< Torati 18 >

1 Makuhani ambao ni Walawi, yaani kabila lote la Lawi, hawatakuwa na mgawo wala urithi pamoja na Israeli. Wataishi kwa sadaka zitolewazo kwa ajili ya Bwana za kuteketezwa kwa moto, kwa maana huo ndio urithi wao.
Makuhani, ambao ni Walawi, na makabila yote ya Lawi, hayatakuwa na mgao wala urithi pamoja na Israel; wanapaswa kula dhabihu ya Yahwe iliyotengenezwa kwa moto kama urithi wao.
2 Hawatakuwa na urithi miongoni mwa ndugu zao; Bwana ndiye urithi wao, kama alivyowaahidi.
Hawatakuwa na urithi miongoni mwa ndugu zao; Yahwe ni urithi wao, kama alivyosema nao.
3 Hili ndilo fungu la makuhani kutoka kwa watu watakaotoa dhabihu ya fahali au kondoo: mguu wa mbele, mataya na matumbo.
Hii ni sababu ya makuhani kutoka kwa watu, kutoka kwa wale wanaotoa dhabihu, kama itakuwa ng'ombe au kondoo: wanapaswa kutoa kwa kuhani bega, mashavu mawili, na sehemu za ndani.
4 Mtawapa malimbuko ya nafaka zenu, divai mpya, mafuta na sufu ya kwanza kutoka manyoya ya kondoo zenu,
Mazao ya kwanza ya nafaka zako, mvinyo wako mpya, na mafuta yako, na manyoya ya kwanza ya kondoo zako, unapaswa umpe.
5 kwa kuwa Bwana Mungu wenu amewachagua pamoja na wazao wao kutoka makabila yenu kusimama na kuhudumu katika jina la Bwana siku zote.
Kwa kuwa Yahwe Mungu wako amemchagua kutoka kwenye makabila yote yako kusimama kutumika kwa jina la Yahwe, yeye na wana wake milele.
6 Ikiwa Mlawi atahama kutoka mmojawapo ya miji yenu popote katika Israeli ambapo anaishi, akaja kwa moyo wote mahali ambapo Bwana atapachagua,
Kama Mlawi anatoka kati ya miji yenu nje ya Israel yote kutoka ambapo anaishi, na utamani kwa moyo wake wote kuja katika eneo Yahwe atachagua,
7 anaweza akahudumu katika jina la Bwana Mungu wake kama Walawi wenzake wote wanaohudumu hapo mbele za Bwana.
basi anapaswa kutumika kwa jina la Yahwe Mungu wake kama ndugu zake wote Walawi wanafanya, wanaosimama mbele ya Yahwe.
8 Atashiriki sawa katika mafao yao, hata kama amepokea fedha kutoka mauzo ya mali ya jamaa yake.
Wanapaswa kuwa na mgao wa kufanana wa kula, badala ya kile kinachokuja kutokana na mauzo ya urithi wa familia yake.
9 Wakati mtakapoingia katika nchi ambayo Bwana Mungu wenu anawapa, msijifunze kuiga njia za machukizo za mataifa ya huko.
Wakati mmekuja katika nchi ambayo Yahwe Mungu wenu anawapa, mnapaswa kujifunza kuangalia machukizo ya mataifa.
10 Asionekane mtu yeyote miongoni mwenu ampitishaye mwanawe au binti yake katika moto, atakayefanya uaguzi, ulozi, anayetabiri nyakati, anayejishughulisha na uchawi,
Pasipatikana miongoni mwenu mmoja anayemweka kijana wake au binti yake kwenye moto, yeyote anatumia uganga, yeyote anatabiri, au mchawi, mchawi yeyote,
11 wala arogaye kwa kupiga mafundo, wala mwaguzi au anayeabudu mizimu, wala awaombaye wafu.
yeyote aongeae na wafu, au yeyote aongeae na roho.
12 Mtu yeyote afanyaye mambo haya ni chukizo kwa Bwana, tena ni kwa sababu ya matendo haya ya kuchukiza wayafanyayo ndiyo maana Bwana Mungu wenu atayafukuza mataifa hayo mbele yenu.
Kwa yeyote afanyae mambo haya ni chukizo kwa Yahwe; ni kwa sababu ya machukizo haya ambayo Yahwe Mungu wenu anawaondosha mbele zenu.
13 Kamwe msilaumiwe mbele za Bwana Mungu wenu.
Mnapaswa kuwa wakamilifu mbele ya Yahwe Mungu wenu.
14 Mataifa mtakayowafukuza husikiliza wale wafanyao ulozi na uaguzi. Lakini kwenu ninyi, Bwana Mungu wenu hajawaruhusu kufanya hivyo.
Kwa mataifa haya ambayo mtayafukuza kusikiliza wale wafanyao uchawi na uganga; lakini kwenu, Yahwe Mungu wenu amewakataza ninyi kufanya hivyo.
15 Bwana Mungu wenu atawainulia nabii kama mimi kutoka miongoni mwa ndugu zenu wenyewe. Msikilizeni yeye.
Yahwe Mungu wenu atainua kwa ajili yenu nabii kutoka miongoni mwenu, mmoja wa ndugu zenu, kama mimi. Mnapaswa kumsikiliza.
16 Kwa kuwa hivi ndivyo mlivyomwomba Bwana Mungu wenu kule Horebu siku ile ya kusanyiko, wakati mliposema, “Na tusiisikie sauti ya Bwana Mungu wetu, wala kuuona moto huu mkubwa tena, ama sivyo tutakufa.”
Hiki ndicho mlichouliza kutoka kwa Yahwe Mungu wenu huko Horebu katika siku ya kusanyiko, kusema, “Acha tusisikie tena sauti ya Yahwe Mungu wetu, wala kuona moto mkuu tena, wala tutakufa.”
17 Bwana akaniambia: “Wanachosema ni vyema.
Yahwe alisema nami, “Kile walichosema ni kizuri.
18 Nitawainulia nabii kama wewe kutoka miongoni mwa ndugu zao; nitaweka maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia kila kitu nitakachomwamuru.
Nitamwinua nabii kwa ajili yao kutoka miongoni mwa ndugu zao, kama wewe. Nitaweka maneno yangu katika kinywa chake, na ataongea nao yote niliyowakuamuru.
19 Kama mtu yeyote hatasikiliza maneno yangu ambayo huyo nabii atayasema kwa Jina langu, mimi mwenyewe nitamwajibisha.
Itakuwa kama yeyote hatasikia maneno yangu ambayo anazungumza kwa jina langu, nitalitaka kwake.
20 Lakini nabii ambaye atathubutu kusema kwa Jina langu kitu chochote ambacho sikumwamuru akiseme, au nabii ambaye husema kwa jina la miungu mingine ni lazima auawe.”
Lakini nabii ambaye anazungumza neno kwa kiburi kwa jina langu, neno ambalo sijamuamuru kusema, au ambaye anayezungumza kwa jina la miungu mingine, huyo nabii atakufa.
21 Mnaweza kuulizana wenyewe, “Tutawezaje kujua wakati ujumbe haukusemwa na Bwana?”
Hivyo ndivyo unapaswa kusema katika mioyo yenu: “Tutagunduaje kuwa ujumbe ambao Yahwe hajazungumza?
22 Ikiwa kile nabii anachotangaza kwa jina la Bwana hakikutokea au kutimia, huo ni ujumbe ambao Bwana hakusema. Nabii huyo amesema kwa ujuaji. Msimwogope huyo.
Mtagundua ujumbe ambao Yahwe amezungumza pindi nabii azungumzapo kwa jina la Yahwe. Kama hiyo haitokei wala kufanyika, basi hicho ni kile ambacho Yahwe hajazungumza na nabii amezungumza kwa kiburi, na hampaswi kumuogopa.

< Torati 18 >