< Waefeso 3 >
1 Kwa sababu hii, mimi Paulo, mfungwa wa Kristo Yesu kwa ajili yenu ninyi watu wa Mataifa:
Kwa sababu ya hii mimi, Paulo, ni mfungwa wa Yesu Kristo kwa ajili yenu Mataifa.
2 Kwa hakika mmekwisha kusikia kuhusu ile huduma ya neema ya Mungu niliyopewa kwa ajili yenu,
Na amini ya kwamba mmesikia juu ya kazi ya neema ya Mungu aliyo nipa kwa ajili yenu.
3 yaani, ile siri iliodhihirishwa kwangu kwa njia ya ufunuo, kama nilivyotangulia kuandika kwa kifupi.
Nawaandikieni kutokana na jinsi ufunuo ulivyo funuliwa kwangu. Huu ni ukweli uliyofichika ambao niliandika kwa kifupi kwenye barua nyingine.
4 Kwa kusoma haya, basi mtaweza kuelewa ufahamu wangu katika siri ya Kristo.
Usomapo kuhusu haya, utaweza kutambua busara yangu katika ukweli huu uliofichika kuhusu Kristo.
5 Siri hii haikudhihirishwa kwa wanadamu katika vizazi vingine kama vile sasa ilivyodhihirishwa na Roho kwa mitume na manabii watakatifu wa Mungu.
Kwa vizazi vingine ukweli huu haukufanywa utambulike kwa wana wa watu. Ila kwa sasa umewekwa wazi kwa Roho kwa Mitume waliotengwa na Manabii.
6 Siri hii ni kwamba, kwa njia ya Injili, watu wa Mataifa ni warithi pamoja na Israeli, viungo vya mwili mmoja na washiriki pamoja wa ahadi katika Kristo Yesu.
Ukweli huu uliofichika ni kwamba watu wa Mataifa ni washiriki wenzetu na wajumbe wenzetu wa mwili. Niwashiriki pamoja na ahadi ya Kristo Yesu kupitia injili.
7 Nimekuwa mtumishi wa Injili hii kwa kipawa cha neema ya Mungu niliyopewa kwa nguvu yake itendayo kazi.
Na kwa hili nimefanyika mtumishi kwa zawadi ya neema ya Mungu iliyotolewa kwangu kupitia utendaji wa nguvu yake.
8 Ingawa mimi ni mdogo kuliko aliye mdogo kabisa miongoni mwa watakatifu wote, nilipewa neema hii: ili niwahubirie watu wa Mataifa kuhusu utajiri usiopimika ulio ndani ya Kristo,
Mungu alitoa zawadi hii kwangu, japo kuwa mimi ni mtu mdogo wa wote katika wale waliotengwa kwa ajili ya Mungu. Zawadi hii ni kwamba inanipasa kuwatangazia mataifa injili yenye utajiri usiochunguzika wa Kristo.
9 na kuweka wazi kwa kila mtu siri hii iliyokuwa imefichwa tangu zamani katika Mungu, aliyeumba vitu vyote. (aiōn )
inanipasa kuwaangazia watu wote juu ya nini ni mpango wa Mungu wa siri. Huu ni mpango ambao ulikuwa umefichwa kwa miaka mingi iliyopita, na Mungu ambaye aliviumba vitu vyote. (aiōn )
10 Ili sasa kwa njia ya Kanisa, hekima yote ya Mungu ipate kujulikana kwa watawala na wenye mamlaka katika ulimwengu wa roho,
Hii ilikuwa kwamba, kupitia Kanisa, watawala na mamlaka katika sehemu za mbingu wapate kujua pande nyingi za asili ya hekima ya Mungu.
11 sawasawa na kusudi lake la milele katika Kristo Yesu Bwana wetu. (aiōn )
Haya yangetokea kupitia mpango wa milele ambao aliukamilisha ndani ya Kristo Yesu Bwana wetu. (aiōn )
12 Ndani yake na kwa njia ya imani katika yeye twaweza kumkaribia Mungu kwa uhuru na kwa ujasiri.
Kwa kuwa katika Kristo tuna ujasiri na uwezo wa kuingia kwa ujasiri kwa sababu ya imani yetu kwake.
13 Kwa hiyo, nawaomba msikate tamaa kwa sababu ya mateso yangu kwa ajili yenu, hayo ni utukufu wenu.
Kwa hiyo nawaomba msikate tamaa kwasababu ya mateso yangu kwa ajili yenu. Haya ni utukufu wenu.
14 Kwa sababu hii nampigia Baba magoti,
Kwa sababu hii napiga magoti kwa Baba.
15 ambaye ubaba wote wa kila jamaa za mbinguni na za duniani unatokana naye.
ambaye kwa yeye kila familia mbinguni na juu ya nchi imeitwa jina.
16 Namwomba Mungu awaimarishe kwa kuwatia nguvu mioyo yenu kwa njia ya Roho wake kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake,
Ninaomba kwamba apate kuwanemesha, kutokana na utajiri wa utukufu wake, awafanye imara kwa nguvu kupitia Roho wake, ambaye yu ndani yenu.
17 ili kwamba, Kristo apate kukaa mioyoni mwenu kwa njia ya imani. Nami ninaomba kwamba ninyi mkiwa wenye mizizi tena imara katika msingi wa upendo,
Ninaomba kwamba Kristo aishi ndani ya mioyo yenu kupitia imani.
18 mwe na uwezo wa kufahamu pamoja na watakatifu wote jinsi ulivyo upana, urefu, kimo na kina upendo wa Kristo,
Ninaomba kwamba muwe na shina na msingi wa upendo wake. Muwe katika pendo lake ili muweze kuelewa, pamoja na wote waaminio, jinsi upana, na urefu na kimo na kina cha upendo wa Kristo.
19 na kujua upendo huu unaopita fahamu, ili mpate kujazwa na kufikia kipimo cha ukamilifu wote wa Mungu.
Ninaomba Kwamba mjue ukuu wa upendo wa Kristo, ambao unazidi ufahamu. Mfanye haya ili mjazwe na ukamilifu wote wa Mungu.
20 Basi kwa yeye awezaye kutenda mambo ya ajabu yasiyopimika kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya uweza wake ule utendao kazi ndani yetu,
Na sasa kwake yeye awezaye kufanya kila jambo, zaidi ya yote tuyaombayo au tuyawazayo, kupitia nguvu yake itendayo kazi ndani yetu,
21 yeye atukuzwe katika kanisa na katika Kristo Yesu kwa vizazi vyote, milele na milele. Amen. (aiōn )
kwake yeye kuwe utukufu ndani ya kanisa na katika Kristo Yesu kwa vizazi vyote milele na milele. Amina. (aiōn )