< Kutoka 13 >
Yahweh akasema na Musa na kumwambia,
2 “Niwekeeni wakfu kila mzaliwa wa kwanza wa kiume. Kila mtoto wa kwanza aliye kifungua tumbo miongoni mwa Waisraeli ni mali yangu, akiwa wa mwanadamu au wa mnyama.”
“Nitengee wazaliwa wote wa kwanza, kila mzaliwa wa kwanza wa Waisraeli, watu na wanyama. Mzaliwa wa kwanza ni wangu.”
3 Ndipo Mose akawaambia watu, “Ikumbukeni siku hii, siku ambayo mlitoka katika nchi ya Misri, katika nchi ya utumwa, kwa sababu Bwana aliwatoa humo kwa mkono wenye nguvu. Msile chochote kilichotiwa chachu.
Musa akawambia watu, “Hii kumbukeni hii siku, siku mliyo toka Misri, kutoka nyumba ya utumwa, kwa mkono hodari wa Yahweh amewatoa kutoka hii sehemu. Hakuna mkate wa hamira waruhusiwa kuliwa.
4 Leo, katika mwezi wa Abibu, mnatoka.
Mnatoka Misri hii siku, mwezi wa Abibu.
5 Bwana atakapokuleta katika nchi ya Wakanaani, Wahiti, Waamori, Wahivi na Wayebusi, nchi aliyowaapia baba zako kukupa, nchi itiririkayo maziwa na asali, utaiadhimisha sikukuu hii katika mwezi huu:
Yahweh atakapo waleta nchi ya Wakanani, Wahiti, Waamori, Wahivi, na Wayebusi, nchi aliyo waapia mababu zenu kuwapa, nchi inayo tiririka kwa maziwa na asali - kisha wapaswa kuadhimisha hili tendo la ibada kila mwezi.
6 Kwa siku saba utakula mikate isiyotiwa chachu na katika siku ya saba utamfanyia Bwana sikukuu.
Kwa siku saba utakula mkate bila hamira; siku ya saba kutakuwa na maakuli ya kumuadhimisha Yahweh.
7 Kwa muda wa siku saba utakula mikate isiyotiwa chachu, pasionekane kitu chochote kilicho na chachu miongoni mwako, wala chachu yoyote isionekane popote ndani ya mipaka yako.
Mkate usio na hamira wapaswa kuliwa kwa siku saba zote; hakuna mkate ulio na hamira wapaswa kuliwa miongoni mwenu. Hakuna hamira yapaswa kuonekana kwenye mipaka yenu.
8 Siku ile utamwambia mwanao, ‘Nafanya hivi kwa sababu ya jambo ambalo Bwana alinitendea nilipotoka katika nchi ya Misri.’
Hiyo siku utasema kwa watoto wako, 'Hii ni kwasababu ya kile Yahweh alichofanya kwangu nilipo taka Misri.'
9 Adhimisho hili, litakuwa kama alama kwenye mkono wako na ukumbusho katika paji lako la uso, kwamba sheria ya Bwana inapaswa iwe kinywani mwako. Kwa kuwa Bwana alikutoa katika nchi ya Misri kwa mkono wake wenye nguvu.
Hii itakuwa kumbukumbu mkononi mwako, na kumbukumbu kwenye paji la uso wako. Hii ni ili sheria ya Yahweh iwe kinywani mwako, maana kwa mkono hodari Yahweh amewatoa kutoka Misri.
10 Ni lazima uishike amri hii kwa wakati uliopangwa mwaka baada ya mwaka.
Kisha basi wapaswa kushika hii sheria kwa wakati uliyo kusudiwa kutoka mwaka hadi mwaka.
11 “Baada ya Bwana kukuingiza katika nchi ya Wakanaani na kukupa nchi hiyo, kama alivyokuahidi kwa kiapo na kwa baba zako,
Yahweh atakapo waleta kwenye nchi ya Wakanani, kama alivyo apa kwenu na kwa mababu zenu kufanya, na atakapo wapa nchi ninyi,
12 inakupasa kumtolea Bwana mzaliwa wa kwanza wa kila tumbo. Wazaliwa wote wa kwanza wa kiume wa mifugo yako ni mali ya Bwana.
lazima umtengee mzaliwa wa kwanza mtoto na uzao wa kwanza wa wanyama wenu. Wakiume watakuwa wa Yahweh.
13 Kila mzaliwa wa kwanza wa punda utamkomboa kwa mwana-kondoo, lakini kama hukumkomboa, utamvunja shingo yake. Kila mzaliwa wa kwanza mwanaume miongoni mwa wana wenu utamkomboa.
Kila mzaliwa wa kwanza wa punda lazima umnunue tena na mwana kondoo. Kama hautamnunua tena, lazima uivunje shingo yake. Lakini kila mzaliwa wa kwanza wakiume miongoni mwenu - lazima umnunue tena.
14 “Katika siku zijazo, mwanao akikuuliza, ‘Hii ina maana gani?’ Mwambie, ‘Kwa mkono wenye nguvu Bwana alitutoa katika nchi ya Misri, kutoka nchi ya utumwa.
Mwanae atakapo kuuliza baadae, 'Hii ina maana gani?' kisha utamwambia, 'Ni kwa mkono hodari Yahweh katutoa Misri, kutoka nyumba ya utumwa.
15 Farao alipokataa kwa ukaidi kuturuhusu kuondoka, Bwana aliua kila mzaliwa wa kwanza wa Wamisri, mwanadamu na wa mnyama. Hii ndiyo sababu ninatoa dhabihu kwa Bwana mzaliwa wa kwanza wa kiume, wa kila tumbo na kumkomboa kila mzaliwa wa kwanza wa wana wangu.’
Farao alipo kataa kwa ujeuri kutuachia twende, Yahweh aliwaua wazaliwa wa kwanza wa nchi ya Misri, wazaliwa wa kwanza wa watu na wa wanyama. Ndio sababu ninatoa dhabihu kwa Yahweh kwa kila mzaliwa wa kwanza wa kila mnyama, na pia sababu nina nunua wazaliwa wa kwanza wa wanangu tena.'
16 Jambo hili litakuwa kama ishara kwenye mkono wako na kama alama kwenye paji la uso wako, kwamba Bwana alikutoa katika nchi ya Misri kwa mkono wake wenye nguvu.”
Hii itakuwa kumbukumbu mikononi mwako na kumbukumbu kwenye paji lako la uso, kwa kuwa ni kwa mkono hodari Yahweh alitutoa kutoka Misri.”
17 Farao alipowaachia watu waende, Mungu hakuwaongoza kufuata njia ipitiayo katika nchi ya Wafilisti, ingawa njia hiyo ilikuwa fupi zaidi. Kwa maana Mungu alisema, “Wakikabiliana na vita, wanaweza kubadili mawazo yao na kurudi Misri.”
Farao alipo waachia watu waende, Mungu akuwaongoza kwa njia ya Wafilisti, japo hiyo njia ilikuwa karibu. Kwa kuwa Mungu alisema, “Labda watu watabadili nia zao watakapo ona vita na watarudi Misri.”
18 Kwa hiyo Mungu akawaongoza watu kupitia njia ya kuzunguka kupitia jangwani, kuelekea Bahari ya Shamu. Waisraeli walipanda kutoka nchi ya Misri wakiwa wamejiandaa kwa vita.
Hivyo Mungu akawaongoza watu kuzunguka nyikani kupita Bahari ya Shamu. Waisraeli waliondoka kutoka nchi ya Misri wakiwa wamejiami kwa pambano.
19 Mose akachukua mifupa ya Yosefu kwa sababu Yosefu alikuwa amewaapisha wana wa Israeli. Alikuwa amewaambia, “Hakika Mungu atakuja kuwasaidia, nanyi ni lazima mwiichukue mifupa yangu mwende nayo kutoka mahali hapa.”
Musa akachukuwa mifupa ya Yusufu pamoja naye, kwa kuwa Yusufu aliwaapisha Waisraeli na kusema, “Mungu atawaokoa, na muibebe mifupa yangu na nyie.”
20 Baada ya Waisraeli kuondoka Sukothi wakapiga kambi huko Ethamu pembeni mwa jangwa.
Waisraeli walisafiri kutoka Sakothi na kuweka kambi Ethamu pembezoni mwa nyikani.
21 Wakati wa mchana Bwana aliwatangulia kwa nguzo ya wingu kuwaongoza katika njia yao, na wakati wa usiku aliwatangulia kwa nguzo ya moto kuwaangazia, ili waweze kusafiri mchana au usiku.
Yahweh alitangulia mbele yao mchana kama nguzo ya wingu kuwaongoza njiani. Usiku alienda kama nguzo ya moto kuwapa mwanga. Kwa namna hii waliweza kusafiri mchana na usiku.
22 Ile nguzo ya wingu wakati wa mchana au ile nguzo ya moto wakati wa usiku haikuondoka mahali pake mbele ya watu.
Yahweh hakuchukuwa kutoka kwa watu nguzo ya wingu mchana wala nguzo ya moto usiku.