< Torati 27 >

1 Mose na wazee wa Israeli wakawaagiza watu: “Yashikeni maagizo haya yote ninayowaagiza leo.
Musa na wazee wa Israeli waliwaamuru watu na kusema, “Zishikeni amri zote ninazowaamuru leo.
2 Mtakapokuwa mmevuka Mto Yordani na kuingia katika nchi awapayo Bwana Mungu wenu, msimamishe mawe makubwa na mkayatie lipu.
Katika siku mtakapopita juu ya Yordani kwenye nchi ambayo Yahwe Mungu wako anawapatia, mnapaswa kutengeneza mawe kiasi makubwa na kuyachapa kwa lipu.
3 Andikeni juu yake maneno yote ya sheria hii wakati mtakapokuwa mmevuka na kuingia katika nchi awapayo Bwana Mungu wenu, nchi itiririkayo maziwa na asali, kama vile Bwana, Mungu wa baba zenu, alivyowaahidi.
Mnatakiwa kuyaandika juu yake maneno yote ya sheria hii pale mtakapovuka; ili muweze kwenda katika nchi ambayo Yahwe Mungu wako anawapatia, nchi inayotiririka kwa maziwa na asali, kama Yahwe, Mungu wa mababu zenu, alivyowaahidi.
4 Mtakapokuwa mmevuka Yordani, simamisheni mawe haya juu ya Mlima Ebali, kama ninavyowaagiza leo, mkayatie lipu.
Mtakapovuka juu ya Yordani, yapangane haya mawe ninayowaamuru leo, juu ya mlima wa Ebali, na myapige kwa lipu.
5 Huko mjengeeni Bwana Mungu wenu madhabahu, madhabahu ya mawe. Msitumie kifaa chochote cha chuma juu yake.
Hapo mnapaswa kujenga dhabahu kwa Yahwe Mungu wako, dhabahu la mawe; lakini hautakiwi kuinua chombo cha chuma kujenga mawe.
6 Jengeni madhabahu ya Bwana Mungu wenu kwa mawe ya shambani, na mtoe sadaka za kuteketezwa juu yake kwa Bwana Mungu wenu.
Unatakiwa kujenga dhabahu ya Yahwe Mungu wako kwa mawe yasiyokuwa na kazi; unatakiwa kutoa dhabihu ya kuteketeza juu yake kwa Yahwe Mungu wako,
7 Toeni sadaka za amani juu yake, mkizila na kufurahia mbele za Bwana Mungu wenu.
na utatoa sadaka ya pamoja na utakula pale; utafurahia mbele ya Yahwe Mungu wako.
8 Nanyi mtaandika maneno yote ya sheria hii kwa wazi sana juu ya mawe haya ambayo mmesimamisha.”
Utaandika juu ya mawe maneno yote ya sheria hii kwa wazi.
9 Kisha Mose na makuhani, ambao ni Walawi, wakawaambia Israeli wote, “Nyamaza ee Israeli, sikiliza! Sasa umekuwa taifa la Bwana Mungu wako.
Musa na makuhani, Walawi, waliongea na Waisraeli wote na kusema, “Nyamazeni na sikilizeni Israel: Leo mmekuwa watu wa Yahwe Mungu wenu.
10 Mtii Bwana Mungu wako, na kufuata amri zake na maagizo ninayokupa leo.”
Mnapaswa basi kutii sauti ya Yahwe Mungu wenu na kutii amri na sheria zake ambazo ninawaamuru leo.”
11 Siku ile ile Mose akawaagiza watu:
Musa aliwaamuru watu siku hiyo hiyo na kusema,
12 Mtakapovuka Mto Yordani, makabila haya yatasimama juu ya Mlima Gerizimu kubariki watu: Simeoni, Lawi, Yuda, Isakari, Yosefu na Benyamini.
“Makabila haya yanapaswa kusimama katika mlima Gerizimu kuwabariki watu baada ya nyinyi kuvuka Yordani; Simeoni, Lawi, Judah, Isakari, Yusufu na Benyamini.
13 Makabila haya yatasimama juu ya Mlima Ebali kwa kutamka laana: Reubeni, Gadi, Asheri, Zabuloni, Dani na Naftali.
Haya ni makabila ambayo lazima yasimame juu yam lima Ebali kutamka laana: Rubeni, Gadi, Asheri, Zabuloni, Dan na Naftali.
14 Nao Walawi watawasomea watu wote wa Israeli kwa sauti kubwa:
Walawi watajibu na kusema kwa wanamume wote wa Israeli kwa sauti kubwa:
15 “Alaaniwe mtu afanyaye sanamu ya kuchonga au mwenye kusubu sanamu, kitu ambacho ni chukizo kwa Bwana, kazi ya mikono ya fundi stadi, na kuisimamisha kwa siri.”
“Alaaniwe mwanamume atakayechonga sanamu au kinyago, chukizo kwa Yahwe, kazi ya mikono ya fundi, ambayo ataifanya sirini”. Kisha watu wote wanapaswa kujibu na kusema, ‘Amina’.
16 “Alaaniwe mtu amdharauye baba yake na mama yake.”
Alaaniwe mwanamume atakayemuaibisha baba yake au mama yake. Kisha watu wote waseme, 'Amina'.
17 “Alaaniwe mtu asogezaye jiwe la mpaka wa jirani yake.”
Alaaniwe mwanamume anayetoa alama ya ardhi.' Kisha watu wote na waseme, 'Amina'.
18 “Alaaniwe mtu ampotoshaye kipofu njiani.”
Alaaniwe mwanamume asababishae kipofu kutoka nje ya barabara. Kisha watu wote waseme, ‘Amina’.
19 “Alaaniwe mtu apotoshaye haki ya mgeni, yatima au mjane.”
Alaaniwe mwanamume atumiaye nguvu kupokonya haki inayomstahili mgeni, yatima, au mjane. Kisha watu wote lazima waseme, ‘Amina’.
20 “Alaaniwe mtu akutanaye kimwili na mke wa baba yake, kwa maana anadharau malazi ya baba yake.”
Alaaniwe mwanamume atakayelala na mke wa baba yake, kwa sababu atakuwa amechukua haki za baba yake’. Kisha watu wote lazima waseme, ‘Amina’.
21 “Alaaniwe mtu akutanaye kimwili na mnyama yeyote.”
Alaaniwe mwanamume atakayelala na aina yoyote ya mnyama’. Kisha watu wote lazima waseme, ‘Amina’.
22 “Alaaniwe mtu akutanaye kimwili na dada yake, binti wa baba yake au binti wa mama yake.”
Alaaniwe mwanamume atakayelala na dada yake, binti wa baba yake, au binti wa mama yake. Kisha watu wote lazima waseme, ‘Amina’.
23 “Alaaniwe mtu akutanaye kimwili na mama mkwe wake.”
Alaaniwe mwanamume atakayelala na mama mkwe’. Kisha watu wote lazima waseme, ‘Amina’.
24 “Alaaniwe mtu amuuaye jirani yake kwa siri.”
Alaaniwe mwanamume atakayemuua jirani yake kwa siri’. Kisha watu wote lazima waseme, ‘Amina’.
25 “Alaaniwe mtu apokeaye rushwa ili kumuua mtu asiye na hatia.”
Alaaniwe mwanamume apokeaye rushwa kumuua mtu asiye na hatia’. Kisha watu wote lazima waseme, ‘Amina’.
26 “Alaaniwe mtu yule ambaye hatashikilia maneno ya sheria hii kwa kuyatekeleza.”
Alaaniwe mwanamume asiyethibitisha maneno ya sheria hii, ili kwamba ayatii.’ Kisha watu wote lazima waseme, ‘Amina’.

< Torati 27 >