< Torati 12 >

1 Hizi ndizo amri na sheria ambazo ni lazima mwe waangalifu kuzifuata katika nchi ambayo Bwana, Mungu wa baba zenu, amewapa kumiliki, kwa muda wote mtakaoishi katika nchi.
These are the statutes and the ordinances which you shall observe to do in the land which the LORD, the God of your fathers, has given you to possess all the days that you live on the earth.
2 Haribuni kabisa kila mahali pao pa kuabudia kwenye milima mirefu, vilima na chini ya kila mti mkubwa ambamo mataifa haya mnayokwenda kuchukua ardhi yao huabudia miungu yao.
You shall surely destroy all the places in which the nations that you shall dispossess served their gods: on the high mountains, and on the hills, and under every green tree.
3 Bomoeni madhabahu zao, vunjeni yale mawe wanayoabudu, chomeni moto nguzo zao za Ashera; katilieni mbali sanamu za miungu yao na mfute majina yao mahali hapo.
You shall break down their altars, dash their pillars in pieces, and burn their Asherah poles with fire. You shall cut down the engraved images of their gods. You shall destroy their name out of that place.
4 Kamwe msimwabudu Bwana Mungu wenu kama wanavyoabudu wao.
You shall not do so to the LORD your God.
5 Bali mtatafuta mahali Bwana Mungu wenu atakapopachagua katika makabila yenu yote ili aliweke jina lake huko kuwa makao yake. Mahali hapo ndipo iwapasapo kwenda;
But to the place which the LORD your God shall choose out of all your tribes, to put his name there, you shall seek his habitation, and you shall come there.
6 hapo ndipo mtakapoleta sadaka zenu za kuteketezwa na dhabihu, zaka zenu na changizo zenu, kile ulichoweka nadhiri kutoa, sadaka zenu za hiari na malimbuko ya makundi yenu ya ngʼombe pamoja na mbuzi na kondoo.
You shall bring your burnt offerings, your sacrifices, your tithes, the wave offering of your hand, your vows, your free will offerings, and the firstborn of your herd and of your flock there.
7 Hapo, katika uwepo wa Bwana Mungu wenu, ninyi pamoja na jamaa zenu, mtakula na kufurahia kila kitu ambacho mmegusa kwa mikono yenu, kwa sababu Bwana Mungu wenu amewabariki.
There you shall eat before the LORD your God, and you shall rejoice in all that you put your hand to, you and your households, in which the LORD your God has blessed you.
8 Msifanye kama tunavyofanya hapa leo, kila mtu anavyopenda mwenyewe,
You shall not do all the things that we do here today, every man whatever is right in his own eyes;
9 kwa kuwa bado hamjafikia mahali pa mapumziko na urithi ambao Bwana Mungu wenu anawapa.
for you have not yet come to the rest and to the inheritance which the LORD your God gives you.
10 Lakini mtavuka Yordani na kuishi katika nchi Bwana Mungu wenu anayowapa kama urithi, naye atawapa pumziko kutokana na adui zenu wote wanaowazunguka ili ninyi mpate kuishi kwa salama.
But when you go over the Jordan and dwell in the land which the LORD your God causes you to inherit, and he gives you rest from all your enemies around you, so that you dwell in safety,
11 Kisha kuhusu mahali Bwana Mungu wenu atakapopachagua kuwa mahali pa makao ya Jina lake, hapo ndipo inapowapasa kuleta kila kitu ninachowaamuru: sadaka zenu za kuteketezwa na dhabihu, zaka zenu na changizo, pamoja na vitu vyote vyenye thamani ambavyo mmeweka nadhiri kumtolea Bwana.
then it shall happen that to the place which the LORD your God shall choose, to cause his name to dwell there, there you shall bring all that I command you: your burnt offerings, your sacrifices, your tithes, the wave offering of your hand, and all your choice vows which you vow to the LORD.
12 Hapo furahini mbele za Bwana Mungu wenu, ninyi, wana wenu na binti zenu, watumishi wenu wa kiume na wa kike, pamoja na Walawi kutoka miji yenu ambao hawana mgawo wala urithi wao wenyewe.
You shall rejoice before the LORD your God—you, and your sons, your daughters, your male servants, your female servants, and the Levite who is within your gates, because he has no portion nor inheritance with you.
13 Kuweni waangalifu, msitoe dhabihu zenu za kuteketezwa mahali popote mnapopapenda.
Be careful that you do not offer your burnt offerings in every place that you see;
14 Mtazitoa tu mahali pale ambapo Bwana atachagua katika mojawapo ya makabila yenu, nanyi hapo zingatieni kila jambo ninalowaamuru.
but in the place which the LORD chooses in one of your tribes, there you shall offer your burnt offerings, and there you shall do all that I command you.
15 Hata hivyo, mnaweza kuwachinja wanyama wenu katika miji yenu yoyote ile na kula nyama nyingi mpendavyo kama vile mmemchinja paa au kulungu, kulingana na baraka mtakazojaliwa na Bwana Mungu wenu. Watu walio najisi au walio safi wanaweza kula.
Yet you may kill and eat meat within all your gates, after all the desire of your soul, according to the LORD your God’s blessing which he has given you. The unclean and the clean may eat of it, as of the gazelle and the deer.
16 Lakini kamwe usinywe damu; imwage juu ya ardhi kama maji.
Only you shall not eat the blood. You shall pour it out on the earth like water.
17 Hamruhusiwi kula katika miji yenu zaka yenu ya nafaka, ya divai mpya na ya mafuta, au mzaliwa wa kwanza wa makundi yenu ya ngʼombe na makundi yenu ya mbuzi na kondoo, wala chochote ambacho mmeweka nadhiri kukitoa, au sadaka zako za hiari, wala matoleo maalum.
You may not eat within your gates the tithe of your grain, or of your new wine, or of your oil, or the firstborn of your herd or of your flock, nor any of your vows which you vow, nor your free will offerings, nor the wave offering of your hand;
18 Badala yake, mtakula vitu hivyo katika uwepo wa Bwana Mungu wenu mahali ambapo Bwana Mungu wenu atapachagua: wewe, wana wako na binti zako, watumishi wako wa kiume na wa kike, na Walawi kutoka miji yenu. Mnatakiwa mfurahi mbele za Bwana Mungu wenu kwa kula kitu mtakachoweka mikono yenu.
but you shall eat them before the LORD your God in the place which the LORD your God shall choose: you, your son, your daughter, your male servant, your female servant, and the Levite who is within your gates. You shall rejoice before the LORD your God in all that you put your hand to.
19 Mwe waangalifu msiwapuuze Walawi kwa muda wote mnaoishi katika nchi yenu.
Be careful that you do not forsake the Levite as long as you live in your land.
20 Bwana Mungu wenu atakapokuwa ameongeza nchi yenu kama alivyowaahidi, nanyi mkitamani nyama na mkisema, “Ningependa nyama,” hapo unaweza kula nyingi upendavyo.
When the LORD your God enlarges your border, as he has promised you, and you say, “I want to eat meat,” because your soul desires to eat meat, you may eat meat, after all the desire of your soul.
21 Kama mahali ambapo Bwana Mungu wenu atapachagua kuweka Jina lake ni mbali sana kutoka kwenu, unaweza kuchinja wanyama kutoka makundi yenu ya ngʼombe, ya mbuzi na ya kondoo ambayo Bwana amewapa, kama nilivyokuamuru, na mkiwa katika miji yenu wenyewe mnaweza kula nyingi mtakavyo.
If the place which the LORD your God shall choose to put his name is too far from you, then you shall kill of your herd and of your flock, which the LORD has given you, as I have commanded you; and you may eat within your gates, after all the desire of your soul.
22 Mle kama vile mngekula paa na kulungu. Wote walio najisi kiibada na walio safi mwaweza kula.
Even as the gazelle and as the deer is eaten, so you shall eat of it. The unclean and the clean may eat of it alike.
23 Lakini hakikisheni kwamba hamkunywa damu, kwa sababu damu ni uhai, kamwe msile uhai pamoja na nyama.
Only be sure that you do not eat the blood; for the blood is the life. You shall not eat the life with the meat.
24 Hamruhusiwi kamwe kunywa damu; imwageni juu ya ardhi kama maji.
You shall not eat it. You shall pour it out on the earth like water.
25 Msinywe damu, ili mweze kufanikiwa ninyi pamoja na watoto wenu baada yenu, kwa sababu mtakuwa mkifanya lililo haki machoni pa Bwana.
You shall not eat it, that it may go well with you and with your children after you, when you do that which is right in the LORD’s eyes.
26 Lakini vichukueni vitu vyenu vilivyowekwa wakfu pamoja na vile mlivyoweka nadhiri, mwende mahali pale Bwana atakapopachagua.
Only your holy things which you have, and your vows, you shall take and go to the place which the LORD shall choose.
27 Leteni sadaka zenu za kuteketezwa juu ya madhabahu ya Bwana Mungu wenu, vyote nyama na damu. Damu ya dhabihu zenu lazima imiminwe kando ya madhabahu ya Bwana Mungu wenu, lakini nyama mnaweza kula.
You shall offer your burnt offerings, the meat and the blood, on the LORD your God’s altar. The blood of your sacrifices shall be poured out on the LORD your God’s altar, and you shall eat the meat.
28 Mwe waangalifu kutii masharti haya yote ninayowapa, ili kwamba siku zote mweze kufanikiwa, ninyi pamoja na watoto wenu baada yenu, kwa sababu mtakuwa mkifanya lililo jema na sahihi mbele za macho ya Bwana Mungu wenu.
Observe and hear all these words which I command you, that it may go well with you and with your children after you forever, when you do that which is good and right in the LORD your God’s eyes.
29 Bwana Mungu wenu atayakatilia mbali mbele yenu mataifa ambayo punde kidogo mtayavamia na kuyaondoa. Lakini mtakapokuwa mmeyafukuza na kuishi katika nchi yao,
When the LORD your God cuts off the nations from before you where you go in to dispossess them, and you dispossess them and dwell in their land,
30 na baada ya kuangamizwa mbele yenu, mwe waangalifu msijiingize katika tanzi kwa kuuliza habari za miungu yao, mkisema, “Je, mataifa haya hutumikiaje miungu yao? Nasi tutafanya vivyo hivyo.”
be careful that you are not ensnared to follow them after they are destroyed from before you, and that you not inquire after their gods, saying, “How do these nations serve their gods? I will do likewise.”
31 Kamwe msimwabudu Bwana Mungu wenu kwa njia wanayoabudu miungu yao, kwa sababu katika kuabudu miungu yao, wanafanya aina zote za machukizo anayoyachukia Bwana. Hata huwateketeza wana wao na binti zao kwa moto kama kafara kwa miungu yao.
You shall not do so to the LORD your God; for every abomination to the LORD, which he hates, they have done to their gods; for they even burn their sons and their daughters in the fire to their gods.
32 Angalieni kwamba mnafanya yote niliyowaamuru; msiongeze kitu wala msipunguze kitu.
Whatever thing I command you, that you shall observe to do. You shall not add to it, nor take away from it.

< Torati 12 >