< Torati 20 >

1 Mtakapokwenda vitani kupigana na adui zenu na mkaona farasi na magari ya vita na jeshi kubwa kuliko lenu, msiwaogope, kwa sababu Bwana Mungu wenu aliyewatoa kutoka Misri, atakuwa pamoja nanyi.
Pindi utokapo kwenda vitani kupigana dhidi ya adui zako, na kuona farasi, magari, na watu wengi zaidi kuliko wewe, haupaswi kuwaogopa; kwa kuwa Yahwe Mungu wako yu pamoja nawe, yeye aliyekuleta kutoka nchi ya Misri.
2 Wakati mtakapokaribia kwenda vitani, kuhani atakuja mbele na kuhutubia jeshi.
Wakati unakaribia kuingia kwenye vita, kuhani anapaswa kuwasogelea na kuongea na watu.
3 Atasema: “Sikia, ee Israeli, leo unakwenda vitani kupigana na adui zako. Usife moyo wala usiogope, usitishwe wala usitiwe hofu mbele yao.
Anapaswa kuwaambia,”Sikilizeni, Israel, mnaenda kupigana dhidi ya maadui zenu. Msidhofishe moyo wenu. Msiohofu au kutetemeka. Msiwaogope.
4 Kwa kuwa Bwana Mungu wenu ndiye huenda pamoja nanyi kuwapigania dhidi ya adui zenu na kuwapatia ushindi.”
Kwa kuwa Yahwe Mungu wenu ndiye aendae pamoja nanyi kupigana kwa ajili yenu dhidi ya maadui zenu na kuwaokoa.
5 Maafisa wataliambia jeshi: “Je, kuna yeyote aliyejenga nyumba mpya ambayo haijawekwa wakfu? Yeye na arudi nyumbani, ama sivyo anaweza kufa vitani na mtu mwingine akaiweka wakfu.
Maakida wanapaswa kuzungumza na watu na kusema, “Ni mtu yupi aliyejenga nyumba mpya na hajaiweka wakfu? Acha aende na arudi nyumbani kwake, ili kwamba asife vitani na mtu mwingine aiweke wakfu.
6 Je, kuna yeyote aliyepanda shamba la mizabibu na hajaanza kulifurahia? Yeye na arudi nyumbani, au sivyo anaweza kufa vitani na mtu mwingine akalifurahia.
Kuna yeyote ambaye amepanda mzabibu na hajafurahia matunda yake? Acha aende nyumbani, ili kwamba asife vitani na mtu mwingine afurahie matunda yake.
7 Je, kuna yeyote aliyeposa mwanamke na hajamwoa? Yeye na arudi nyumbani, ama sivyo anaweza kufa vitani na mtu mwingine akamwoa.”
Ni mtu yupi aliyeposa kuoa mwanamke lakini bado hajamuoa? Acha aende nyumbani ili kwamba asife vitani na mume mwingine amuoa.”
8 Kisha maafisa wataongeza haya, “Je, kuna mtu anayeogopa ama kufa moyo? Yeye na arudi nyumbani ili ndugu zake nao wasije wakafa moyo pia.”
Maakida wanapaswa kuzungumza zaidi kwa watu na kusema, “Ni mwanaume gani aliye hapa ambaye ni mwenye hofu au mnyonge? Acha aende na arudi nyumbani kwake, ili kwamba moyo wa ndugu yake usiyeyuke kama moyo wake.
9 Wakati maafisa watakapomaliza kuzungumza na jeshi, watawateua wakuu wa vikosi.
Wakati maakida wamemaliza kuzungumza na watu, wanapaswa kuteua majemedari juu yao.
10 Wakati mtakapokwenda kushambulia mji, wapeni watu wake masharti ya amani.
Wakati mtokapo kuteka mji, wafanye watu hao toleo la amani.
11 Wakikubali na kuwafungulia malango yao, watu wake wote watawatumikia kwa kufanya kazi ngumu na watawatumikia.
Kama watapokea amani na kufungua malango yao kwako, watu wote wanaopatikana ndani yake wanapaswa kulazimishwa kukufanyia kazi na wanapaswa kukutumikia.
12 Ikiwa watakataa kufanya mapatano ya amani na wakiwaingiza katika vita, basi mtauzunguka mji huo kwa vita.
Lakini kama haitengenezi amani kwenu, lakani badala yake inatengeneza vita dhidi yenu, basi mnapaswa kumruhusu,
13 Wakati Bwana Mungu wenu atakapouweka mji huo mkononi mwenu, waueni kwa upanga wanaume wote waliomo ndani yake.
na wakati Yahwe Mungu wenu anawapa ushindi na kuwaweka chini ya utawala wenu, mnapaswa kuua kila mtu katika mji.
14 Kwa upande wa wanawake, watoto, mifugo na kila kitu kingine chochote ndani ya huo mji, mnaweza kuvichukua kama nyara kwa ajili yenu. Nanyi mnaweza kuzitumia hizo nyara ambazo Bwana Mungu wenu amewapa kutoka kwa adui zenu.
Lakini wanawake, wadogo, ng'ombe, na kila kitu kilicho ndani ya mji, na nyara zake zote, utavichukua kama mateka yako. Nawe utawamaliza mateka wa maadui zako, ambao Yahwe Mungu amekupa.
15 Hivi ndivyo mtakavyofanya kwa miji yote ambayo iko mbali nanyi, ambayo haimilikiwi na mataifa ya karibu.
Unapaswa kuifanyia hivyo kuelekea miji yote ambayo iko mbali nawe, miji ambayo siyo miji ya mataifa yafuatayo.
16 Hata hivyo, katika miji ya mataifa ambayo Bwana Mungu wenu anawapa kama urithi, msiache kitu chochote hai kinachopumua.
Katika miji ya watu hawa ambayo Yahwe Mungu wenu anawapa kama urithi, mnapaswa kutunza chochote kilicho na uhai.
17 Waangamizeni kabisa Wahiti, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi na Wayebusi, kama Bwana Mungu wenu alivyowaamuru.
Badala yake, mnapaswa kabisa kuagamiza: Hittite, na Amorite, Wakanani, Waperezi, Hivite, na Wabusi, kama Yahwe Mungu wenu alivyowaamuru.
18 La sivyo, watawafundisha kufuata mambo yote ya machukizo wanayofanya wakiabudu miungu yao, nanyi mtatenda dhambi dhidi ya Bwana Mungu wenu.
Fanya hivi ili kwamba wasiwafundishe kufanya katika njia za machukizo, kama walivyofanya kwa miungu yao. Kama mtafanya, mtafanya dhambi dhidi ya Yahwe Mungu wenu.
19 Wakati mtakapouzunguka mji kwa vita kwa muda mrefu, mkipigana dhidi yake ili kuuteka, msiharibu miti yake kwa kuikata kwa shoka, kwa sababu mtaweza kula matunda yake. Hivyo msiikate. Je, miti hiyo ya mashambani ni watu, hata muizingire?
Wakati mtakapouzingira mji kwa muda mrefu, huku mkipigana dhidi yake kuuteka, hampaswi kuharibu miti yake kwa kushika shoka dhidi yake. Kwa kuwa utaweza kula matunda yake, kwa hiyo usiikate. Kwa maana mti wa kondeni mtu ambaye atauzingira?
20 Hata hivyo, mnaweza kuikata miti ambayo sio miti ya matunda na kuitumia kujenga ngome, mpaka mji ulio katika vita na ninyi utakapoanguka.
Ila miti ambayo unaijua siyo miti ya chakula, unaweza kuharibu na kuikata chini; utajenga maburuji dhidi ya mji unaofanya vita nawe, mpaka uanguke.

< Torati 20 >