Yerusalemu na kuona maono ya amani kwa ajili yake wakati kulipokuwa hakuna amani, asema Bwana Mwenyezi.”’
manabii wa Israeli wale waliotabiri kuhusu Yerusalemu na wale waliokuwa wameona amani kwa ajili yake. Lakini hakuna amani! -hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.”
17 “Sasa, mwanadamu, kaza uso wako dhidi ya binti za watu wako wanaotabiri mambo kutoka mawazo yao wenyewe. Tabiri dhidi yao
Hivyo wewe, mwanadamu, weka uso wako dhidi ya binti za watu wako wale wanaotabiri kwa akili zao wenyewe, na kutabiri dhidi yao.
18 na useme, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Ole wao wanawake washonao hirizi za uchawi juu ya viwiko vyao vyote na kutengeneza shela za urefu wa aina mbalimbali kwa ajili ya kufunika vichwa vyao kwa makusudi ya kuwanasa watu. Je, mtatega uhai wa watu wangu lakini ninyi mponye wa kwenu?
Sema, 'Bwana Yahwe asema hivi: Ole kwa wanawake washonao hiziri kwenye kila sehemu ya mkono wao na kutengeza vitambaa vya shela kwa ajili ya vichwa vyao kwa kila kipimo, ili kuwinda watu. Je mtawawinda watu wangu ila kuokoa maisha yenu wenyewe?
19 Ninyi mmeninajisi miongoni mwa watu wangu kwa ajili ya konzi chache za shayiri na chembe za mkate. Kwa kuwaambia uongo watu wangu, wale ambao husikiliza uongo, mmewaua wale watu ambao wasingekufa na kuwaacha hai wale ambao wasingeishi.
Ninyi mmenikufuru mbele ya watu wangu kwa ajili ya makonzi ya shayiri na vipande vya mkate, kuwaua watu ambao hawakutakiwa kufa, na kuyalinda maisha ya wale ambao hawatakiwi kuendelea kuishi, kwa sababu ya uongo wenu kwa watu wangu walio wasikiliza.
20 “‘Kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Mimi niko kinyume na hizo hirizi zenu za uchawi ambazo kwa hizo mnawatega watu kama ndege, nami nitazirarua kutoka mikononi mwenu, nitawaweka huru watu wale mliowatega kama ndege.
Kwa hiyo Bwana Yahwe asema hivi: Niko kinyume dhidi ya hirizi ambazo mlizozitumia kuyakamata kwa hila maisha ya watu kana kwamba wamekuwa ndege. Naam, nitazichana kutoka kwenye mikono yenu; na wale watu mlio watega kama ndege-nitawaacha waende huru.
21 Nitazirarua shela zenu na kuwaokoa watu wangu kutoka mikononi mwenu, nao hawatakuwa tena mawindo ya nguvu zenu. Ndipo mtakapojua kuwa Mimi ndimi Bwana.
Nitavichana mbali vitambaa vya shela na kuwaokoa watu wangu kutoka kwenye mikono yangu, kwa hiyo hawatategwa tena kwenye mikono yenu. Mtajua kwamba mimi ni Yahwe.
22 Kwa sababu mliwavunja moyo wenye haki kwa uongo wenu, wakati mimi sikuwaletea huzuni na kwa kuwa mliwatia moyo waovu ili wasiziache njia zao mbaya na hivyo kuokoa maisha yao,
Kwa sababu mmeuvunja moyo wa mtu mwenye haki kwa uongo, ingawa hata mimi sikutamani kuvunjwa kwake moyo, na kwa sababu mmemtia moyo badala yake matendo ya mtu mwovu ili kwamba asitaweze kurudi kutoka kwenye njia yake kuokoa maisha yake-
23 kwa hiyo hamtaona tena maono ya uongo wala kufanya ubashiri. Nitawaokoa watu wangu kutoka mikononi mwenu. Nanyi ndipo mtakapojua kuwa Mimi ndimi Bwana.’”
kwa hiyo hamtayaona tena maono ya uongo au kuendelea kufanya utabiri, kwa kuwa nitawaokoa watu wangu kutoka kwenye mkono wako. Nanyi mtajua kwamba mimi ni Yahwe.'”