< Ezekieli 10 >
1 Nikatazama, nikaona juu ya ile nafasi iliyokuwa juu ya vichwa vya wale makerubi kulikuwa na kitu mfano wa kiti cha enzi cha yakuti samawi.
Nilipokuwa nikingalia mbele ya anga ambalo liliyokuwa juu ya vichwa vya kerubi; kitu kikawatokea juu yao kama rangi ya samawati mwonekano wake ulikuwa kama kiti cha enzi.
2 Bwana akamwambia mtu yule aliyekuwa amevaa nguo ya kitani, “Ingia katikati ya yale Magurudumu yaliyo chini ya makerubi. Ukaijaze mikono yako makaa ya mawe ya moto kutoka katikati ya makerubi na uyatawanye juu ya mji.” Nilipokuwa nikiangalia, akaingia ndani.
Kisha Yahwe akaongea na yule mtu alikuwa maevaa nguo za kitani na kusema, “Nenda kati ya magurudumu chini ya kerubi, na jaza mikono yako yote na watawanye juu ya mji.” Kisha yule mtu akaenda ndani nikiwa natazama.
3 Basi wale makerubi walikuwa wamesimama upande wa kusini wa Hekalu wakati yule mtu alipoingia ndani, wingu likaujaza ule ukumbi wa ndani.
Kerubi likasimama juu ya upande wa kulia wa nyumba wakati yule mtu alipoingia, na wingu likaja a ndani ya uzio.
4 Kisha utukufu wa Bwana ukainuka kutoka juu ya wale makerubi ukaenda kwenye kizingiti cha Hekalu. Wingu likajaza Hekalu, nao ukumbi ukajawa na mngʼao wa utukufu wa Bwana.
Utukufu wa Yahwe ukainuka kutoka kwenye kerubi na kusimama kwenye kizingiti cha nyumba. Ukaijaza nyumaba kwa wingu, na uzio ulikuwa umejaa nuru ya utukufu wa Yahwe.
5 Sauti ya mabawa ya wale makerubi ingeweza kusikika mpaka kwenye ukumbi wa nje, kama sauti ya Mungu Mwenyezi wakati anapoongea.
Sauti ya mabawa ya kerubi ikasikika kwa mbali nje ya uzio, kama sauti ya Mungu mwenyezi wakati akiwa anaongea.
6 Bwana alipomwamuru yule mtu aliyevaa nguo za kitani akisema, “Chukua moto toka katikati ya magurudumu, kutoka katikati ya makerubi,” yule mtu aliingia ndani akasimama pembeni mwa gurudumu.
Ikawa kuhusu, Mungu alipoamwamuru yule mtu aliyekuwa amevaa nguo za kitani na kusema, “Chukua moto kutoka kwenye ya kerubi,” yule mtu akaenda na kusimama karibu na gurudumu.
7 Ndipo mmoja wa wale makerubi akanyoosha mkono wake kwenye moto uliokuwa katikati yao. Akachukua baadhi ya moto na kuutia mikononi mwa yule mtu aliyevaa mavazi ya kitani, naye akaupokea akatoka nje.
Kerubi akaunyoosha mkono wake kwenye kerubi kwenye moto uliokuwa miongoni mwa kerubi, na kuiacha juu na kuiweka kwenye mikono ya yule mtu aliyekuwa amevaa vazi la kitani. Yule mtu akaichukua na kurudi.
8 (Chini ya mabawa ya makerubi paliweza kuonekana kitu kilichofanana na mikono ya mwanadamu.)
Nikaona juu ya kerubi kitu kama mkono wa mtu juu ya mabawa yao.
9 Nikatazama, nikaona magurudumu manne kando ya makerubi, moja kando ya kila kerubi. Magurudumu hayo yalimetameta kama kito cha zabarajadi.
Hivyo nikaona, na tazama! Magurudumu manne yalikuwa karibu na kerubi-gurudumu moja karibu na kila kerubi-na mwonekano wa hayo magurudumu ulikuwa kama jiwe la zabarajadi.
10 Kule kuonekana kwake, yote manne yalifanana kila gurudumu lilikuwa kama linazunguka ndani ya lingine.
Mwonekano wake ulikuwa unaofanana kama wa wote wanne, kama gurudumu lililokuwa kwenye gurudumu lingine.
11 Yalipozunguka, yalikwenda kokote katika pande nne walikoelekea wale makerubi. Magurudumu hayakugeuka wakati makerubi yalipokwenda. Makerubi walikwenda upande wowote kichwa kilikoelekea pasipo kugeuka walipokuwa wakienda.
wakati walipokuwa wakitembea, walienda katika pande zote nne bila kugeuka katika kwenye njia nyingine. Badala yake, popote kichwa kilipoelekea, walilifuata. Hawakugeuka kwenye njia yeyote nyingine walipokuwa wakienda.
12 Miili yao yote, pamoja na migongo yao, mikono na mabawa yao yote yalikuwa yamejaa macho kabisa kama yalivyokuwa yale magurudumu yao manne.
Mwili wao wote-pamoja na migongo yao, mikono yao, na mabawa yao-vilikuwa vimefunikwa kwa macho, na macho kufunika magurudumu manne kuzunguka pote pia.
13 Nikasikia magurudumu yakiitwa, “Magurudumu ya kisulisuli.”
Nilikuwa nasikia, magurudumu yalikuwa yakiita, “Kuzunguka.”
14 Kila mmoja wa wale makerubi alikuwa na nyuso nne: Uso mmoja ulikuwa kama vile wa kerubi, uso wa pili ulikuwa wa mwanadamu, uso wa tatu ulikuwa wa simba na uso wa nne ulikuwa wa tai.
Walikuwa na nyuso nne kila moja; uso wa kwanza ulikuwa uso wa kerubi, uso wa pili ulikuwa uso wa mtu, uso wa tatu ulikuwa uso wa simba, na uso wa nne ulikuwa uso wa malaika.
15 Kisha makerubi wakapaa juu. Hawa ndio wale viumbe walio hai niliowaona kando ya Mto Kebari.
Kisha makerubi-hawa walikuwa viumbe hai nilivyokuwa nimeviona karibu na Keberi Kanali-wakainuka juu.
16 Wakati makerubi walipokwenda, magurudumu yaliyoko kando yao yalikwenda na wakati makerubi walipotanda mabawa yao wapate kupaa juu kutoka ardhi, magurudumu yale hayakuondoka pembeni mwao.
Popote makerubi walipoenda, magurudumu yalienda karibu nao, na popote makerubi walipoinua juu mabawa yao kupaa juu kutoka kwenye nchi, magurudumu hayakugeuka. Yaliendelea kuwa karibu nao.
17 Makerubi yaliposimama kimya, nayo pia yalitulia kimya, nao makerubi yalipoinuka juu, magurudumu nayo yaliinuka juu pamoja nao, kwa sababu roho ya vile viumbe hai ilikuwa ndani yake.
Wakati makerubi waliposimama, magurudumu yalisimama pia, na wakati walipoinuka juu, magurudumu yaliinuka juu pamoja nao, kwa kuwa roho wa vile viumbe hai walikuwa kwenye magurudumu.
18 Kisha utukufu wa Bwana ukaondoka pale kwenye kizingiti cha Hekalu na kusimama juu ya wale makerubi.
Kisha utukufu wa Yahwe ukaja kutoka juu ya kizingiti cha nyumba na kusimama juu ya kerubi.
19 Nilipokuwa nikitazama, makerubi yakatanda mabawa yao na kuinuka kutoka ardhini, nao walipokuwa wakienda, yale magurudumu yakaenda pamoja nao. Wakasimama kwenye ingilio la lango la mashariki la nyumba ya Bwana, nao utukufu wa Mungu wa Israeli ukawa juu yao.
Lile kerubi likaacha juu mabawa na kuinuka kutoka kwenye jicho langu wakati walipotoka nje, na yale magurudumu yakafanya vivyo hivyo karibu yao. Wakasimama upande wa mashariki kuingia kwenye nyumba ya Yahwe, na utukufu wa Mungu wa Israeili ukaja juu yao kutoka juu.
20 Hawa walikuwa ndio viumbe hai niliokuwa nimewaona chini ya Mungu wa Israeli kando ya Mto Kebari, nami nikatambua ya kuwa hao walikuwa makerubi.
Hawa walikuwa viumbe hai ambao niliokuwa nimewaona chini ya Mungu wa Israeli karibu na Kebari Kanali, hivyo nilijua kwamba walikuwa makerubi!
21 Kila mmoja alikuwa na nyuso nne, mabawa manne, chini ya mabawa yao kulikuwa na kile kilichoonekana kama mikono ya mwanadamu.
Walikuwa na macho manne kila mmoja na mabawa manne, na mfanano wa nyuso zao zilikuwa na mfanano wa mikono ya mwanadamu chini ya mabawa yao,
22 Nyuso zao zilifanana kama zile nilizokuwa nimeziona kando ya Mto Kebari. Kila mmoja alikwenda mbele moja kwa moja.
na mfanano wa nyuso zao ulikuwa kama nyuso nilizokuwa nimeziona kwa maono huko Keberi Kanali, na kila mmoja wao alienda mbele.