< Kutoka 24 >
1 Kisha Mungu akamwambia Mose, “Njooni huku juu kwa Bwana, wewe na Aroni, Nadabu na Abihu, pamoja na wazee sabini wa Israeli. Mniabudu kwa mbali,
Kisha Yahweh akamwabia Musa, “Njoo juu kwangu -wewe, Aruni, Nadabu, Abihu, na wazee sabini wa Israeli, na kuniabudu kwa mbali.
2 lakini Mose peke yake ndiye atakayemkaribia Bwana; wengine wasije karibu. Nao watu wasije wakapanda pamoja naye.”
Musa peke yake anaweza kuja karibu yangu. Wengine hawapaswi kuja karibu, wala watu kuja juu na yeye.”
3 Mose alipokwenda na kuwaambia watu maneno yote na sheria zote za Bwana, wakaitikia kwa sauti moja, “Kila kitu alichosema Bwana tutakifanya.”
Musa akaenda juu na kuwaambia watu maneno yote ya Yahweh na amri zake. Watu wote wakajibu kwa sauti moja na kusema, “Tutafanya maneno yote Yahweh aliyo tuamuru.”
4 Ndipo Mose akaandika kila kitu Bwana alichokuwa amesema. Akaamka kesho yake asubuhi na mapema na kujenga madhabahu chini ya mlima na kusimamisha nguzo kumi na mbili za mawe kuwakilisha makabila kumi na mawili ya Israeli.
Kisha Musa akaandika chini maneno yote ya Yahweh. Asubui mapema, Musa akajenga madhabahu chini ya mguu wa mlima na kupanga nguzo kumi na mbili za mawe, ili mawe yawakilishe makabila kumi na mbili ya Israeli.
5 Kisha akawatuma vijana wanaume wa Kiisraeli, nao wakatoa sadaka za kuteketezwa na dhabihu za mafahali wachanga kuwa sadaka za amani kwa Bwana.
Aliwatuma vijana Wakiisraeli kutoa sadaka ya kuteketeza na kutoa dhabihu za ng'ombe za sadaka ya ushirika kwa Yahweh.
6 Mose akachukua nusu ya damu ya wale wanyama na kuiweka kwenye mabakuli na nusu nyingine akainyunyiza juu ya madhabahu.
Musa allichukuwa nusu ya damu na kuweka kwenye mabeseni; alinyunyuzia nusu ingine kwenye madhabahu.
7 Kisha akachukua kile Kitabu cha Agano na kuwasomea watu. Nao wakajibu, “Tutafanya kila kitu alichosema Bwana, nasi tutatii.”
Alichukuwa kitabu cha agano na kuwasomea kwa nguvu watu. Walisema, “Tutafanya yote Yahweh aliyo sema. Tutakuwa watiifu.”
8 Ndipo Mose akachukua ile damu, akawanyunyizia wale watu, akasema, “Hii ni damu ya agano ambalo Bwana amelifanya nanyi kufuatana na maneno haya yote.”
Kisha Musa akachukuwa damu na kunyunyiza kwa watu. Alisema, “Hii ni damu ya agano Yahweh alilo lifanya nanyi kwa kuwapa hii ahadi kwa maneno yote haya.”
9 Mose na Aroni, Nadabu na Abihu, pamoja na wazee sabini wa Israeli wakapanda mlimani,
Kisha Musa, Aruni, Nadabu, Abihu, na wazee sabini wa Israeli wakaenda juu ya mlima.
10 nao wakamwona Mungu wa Israeli. Chini ya miguu yake kulikuwa na kitu kama sakafu ya mawe ya yakuti samawi, iliyo safi kama anga angavu.
Walimuona Mungu wa Israeli.
11 Lakini Mungu hakuinua mkono wake dhidi ya hawa viongozi wa Waisraeli; walimwona Mungu, nao wakala na kunywa.
Chini ya miguu yake kulikuwa na sakafu iliyo jengwa kwa jiwe la yakuti samawi, safi kama mbingu yenyewe. Mungu hakugusa na mkono kwa hasira viongozi Waisraeli. Walimuona Mungu, na wakanywa na kula.
12 Bwana akamwambia Mose, “Panda uje kwangu huku mlimani na ukae hapa, nami nitakupa vibao vya mawe, vyenye sheria na amri ambazo nimeziandika ziwe mwongozo wao.”
Yahweh akamwambia Musa, “Njoo juu kwangu mlimani na ubaki pale. Nitakupa saani za mawe na sheria na amri nilizo ziandika, ili uwafundishe.”
13 Basi Mose akaondoka na Yoshua mtumishi wake, naye Mose akapanda juu kwenye mlima wa Mungu.
Hivyo Musa akaenda na msaidizi wake Yoshua na kwenda juu mlima wa Mungu.
14 Mose akawaambia wazee wa Israeli, “Tungojeni hapa mpaka tutakapowarudia. Aroni na Huri wako pamoja nanyi, na kila aliye na neno aweza kuwaendea wao.”
Musa akawaambia wazee, “Baki hapa na mtusubiri hadi tutakapo warudia. Aruni na Huri wapo nanyi. Kama kuna mtu mwenye malalamiko, acha awaende.”
15 Mose alipopanda juu mlimani, wingu liliufunika huo mlima,
Hivyo Musa akaenda juu ya mlima, na wingu likafunika.
16 nao utukufu wa Bwana ukatua juu ya Mlima Sinai. Kwa muda wa siku sita wingu lilifunika mlima, na siku ya saba Bwana akamwita Mose kutoka katikati ya lile wingu.
Utukufu wa Yahweh ukabaki juu ya Mlima wa Sinai, na wingu likafunika kwa siku sita. Siku ya saba alimuita Musa kutoka ndani ya wingu.
17 Kwa Waisraeli utukufu wa Bwana ulionekana kama moto uteketezao juu ya mlima.
Utukufu wa Yahweh ulikuwa kama moto ulao juu ya mlima kwenye macho ya Waisraeli.
18 Kisha Mose akaingia ndani ya lile wingu alivyokuwa akipanda mlimani. Naye akakaa huko mlimani kwa muda wa siku arobaini, usiku na mchana.
Musa akaingia kwenye wingu na kwenda juu ya mlima. Alikuwa mlimani siku arobaini na usiku arobaini.