< Kutoka 11 >

1 Basi Bwana alikuwa amemwambia Mose, “Nitaleta pigo moja zaidi kwa Farao na katika nchi ya Misri. Baada ya hilo, atawaacha mwondoke hapa na atakapofanya hivyo, atawafukuza mtoke kabisa.
Kisha Yahweh akamwambia Musa, “Bado kuna pigo moja nitalo lileta kwa Farao na Misri. Baada ya hilo, atakuacha uondoke hapa. Atakapo kuachia uende, ata kuondoa kabisa.
2 Waambie watu wote waume kwa wake wawaombe majirani zao vitu vya fedha na vya dhahabu.”
Waelekeze watu kwamba kila mwanaume na mwanamke amuulizie jirani yake vitu vya fedha na vitu vya dhahabu.”
3 (Bwana akawafanya Wamisri wawe na moyo wa ukarimu kwa Waisraeli, naye Mose mwenyewe akaheshimiwa sana na maafisa wa Farao na watu wote katika nchi ya Misri.)
Sasa Yahweh aliwafanya Wamisri kuwa na shauku ya kuwapendeza Waisraeli. Aidha, Musa alikuwa wakuvutia sana machoni pa watumishi wa Farao na watu wa Misri.
4 Kwa hiyo Mose akasema, “Hili ndilo Bwana asemalo: ‘Panapo usiku wa manane Mimi nitapita katika nchi yote ya Misri.
Musa akasema, “Yahweh asema hivi: 'Wakati wa usiku wa manane nitaenda Misri yote.
5 Kila mwanaume kifungua mimba katika Misri atakufa, kuanzia mzaliwa wa kwanza wa kiume wa Farao, aketiye penye kiti cha ufalme, hadi mzaliwa wa kwanza wa kiume wa mtumwa wa kike, anayesaga nafaka kwa jiwe, pamoja na kila mzaliwa wa kwanza wa mifugo.
Wazaliwa wa kwanza wote wa nchi ya Misri watakufa, kuanzia mzaliwa wa kwanza wa Farao, anaye keti kiti chake cha enzi, mpaka mzaliwa wa kwanza wa misichana mtumwa anaye saga mbegu, na kwa wazaliwa wa kwanza wa mifugo.
6 Patakuwepo kilio kikubwa katika nchi yote ya Misri, kilio kibaya ambacho hakijakuwepo wala kamwe hakitakuwepo tena.
Kisha kutakuwa na kilio kikubwa nchi yote ya Misri, kama ambacho hakijawai wala hakitatokea tena.
7 Lakini miongoni mwa Waisraeli hakuna hata mbwa atakayembwekea mwanadamu wala mnyama yeyote.’ Ndipo mtakapojua kuwa Bwana huweka tofauti kati ya Misri na Israeli.
Lakini ata mbwa hata bweka kwa watu wa Israeli, dhidi ya mtu au mnyama. Kwa hili utajuwa kuwa nina watendea Wamisri na Waisraeli tofauti.'
8 Maafisa hawa wako wote watanijia, wakisujudu mbele yangu, wakisema, ‘Ondoka, wewe pamoja na watu wako wote wanaokufuata!’ Baada ya haya nitaondoka.” Kisha Mose, huku akiwa amewaka hasira, akamwacha Farao.
Watumishi wote hawa wako, Farao, watakuja chini yangu na kunisujudu mimi. Watasema, 'Nenda, wewe na watu wote wanao kufuata!' Baada ya hapo nitaondoka.” Kisha akaondoka mbele ya Farao kwa hasira kubwa.
9 Bwana alikuwa amemwambia Mose, “Farao atakataa kukusikiliza, ili maajabu yangu yapate kuongezeka katika nchi ya Misri.”
Yahweh akamwambia Musa, Farao hatakusikiliza. Hii ni ili nifanye mambo ya ajabu katika nchi ya Misri.”
10 Mose na Aroni wakafanya maajabu haya yote mbele ya Farao, lakini Bwana akaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu, wala hakuwaachia Waisraeli waondoke katika nchi yake.
Musa na Aruni wakafanya mambo haya ya kushangaza mbele za Farao. Lakini Yahweh aliufanya moyo wa Farao mgumu, na Farao hakuwaacha watu wa Israeli kuondoka katika nchi yake.

< Kutoka 11 >