< Mhubiri 10 >

1 Kama vile nzi waliokufa huacha harufu mbaya kwenye manukato, ndivyo upumbavu kidogo huzidi nguvu hekima na heshima.
זבובי מות יבאיש יביע שמן רוקח יקר מחכמה מכבוד סכלות מעט
2 Moyo wa mwenye hekima huelekea kuume, lakini moyo wa mpumbavu huelekea kushoto.
לב חכם לימינו ולב כסיל לשמאלו
3 Hata anapotembea barabarani, mpumbavu hukosa ufahamu na kudhihirisha kwa kila mmoja jinsi alivyo mpumbavu.
וגם בדרך כשהסכל (כשסכל) הלך לבו חסר ואמר לכל סכל הוא
4 Kama hasira ya mtawala ikiwaka dhidi yako, usiache mahali pako, utulivu huweza kuzuia makosa mengi.
אם רוח המושל תעלה עליך מקומך אל תנח כי מרפא יניח חטאים גדולים
5 Kuna ubaya niliouona chini ya jua, aina ya kosa litokalo kwa mtawala:
יש רעה ראיתי תחת השמש--כשגגה שיצא מלפני השליט
6 Wapumbavu kuwekwa kwenye nafasi nyingi za juu, wakati matajiri hushika nafasi za chini.
נתן הסכל במרומים רבים ועשירים בשפל ישבו
7 Mimi nimeona watumwa wamepanda farasi, wakati wakuu wakitembea kwa miguu kama watumwa.
ראיתי עבדים על סוסים ושרים הלכים כעבדים על הארץ
8 Yeye achimbaye shimo aweza kutumbukia ndani yake, yeyote abomoaye ukuta anaweza kuumwa na nyoka.
חפר גומץ בו יפול ופרץ גדר ישכנו נחש
9 Yeyote apasuaye mawe inawezekana yakamuumiza, yeyote apasuaye magogo inawezekana yakamuumiza.
מסיע אבנים יעצב בהם בוקע עצים יסכן בם
10 Kama shoka ni butu na halikunolewa, nguvu nyingi zinahitajika, lakini ustadi utaleta mafanikio.
אם קהה הברזל והוא לא פנים קלקל וחילים יגבר ויתרון הכשיר חכמה
11 Kama nyoka akiuma kabla ya kufanyiwa uaguzi, mwaguzi hatahitajika tena.
אם ישך הנחש בלוא לחש ואין יתרון לבעל הלשון
12 Maneno yatokayo kinywani mwa mtu mwenye hekima yana neema, bali mpumbavu huangamizwa na midomo yake mwenyewe.
דברי פי חכם חן ושפתות כסיל תבלענו
13 Mwanzoni maneno yake ni upumbavu, mwishoni ni wazimu mbaya,
תחלת דברי פיהו סכלות ואחרית פיהו הוללות רעה
14 naye mpumbavu huzidisha maneno. Hakuna yeyote ajuaye linalokuja, ni nani awezaye kueleza ni jambo gani litakalotokea baada yake?
והסכל ירבה דברים לא ידע האדם מה שיהיה ואשר יהיה מאחריו מי יגיד לו
15 Kazi ya mpumbavu humchosha mwenyewe, hajui njia iendayo mjini.
עמל הכסילים תיגענו--אשר לא ידע ללכת אל עיר
16 Ole wako, ee nchi ambayo mfalme wako alikuwa mtumwa na ambayo wakuu wako hufanya karamu asubuhi.
אי לך ארץ שמלכך נער ושריך בבקר יאכלו
17 Heri wewe, ee nchi ambayo mfalme wako ni wa uzao wenye kuheshimika na ambayo wakuu wako hula chakula kwa wakati unaofaa: ili kupata nguvu na si kwa ajili ya ulevi.
אשריך ארץ שמלכך בן חורים ושריך בעת יאכלו בגבורה ולא בשתי
18 Kama mtu ni mvivu paa la nyumba huinama, kutokana na mikono milegevu, nyumba huvuja.
בעצלתים ימך המקרה ובשפלות ידים ידלף הבית
19 Karamu hufanywa kwa ajili ya kicheko, nao mvinyo hufurahisha maisha, lakini fedha ni jawabu la mambo yote.
לשחוק עשים לחם ויין ישמח חיים והכסף יענה את הכל
20 Usimshutumu mfalme hata ikiwa ni katika mawazo yako, au kumlaani tajiri katika chumba chako cha kulala, kwa sababu ndege wa angani wanaweza kuchukua maneno yako, naye ndege anayeruka anaweza kutoa taarifa ya yale uliyosema.
גם במדעך מלך אל תקלל ובחדרי משכבך אל תקלל עשיר כי עוף השמים יוליך את הקול ובעל הכנפים (כנפים) יגיד דבר

< Mhubiri 10 >