< Mhubiri 6 >
1 Nimeona ubaya mwingine chini ya jua, nao unalemea sana wanadamu:
Kuna ubaya ambao nimeuona chini ya jua, na ni mbaya kwa watu.
2 Mungu humpa mwanadamu utajiri, mali na heshima, hivyo hakukosa chochote moyo wake unachokitamani. Lakini Mungu hamwezeshi kuvifurahia, badala yake mgeni ndiye anayevifurahia. Hili ni ubatili, ni ubaya unaosikitisha.
Mungu anaweza kumpa mtu mali na utajiri na heshima kwa kiasi kwamba hakosi chochote anachokitamani mwenyewe, lakini kisha hampi uwezo wa kukifurahia. Badala yake mtu mwingine hutumia vitu vyake. Huu ni mvuke, teso baya.
3 Mtu anaweza kuwa na watoto mia moja naye akaishi miaka mingi, lakini haidhuru kuwa ataishi muda mrefu kiasi gani, kama hawezi kufurahia mafanikio yake na kwamba hapati mazishi ya heshima, ninasema afadhali mtoto aliyezaliwa akiwa amekufa kuliko yeye.
Kama mtu akizaa watoto mia moja na kuishi miaka mingi, ili kwamba siku za miaka yake ni nyingi, lakini kama moyo wake hautosheki kwa mema na hazikwi kwa heshima, kisha ninasema kwamba, mtoto aliyezaliwa akiwa amekufa ni bora kuliko alivyo.
4 Kuzaliwa kwake hakuna maana, huondokea gizani na gizani jina lake hufunikwa.
Hata mtoto huyo amezaliwa bila faida na anapita katika giza, na jina lake linabaki limefichika.
5 Ingawa hakuwahi kuliona jua wala kujua kitu chochote, yeye ana pumziko zaidi kuliko mtu huyo,
Ingawa mtoto huyu haoni jua au kujua kitu chochote, ana pumziko ingawa mtu huyo hakupumzika.
6 Hata kama huyo mtu ataishi miaka elfu mara mbili na zaidi, lakini akashindwa kufurahia mafanikio yake, je, wote hawaendi sehemu moja?
Hata kama mtu akiishi miaka elfu mbili lakini hajifunzi kufuraia vitu vizuri, aenda sehemu moja kama mtu yeyote yule.
7 Juhudi zote za binadamu ni kwa ajili ya kinywa chake, hata hivyo hamu yake kamwe haitoshelezwi.
Ingawa kazi yote ya mtu ni kujaza mdomo wake, ila hamu yake haishibi.
8 Mtu mwenye hekima ana faida gani zaidi ya mpumbavu? Mtu maskini anapata faida gani kwa kujua jinsi ya kujistahi mbele ya watu wengine?
Hakika ni faida gani aliyo nayo mwenye hekima kuliko mpumbavu? Ni faida gani aliyo nayo masikini hata kama anajua jinsi ya kutenda mbele ya watu?
9 Ni bora kile ambacho jicho linakiona kuliko hamu isiyotoshelezwa. Hili nalo ni ubatili, ni kukimbiza upepo.
Ni bora kuridhika na kile ambacho macho hukiona kuliko kutamani kile ambacho hamu isiyo tulia inatamani, ambayo pia ni mvuke na kujaribu kuuchunga upepo.
10 Lolote lililopo limekwisha kupewa jina, naye mwanadamu alivyo ameshajulikana; hakuna mtu awezaye kushindana na mwenye nguvu kuliko yeye.
Chochote ambacho kimekuwepo, tayari kimekwisha kupewa jina lake, na vile mtu alivyo ni kama tayari amekwisha fahamika. Hivyo imekuwa haifai kugombana na yule ambaye ni muhukumu mkuu wa wote.
11 Maneno yanavyokuwa mengi, ndivyo yanavyokosa maana, Je, hilo linamfaidia vipi yeyote?
Maneno mengi ambayo yanaongelewa, ndivyo yasiyo na maana yanaongezeka, kwa hiyo ni faida gani iliyopo kwa mwanadamu?
12 Kwa maana ni nani anayejua lililo jema kwa ajili ya maisha ya mwanadamu, katika siku chache na za ubatili anazopita kama kivuli? Ni nani awezaye kumwambia yatakayotokea chini ya jua baada ya yeye kuondoka?
Kwa kuwa ni nani ajuaye nini kilicho kizuri kwa mtu katika maisha yake wakati wa ubatili wake, siku zilizo hesabika ambazo kwa hizo anapita kama kivuri? Ni nina anayeweza kumwambia mtu kile kitakacho kuja chini ya jua baada ya kupita?