< Amosi 6 >

1 Ole wenu ninyi mnaostarehe na kuridhika katika Sayuni, na ninyi mnaojisikia salama juu ya Mlima Samaria, ninyi watu mashuhuri wa taifa lililoendelea kuliko mataifa mengine, ambao watu wa Israeli wanawategemea!
Ole wao wanaostarehe katika Sayuni, na kwa wale ambao wameokoka katika nchi ya mlima wa Samaria, watu mashuhuri bora wa mataifa, ambao nyumba ya Israeli huja kwa ajili ya msaada!
2 Nendeni Kalne mkaone kutoka huko; mwende hadi Hamathi iliyo kuu, kisha mshuke hadi Gathi ya Wafilisti. Je, wao ni bora kuliko falme zenu mbili? Je, nchi yao ni kubwa kuliko yenu?
Viongozi wenu husema, “Pita kwenda Kalne na mkatazame; kutoka huko nendeni hadi Hamathi, mji mkubwa; kisha nendeni chini hata Gathi ya Wapelestina. Je ni wabora kuliko falme zenu mbili? Je kuna mpaka mkubwa kuliko mpaka wenu?”
3 Mnaiweka mbali siku iliyo mbaya na kuleta karibu utawala wa kuogofya.
Ole wao wale waiwekao siku ya majanga na kufanya ufalme kuwa kinyume kusogea karibu.
4 Ninyi mnalala juu ya vitanda vilivyofunikwa kwa pembe za ndovu, na kujinyoosha juu ya viti vya fahari. Mnajilisha kwa wana-kondoo wazuri na ndama walionenepeshwa.
Wamelala juu ya vitanda vya pembe na kupumzika juu ya viti vyao. Wakala wana kondoo kutoka kwenye kundi na ndama kutoka kwenye zizi.
5 Ninyi mnapiga vinubi kama Daudi, huku mkitunga nyimbo za vinanda mbalimbali.
Wanaimba nyimbo za kijinga kwenye muziki wa kinubi; wanatunga kwenye vyombo kama vya Daudi.
6 Mnakunywa mvinyo kwa bakuli zilizojazwa, na mnajipaka mafuta mazuri, lakini hamhuzuniki kwa maangamizi ya Yosefu.
Wanakunywa mvinyo kutoka kwenye bakuli na kujipaka mafuta wenyewe kwa mafuta ya marahamu, lakini hawahuzuniki juu ya mateso ya Yusufu.
7 Kwa hiyo mtakuwa miongoni mwa watu wa kwanza kwenda uhamishoni; karamu zenu na kustarehe kutakoma.
Hivyo sasa watakwenda utumwani pamoja na watumwa wakwanza, na kelele za hao waliojinyoosha zitapita.
8 Bwana Mwenyezi ameapa kwa nafsi yake mwenyewe: Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote asema: “Nachukia kiburi cha Yakobo, nachukia ngome zake; nitautoa mji wao na kila kitu kilichomo ndani mwake.”
“Mimi Bwana Yahwe, nimeapa kwa nafsi yangu -hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo, Mungu wa majeshi, naizira fahari ya Yakobo; nachukia boma zake. Kwa hiyo nitautoa huo mji pamoja vyote vilivyomo humo.”
9 Kama watu kumi watabaki katika nyumba moja, wao pia watakufa.
Itakuja kuhusu kwamba kama kuna wanaume kumi waliobakia kwenye nyumba moja, watakufa.
10 Kama jamaa ambaye atachoma miili akija ili kuitoa nje ya nyumba, na kumuuliza yeyote ambaye bado anajificha humo, “Je, yuko mtu yeyote pamoja nawe?” Naye akisema, “Hapana,” ndipo atakaposema, “Nyamaza kimya! Haturuhusiwi kutaja jina la Bwana.”
Wakati ndugu wa mtu huyo atakapokuja kuchukua miili yao-yule ambaye awachomaye baada ya kuleta maiti katika nyumba-kama akisema kwa mtu katika nyumba, “Je kuna mtu yuko pamoja nawe?” Vipi kama yule akisema, “Hapana.” Kisha atasema, “Kaa kimya, kwa kuwa hatulitaja jina la Yahwe.”
11 Kwa kuwa Bwana ameamuru, naye atabomoa jumba kubwa vipande vipande na nyumba ndogo vipande vidogo vidogo.
Tazama, Yahwe atatoa amri, na nyumba kubwa itapigwa kuwa vipande vipande, na nyumba ndogo kuwa na nyufa.
12 Je, farasi waweza kukimbia kwenye miamba mikali? Je, aweza mtu kulima huko kwa maksai? Lakini mmegeuza haki kuwa sumu na matunda ya uadilifu kuwa uchungu:
Je farasi watakimbia juu ya mteremko wa miamba? Je mtu atalima huko na ng'ome? Bado mmegeuza haki kuwa sumu na tunda la haki kuwa uchungu.
13 ninyi mnaoshangilia kushindwa kwa Lo-Debari na kusema, “Je, hatukuteka Karnaimu kwa nguvu zetu wenyewe?”
Ninyi mnaofurahia juu ya Lo Debari, msemao, “Je hatukuchukua Karnaimu kwa nguvu zetu wenyewe?”
14 Maana Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote asema, “Nitainua taifa dhidi yenu, ee nyumba ya Israeli, nalo litawatesa kuanzia Lebo-Hamathi hadi Bonde la Araba.”
Lakini tazama, nitainua juu yenu taifa, nyumba ya Israeli-hivi ndivyo asemavyo Bwana Yahwe, Mungu wa majeshi. Watawatesa ninyi kutoka Lebo Hamathi hata kijito cha Araba.”

< Amosi 6 >