< Ezekieli 10 >
1 Nikatazama, nikaona juu ya ile nafasi iliyokuwa juu ya vichwa vya wale makerubi kulikuwa na kitu mfano wa kiti cha enzi cha yakuti samawi.
我觀望時,見在革魯賓頭上,穹蒼之上,有一塊像碧玉的石頭,看似寶座,出現在他們上邊。
2 Bwana akamwambia mtu yule aliyekuwa amevaa nguo ya kitani, “Ingia katikati ya yale Magurudumu yaliyo chini ya makerubi. Ukaijaze mikono yako makaa ya mawe ya moto kutoka katikati ya makerubi na uyatawanye juu ya mji.” Nilipokuwa nikiangalia, akaingia ndani.
上主問那身穿細麻衣的人說:「你到革魯賓下邊的輪子中間,由革魯賓中間取一滿掬火炭,撒在城上。」他就在我眼前進去了。
3 Basi wale makerubi walikuwa wamesimama upande wa kusini wa Hekalu wakati yule mtu alipoingia ndani, wingu likaujaza ule ukumbi wa ndani.
當那人進去時,革魯賓站在聖殿的右邊,雲彩瀰漫了內院。
4 Kisha utukufu wa Bwana ukainuka kutoka juu ya wale makerubi ukaenda kwenye kizingiti cha Hekalu. Wingu likajaza Hekalu, nao ukumbi ukajawa na mngʼao wa utukufu wa Bwana.
上主的光榮,由革魯賓之間升起,停在聖殿的門限上,聖殿內充滿了雲彩,庭院中也充滿了上主光榮的燦爛。
5 Sauti ya mabawa ya wale makerubi ingeweza kusikika mpaka kwenye ukumbi wa nje, kama sauti ya Mungu Mwenyezi wakati anapoongea.
革魯賓展翅的響聲達於外院,像全能的天主講話的聲音。
6 Bwana alipomwamuru yule mtu aliyevaa nguo za kitani akisema, “Chukua moto toka katikati ya magurudumu, kutoka katikati ya makerubi,” yule mtu aliingia ndani akasimama pembeni mwa gurudumu.
以後他吩咐那身穿細麻衣的人說:「從輪子中間,從革魯賓中間取火罷! 」那人就前去,站在輪子旁邊。
7 Ndipo mmoja wa wale makerubi akanyoosha mkono wake kwenye moto uliokuwa katikati yao. Akachukua baadhi ya moto na kuutia mikononi mwa yule mtu aliyevaa mavazi ya kitani, naye akaupokea akatoka nje.
一位革魯賓由革魯賓中間伸手,到革魯賓中間的火上取了火,放在那身穿細麻衣的手中;那人接過去就走了。
8 (Chini ya mabawa ya makerubi paliweza kuonekana kitu kilichofanana na mikono ya mwanadamu.)
我看見革魯賓在翅膀下的手好像人手。
9 Nikatazama, nikaona magurudumu manne kando ya makerubi, moja kando ya kila kerubi. Magurudumu hayo yalimetameta kama kito cha zabarajadi.
我觀望時,見革魯賓旁邊有四個輪子,每一位革魯賓旁有一個輪子,輪子的外表光澤有如橄欖玉石。
10 Kule kuonekana kwake, yote manne yalifanana kila gurudumu lilikuwa kama linazunguka ndani ya lingine.
輪子的外表,四個都有同樣的形狀,好像輪子套在輪子中。
11 Yalipozunguka, yalikwenda kokote katika pande nne walikoelekea wale makerubi. Magurudumu hayakugeuka wakati makerubi yalipokwenda. Makerubi walikwenda upande wowote kichwa kilikoelekea pasipo kugeuka walipokuwa wakienda.
轉動時可向四面旋轉,前行時不必回轉。
12 Miili yao yote, pamoja na migongo yao, mikono na mabawa yao yote yalikuwa yamejaa macho kabisa kama yalivyokuwa yale magurudumu yao manne.
在他們的身體、背、手、翅膀和四個輪子上,佈滿了眼睛。
13 Nikasikia magurudumu yakiitwa, “Magurudumu ya kisulisuli.”
我所說的輪子名叫「加耳加耳。」
14 Kila mmoja wa wale makerubi alikuwa na nyuso nne: Uso mmoja ulikuwa kama vile wa kerubi, uso wa pili ulikuwa wa mwanadamu, uso wa tatu ulikuwa wa simba na uso wa nne ulikuwa wa tai.
每一個革魯賓有四個形狀:第一個形狀是牛形,第二個形狀是人形,第三個形狀是獅形,第四個形狀是鷹形。
15 Kisha makerubi wakapaa juu. Hawa ndio wale viumbe walio hai niliowaona kando ya Mto Kebari.
以後革魯賓上升去了;這是我在革巴爾河岸所見的活物。
16 Wakati makerubi walipokwenda, magurudumu yaliyoko kando yao yalikwenda na wakati makerubi walipotanda mabawa yao wapate kupaa juu kutoka ardhi, magurudumu yale hayakuondoka pembeni mwao.
革魯賓前行時,輪子也在他們旁邊轉動;革魯賓展開翅膀,由地面升起時,輪子也不離他們左右。
17 Makerubi yaliposimama kimya, nayo pia yalitulia kimya, nao makerubi yalipoinuka juu, magurudumu nayo yaliinuka juu pamoja nao, kwa sababu roho ya vile viumbe hai ilikuwa ndani yake.
他們站住,輪子也停下;他們升起,輪子也同他們一起升起,因為輪子內有活物的神力。
18 Kisha utukufu wa Bwana ukaondoka pale kwenye kizingiti cha Hekalu na kusimama juu ya wale makerubi.
那時,上主的光榮離開了聖殿的門限,停在革魯賓上。
19 Nilipokuwa nikitazama, makerubi yakatanda mabawa yao na kuinuka kutoka ardhini, nao walipokuwa wakienda, yale magurudumu yakaenda pamoja nao. Wakasimama kwenye ingilio la lango la mashariki la nyumba ya Bwana, nao utukufu wa Mungu wa Israeli ukawa juu yao.
革魯賓展開翅膀,在我眼前由地面升起;當他們離去時,輪子也跟著離去。他們停在上主聖殿的東門門口時,以色列的天主的光榮就停在他們上面。
20 Hawa walikuwa ndio viumbe hai niliokuwa nimewaona chini ya Mungu wa Israeli kando ya Mto Kebari, nami nikatambua ya kuwa hao walikuwa makerubi.
這就是我靠近革巴爾河,在以色列的天主下面所見的那些活物,現在我明白他們是革魯賓。
21 Kila mmoja alikuwa na nyuso nne, mabawa manne, chini ya mabawa yao kulikuwa na kile kilichoonekana kama mikono ya mwanadamu.
每個有四樣形狀,每個有四個翅膀,在他們翅膀下有相似人的手。
22 Nyuso zao zilifanana kama zile nilizokuwa nimeziona kando ya Mto Kebari. Kila mmoja alikwenda mbele moja kwa moja.
關於他們的形像,和我靠近革巴爾河所見的形像一樣,每個朝自己的前面進行。