< 2 Wathesalonike 2 >
1 Ndugu, kuhusu kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo na kukusanyika kwetu pamoja mbele zake, tunawasihi,
Sasa kuhusu kuja kwa Bwana wetu Yesu Kristo na kukusanywa pamoja ili tuwe naye: tunawaomba ninyi ndugu zetu,
2 msiyumbishwe kwa urahisi wala msitiwe wasiwasi na roho wala neno au barua inayosemekana kuwa imetoka kwetu, isemayo kwamba siku ya Bwana imekwisha kuwako.
kwamba msisumbuliwe wala kutabishwa kwa urahisi, kwa roho, au kwa ujumbe au kwa barua inayoonkana kuwa imetoka kwetu, ikisema ya kuwa siku ya Bwana tayari imekuja.
3 Mtu yeyote na asiwadanganye kwa namna yoyote kwa maana siku ile haitakuja mpaka uasi utokee kwanza, na yule mtu wa kuasi adhihirishwe, yule ambaye amehukumiwa kuangamizwa kabisa.
Mtu na asiwadanganye kwa namna yoyote. Kwa kuwa haitakuja mpaka lile anguko litokee kwanza na mtu wa uasi afunuliwe, yule mwana wa uharibifu.
4 Yeye atapingana na kujitukuza juu ya kila kitu kiitwacho Mungu au kinachoabudiwa, ili kujiweka juu katika Hekalu la Mungu, akijitangaza mwenyewe kuwa ndiye Mungu.
Huyu ndiye apingaye naye hujiinua mwenyewe akimpinga Mungu na chochote kinachoabudiwa. Na matokeo yake, hukaa kwenye hekalu la Mungu na kujionyesha yeye kuwa kama Mungu.
5 Je, hamkumbuki ya kwamba nilipokuwa pamoja nanyi niliwaambia mambo haya?
Je, hamkumbuki kuwa nilipokuwa nanyi niliwaambia juu ya mambo haya?
6 Nanyi sasa mnajua kinachomzuia, ili apate kudhihirishwa wakati wake utakapowadia.
Sasa mnajua kile kinachomzuia, ili kwamba aweze kufunuliwa kwa wakati sahihi utakapowadia.
7 Maana ile nguvu ya siri ya uasi tayari inatenda kazi, lakini yule anayeizuia ataendelea kufanya hivyo mpaka atakapoondolewa.
Kwa kuwa siri ya yule mtu mwenye kuasi inafanya kazi mpaka sasa, ila tu kuna anaye mzuia sasa mpaka atakapotolewa njiani.
8 Hapo ndipo yule mwasi atafunuliwa, ambaye Bwana Yesu atamteketeza kwa pumzi ya kinywa chake na kumwangamiza kabisa kwa utukufu wa kuja kwake.
Ndipo yule mwenye kuasi atakapofunuliwa, amabaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake. Bwana atamfanya kuwa si chochote kwa ufunuo wa ujio wake.
9 Kuja kwa yule mwasi kutaonekana kana kwamba ni kutenda kazi kwake Shetani ambaye hutumia nguvu zote, ishara, maajabu ya uongo,
Ujio wa yule mwenye kuasi utakuwa kwa sababu ya kazi ya shetani kwa nguvu zote, ishara na maajabu ya uongo,
10 na kila aina ya uovu kwa wale wanaoangamia kwa sababu walikataa kuipenda kweli wapate kuokolewa.
na uongo wote wenye udhalimu. Mambo haya yatakuwepo kwa wale wanaopotea, kwa sababu hawakuupokea upendo wa kweli kwa ajili ya kuokolewa kwao.
11 Kwa sababu hii, Mungu ameruhusu watawaliwe na nguvu ya udanganyifu, ili waendelee kuamini uongo,
Kwa sababu hiyo Mungu anawatumia kazi yenye uovu ili waamini uongo.
12 na wahukumiwe wote ambao hawakuiamini ile kweli, bali wamefurahia uovu.
Matokeo yake ni kwamba wote watahukumiwa, wale ambao hawakuamini ukweli bali wao hujifurahisha katika udhalimu.
13 Lakini imetupasa sisi kumshukuru Mungu daima kwa ajili yenu, ndugu mpendwao na Bwana, kwa sababu Mungu aliwachagua ninyi tangu mwanzo ili mwokolewe kwa kutakaswa na Roho kwa kuiamini kweli.
Lakini inatupasa tumshukuru Mungu kila mara kwa ajili yenu ndugu mpendwao na Bwana. Kwa sababu Bwana aliwachagua ninyi kama malimbuko ya wokovu kwa utakaso wa Roho na imani katika ile kweli.
14 Kwa kusudi hili Mungu aliwaita kwa njia ya kuhubiri kwetu Injili, ili mpate kushiriki katika utukufu wa Bwana Yesu Kristo.
Hiki ndicho alichowaitieni ninyi, kwamba kupitia injili muweza kuupata utukufu wa Bwana wetu Yesu Kristo.
15 Hivyo basi, ndugu wapendwa, simameni imara na myashike sana yale mafundisho tuliyowapa ikiwa ni kwa maneno ya kinywa au kwa barua.
Kwa hiyo, ndugu, simameni imara. Ueleweni ule utamaduni mliofundishwa, kwa neno au kwa barua yetu.
16 Bwana wetu Yesu Kristo mwenyewe na Mungu Baba yetu, aliyetupenda na kwa neema yake akatupatia faraja ya milele na tumaini jema, (aiōnios )
Sasa, Bwana wetu Yesu Kristo mwenyewe, na Mungu Baba yetu aliyetupenda na kutupa faraja ya milele na ujasiri mwema kwa ajili ya maisha yajayo kupitia neema, (aiōnios )
17 awafariji mioyo yenu na kuwaimarisha katika kila neno na tendo jema.
awafariji na kuifanya imara mioyo yenu katika kila neno na kazi njema.