< Mhubiri 3 >

1 Kuna wakati kwa ajili ya kila jambo, nayo majira kwa kila tendo chini ya mbingu:
For everything there is a season, and a time for every purpose under heaven:
2 wakati wa kuzaliwa na wakati wa kufa, wakati wa kupanda na wakati wa kungʼoa yaliyopandwa,
a time to be born, and a time to die; a time to plant, and a time to pluck up that which is planted;
3 wakati wa kuua na wakati wa kuponya, wakati wa kubomoa, na wakati wa kujenga,
a time to kill, and a time to heal; a time to break down, and a time to build up;
4 wakati wa kulia na wakati wa kucheka, wakati wa kuomboleza na wakati wa kucheza,
a time to weep, and a time to laugh; a time to mourn, and a time to dance;
5 wakati wa kutawanya mawe na wakati wa kukusanya mawe, wakati wa kukumbatia na wakati wa kutokumbatia,
a time to cast away stones, and a time to gather stones together; a time to embrace, and a time to refrain from embracing;
6 wakati wa kutafuta na wakati wa kupoteza, wakati wa kuweka na wakati wa kutupa,
a time to seek, and a time to lose; a time to keep, and a time to cast away;
7 wakati wa kurarua na wakati wa kushona, wakati wa kunyamaza na wakati wa kuzungumza,
a time to tear, and a time to sew; a time to keep silence, and a time to speak;
8 wakati wa kupenda na wakati wa kuchukia, wakati wa vita na wakati wa amani.
a time to love, and a time to hate; a time for war, and a time for peace.
9 Mfanyakazi anapata faida gani kutokana na taabu yake?
What profit has he who works in that in which he labors?
10 Nimeona mzigo Mungu alioweka juu ya wanadamu.
I have seen the burden which God has given to the sons of men to be afflicted with.
11 Amefanya kila kitu kiwe kizuri kwa wakati wake. Pia ameiweka hiyo milele katika mioyo ya wanadamu, wala hawawezi kutambua kwa kina yale ambayo Mungu amefanya tangu mwanzo hadi mwisho.
He has made everything beautiful in its time. He has also set eternity in their hearts, yet so that man can’t find out the work that God has done from the beginning even to the end.
12 Ninajua kwamba hakuna kitu bora kwa wanadamu kuliko kuwa na furaha na kutenda mema wakati wanapoishi.
I know that there is nothing better for them than to rejoice, and to do good as long as they live.
13 Tena ni karama ya Mungu kila mtu apate kula na kunywa na kujiburudisha kwa mema katika kazi yake yote.
Also that every man should eat and drink, and enjoy good in all his labor, is the gift of God.
14 Ninajua kwamba kila kitu anachokifanya Mungu kitadumu milele, hakuna kinachoweza kuongezwa au kupunguzwa. Mungu hufanya hivyo ili watu wamche yeye.
I know that whatever God does, it shall be forever. Nothing can be added to it, nor anything taken from it; and God has done it, that men should fear before him.
15 Chochote kilichopo kilishakuwepo, na kitakachokuwepo kimekwishakuwepo kabla; naye Mungu huyaita yale yaliyopita yarudi tena.
That which is has been long ago, and that which is to be has been long ago. God seeks again that which is passed away.
16 Pia nikaona kitu kingine tena chini ya jua: Mahali pa kutolea hukumu, uovu ulikuwepo, mahali pa kupatia haki, uovu ulikuwepo.
Moreover I saw under the sun, in the place of justice, that wickedness was there; and in the place of righteousness, that wickedness was there.
17 Nikafikiri moyoni mwangu, “Mungu atawaleta hukumuni wote wawili wenye haki na waovu, kwa maana kutakuwako na wakati kwa ajili ya kila jambo, wakati kwa ajili ya kila tendo.”
I said in my heart, “God will judge the righteous and the wicked; for there is a time there for every purpose and for every work.”
18 Pia nikafikiri, “Kuhusu wanadamu, Mungu huwajaribu ili wajione kwamba wao ni kama wanyama.
I said in my heart, “As for the sons of men, God tests them, so that they may see that they themselves are like animals.
19 Hatima ya mwanadamu ni kama ile ya wanyama; wote wana mwisho unaofanana: Jinsi anavyokufa mnyama, ndivyo anavyokufa mwanadamu. Wote wana pumzi inayofanana; mwanadamu hana cha zaidi kuliko mnyama. Kila kitu ni ubatili.
For that which happens to the sons of men happens to animals. Even one thing happens to them. As the one dies, so the other dies. Yes, they have all one breath; and man has no advantage over the animals, for all is vanity.
20 Wote huenda mahali panapofanana; wote hutoka mavumbini, mavumbini wote hurudi.
All go to one place. All are from the dust, and all turn to dust again.
21 Ni nani ajuaye kama roho ya mtu huenda juu na roho ya mnyama hushuka chini ardhini?”
Who knows the spirit of man, whether it goes upward, and the spirit of the animal, whether it goes downward to the earth?”
22 Kwa hiyo nikaona kwamba hakuna kitu kilicho bora zaidi kwa mwanadamu kuliko kuifurahia kazi yake, kwa sababu hilo ndilo fungu lake. Kwa maana ni nani awezaye kumrudisha ili aje kuona kile kitakachotendeka baada yake?
Therefore I saw that there is nothing better than that a man should rejoice in his works, for that is his portion; for who can bring him to see what will be after him?

< Mhubiri 3 >