< Matendo 19 >
1 Apolo alipokuwa huko Korintho, Paulo alisafiri sehemu za bara, akafika Efeso. Huko akawakuta wanafunzi kadhaa,
Ikawa kwamba Apolo alipokuwa Korintho, Paulo akapita nyanda za juu na kufika katika mji wa Efeso, na akakuta wanafunzi kadhaa huko.
2 akawauliza, “Je, mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini?” Wakajibu, “Hapana, hata hatukusikia kuwa kuna Roho Mtakatifu.”
Paulo akawaambia, “Je, mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini?” Wakamwambia, “Hapana, hatukuweza hata kusikia kuhusu Roho Mtakatifu.”
3 Ndipo Paulo akawauliza, “Je, mlibatizwa kwa ubatizo gani?” Wakajibu, “Kwa ubatizo wa Yohana.”
Paul alisema, “Sasa ninyi mlibatizwaje?” Wakasema, “Katika ubatizo wa Yohana.
4 Paulo akasema, “Ubatizo wa Yohana ulikuwa wa toba, aliwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja baada yake, yaani, Yesu.”
Basi Paulo akajibu, “Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba. Akawaambia wale watu kwamba wanapaswa kumwamini yule ambaye angekuja baada yake, yaani, Yesu.”
5 Waliposikia haya, wakabatizwa katika jina la Bwana Yesu.
Watu waliposikia habari hii, wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesu.
6 Paulo alipoweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akawashukia, nao wakanena kwa lugha mpya na kutabiri.
Na ikawa Paulo alipoweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao na wakaanza kunena kwa lugha na kutabiri.
7 Walikuwa kama wanaume kumi na wawili.
Jumla yao walikuwa wanaume wapatao kumi na wawili.
8 Paulo akaingia katika sinagogi na kunena humo kwa ujasiri kwa muda wa miezi mitatu, akijadiliana na watu na kuwashawishi katika mambo ya Ufalme wa Mungu.
Paulo alienda katika sinagogi akanena kwa ujasiri kwa muda wa miezi mitatu. Alikuwa akiongoza majadiliano na kuwavuta watu kuhusu mambo yanayohusu ufalme wa Mungu.
9 Lakini baadhi yao walikaidi. Walikataa kuamini, na wakakashifu ujumbe wake mbele ya umati wa watu. Basi Paulo aliachana nao. Akawachukua wanafunzi naye, akahojiana nao kila siku katika darasa la Tirano.
Lakini Wayahudi wengine walikuwa wakaidi na wasiotii, walianza kusema mabaya kuhusu njia ya Kristo mbele ya umati. Basi Paulo aliachana nao na akawatenga waaminio mbali nao. Naye alianza kuongea kila siku katika ukumbi wa Tirano.
10 Jambo hili likaendelea kwa muda wa miaka miwili, kiasi kwamba Wayahudi na Wayunani wote walioishi huko Asia wakawa wamesikia neno la Bwana.
Hii iliendelea kwa miaka miwili, kwa hiyo wote waliokuwa wanaishi katika Asia walisikia neno la Bwana, wote Wayahudi na Wayunani.
11 Mungu akafanya miujiza mingi isiyo ya kawaida kwa mkono wa Paulo,
Mungu alikuwa akifanya matendo makuu kwa mikono ya Paulo,
12 hivi kwamba leso au vitambaa vilivyokuwa vimegusa mwili wa Paulo viliwekwa juu ya wagonjwa, nao wakapona magonjwa yao, na pepo wachafu wakawatoka.
kwamba hata wagonjwa waliponywa, na roho chafu waliwatoka, wakati walipochukua leso na nguo zilizotoka mwilini mwa Paulo.
13 Basi baadhi ya Wayahudi wenye kutangatanga huku na huko wakitoa pepo wachafu wakajaribu kutumia jina la Bwana Yesu wale wenye pepo wakisema, “Kwa jina la Yesu, yule anayehubiriwa na Paulo, nakuamuru utoke.”
Lakini palikuwapo Wayahudi wapunga pepo wakisafiri kupitia eneo hilo, wakilitumia jina la Yesu kwa ajili ya matumizi yao wenyewe. Wakiwaambia wale walikuwa na pepo wachafu; Wakisema, “Ninawaamuru mtoke kwa jina la Yesu ambaye Paulo anamhubiri.”
14 Wana saba wa Skewa, Myahudi aliyekuwa kiongozi wa makuhani, walikuwa wanafanya hivyo.
Waliofanya haya walikuwa wana saba wa kuhani Mkuu wa Kiyahudi, Skewa.
15 Lakini pepo mchafu akawajibu, “Yesu namjua na Paulo pia namjua, lakini ninyi ni nani?”
Roho wachafu wakawajibu, “Yesu namjua, na Paulo namjua; lakini ninyi ni nani? “
16 Kisha yule mtu aliyekuwa na pepo mchafu akawarukia, akawashambulia vikali, akawashinda nguvu wote, wakatoka ndani ya ile nyumba wakikimbia wakiwa uchi na wenye majeraha.
Yule roho mchafu ndani ya mtu akawarukia wapunga pepo na akawashinda nguvu na kuwapiga. Ndipo wakakimbia kutoka ile nyumba wakiwa uchi na kujeruhiwa.
17 Habari hii ikajulikana kwa Wayahudi wote na Wayunani waliokaa Efeso, hofu ikawajaa wote, nalo jina la Bwana Yesu likaheshimiwa sana.
Jambo hili likajulikana kwa wote, Wayahudi na Wayunani, ambao waliishi huko Efeso. Wakawa na hofu sana, na jina la Bwana likazidi kuheshimiwa.
18 Wengi wa wale waliokuwa wameamini wakati huu wakaja na kutubu waziwazi kuhusu matendo yao maovu.
Pia, wengi wa waumini walikuja na wakaungama na wakidhihirisha matendo mabaya waliyoyafanya.
19 Idadi kubwa ya wale waliofanya mambo ya uganga wakaleta vitabu vyao na kuviteketeza kwa moto hadharani. Walipofanya hesabu ya thamani ya vitabu vilivyoteketezwa ilikuwa drakma 50,000 za fedha.
Wengi waliokuwa wakifanya uganga wakakusanya vitabu vyao, wakavichoma mbele ya kila mtu. Wakati wao walipohesabu thamani ya vitu hivyo, ilikuwa vipande hamsini elfu vya fedha.
20 Hivyo neno la Bwana likaenea sana na kuwa na nguvu.
Hivyo Neno la Bwana likaenea kwa upana sana katika nguvu.
21 Baada ya mambo haya kutukia, Paulo akakusudia rohoni kwenda Yerusalemu kupitia Makedonia na Akaya. Akasema, “Baada ya kufika huko, yanipasa pia kwenda Rumi.”
ya Paulo kukamilisha huduma yake kule Efeso, Roho akamwongoza kwenda Yerusalemu kupitia Makedonia na Akaya; Akasema, “Baada ya kuwako huko, yanipasa kuiona Rumi pia.”
22 Hivyo akatuma wasaidizi wake wawili, Timotheo na Erasto, waende Makedonia, wakati yeye mwenyewe alibaki kwa muda kidogo huko Asia.
Paul akawatuma Makedonia wanafunzi wake wawili, Timotheo na Erasto, ambao walikuwa wamemsaidia. Lakini yeye mwenyewe akabaki Asia kwa muda.
23 Wakati huo huo pakatokea dhiki kubwa kwa sababu ya Njia ile ya Bwana.
Wakati huo kulitokea ghasia kubwa huko Efeso kuhusu ile Njia.
24 Mtu mmoja jina lake Demetrio mfua fedha aliyekuwa akitengeneza vinyago vya fedha vya Artemi na kuwapatia mafundi wake biashara kubwa,
Sonara mmoja jina lake Demetrio, ambaye aliyetengeneza visanamu vya fedha vya mungu Diana, alileta biashara kubwa kwa mafundi.
25 aliwaita pamoja watu wengine waliofanya kazi ya ufundi kama yake na kusema, “Enyi watu, mnajua ya kuwa utajiri wetu unatokana na biashara hii!
Hivyo akawakusanya mafundi wa kazi hiyo na kusema, “Waheshimiwa, mnajua kwamba katika biashara hii sisi tunaingiza pesa nyingi.
26 Pia ninyi mmeona na kusikia jinsi ambavyo si huku Efeso peke yake lakini ni karibu Asia yote, huyu Paulo amewashawishi na kuvuta idadi kubwa ya watu kwa kusema kuwa miungu iliyotengenezwa na watu si miungu.
Mnaona na kusikia kwamba, si tu hapa Efeso, bali karibia Asia yote, huyu Paulo amewashawishi na kuwageuza watu wengi. Anasema kwamba hakuna miungu ambayo imefanywa kwa mikono.
27 Kwa hiyo kuna hatari si kwa kazi yetu kudharauliwa tu, bali pia hata hekalu la mungu mke Artemi, aliye mkuu, anayeabudiwa Asia yote na ulimwengu wote, litakuwa limepokonywa fahari yake ya kiungu.”
Na si tu iko hatari kwamba biashara yetu itakuwa haihitajiki tena, lakini pia na hekalu la mungu mke aliye mkuu Diana anaweza kuchukuliwa kuwa hana maana. Tena angeweza hata kupoteza ukuu wake, yeye ambaye Asia na dunia humwabudu.”
28 Waliposikia maneno haya, wakaghadhibika, wakaanza kupiga kelele, “Artemi wa Waefeso ni mkuu!”
Waliposikia haya, walijawa na hasira na wakapiga kelele, wakisema, “Diana wa Waefeso ni mkuu.”
29 Mara mji wote ukajaa ghasia. Wakawakamata Gayo na Aristarko, watu wa Makedonia waliokuwa wakisafiri pamoja na Paulo, na watu wakakimbilia katika ukumbi wa michezo kama mtu mmoja.
Mji wote ukajaa ghasia, na watu wakakimbia pamoja ndani ya ukumbi wa michezo. wakawakamata wasafiri wenzake na Paulo, Gayo na Aristariko, waliotoka Makedonia.
30 Paulo akataka kuingia katikati ya umati huo, lakini wanafunzi hawakumruhusu.
Paulo alitaka kuingia katika umati wa watu, lakini wanafunzi walimzuia.
31 Hata baadhi ya viongozi wa sehemu ile, waliokuwa rafiki zake Paulo, wakatuma watu wakitamani asiingie katika ule ukumbi.
Pia, baadhi ya maafisa wa mkoa wa Asia ambao walikuwa marafiki zake wakampelekea ujumbe kwa nguvu kumwomba asiingie katika ukumbi wa michezo.
32 Ule umati ulikuwa na taharuki. Wengine walikuwa wakipiga kelele, hawa wakisema hili na wengine lile. Idadi kubwa ya watu hawakujua hata ni kwa nini walikuwa wamekusanyika huko.
Baadhi ya watu walikuwa wakisema kitu hiki na wengine jambo lile, kwa sababu umati wa watu ulikuwa umechanganyikiwa. Wengi wao hawakuweza hata kujua kwa nini walikuja pamoja.
33 Wayahudi wakamsukumia Aleksanda mbele na baadhi ya watu kwenye ule umati wakampa maelekezo. Akawaashiria kwa mkono ili watulie aweze kujitetea mbele ya watu.
Wayahudi wakamleta Iskanda nje ya umati wa watu na kumuweka juu mbele ya watu. Iskanda akatoa ishara kwa mkono wake kutoa maelezo kwa watu.
34 Lakini walipotambua kwamba alikuwa Myahudi, wote wakapiga kelele kwa sauti moja kwa karibu muda wa saa mbili, wakisema, “Artemi wa Efeso ni mkuu!”
Lakini walipotambua kuwa yeye ni Myahudi, wote wakapiga kelele kwa sauti moja kwa muda wa saa mbili, “Diana ni mkuu wa Wafeso.”
35 Baadaye karani wa mji akaunyamazisha ule umati wa watu na kusema, “Enyi watu wa Efeso, je, ulimwengu wote haujui ya kuwa mji wa Efeso ndio unaotunza hekalu la Artemi aliye mkuu na ile sanamu yake iliyoanguka kutoka mbinguni?
Baada ya karani wa mji kuunyamazisha umati, alisema, 'Enyi wanaume wa Efeso, ni nani asiyejua kwamba mji huu wa Efeso ni mtunzaji wa hekalu la Diana mkuu na ile picha ilivyoanguka kutoka mbinguni?
36 Kwa hiyo, kwa kuwa mambo haya hayakanushiki, inawapasa mnyamaze na wala msifanye lolote kwa haraka.
Kuona Basi kwamba mambo haya hayatawezekana, tunapaswa kuwa na utulivu na msifanye chochote kwa haraka.
37 Kwa kuwa mmewaleta hawa watu hapa, ingawa hawajaiba hekaluni wala kumkufuru huyu mungu wetu wa kike.
Kwa maana mmewaita watu hawa hapa mahakamani ambao si wezi wa hekalu wala si wenye kumkufuru mungu wetu mke.
38 Basi, ikiwa Demetrio na mafundi wenzake wana jambo zito dhidi ya mtu yeyote, mahakama ziko wazi na wasaidizi wa mwakilishi wa mtawala. Wanaweza kufungua mashtaka.
Kwa hiyo, kama Demetrio na mafundi waliopamoja naye wana mashtaka dhidi ya mtu yeyote, mahakama ziko wazi na maliwali wapo. Na waletwe mbele ya shauri.
39 Lakini kama kuna jambo jingine lolote zaidi mnalotaka kulileta, itabidi lisuluhishwe katika kusanyiko halali.
Lakini kama wewe ukitafuta chochote kuhusu mambo mengine, yatashughurikiwa katika kikao halali.
40 Kama ilivyo sasa, tuko hatarini kushtakiwa kwa kufanya ghasia kwa sababu ya tukio la leo. Kwa kuwa hakuna sababu tutakayoweza kutoa kuhalalisha msukosuko huu.”
Kwa kweli tuko katika hatari ya kutuhumiwa kuhusu ghasia siku hii. Hakuna sababu ya machafuko haya, na hatutakuwa na uwezo wa kuyaeleza.
41 Baada ya kusema haya akavunja mkutano.
Baada ya kusema haya, aliwatawanya makutano.