< Mhubiri 4 >
1 Nikatazama tena nikaona uonevu wote uliokuwa unafanyika chini ya jua: Nikaona machozi ya walioonewa, wala hawana wa kuwafariji; uwezo ulikuwa upande wa wale wanaowaonea, wala hawana wa kuwafariji.
Kisha tena nikafikiri kuhusu mateso yote yaliyo chini ya jua. Tazama machozi ya watu walioteswa. Hakuna anaye mfariji kwa ajili yao. Nguvu iko katika mikononi mwa watesaji, lakini wateswaji hawana mfariji.
2 Nami nikasema kwamba wafu, waliokwisha kufa, wana furaha kuliko watu walio hai, ambao bado wanaishi.
Hivyo nikawapongeza watu walio kufa, wale ambao tayari wamekufa, sio wanaoishi, wale ambao wako hai.
3 Lakini aliye bora kuliko hao wawili ni yule ambaye hajazaliwa bado, ambaye hajaona ule uovu unaofanyika chini ya jua.
Ingawa, bahati zaidi kuliko wote wawili ni yule ambaye hajaishi, yeye ambaye hajaona matendo yoyote mabaya ambayo yanafanyika chini ya jua.
4 Tena nikaona kuwa kazi zote na mafanikio yote huchipuka kutokana na wivu wa mtu kwa jirani yake. Hili nalo ni ubatili, ni kukimbiza upepo.
Kisha nikaona kwamba kila tendo la kazi na kila kazi ya utashi ikawa wivu wa jirani ya mtu. Huu pia ni mvuke na kujaribu kuchunga upepo.
5 Mpumbavu hukunja mikono yake na kujiangamiza mwenyewe.
Mpumbavu hukunja mikono yake na hafanyi kazi, hivyo chakula chake in mwili wake.
6 Afadhali konzi moja pamoja na utulivu kuliko konzi mbili pamoja na taabu na kukimbiza upepo.
Lakini afadhari konzi ya faida pamoja na kazi ya haraka kuliko konzi mbili pamoja na kazi ambayo hujaribu kuuchunga upepo.
7 Tena nikaona kitu kingine kilicho ubatili chini ya jua:
Kisha nikafikiri tena zaidi kuhusu ubatili, mvuke upoteao zaidi chini ya jua.
8 Kulikuwepo mwanadamu aliye peke yake, hakuwa na mwana wala ndugu. Hapakuwa na mwisho wa kazi yake, hata hivyo macho yake hayakutosheka na utajiri wake. Aliuliza, “Ninajitaabisha hivi kwa ajili ya nani, nami kwa nini ninajinyima kufurahia?” Hili pia ni ubatili, ni shughuli yenye taabu!
Kuna aina ya mtu ambaye yuko peke yake. Hana mtu, hana mwana, wala ndugu. Hakuna mwisho wa kazi zake zote, na macho yake hayatosheki kwa kupata utajiri. Anashangaa, “Ninajishumbua na kuharibu furaha yangu kwa ajili ya nani?” Huu pia ni mvuke, hali mbaya.
9 Wawili ni afadhali kuliko mmoja, kwa sababu wana malipo mazuri kwa kazi yao:
Watu wawili wanafanya vizuri zaidi ya mmoja; kwa pamoja wanaweza kupata malipo mazuri kwa ajili ya kazi yao.
10 Kama mmoja akianguka, mwenzake atamwinua. Lakini ni jambo la kuhuzunisha kwa mtu yule aangukaye naye hana wa kumwinua!
Kwa kuwa kama mmoja akianguka, mwingine anaweza kumwinua rafiki yake. Ingawa, huzuni humfuata yeye aliye peke yake anapoanguka kama hakuna mtu wa kumwinua.
11 Pia, kama wawili wakilala pamoja watapashana joto. Lakini ni vipi mtu aweza kujipasha joto mwenyewe?
Na kama wawili wakilala pamoja, wanaweza kupata joto, lakini mtu mmoja anawezaje kupata joto akiwa mwenyewe?
12 Ingawa mtu mmoja aweza kushindwa, watu wawili wanaweza kumkabili adui na kumshinda. Kamba ya nyuzi tatu haikatiki kwa urahisi.
Mtu akiwa peke yake anaweza kushindwa nguvu, lakini wawili wanaweza kusimama katika shambulio, na kama ya nyuzi tatu haikatika upesi.
13 Afadhali kijana maskini mwenye hekima kuliko mfalme mzee mpumbavu ambaye hajui tena kupokea maonyo.
Ni bora kuwa kijana masikini kuliko kuwa mfalme mzee na mpumbavu ambaye hajui jinsi ya kusikiliza maonyo.
14 Kijana huyo angeweza kutokea gerezani akapata ufalme, au angeweza kuwa amezaliwa katika umaskini kwenye huo ufalme.
Hii ni kweli hata kama mtu mdogo anapokuwa mfalme kutoka gerezani, au hata kama alizaliwa masikini katika ufalme wake.
15 Nikaona kwamba wote walioishi na kutembea chini ya jua walimfuata kijana, aliyepokea ufalme.
Ingawa, niliona kila mmoja aliye kuwa hai na kuzunguka chini ya jua wakijitia chini kwa kijana mdogo aliyeinuka kama mfalme.
16 Hapakuwa na kikomo cha watu wote aliowatawala. Lakini wale waliokuja baadaye hawakufurahia kazi ya yule aliyepokea ufalme. Hili nalo pia ni ubatili, ni kukimbiza upepo.
Hakuna mwisho kwa watu wote wanaotaka kumtii mfalme mpya, lakini wengi wao hawatamsifu yeye. Hakika hali hii ni mvuke na kujaribu kuuchunga upepo.