< Torati 10 >

1 Wakati ule Bwana aliniambia, “Chonga vibao viwili vya mawe kama vile vya kwanza uje kwangu juu mlimani. Pia utengeneze Sanduku la mbao.
Kwa wakati ule Yahwe alisema kwangu, 'Chonga mbao mbili za mawe kama zile za kwanza, na njoo kwangu huku juu ya mlima, na utengeneze sanduku la mbao.
2 Nitaandika juu ya vibao maneno yaliyokuwa katika vile vibao vya kwanza, ambavyo ulivivunja. Kisha utaviweka ndani ya Sanduku.”
Nitaandika kwenye mbao maneno ambayo yalikuwa kwenye mbao za kwanza ulizozivunja, na utaziweka ndani ya sanduku.
3 Hivyo nikatengeneza Sanduku kwa mti wa mshita, nikachonga pia vibao vya mawe kama vile vya kwanza, kisha nikakwea mlimani nikiwa na vibao viwili mikononi mwangu.
Basi nilitengeneza sanduku la mbao za mikaratusi, na nikachonga mbao mbili za mawe kwa zile za kwanza, na nikaenda juu ya mlima, nikiwa na mbao mbili mkononi mwangu.
4 Bwana akaandika juu ya hivi vibao kile alichokuwa amekiandika kabla, Amri Kumi alizokuwa amewatangazia juu mlimani, kutoka kwenye moto siku ile ya kusanyiko. Bwana akanikabidhi.
Aliandika kwenye mbao, kama maandishi ya kwanza, amri kumi ambazo Yahwe amesema nanyi kwenye mlima kutoka katikati mwa moto katika siku ya kusanyiko; ndipo Yahwe alilinipa mimi.
5 Kisha nikashuka kutoka mlimani na kuweka vibao ndani ya Sanduku nililokuwa nimelitengeneza, kama Bwana alivyoniagiza, navyo viko huko sasa.
Niligeuka na kushuka chini kutoka mlimani, na kuweka mbao ndani ya sanduku nililokuwa nimetengeneza; hapo zilikaa, kama Yahwe alivyoniamuru.”
6 (Waisraeli walisafiri kutoka visima vya Yaakani hadi Mosera. Huko Aroni alifariki na kuzikwa, naye Eleazari mwanawe akachukua nafasi yake kama kuhani.
(Watu wa Israeli walisafiri kutoka Beerothi ya Bene Jaakan kwenda Moserathi. Huko Aaroni alikufa, na huko alizikwa; Eleazar, mwana wake, alitumika katika ofisi ya ukuhani kwenye nafasi yake.
7 Kutoka pale, walisafiri hadi Gudgoda wakaendelea mpaka Yotbatha, nchi yenye vijito vya maji.
Kutokea huko walisafiri kwenda Gudgodah, na kutoka Gudgodah kwenda Jotbathah, nchi yenye mikondo ya maji.
8 Wakati huo Bwana aliteua kabila la Lawi kulibeba Sanduku la Agano la Bwana, kusimama mbele za Bwana ili kutoa huduma, na kutangaza baraka kwa Jina lake, kama wanavyofanya mpaka leo.
Kwa wakati huo Yahwe alichagua kabila la Lawi kubeba sanduku la agano la Yahwe, kusimama mbele ya Yahwe kumtumikia na kubariki watu kwa jina lake, kama ilivyo leo.
9 Hiyo ndiyo sababu ya Walawi kutokuwa na sehemu wala urithi miongoni mwa ndugu zao; Bwana ndiye urithi wao, kama Bwana Mungu wao alivyowaambia.)
Kwa hiyo Lawi hawana sehemu wala urithi wa nchi pamoja na ndugu zake; Yahwe ni urithi wao, kama Yahwe Mungu wenu alizungumza naye)
10 Basi nilikaa mlimani kwa siku arobaini usiku na mchana, kama nilivyofanya mara ya kwanza, pia Bwana alinisikiliza hata wakati huu. Haikuwa nia yake kuwaangamiza.
“Nilibaki kwenye mlima kama ilivyokuwa mara ya kwanza, siku arobaini na usiku arobaini. Yahwe alinisikiliza wakati huo pia; Yahwe hakutaka kukuangamiza.
11 Bwana akaniambia, “Nenda, ukawaongoze watu katika njia yao ili kwamba waweze kuingia na kuimiliki nchi ile niliyowaapia baba zao kuwapa.”
Yahwe alisema nami, “Inuka, nenda mbele ya watu uwaongoze katika safari yao; wataingia na kumiliki nchi ambayo niliapa kwa mababu zao kuwapa.'
12 Na sasa, ee Israeli, Bwana Mungu wako anataka nini kwako ila kumcha Bwana Mungu wako, kwenda katika njia zake, kumpenda na kumtumikia Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote,
Sasa, Israeli, Yahwe Mungu wenu ataka nini kwenu, isipokuwa hofu ya Yahwe Mungu wenu, kutembea katika njia zake zote, kumpenda yeye, na kumwabudu Yahwe Mungu wenu kwa moyo wenu wote na roho yenu yote.
13 na kuyashika maagizo ya Bwana na amri zake ninazokupa leo kwa mafanikio yako mwenyewe?
Kuzishika amri za Yahwe, na maagizo ambayo ninawaamuru ninyi leo kwa ajili ya uzuri wenu?
14 Mbingu, hata mbingu za juu sana, dunia na kila kitu kilichomo ndani yake, ni mali ya Bwana Mungu wako.
Tazama, kwa Yahwe Mungu wenu mbingu ni zake na mbingu za mbingu, dunia, vyote vilivyomo.
15 Hata hivyo Bwana alikuwa na shauku na baba zako, akawapenda na akawachagua ninyi, wazao wao, kuliko mataifa yote, kama ilivyo leo.
Yahwe peke alichukua furaha kwa baba zenu ili kwamba awapende, na aliwachagua ninyi, wazao wao, baada yao, zaidi kuliko ya watu wengine wowote, kama afanyavyo leo.
16 Kwa hiyo tahirini mioyo yenu, na msiwe na shingo ngumu tena.
Kwa hiyo basi wataili govi la mioyo yao, na msiwe wakaidi tena.
17 Kwa kuwa Bwana Mungu wenu ni Mungu wa miungu na Bwana wa mabwana, Mungu mkuu, mwenye uweza na wa kutisha, ambaye hana upendeleo na hapokei rushwa.
Kwa kuwa Yahwe Mungu wenu, ni Mungu wa miungu na Bwana wa bwana, Mungu mkuu, mwenye nguvu na wakutisha, ambaye hapendelei yeyote na hapokei rushwa-
18 Huwapigania yatima na wajane, humpenda mgeni, akimpa chakula na mavazi.
Hutekeleza haki kwa yatima na wajane, na huonesha upendo kwa mgeni kwa kumpa chakula na mavazi.
19 Nanyi wapendeni wageni, kwa kuwa ninyi wenyewe mlikuwa wageni huko Misri.
Kwa hiyo basi mpende mgeni; kwa kuwa mlikuwa wageni kutoka nchi ya Misri.
20 Mche Bwana Mungu wako na umtumikie yeye. Shikamana naye kwa uthabiti na kuapa kwa jina lake.
Mtamche Yahwe Mungu wenu yeye mtamwabudu. Mtashikamana kwake, na kwa jina lake mtaapa.
21 Yeye ni sifa yako; yeye ni Mungu wako, ambaye alikutendea yale maajabu makubwa na ya kutisha uliyoyaona kwa macho yako mwenyewe.
Yeye ni sifa yenu, ni Mungu wenu, ambaye amefanya kwa ajili yenu haya mambo makuu na kutisha, ambayo macho yenu yameyaona.
22 Baba zako walioshuka kwenda Misri jumla yao walikuwa sabini, na sasa Bwana Mungu wako amekufanya wengi kama nyota za angani.
Baba zako walienda Misri kama watu sabini; sasa Yahwe Mungu wako amekufanya wewe kuwa wengi kama nyota za mbinguni.

< Torati 10 >