< Torati 7 >
1 Bwana Mungu wako akuletapo katika nchi unayoingia kuimiliki, na awafukuzapo mbele yako mataifa mengi, yaani Wahiti, Wagirgashi, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi na Wayebusi, mataifa saba makubwa tena yenye nguvu kuliko wewe,
Wakati Yahwe Mungu wenu atuleta katika nchi ambayo mnaenda kuimiliki na kuwaondoa mataifa mengi mbele zenu- Mhiti, Mgirgashi na Mwamori, na Mkanaani, na Mperizi, Mhivi, Myebusi- mataifa saba makubwa na yenye nguvu kuliko wewe.
2 pia Bwana Mungu wako atakapowatia mkononi mwako na ukawashinda, basi ni lazima uwaangamize wote kabisa. Usifanye agano nao, wala usiwahurumie.
Na wakati Yahwe Mungu wenu awapa ninyi ushindi juu yao pindi mnakutana nao katika vita, mtawashambulia, basi mnapaswa kuwateketeza kabisa. Hamtafanya agano nao, wala kuonesha huruma kwao.
3 Usioane nao. Usimtoe binti yako kuolewa na mwanawe, au kumchukua binti yake aolewe na mwanao.
Wala hamtapanga ndoa zozote pamoja nao, hamtawatoa binti zenu kwa vijana wao, na hamtawachukua binti zao kwa vijana wenu.
4 Kwa maana watamgeuza mwanao aache kunifuata, ili aitumikia miungu mingine, nayo hasira ya Bwana itawaka dhidi yako, naye atakuangamiza ghafula.
Kwa kuwa watawabadilisha vijana wenu kutonifuata mimi, ili kwamba waweze kuabudu miungu yao. Kwa hiyo hasira ya Yahwe itawashwa dhidi yenu na atawaangamiza haraka.
5 Hili ndilo utakalowafanyia: Vunja madhabahu yao, vunja mawe yao ya kuabudia, katakata nguzo zao za Ashera na kuchoma sanamu zao kwa moto.
Hivi ndivyo mtakavyo washughulikia nao; mtavunja madhabahu zao, vunja nguzo zao za mawe katika vipande, kata chini ncha za Asherahi, na kuzichoma sanamu za kutupwa.
6 Kwa kuwa wewe ni taifa takatifu kwa Bwana Mungu wako. Bwana Mungu wako amekuchagua wewe kutoka mataifa yote juu ya uso wa dunia kuwa watu wake, hazina yake ya thamani.
Kwa kuwa wewe ni taifa uliyetengwa kwa Yahwe Mungu wako. Amekuchagua wewe kuwa watu kwa ajili yake kumiliki, zaidi ya watu wengine wote ambao wako katika uso wa dunia.
7 Bwana hakuweka upendo wake juu yenu na kuwachagua kwa sababu mlikuwa wengi mno kuliko watu wengine, kwa maana ninyi ndio mliokuwa wachache sana kuliko mataifa yote.
Yahwe hakuweka upendo wake juu yenu au kuwachagua kwa sababu mlikuwa zaidi katika idadi kuliko watu wowote, kwa kuwa mlikuwa wachache kuliko watu wote-
8 Lakini ni kwa sababu Bwana aliwapenda ninyi na kutunza kiapo alichowaapia babu zenu kwamba atawatoa ninyi kwa mkono wenye nguvu na kuwakomboa kutoka nchi ya utumwa, kutoka nguvu za Farao mfalme wa Misri.
Lakini kwa sababu anawapenda ninyi, anataka kushika kiapo alichoapa kwa baba zenu. Huyu ni Yahwe aliyewatoa kwa mkono wa uweza na kuwakomboa kutoka nyumba ya utumwa, kutoka mkono wa Farao, mfalme wa Misri.
9 Basi ujue kwamba Bwana Mungu wako ndiye Mungu; ni Mungu mwaminifu, anayetunza Agano la upendo kwa maelfu ya vizazi vya wale wanaompenda na kuzishika amri zake.
Kwa hiyo tambua ya kuwa Yahwe Mungu wako-ni Mungu, Mungu mwaminifu, anayetunza maagano na uaminifu kwa vizazi elfu kwa wale wanaompenda na kuyashika maagizo yake,
10 Lakini kwa wale wanaomchukia atawalipiza kwenye nyuso zao kwa maangamizi; hatachelewa kuwalipiza kwenye nyuso zao wale wamchukiao.
lakini huwalipa wale wanaomchukia kwa sura zao, kuwaangamiza, hatakuwa na huruma kwa yeyote anayemchukia; atamlipa kwa uso wake.
11 Kwa hiyo, kuweni waangalifu kufuata maagizo, amri na sheria ninazowapa leo.
Kwa hiyo utashika maagizo, amri, na sheria ninazokuamuru leo, ili kwamba uzifanye.
12 Kama mkizingatia sheria hizi na kuzifuata kwa uangalifu, basi Bwana Mungu wenu atatunza Agano lake la upendo nanyi, kama alivyowaapia baba zenu.
Kama mtasikiliza maagizo haya, kuyashika na kuyafanya, itakuwa Yahwe Mungu wenu atawashika pamoja na agano na uaminifu ambao aliapa kwa baba zenu.
13 Atawapenda ninyi na kuwabariki na kuongeza idadi yenu. Atabariki uzao wa tumbo lenu, mazao ya nchi yenu, nafaka, divai mpya na mafuta, ndama za ngʼombe wa makundi yenu, na kondoo za makundi yenu katika nchi ile aliyoapa kuwapa baba zenu.
Atawapenda, atawabariki, na kuwazidisha, pia atabariki tunda la miili yenu na tunda la ardhi yenu, nafaka zenu, divai mpya, mafuta yenu, atazidisha mifugo na kundi lako la mifugo michanga, katika nchi ambayo aliapa kwa baba zenu kuwapa.
14 Mtabarikiwa kuliko mataifa mengine yote, hakuna wanaume wala wanawake kwenu watakaokosa watoto, wala mifugo yenu haitakuwa tasa.
Mtabarikiwa zaidi kuliko watu wengine wote; hapatakuwa na mwanaume asiyekuwa na mtoto au mwanamke tasa miongoni mwenu au miongoni mwa mifugo.
15 Bwana atawakinga na kila ugonjwa. Mungu hatatia juu yenu ugonjwa wowote mbaya mlioufahamu huko Misri, lakini atatia ugonjwa juu ya wale wote wanaokuchukia.
Yahwe atawaondolea magonjwa yote; hakuna magonjwa mabaya ya Misri ambayo mnayajua yatawekwa juu yenu, Lakini atayaweka kwa wote wanaowachukia ninyi.
16 Ni lazima mwangamize watu wote ambao Bwana Mungu wenu atawatia mikononi mwenu. Msiwatazame kwa kuwahurumia na msiitumikie miungu yao, kwa kuwa itakuwa mtego kwenu.
Mtayaondoa makundi ya watu wote ambayo Yahwe Mungu wenu awapa ushindi, na jicho lenu halitawaonea huruma. Na hamtaabudu miungu yao, kwa kuwa huo utakuwa mtego kwenu.
17 Mnaweza kujiuliza wenyewe “Mataifa haya ni yenye nguvu kuliko sisi. Tutawezaje kuwafukuza?”
Kama mtasema kwenye mioyo, Haya mataifa ni mengi zaidi kuliko mimi; nitawezaje kuwafukuza?
18 Lakini msiwaogope. Kumbukeni vyema jinsi Bwana Mungu wenu alivyofanya kwa Farao na kwa wote huko Misri.
Usiwaogope; utakumbuka akilini Yahwe nini Mungu wenu alifanya kwa Farao na Misri yote?
19 Mliona kwa macho yenu wenyewe majaribu makubwa, ishara za miujiza na maajabu, mkono wenye nguvu na ulionyooshwa, ambao kwa huo Bwana Mungu wenu aliwatoa mtoke Misri. Bwana Mungu wenu atawafanyia hivyo watu wote ambao mnawaogopa sasa.
Mateso makuu ambayo macho yenu yaliona, ishara, maajabu, mkono wa uweza, mkono ulionyoshwa ambao Yahwe Mungu wenu alivyowatoa. Yahwe Mungu wenu atafanya kile kile kwa watu wote ambao mnawaogopa.
20 Zaidi ya hayo, Bwana Mungu wenu atatuma manyigu miongoni mwao hadi yale mabaki watakaojificha waangamie.
Zaidi ya yote, Yahwe Mungu wenu atatuma nyigu miongoni mwao, mpaka wale waliobaki na wale wanaojificha wenyewe mbele yenu waangamizwa mbele ya uwepo wenu.
21 Msiingiwe na hofu kwa sababu yao, kwa kuwa Bwana Mungu wenu, ambaye yupo miongoni mwenu ni mkuu naye ni Mungu wa kutisha.
Hamtatishikeni nao, kwa kuwa Yahwe Mungu wenu yuko miongoni mwenu, Mungu mkuu na wa kuogofya.
22 Bwana Mungu wenu atawafukuza mataifa hayo mbele yenu kidogo kidogo. Hamtaruhusiwa kuwaondoa wote kwa mara moja, la sivyo wanyama mwitu wataongezeka na kuwa karibu nanyi.
Yahwe Mungu wenu atayaondoa mataifa mbele zenu kidogo kidogo. Hamtayashinda yote kwa wakati mmoja, au wanyama wa mwitu watakuwa wengi karibu yenu.
23 Lakini Bwana Mungu wenu atawatia watu hao mikononi mwenu, akiwatia katika kuchanganyikiwa kukubwa mpaka wawe wameangamizwa.
Lakini Yahwe Mungu wenu atawapa ninyi ushindi dhidi yao wakati mkutanapo vitani; atawachanganya kwa kiasi kikubwa mpaka wameangamizwa.
24 Atawatia wafalme wao mikononi mwenu, nanyi mtayafuta majina yao chini ya mbingu. Hakuna hata mmoja atakayeweza kusimama dhidi yenu bali mtawaangamiza.
Atawaweka wafalme wao chini ya utawala wenu, na mtafanya jina lao kuangamia toka chini ya mbingu. Hakuna atakayeweza kusimama mbele yenu, mpaka muwaangamize.
25 Vinyago vya miungu yao mtavichoma moto. Msitamani fedha wala dhahabu iliyo juu yao, wala msizichukue kwa ajili yenu, la sivyo mtakuwa mmetekwa navyo. Kwa kuwa ni chukizo kwa Bwana Mungu wenu.
Utazichoma sanamu za kuchonga za miungu yao- usitamani madini ya fedha au dhahabu yanayofunika na kuichukua kwa ajili yenu, kwa sababu mkifanya, mtanaswa nayo-kwa kuwa ni chukizo kwa Yahwe Mungu wenu.
26 Msilete vitu vya machukizo katika nyumba zenu kwani ninyi, mtatengwa kama vitu hivyo kwa maangamizo. Ukichukie kabisa kitu hicho kwa kuwa kimetengwa kwa maangamizo.
Hamtaleta chukizo lolote ndani ya nyumba zenu na kuanza kuiabudu. Mtachukizwa kabisa na kuchukia kwa kuwa imetengwa kwa ajili ya uharibifu.