< Torati 13 >

1 Kama nabii, au yule anayetabiri kwa njia ya ndoto, akijitokeza miongoni mwenu na akawatangazia ishara ya miujiza na ajabu,
Kama miongoni mwenu ainuka nabii au muota ndoto,
2 ikiwa ishara au ajabu ya aliyozungumza ikatokea, naye akasema, “Na tufuate miungu mingine” (miungu ambayo hamjaifahamu) “na tuiabudu,”
na kama anawapa ishara au maajabu, na kama ishara au maajabu yanatokea, kama alivyozungumza kwenu na kusema, “Ebu tuifuate miungu mingine, ambayo hatuijui, na tuiabudu.
3 kamwe msiyasikilize maneno ya nabii wala mwota ndoto huyo. Bwana Mungu wenu anawajaribu kuangalia kama mnampenda kwa moyo wenu wote na kwa roho yenu yote.
Usisikilize maneno ya nabii huyo, au kwa huyo muota ndoto, kwa kuwa Yahwe Mungu wako anakujaribu kujua kama unampenda Yahwe Mungu wako kwa moyo wako wote na roho yako yote.
4 Ni Bwana Mungu wenu ambaye mnapaswa kumfuata tena ni yeye mnapaswa kumheshimu. Shikeni maagizo yake na kumtii, mtumikieni na kushikamana naye.
Mtatembea baada ya Yahwe Mungu wenu, mheshimu, mzishike amri zake, na mtii sauti yake, na mtamwabudu na kushikamana naye.
5 Huyo nabii au mwota ndoto lazima auawe, kwa sababu amehubiri uasi dhidi ya Bwana Mungu wenu, ambaye aliwatoa kutoka nchi ya Misri na kuwakomboa kutoka nchi ya utumwa; amejaribu kuwageuza kutoka njia ambayo Bwana Mungu wenu aliwaagiza mfuate. Ni lazima mwondoe uovu miongoni mwenu.
Nabii huyo au muota ndoto atauwawa, kwa sababu amezungumza uasi dhidi ya Yahwe Mungu wenu, ambaye aliwaleta toka nchi ya Misri, na aliyewakomboa kutoka nyumba ya utumwa. Hivyo nabii anataka kuwaondoa katika njia ambayo Yahwe Mungu wenu aliwaamuru kutembea. Kwa hiyo weka mbali maouvu kutoka kwenu.
6 Kama ndugu yako hasa, au mwanao au binti yako, au mke umpendaye, au rafiki yako wa karibu sana akikushawishi kwa siri, akisema, “Na twende tukaabudu miungu mingine” (miungu ambayo ninyi wala baba zenu hamkuifahamu,
Tuseme kwamba ndugu yako, mwana wa mama yako, au mwana wako, au binti yako, au mke wa karibu nawe, au rafiki yako ambaye ni kama roho yako, kukushawishi kwa siri na kusema, “Acha tuende na tukaabudu miungu mingine ambayo hatujazijua, wala wewe wala mababu zako-
7 miungu ya watu wanaowazunguka, ikiwa karibu au mbali, kutoka mwisho mmoja wa nchi mpaka mwingine),
Miungu yeyote ya watu ambayo imewazunguka, karibu nanyi au mbali kutoka, kutoka mwisho wa dunia kwenda mwisho mwingine wa dunia.
8 usikubali wala usimsikilize. Usimhurumie! Usimwache wala usimkinge.
Usimkubali au kumsikiliza. Wala macho yako yasione huruma, wala hautamuacha akiba au kumficha.
9 Hakika ni lazima auawe. Ni lazima mkono wako uwe wa kwanza katika kumuua kisha mikono ya watu wengine wote.
Badala yake, utamuacha hakika; mkono wako utakuwa wa kwanza kumuua, na badae mkono wa watu wote.
10 Mpigeni kwa mawe mpaka afe, kwa sababu alijaribu kuwageuza mtoke kwa Bwana Mungu wenu ambaye aliwatoa Misri, kutoka nchi ya utumwa.
Mtamponda mpaka kufa kwa mawe, kwa sababu amejaribu kuwaondoa kutoka kwa Yahwe Mungu wenu, ambaye aliwatoa kutoka nchi ya Misri, nje ya nyumba ya utumwa.
11 Kisha Israeli wote watasikia na kuogopa, wala hakuna mmoja miongoni mwenu atakayefanya uovu tena.
Israel yote itasikia na kuogopa, na haitaendelea kufanya aina ya uovu miongoni mwenu.
12 Kama mkisikia ikisemwa kwamba moja ya miji ambayo Bwana Mungu wenu anawapa mkae ndani yake
Kama utasikia yeyote anasema kuhusu moja ya miji yenu, kwamba Yahwe Mungu wenu anawapa kuishi ndani yake.
13 kuna wanaume waovu wameinuka miongoni mwenu na wamewapotosha watu wa mji, wakisema, “Twendeni tukaabudu miungu mingine” (miungu ambayo hamkuifahamu),
Baadhi ya wenzuni waovu wamewaacha miongoni mwenu na kuacha kwa mbali wakazi wa miji yao na kusema, “Acha tuende na kuabudu miungu mingine ambayo hamjaijua.
14 ndipo itakubidi kuuliza, kupima na kuchunguza kwa makini. Kama ni kweli, tena ikihakikishwa kwamba jambo hili lichukizalo limefanyika miongoni mwenu,
Basi utaichunguza uthibitisho, kufanya utafiti na kuipeleleza kwa kina. Wakati unagundua kwamba ni kweli na hakuna shaka kwamba chukizo hilo lililofanyika miongoni mwenu, kisha utachukua hatua.
15 kwa hakika ni lazima mwaue kwa upanga wale wote wanaoishi katika mji ule. Uharibuni kabisa, pamoja na watu wake na mifugo yake.
Utawashambulia hakika wenyeji wa mji huo kwa makali ya upanga. Utaangamiza kabisa na watu wote walio ndani yake, pamoja na mifugo yake, pamoja na makali ya upanga.
16 Kusanyeni nyara zote za mji katika uwanja wa wazi na kuuchoma mji kabisa pamoja na nyara zake zote kama sadaka ya kuteketezwa kwa Bwana Mungu wenu. Utabaki kuwa magofu milele na hautajengwa tena.
Utakusanya nyara zote kutoka katikati mwa mitaa yake na utuunguza mji, pamoja na nyara zake zote - kwa kuwa Yahwe Mungu wako. Mji utakuwa mchungu wa uharibifu milele; haupaswi kujengwa tena.
17 Hakuna kimoja kati ya vitu vilivyolaaniwa kitakachokutwa mikononi mwenu, ili Bwana ageuze hasira yake kali. Atawahurumia na kuwa na rehema kwenu pia kuongeza idadi yenu, kama alivyowaahidi baba zenu,
Hakuna hata kimoja kati ya vitu hivyo vimewekwa wakfu kwa ajili ya kuangamizwa vinapaswa kugadamana kwenye mkono wako. Hii inapaswa kuwa kesi, ili kwamba Yahwe atageuka kutoka kwenye ukali wa hasira yake, kumuonyesha rehema, kuwa na huruma kwako, na kukufanya wewe kuogezeka katika idadi, kama alivyoapa kwa baba zako.
18 kwa sababu mnamtii Bwana Mungu wenu, mkizishika amri zake zote zile ninazowapa leo na kufanya lile lililo jema machoni pake.
Atafanya hivi kwa sababu unasikiliza sauti ya Yahwe Mungu wako, kuzishika amri zake ambazo ninakuamuru leo, kufanya kile kilicho sahihi mbele ya macho ya Yahwe Mungu wako.

< Torati 13 >