< Kutoka 27 >
1 “Jenga madhabahu ya mbao za mti wa mshita, kimo chake kiwe dhiraa tatu; itakuwa mraba, urefu wake dhiraa tano, na upana wake dhiraa tano.
Nawe fanya madhabahu ya mti wa mshita, urefu wake utakuwa ni dhiraa tano na upana wake dhiraa tano. Hiyo madhabahu itakuwa mraba na kwenda juu kwake kutakuwa dhiraa tatu.
2 Tengeneza upembe kwenye kila pembe ya hizo pembe nne, ili zile pembe na madhabahu ziwe zimeungana, na ufunike madhabahu kwa shaba.
Nawe fanya pembe nne kama mfano wa pembe za ng'ombe. Hizo pembe zitakuwa za kitu kimoja na madhabahu, nawe utayafunika kwa shaba.
3 Tengeneza vyombo vyake vyote kwa shaba: vyungu vyake vya kuondolea majivu, masepetu, mabakuli ya kunyunyizia, uma za nyama, na vyombo vya kuchukulia moto.
Lazima vyombo vyake vya kuyaondoa majivu yake utavifanya, na majembe yake, na mabakuli yake, na uma zake, na meko yake. Vyombo vyake vyote utavifanya vya shaba.
4 Kisha tengenezea hayo madhabahu wavu wa shaba, na utengeneze pete za shaba kwenye kila moja ya hizo pembe nne za huo wavu.
Nawe uifanyie hiyo madhabahu wavu wa shaba. Kisha utie pete nne za shaba katika hizo pembe nne za ule wavu.
5 Weka wavu huo chini ya ukingo wa madhabahu ili ufikie nusu ya kimo cha madhabahu.
Nawe lazima uweke huo wavu chini ya kizingo kiizungukacho madhabahu upande wa chini.
6 Tengeneza mipiko ya mti wa mshita kwa ajili ya madhabahu, na uifunike kwa shaba.
Nawe fanya miti kwa ajili ya madhabahu, miti ya mshita, na kuifunika shaba.
7 Hiyo mipiko itaingizwa kwenye zile pete ili iwe pande mbili za madhabahu inapobebwa.
Na hiyo miti itatiwa katika viduara, na ile miti itakuwa katika pande mbili za madhabahu, wakati wa kuichukua.
8 Tengeneza madhabahu yawe na uvungu ndani yake ukitumia mbao. Utaitengeneza sawasawa na vile ulivyoonyeshwa mlimani.
Uifanye ya mbao, yenye mvungu ndani yake kama ulivyooneshwa mlimani.
9 “Tengeneza ua kwa ajili ya Hema la Kukutania. Upande wa kusini utakuwa na urefu wa dhiraa mia moja, na utakuwa na mapazia ya kitani iliyosokotwa vizuri,
Nawe ufanye ua wa maskani. Upande wa kusini wa kuelekea kusini kutakuwa na chandarua ya nguo ya kitani nzuri yenye kusokotwa, kwa huo ua, urefu wake upande mmoja utakuwa ni dhiraa mia moja.
10 pamoja na nguzo ishirini na vitako vya shaba ishirini, na kulabu na tepe za fedha juu ya hizo nguzo.
Na nguzo zake zitakuwa nguzo ishirini, na vitako vyake ishirini, vitako vyake vitakuwa vya shaba kulabu za zile nguzo na vitanzi vyake vitakuwa vya fedha.
11 Upande wa kaskazini utakuwa na urefu wa dhiraa mia moja, nao utakuwa na mapazia, pamoja na nguzo ishirini na vitako vya shaba ishirini, pamoja na kulabu na tepe za fedha juu ya hizo nguzo.
Ni vivyo hivyo upande wa kaskazini, urefu wake hiyo chandarua utakuwa ni dhiraa mia moja, na nguzo zake ishirini, na vitako vyake ishirini vitakuwa vya shaba, kulabu za zile nguzo na vitanzi vyake vitakuwa vya fedha.
12 “Upande wa magharibi wa ua utakuwa na upana wa dhiraa hamsini, nao utakuwa na mapazia, na nguzo kumi na vitako vyake kumi.
Na upande wa magharibi, upana wa ua kutakuwa na chandarua ya dhiraa hamsini; nguzo zake kumi, na vitako vyake kumi.
13 Upande wa mwisho wa mashariki jua linakochomoza, ua pia utakuwa na upana wa dhiraa hamsini.
Na upana wa ule ua upande wa mashariki kuelekea mashariki utakuwa ni dhiraa hamsini.
14 Mapazia yenye urefu wa dhiraa kumi na tano yatakuwa upande mmoja wa ingilio, pamoja na nguzo tatu na vitako vitatu.
Chandarua upande mmoja wa lango itakuwa dhiraa kumi na tano upana wake. Lazima nguzo zake zitakuwa tatu na vitako vyake vitatu.
15 Kutakuwepo tena na mapazia ya dhiraa kumi na tano kwa upande mwingine wa ingilio, pamoja na nguzo tatu na vitako vitatu.
Upande wa pili ni vivyo hivyo chandarua ya dhiraa kumi na tano; nguzo zake tatu, na vitako vyake vitatu.
16 “Kuhusu ingilio la ua, weka pazia lenye urefu wa dhiraa ishirini la nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu pamoja na kitani iliyosokotwa vizuri, kazi ya mtarizi. Pazia hilo litashikiliwa na nguzo nne na vitako vinne.
Na kwa lile lango la ua patakuwa na kisitiri cha dhiraa ishirini, kitakuwa cha nguo ya rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na kitani nzuri yenye kusokotwa, kazi ya mshonaji taraza; nguzo zake zitakuwa nne, na vitako vyake vinne.
17 Nguzo zote zinazozunguka ua zitakuwa na tepe na kulabu za fedha, na vitako vya shaba.
Nguzo zote za ule ua ziuzungukao pande zote zitakuwa na vitanzi vya fedha; kulabu zake za fedha, na vitako vyake vya shaba.
18 Ua wa kukutania utakuwa na urefu wa dhiraa mia moja na upana wa dhiraa hamsini, ukiwa na mapazia ya kitani yaliyosokotwa vizuri yenye urefu wa dhiraa tano kwenda juu na vitako vya shaba.
Urefu wa huo ua utakuwa dhiraa mia moja, na upana wake utakuwa dhiraa hamsini kotekote, na kwenda juu kwake dhiraa tano; yawe ya nguo ya kitani nzuri, na vitako vyake vitakuwa vya shaba.
19 Vyombo vingine vyote vinavyotumika katika maskani kwa shughuli yoyote, pamoja na vigingi vyote na hata vile vya ua, vitakuwa vya shaba.
Vyombo vyote vya maskani vitumiwavyo katika utumishi wake wote, na vigingi vyake vyote, na vigingi vyote vya ule ua, vitakuwa vya shaba.
20 “Utawaamuru Waisraeli wakuletee mafuta safi ya zeituni yaliyokamuliwa kwa ajili ya mwanga ili zile taa ziwake mfululizo.
awe waamuru wana wa Israeli wakuletee mafuta ya zeituni safi ya kupondwa kwa ajili ya nuru, ili kufanya ile taa kuwaka daima.
21 Katika Hema la Kukutania, nje ya pazia lililo mbele ya Sanduku la Ushuhuda, Aroni na wanawe watahakikisha kuwa taa hizo zinawaka kuanzia jioni mpaka asubuhi mbele za Bwana. Hili litakuwa agizo la milele miongoni mwa Waisraeli kwa vizazi vyote vijavyo.
Ndani ya ile hema ya kukutania, nje ya hilo pazia, lililo mbele ya huo ushuhuda, Haruni na wanawe wataitengeza tangu jioni hadi asubuhi mbele ya BWANA; itakuwa ni amri ya milele katika vizazi vyao vyote kwa ajili ya wana wa Israeli.