< Torati 6 >

1 Haya ndiyo maagizo, amri na sheria ambazo Bwana Mungu wenu aliniagiza niwafundishe ninyi ili mpate kuyashika katika nchi ambayo ninyi mnavuka Yordani kuimiliki,
וזאת המצוה החקים והמשפטים אשר צוה יהוה אלהיכם ללמד אתכם--לעשות בארץ אשר אתם עברים שמה לרשתה
2 ili kwamba ninyi, watoto wenu na watoto wao baada yao wamche Bwana Mungu wenu siku zote kwa kushika amri na maagizo yake yote ninayowapa, ili mweze kuyafurahia maisha marefu.
למען תירא את יהוה אלהיך לשמר את כל חקתיו ומצותיו אשר אנכי מצוך אתה ובנך ובן בנך כל ימי חייך--ולמען יארכן ימיך
3 Sikia, ee Israeli, nawe uwe mwangalifu kutii ili upate kufanikiwa na kuongezeka sana katika nchi itiririkayo maziwa na asali, kama Bwana, Mungu wa baba zenu, alivyowaahidi ninyi.
ושמעת ישראל ושמרת לעשות אשר ייטב לך ואשר תרבון מאד כאשר דבר יהוה אלהי אבתיך לך--ארץ זבת חלב ודבש
4 Sikia, ee Israeli: Bwana Mungu wako, Bwana ni mmoja.
שמע ישראל יהוה אלהינו יהוה אחד
5 Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote.
ואהבת את יהוה אלהיך בכל לבבך ובכל נפשך ובכל מאדך
6 Amri hizi ninazokupa leo zitakuwa katika moyo wako.
והיו הדברים האלה אשר אנכי מצוך היום--על לבבך
7 Wafundishe watoto wako kwa bidii. Nena kuhusu amri hizi uketipo nyumbani na wakati utembeapo njiani, ulalapo na uamkapo.
ושננתם לבניך ודברת בם בשבתך בביתך ובלכתך בדרך ובשכבך ובקומך
8 Zifunge kama alama juu ya mkono wako, na uzifunge juu ya paji la uso wako.
וקשרתם לאות על ידך והיו לטטפת בין עיניך
9 Ziandike kwenye miimo ya milango ya nyumba yako na juu ya malango yako.
וכתבתם על מזזות ביתך ובשעריך
10 Wakati Bwana Mungu wako atakapokuleta katika nchi aliyowaapia baba zako, Abrahamu, Isaki na Yakobo, kukupa wewe, nchi kubwa, ina miji inayopendeza ambayo hukuijenga,
והיה כי יביאך יהוה אלהיך אל הארץ אשר נשבע לאבתיך לאברהם ליצחק וליעקב--לתת לך ערים גדלת וטבת אשר לא בנית
11 nyumba zilizojaa vitu vizuri vya aina nyingi ambavyo hukuvijaza, visima ambavyo hukuchimba, na mashamba ya mizabibu na mizeituni ambayo hukupanda wewe, basi, utakapokula na kushiba,
ובתים מלאים כל טוב אשר לא מלאת וברת חצובים אשר לא חצבת כרמים וזיתים אשר לא נטעת ואכלת ושבעת
12 jihadhari usije ukamwacha Bwana, aliyekutoa katika nchi ya Misri, kutoka nchi ya utumwa.
השמר לך פן תשכח את יהוה אשר הוציאך מארץ מצרים מבית עבדים
13 Utamcha Bwana Mungu wako, na umtumikie yeye peke yake na kuapa kwa jina lake.
את יהוה אלהיך תירא ואתו תעבד ובשמו תשבע
14 Usifuate miungu mingine, miungu ya mataifa yanayokuzunguka;
לא תלכון אחרי אלהים אחרים--מאלהי העמים אשר סביבותיכם
15 kwa kuwa Bwana Mungu wako, ambaye yuko katikati yako, ni Mungu mwenye wivu na hasira yake itawaka dhidi yako, naye atakuangamiza kutoka uso wa nchi.
כי אל קנא יהוה אלהיך בקרבך פן יחרה אף יהוה אלהיך בך והשמידך מעל פני האדמה
16 Usimjaribu Bwana Mungu wako kama ulivyofanya huko Masa.
לא תנסו את יהוה אלהיכם כאשר נסיתם במסה
17 Utayashika maagizo ya Bwana Mungu wako kwa bidii, na masharti na amri alizokupa.
שמור תשמרון את מצות יהוה אלהיכם ועדתיו וחקיו אשר צוך
18 Fanya lililo haki na jema mbele za Bwana, ili upate kufanikiwa, uweze kuingia na kuimiliki nchi nzuri ambayo Bwana aliahidi kwa kiapo kwa baba zako,
ועשית הישר והטוב בעיני יהוה--למען ייטב לך ובאת וירשת את הארץ הטבה אשר נשבע יהוה לאבתיך
19 kuwafukuza kwa nguvu adui zako mbele yako kama Bwana alivyosema.
להדף את כל איביך מפניך כאשר דבר יהוה
20 Siku zijazo, mtoto wako atakapokuuliza, “Ni nini maana ya masharti haya, amri na sheria hizi ambazo Bwana Mungu wako alikuagiza wewe?”
כי ישאלך בנך מחר לאמר מה העדת והחקים והמשפטים אשר צוה יהוה אלהינו אתכם
21 Mwambie: “Tulikuwa watumwa wa Farao huko Misri, lakini Bwana alitutoa sisi kutoka Misri kwa mkono wenye nguvu.
ואמרת לבנך עבדים היינו לפרעה במצרים ויציאנו יהוה ממצרים ביד חזקה
22 Bwana akapeleka mbele yetu ishara za miujiza na maajabu makubwa na ya kutisha mno juu ya Misri na Farao pamoja na nyumba yake yote.
ויתן יהוה אותת ומפתים גדלים ורעים במצרים בפרעה ובכל ביתו--לעינינו
23 Lakini Mungu akatutoa huko, akatuleta na kutupa nchi hii ambayo aliwaahidi baba zetu kwa kiapo.
ואותנו הוציא משם--למען הביא אתנו לתת לנו את הארץ אשר נשבע לאבתינו
24 Bwana akatuagiza tutii amri hizi zote na kumcha Bwana Mungu wetu, ili tupate kustawi na kuendelea kuwa hai kama ilivyo leo.
ויצונו יהוה לעשות את כל החקים האלה ליראה את יהוה אלהינו--לטוב לנו כל הימים לחיתנו כהיום הזה
25 Kama tukizitii kwa bidii amri hizi zote mbele za Bwana Mungu wetu, kama alivyotuamuru sisi, hiyo itakuwa haki yetu.”
וצדקה תהיה לנו כי נשמר לעשות את כל המצוה הזאת לפני יהוה אלהינו--כאשר צונו

< Torati 6 >