< Matendo 13 >

1 Katika kanisa huko Antiokia ya Shamu walikuwako manabii na walimu, yaani: Barnaba, Simeoni aitwaye Nigeri, Lukio Mkirene, Manaeni aliyekuwa amelelewa pamoja na Mfalme Herode Agripa, na Sauli.
Nambeambe katika likanisa lya Antiokia, pabile na baadhi ya manabii na baalimu. Babile Barnaba, Simeoni(ywakemwa Nigeri). Lukio ba Kirene, Manaeni (nongowe abile wa myai kwaa Herode kiongozi wa mkoa), na Sauli.
2 Walipokuwa wakimwabudu Bwana na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, “Nitengeeni Sauli na Barnaba kwa kazi ile maalum niliyowaitia.”
Pababile bakimwabudu Ngwana na kufunga, Roho Mtakatifu kabaya, “Munitengee pembeni Barnaba na Sauli, baipange kazi yaanibakemule kuipanga.”
3 Ndipo baada ya kufunga na kuomba, wakawawekea mikono yao na wakawatuma waende zao.
Baada ya likanisa kufunga, kuloba na kubeka maboko gabe nnani ya bandu aba, batibaleka bayende.
4 Hivyo, wakiwa wametumwa na Roho Mtakatifu, wakashuka kwenda Seleukia na kutoka huko wakasafiri baharini mpaka kisiwa cha Kipro.
Kwa eyo Barnaba na Sauli batimweshimu Roho Mtakatifu na batiuluka kuelekea Seleukia; boka kolyo balisafiri mu'bahari kuyenda kisiwa cha Kipro.
5 Walipowasili katika mji wa Salami, wakahubiri neno la Mungu katika sinagogi la Wayahudi. Pia walikuwa na Yohana Marko kuwa msaidizi wao.
Pababile katika mji ba Salami, batilitangaza neno lya Nnongo mu'masinagogi ga Ayahudi. Babile pamope ni Yohana Marko kati msaidizi wabe.
6 Walipokwisha kupita katika nchi zote hizo wakafika Pafo, ambapo walikutana na Myahudi mmoja mchawi aliyekuwa nabii wa uongo, jina lake Bar-Yesu.
Pabayenda mu'kisiwa chote mpaka Pafo, bakwembine na mundu fulani mwaabe, Myahudi nabii wa ubocho, ambaye lina lyake lyabile Bar Yesu.
7 Mtu huyu alikuwa pamoja na Sergio Paulo, mtu mwenye hekima aliyekuwa msaidizi wa mwakilishi wa mtawala wa kile kisiwa. Sergio Paulo akawaita Sauli na Barnaba akitaka kusikia neno la Mungu.
Mwaabe yolo atishirikiana na Liwali Sergio Paulus, ywabile mundu ywaabile na malango. Mundu yolo atibaarika Barnaba na Sauli, kwa mana atipala kuliyowa neno lya Nnongo.
8 Lakini Elima yule mchawi (hii ndiyo maana ya jina lake), aliwapinga Barnaba na Sauli na kujaribu kumpotosha yule mkuu wa kile kisiwa aiache imani.
Lakini Elima “yolo mwaabe” (alee nga lina lyake lyatitafsiriwa) atibapinga; ajaribie kumgeuza yolo liwali aboke mu'imani.
9 Ndipo Sauli, ambaye pia aliitwa Paulo, akiwa amejawa na Roho Mtakatifu, akamkazia macho Elima huyo mchawi,
Lakini Sauli ywakemwa Paulo, abile atijazwa na Roho Mtakatifu, kamtumbulya minyo
10 akamwambia, “Ewe mwana wa ibilisi, wewe ni adui wa kila kilicho haki! Umejaa kila aina ya udanganyifu na ulaghai. Je, hutaacha kuzipotosha njia za Bwana zilizonyooka?
no baya “Wenga wa mwana wa ibilisi, utwelilwe na aina zote za udanganyifu na udhaifu. Wenga ni adui wa kila aina ya haki. Ukoma kwaa kuzigeuza ndela za Ngwana, zazinyoka, je walowa weza?
11 Nawe sasa sikiliza, mkono wa Bwana u dhidi yako. Utakuwa kipofu, wala hutaona jua kwa muda.” Mara ukungu na giza vikamfunika, naye akaenda huku na huko akitafuta mtu wa kumshika mkono ili amwonyeshe njia.
Nambeambe linga, luboko lwa Ngwana libile nnani yako, na upangika ipofu. Walowa libonekeya kwaa liumu kwa muda”mara yimo ukungu na libendo lyatomboka nnani ya Elimas; atumbwi zunguka palyo aaloba bandu bamwongoze kwa kunkamwa luboko.
12 Yule mkuu wa kile kisiwa alipoona yaliyotukia, akaamini kwa sababu alistaajabishwa na mafundisho kuhusu Bwana.
Baada ya liwali kubona chakipangike, aaminiya, kwa mana atishangala kwa mapundisho kuhusu Ngwana.
13 Kisha Paulo na wenzake wakasafiri toka Pafo wakafika Perga huko Pamfilia. Lakini, Yohana Marko akawaacha huko, akarejea Yerusalemu.
Nambeambe Paulo na mbwiga bake batisafiri mu'mase boka Pafo na baikite Perge katika Pamfilia. Lakini Yohana abalekite na kukerebuka Yerusalemu.
14 Kutoka Perga wakaendelea hadi Antiokia ya Pisidia. Siku ya Sabato wakaingia ndani ya sinagogi, wakaketi.
Paulo ni mbwiga wake batisafiri na baikite Antiokia ya Pisidia. Kolyo batiyenda mu'lisinagogi lisoba lya Sabato na tama pae.
15 Baada ya Sheria ya Mose na Kitabu cha Manabii kusomwa, viongozi wa sinagogi wakawatumia ujumbe wakisema, “Ndugu, kama mna neno la kuwafariji watu hawa, tafadhali lisemeni.”
Baada ya kuisoma saliya ya manabii, viongozi ba lisinagogi batumite ujumbe kababaya, “Alongo, mana mubile na ujumbe wa kutia mwoyo bandu pano, muubaye”
16 Paulo akasimama, akawapungia mkono na kusema: “Enyi wanaume wa Israeli na ninyi nyote mnaomcha Mungu.
Kwa eyo Paulo kayema na kubapungia luboko; kabaya, “Analome ba Israeli na mwenga mwamuheshimia Nnongo, sikilizeni.
17 Mungu wa watu hawa wa Israeli aliwachagua baba zetu, akawafanya kustawi walipokuwa huko Misri, kwa uwezo mwingi akawaongoza na kuwatoa katika nchi ile.
Nnongo wa aba bandu ba Israeli awachawi tate bitu na kuwapanga bandu banyansima batami katika nchi Misri, na kwa luboko lwake kuinuliwa na kubakengama panja yake.
18 Kwa muda wa miaka arobaini alivumilia matendo yao walipokuwa jangwani.
Kwa miaka arobaini atibavumilia mu'lijangwa.
19 Naye baada ya kuyaangamiza mataifa saba waliokuwa wakiishi katika nchi ya Kanaani, akawapa Waisraeli nchi yao iwe urithi wao.
Baada ya kugaharibia mataifa saba katika nchi ya Kaanani, abapeya bandu bitu nchi yabe kwa urithi.
20 Haya yote yalichukua kama muda wa miaka 450. “Baada ya haya, Mungu akawapa waamuzi mpaka wakati wa nabii Samweli.
Matendo aga gote gapangike zaidi ya miaka mia ncheche na hamsini. Baada ya ilebe yelo yote, Nnongo abapeile baamuzi mpaka Samweli nabii.
21 Ndipo watu wakaomba wapewe mfalme, naye Mungu akawapa Sauli mwana wa Kishi wa kabila la Benyamini, aliyetawala kwa miaka arobaini.
Baada ya aga, bandu batinloba mpwalume, nga nyoo Nnongo abapea Sauli mwana wa Kishi, mundu wa likabila lya Benjamini, kuwa mpwalume kwa miaka arobaini.
22 Baada ya kumwondoa Sauli katika ufalme, akawainulia Daudi kuwa mfalme wao. Mungu pia alimshuhudia, akisema, ‘Nimemwona Daudi mwana wa Yese, mtu anayeupendeza moyo wangu, atakayetimiza mapenzi yangu yote.’
Boka po baada ya Nnongo kumwondoa mpwalume, atimwinua Daudi kuwa mplwalume wabe. Ibile ni kuhusu Daudi panga Nnongo kabaya, “Nimpatike Daudi mwana wa Yese kiwa mundu ywaapendezwaye na mwoyo wango; ambaye alowa panga kila kilebe chanikipendile.'
23 “Kutoka uzao wa mtu huyu, Mungu amewaletea Israeli Mwokozi Yesu, kama alivyoahidi.
Boka mu'ukoo ba mundu yolo Nnongo atiiletya Israeli mkochopoli, Yesu, kati yaatiahidi kupanga.
24 Kabla ya kuja kwa Yesu, Yohana alihubiri toba na ubatizo kwa watu wote wa Israeli.
Alee litumbwile pangika, kabla ya Yesu kuisa, Yohana kwanza atitangaza ubatizo wa toba kwa bandu bote ba Israeli.
25 Yohana alipokuwa anakamilisha kazi yake, alisema: ‘Ninyi mnadhani mimi ni nani? Mimi si yeye. La hasha, lakini yeye yuaja baada yangu, ambaye mimi sistahili kufungua kamba za viatu vya miguu yake.’
Ni ywembe Yohana paabile atimaliza kazi yake, abayite,'Mwawaza nenga na nyai? nenga na yolo kwaa. Lakini muisikilize, yolo ywaisa kunchogo yango, nastahili kwaa hata legeza ilatu ya magolo gake.'
26 “Ndugu zangu, wana wa Abrahamu, nanyi watu wa Mataifa mnaomcha Mungu, ujumbe huu wa wokovu umeletwa kwetu.
Alongo, bana ba ukolo ba Abrahamu, na balo ambao kati yinu mwamwabudu Nnongo, ni kwa ajili yitu panga ujumbe woo wa ukombozi utumilwe.
27 Kwa sababu wakaao Yerusalemu na viongozi wao hawakumtambua wala kuelewa maneno ya manabii yasomwayo kila Sabato, bali waliyatimiza maneno hayo kwa kumhukumu yeye.
Kwa balo batama Yerusalemu, ba batawala babe, bantangite kwa kwa uhalisia, na wala bautangite kwaa ujumbe ba manabii abao husomwa kila Sabato; kwa eyo batiutimiza ujumbe wa manabii kwa kumhukumu kiwo Yesu.
28 Ijapokuwa hawakupata sababu yoyote ya kumhukumu kifo, walimwomba Pilato aamuru auawe.
Japokuwa bapatike kwaa sababu inoite kwa kiwo nkati yake, batinloba Pilato amulage.
29 Walipokwisha kufanya yale yote yaliyoandikwa kumhusu, walimshusha kutoka msalabani na kumzika kaburini.
Payomwile makowe gote yaandikilwe kuhusu ywembe, batiuuluya yega yake boka mu'nkongo na kagonja mu'likaburi.
30 Lakini Mungu alimfufua kutoka kwa wafu.
Lakini Nnongo atimfufua boka kwa bandu ba kiwo.
31 Naye kwa siku nyingi akawatokea wale waliokuwa pamoja naye kuanzia Galilaya hadi Yerusalemu. Nao sasa wamekuwa mashahidi wake kwa watu wetu.
Atibonekana kwa masoba ganyansima kwa balo bayenda pamope ni ywembe boka Galilaya yenda Yerusalemu. Bandu aba nambeambe nga mashaidi ba bandu.
32 “Nasi tunawaletea habari njema, kwamba yale Mungu aliyowaahidi baba zetu
Nga nyo twaletya habari njema kuhusu ahadi yawapeilwe apindo bitu.
33 sasa ameyatimiza kwetu sisi watoto wao, kwa kumfufua Yesu, kama ilivyoandikwa katika Zaburi ya pili: “‘Wewe ni Mwanangu; leo mimi nimekuzaa.’
Nnongo abekite ahadi yee kwitu, bana babe, katika lee atimfufua Yesu na kukerebuka kae katika ukoto. Alee liandikilwe kae katika Zaburi ya pili;'Wenga mwana wango, leno nibile Tate bako'
34 Kwa kuwa Mungu alimfufua kutoka kwa wafu asioze kamwe, alitamka maneno haya: “‘Nitakupa wewe baraka takatifu zilizo za hakika nilizomwahidi Daudi.’
Kuhusu ukweli ni panga atimfufua boka mu'kiwo ili panga yega yake uharibike kwaa, atilongela nyoo:'Nalowa kukupeya utakatifu na baraza halisi za Daudi'
35 Kama ilivyosemwa mahali pengine katika Zaburi, “‘Hutamwacha Aliye Mtakatifu wako kuona uharibifu.’
Ayee nga sababu abaya katika Zaburi yenge,'Huruhusu kwaa mtakatifuwako kuubonekeya uozo.”
36 “Kwa maana Daudi akiisha kulitumikia kusudi la Mungu katika kizazi chake, alilala; akazikwa pamoja na baba zake na mwili wake ukaoza.
Kwa mana baada ya Daudi tumikiya mapenzi ga Nnongo katika ubeleki wake, agonjike, atigonja pamope na tate bake, na aubweni uharibifu,
37 Lakini yule ambaye Mungu alimfufua kutoka kwa wafu hakuona uharibifu.
Lakini ywafufuliwe na Nnongo aubweni kwaa uharibifu.
38 “Kwa hiyo ndugu zangu, nataka ninyi mjue kwamba kwa kupitia huyu Yesu msamaha wa dhambi unatangazwa kwenu.
Nga nyoo iyowanike kwinu, alongo, pitya mundu yolo, msamaha wa sambi watihubiriwa.
39 Kwa kupitia yeye, kila mtu amwaminiye anahesabiwa haki kwa kila kitu ambacho asingeweza kuhesabiwa haki kwa sheria ya Mose.
Kwa ywembe kila aminiye abalangilwa haki na makowe yote ambayo saliya ya Musa yawapeya kwaa.
40 Kwa hiyo jihadharini ili yale waliyosema manabii yasiwapate:
Nga nyo bai mube baangalifu panga kilebe saakilongela manabii kana kiboke kwinu.
41 “‘Angalieni, enyi wenye dhihaka, mkastaajabu, mkaangamie, kwa maana nitatenda jambo wakati wenu ambalo hamtasadiki, hata kama mtu akiwaambia.’”
'Linga, mwenga mubile na dharau, na mwamushangala na kuangamiya; kwa mana napanga kazi katika masoba yinu, Kazi ambayo mwaweza kwaa kuiamnia, hata mana mundu alowa kubaeleza.”
42 Paulo na Barnaba walipokuwa wakitoka nje ya sinagogi, watu wakawaomba wazungumze tena mambo hayo Sabato iliyofuata.
Muda Paulo na Barnaba babokite, bandu baalobite balongele maneno aga lisoba lya Sabato yenge.
43 Baada ya kusanyiko la Sinagogi kutawanyika, wengi wa Wayahudi na waongofu wa dini ya Kiyahudi wakawafuata Paulo na Barnaba, wakazungumza nao na kuwahimiza wadumu katika neema ya Mungu.
Muda mkutano wa lisinagogi pauyomwile thabiti batibakengama Paulo na Barnaba, ambao batilongela nabo na babahimiza bayendelee katika neema ya Nnongo.
44 Sabato iliyofuata, karibu watu wote wa mji walikuja kusikiliza neno la Bwana.
Sabato yenge, karibu mji mzima watikwembana kulisikiliza lineno lya Nnongo.
45 Lakini Wayahudi walipoona ule umati mkubwa wa watu walijawa na wivu, wakayakanusha maneno Paulo aliyokuwa akisema.
Bayahudi paababweni makutano, batolilwe ni wivu na longela maneno yagapinga ilebe yatilongelwa na Paulo na kuntukana.
46 Ndipo Paulo na Barnaba wakawajibu kwa ujasiri, wakisema, “Ilitupasa kunena nanyi neno la Mungu kwanza. Lakini kwa kuwa mmelikataa, mkajihukumu wenyewe kuwa hamstahili uzima wa milele, sasa tunawageukia watu wa Mataifa. (aiōnios g166)
Lakini Paulo na Barnaba batilongela kwa ujasiri no baya, “Ibile muhimu panga neno lya Nnongo lilongelwa kwanza kwinu. Kwa mana mwatilisukumiya kutalu boka kwinu nakuibona kuwa mwastahili kwaa ukoto wangayomoka, mulinge twalowakerebukya Mataifa. (aiōnios g166)
47 Kwa maana hili ndilo Bwana alilotuamuru: “‘Nimewafanya ninyi kuwa nuru kwa watu wa Mataifa, ili mpate kuuleta wokovu hadi miisho ya dunia.’”
Kati ambavyo Ngwana atituamuru, kabaya,'Niabekite mwenga kati bweya kwa bandu ba mataifa, panga mlete wokovu kwa pande zote za dunia.”
48 Watu wa Mataifa waliposikia haya wakafurahi na kulitukuza neno la Bwana; nao wote waliokuwa wamekusudiwa uzima wa milele wakaamini. (aiōnios g166)
Mataifa pabayowine lee, batipuraika na kulisifu neno lya Ngwana. Baingi batichauliwa kwa ukoto wangayomoka baliaminia. (aiōnios g166)
49 Neno la Bwana likaenea katika eneo lile lote.
Neno lya Ngwana lilienea nchi yote.
50 Lakini Wayahudi wakawachochea wanawake wenye kumcha Mungu, wenye vyeo pamoja na watu maarufu katika mji, wakachochea mateso dhidi ya Paulo na Barnaba na kuwafukuza kutoka eneo hilo.
Lakini Ayahudi batibasihi baliojitoa na anwawa muhimu, na viongozi wa mji. Aga yalichochea mateso dhidi ya Paulo na Barnaba na baliatupa panja ya mipaka ya mji.
51 Hivyo Paulo na Barnaba wakakungʼuta mavumbi ya miguu yao ili kuwapinga, nao wakaenda Ikonio.
Lakini Paulo na Barnaba batikung'uta vumbi lya magolo gabe. Boka po batiyenda katika mji wa Ikonia.
52 Wanafunzi wakajawa na furaha na Roho Mtakatifu.
Na banafunzi batweliwe na furaha pamope na Roho Mtakatifu.

< Matendo 13 >