< Torati 5 >

1 Mose akawaita Israeli wote, akawaambia: Ee Israeli, sikilizeni amri na sheria ninazowatangazia leo. Jifunzeni, na mwe na hakika kuzifuata.
Moses called to all Israel, and said to them, Hear, Israel, the statutes and the ordinances which I speak in your ears this day, that you may learn them, and observe to do them.
2 Bwana Mungu wetu alifanya Agano nasi katika mlima wa Horebu.
The LORD our God made a covenant with us in Horeb.
3 Si kwamba Bwana alifanya Agano na baba zetu, bali alifanya nasi, nasi sote ambao tuko hai hapa leo.
The LORD did not make this covenant with our fathers, but with us, even us, who are all of us here alive this day.
4 Bwana alisema nanyi uso kwa uso kutoka moto juu ya mlima.
The LORD spoke with you face to face on the mountain out of the midst of the fire,
5 (Wakati huo nilisimama kati ya Bwana na ninyi kuwatangazia neno la Bwana, kwa sababu mliogopa ule moto, nanyi hamkupanda mlimani.) Naye Mungu alisema:
(I stood between the LORD and you at that time, to show you the words of the LORD: for you were afraid because of the fire, and did not go up onto the mountain; ) saying,
6 “Mimi ndimi Bwana Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, kutoka nchi ya utumwa.
"I am the LORD your God, who brought you out of the land of Egypt, out of the house of bondage.
7 Usiwe na miungu mingine ila mimi.
"Do not have no other gods before me.
8 Usijitengenezee sanamu katika umbo la kitu chochote kilicho juu mbinguni au duniani chini au ndani ya maji.
"Do not make an engraved image for yourself, or any likeness of what is in heaven above, or on the earth below, or that is in the waters below the earth.
9 Usivisujudie wala kuviabudu; kwa kuwa Mimi, Bwana Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu, ninayewaadhibu watoto kwa ajili ya dhambi za baba zao hadi kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
You must not bow down yourself to them, nor serve them; for I, the LORD, your God, am a jealous God, visiting the iniquity of the fathers on the children, upon the third and upon the fourth [generation] of those who hate me;
10 lakini ninaonyesha upendo kwa maelfu ya vizazi vya wale wanipendao na kuzishika amri zangu.
and showing loving kindness to thousands of those who love me and keep my commandments.
11 Usilitaje bure jina la Bwana Mungu wako, kwa kuwa Bwana hataacha kumhesabia hatia yeye alitajaye jina lake bure.
"Do not take the name of the LORD your God in vain: for the LORD will not hold him guiltless who takes his name in vain.
12 Adhimisha siku ya Sabato na kuiweka takatifu, kama Bwana Mungu wako alivyokuagiza.
"Observe the Sabbath day, to keep it holy, as the LORD your God commanded you.
13 Kwa siku sita utafanya kazi na kutenda shughuli zako zote.
Six days you may labor, and do all your work;
14 Lakini siku ya Saba ni Sabato kwa Bwana, Mungu wako. Siku hiyo hutafanya kazi yoyote, wewe, wala mwanao au binti yako, wala mtumishi wa kiume au mtumishi wa kike, wala ngʼombe wako, punda wako au mnyama wako yeyote, wala mgeni aliyeko malangoni mwako, ili kwamba mtumishi wako wa kiume na wa kike wapate kupumzika kama wewe.
but the seventh day is a Sabbath to the LORD your God. On it you must not do any work, you, your son, your daughter, your male servant, nor your female servant, your ox, nor your donkey, nor your livestock, your stranger who is within your gates; that your male servant and your female servant may rest as well as you.
15 Kumbuka mlikuwa watumwa huko Misri, na Bwana Mungu wenu aliwatoa huko kwa mkono wenye nguvu na kwa mkono ulionyooshwa. Kwa hiyo Bwana Mungu wako amekuagiza kuiadhimisha siku ya Sabato.
Remember that you were a slave in the land of Egypt, and the LORD your God brought you out of there by a mighty hand and by an outstretched arm: therefore the LORD your God commanded you to keep the Sabbath day.
16 Waheshimu baba yako na mama yako, kama Bwana Mungu wako alivyokuagiza, ili siku zako zipate kuwa nyingi na kufanikiwa katika nchi Bwana Mungu wako anayokupa.
"Honor your father and your mother, as the LORD your God commanded you; that your days may be long, and that it may go well with you, in the land which the LORD your God gives you.
17 Usiue.
"Do not commit adultery.
18 Usizini.
"Do not murder.
19 Usiibe.
"Do not steal.
20 Usimshuhudie jirani yako uongo.
"Do not give false testimony against your neighbor.
21 Usitamani mke wa jirani yako. Usitamani nyumba ya jirani yako au shamba lake, mtumishi wake wa kiume au wa kike, ngʼombe au punda wake, wala kitu chochote cha jirani yako.”
"Do not covet your neighbor's wife. Do not crave your neighbor's house, his field, or his male servant, or his female servant, his ox, or his donkey, or anything that is your neighbor's."
22 Hizi ndizo amri alizozitangaza Bwana kwa sauti kubwa kwa kusanyiko lenu lote huko mlimani kutoka kwenye moto, wingu na giza nene, wala hakuongeza chochote zaidi. Kisha akaziandika juu ya vibao viwili vya mawe, naye akanipa mimi.
These words the LORD spoke to all your assembly on the mountain out of the midst of the fire, of the cloud, and of the thick darkness, with a great voice; and he added no more. And he wrote them on two tablets of stone, and gave them to me.
23 Mliposikia sauti kutoka kwenye giza, mlima ulipokuwa ukiwaka moto, viongozi wenu wote wa makabila yenu na wazee wenu walinijia mimi.
It happened, when you heard the voice out of the midst of the darkness, while the mountain was burning with fire, that you came near to me, even all the heads of your tribes, and your elders;
24 Nanyi mkasema, “Bwana Mungu wetu ametuonyesha utukufu na enzi yake, nasi tumesikia sauti yake kutoka kwenye moto. Leo tumeona kwamba mwanadamu anaweza kuishi hata kama Mungu akizungumza naye.
and you said, "Look, the LORD our God has shown us his glory and his greatness, and we have heard his voice out of the midst of the fire: we have seen this day that God does speak with man, and he lives.
25 Lakini sasa, kwa nini tufe? Moto huu mkubwa utatuteketeza sisi na tutakufa kama tukiendelea kusikia sauti ya Bwana Mungu wetu zaidi.
Now therefore why should we die? For this great fire will consume us: if we hear the voice of the LORD our God any more, then we shall die.
26 Ni mtu yupi mwenye mwili ambaye amewahi kuisikia sauti ya Mungu aliye hai akizungumza kutoka kwenye moto, kama sisi tulivyoisikia, naye akaishi?
For who is there of all flesh, that has heard the voice of the living God speaking out of the midst of the fire, as we have, and lived?
27 Sogea karibu usikie yale yote asemayo Bwana Mungu wetu. Kisha utuambie chochote kile ambacho Bwana Mungu wetu anakuambia. Tutasikiliza na kutii.”
Go near, and hear all that the LORD our God shall say to you, and tell us all that the LORD our God speaks to you; and we will hear it, and do it."
28 Bwana aliwasikia wakati mlipozungumza nami, na Bwana akaniambia, “Nimesikia kile hawa watu walichokuambia. Kila kitu walichokisema ni kizuri.
The LORD heard the voice of your words, when you spoke to me; and the LORD said to me, "I have heard the voice of the words of this people, which they have spoken to you: they have well said all that they have spoken.
29 Laiti kama mioyo yao ingekuwa na mwelekeo wa kuniogopa na kuzishika amri zangu zote daima, ili kwamba wafanikiwe wao pamoja na watoto wao milele!
Oh that there were such a heart in them, that they would fear me, and keep my commandments always, that it might be well with them, and with their children forever.
30 “Nenda uwaambie warudi kwenye mahema yao.
"Go tell them, Return to your tents.
31 Lakini wewe baki hapa pamoja nami ili niweze kukupa maagizo yote, amri na sheria ambazo utawafundisha wazifuate katika nchi ninayokwenda kuwapa waimiliki.”
But as for you, stand here by me, and I will tell you all the commandment, and the statutes, and the ordinances, which you shall teach them, that they may do them in the land which I give them to possess it."
32 Hivyo kuweni waangalifu kuyafanya yale Bwana Mungu wenu aliyowaagiza; msigeuke upande wa kuume wala wa kushoto.
You shall observe to do therefore as the LORD your God has commanded you: you shall not turn aside to the right hand or to the left.
33 Fuateni yale yote ambayo Bwana Mungu wenu aliwaagiza, ili mpate kuishi, kustawi na kuziongeza siku zenu katika nchi mtakayoimiliki.
You shall walk in all the way which the LORD your God has commanded you, that you may live, and that it may be well with you, and that you may prolong your days in the land which you shall possess.

< Torati 5 >