< 2 Samweli 6 >

1 Tena Daudi akakusanya watu 30,000 wa Israeli waliochaguliwa.
Basi kwa mara nyingine Daudi akawakusanya wateuli wa Israeli, elfu thelathini.
2 Yeye na watu wake wote wakatoka Baala ya Yuda kulipandisha Sanduku la Mungu kutoka huko, linaloitwa kwa Jina, naam, jina la Bwana Mwenye Nguvu Zote, ambaye anaketi katika kiti cha enzi kati ya makerubi walioko juu ya hilo Sanduku.
Daudi akainuka na akaenda na watu wake wote waliokuwa pamoja naye kutoka Baala ulioko Yuda ili alilete sanduku la Mungu, liitwalo kwa jina la Yahwe wa majeshi, akaaye juu ya makerubi.
3 Wakaweka hilo Sanduku la Mungu juu ya gari jipya la kukokotwa na kulileta kutoka nyumba ya Abinadabu, iliyokuwa juu ya kilima. Uza na Ahio, wana wa Abinadabu, walikuwa wakiongoza hilo gari jipya la kukokotwa
Wakaliweka sanduku la Mungu juu ya mkokoteni mpya. Wakalitoa katika nyumba ya Abinadabu, iliyokuwa juu ya kilima. Uza na Ahio, wanawe, wakauongoza mkokoteni.
4 likiwa na Sanduku la Mungu juu yake, naye Ahio alikuwa anatembea akiwa mbele yake.
Wakautoa mkokoteni na sanduku la Mungu juu yake nyumbani mwa Abinadabu juu ya kilima. Ahio alikuwa ametangulia mbele ya sanduku.
5 Daudi na nyumba yote ya Israeli walikuwa wanacheza mbele za Bwana kwa nguvu zao zote, kwa nyimbo, vinubi, zeze, matari, kayamba na matoazi.
Kisha Daudi na nyumba yote ya Israeli wakaanza kucheza mbele ya Yahwe, wakishangilia kwa vyombo vya mziki, vinubi, vinanda, matari, kayamba na matowazi.
6 Walipofika kwenye uwanja wa kupuria nafaka wa Nakoni, Uza akanyoosha mkono na kulishika Sanduku la Mungu kwa sababu maksai walijikwaa.
Hata walipofika katika shinikizo la Nasoni, wale ng'ombe wakakwama, Uza akanyosha mkono wake na kulikumbatia sanduku la Mungu, naye akalishikilia.
7 Hasira ya Bwana ikawaka dhidi ya Uza kwa sababu ya kitendo chake cha kukosa heshima, kwa hiyo Mungu akampiga akafia papo hapo kando ya Sanduku la Mungu.
Kisha asira ya Yahweh ikawaka dhidi ya Uza. Mungu akampiga kwa ajili ya dhambi yake. Uza akafa pale pale kando ya sandaku la Mungu.
8 Ndipo Daudi akakasirika kwa sababu ghadhabu ya Bwana ilifurika dhidi ya Uza, hivyo hadi leo mahali hapo panaitwa Peres-Uza.
Daudi akakasirika kwa kuwa Yahwe alimpiga Uza, naye akapaita mahali pale Peresi Uza. Eneo hilo linaitwa Peres Uza hata leo.
9 Daudi akamwogopa Bwana siku ile, akasema, “Ni jinsi gani Sanduku la Bwana litakavyoweza kunijia?”
Daudi akamwogopa Yahweh siku hiyo. Akasema, “Sanduku la Yahwe lawezaje kuja kwangu?”
10 Hakuwa radhi kulichukua Sanduku la Bwana kwake katika Mji wa Daudi. Badala yake akalipeleka kwenye nyumba ya Obed-Edomu, Mgiti.
Hivyo Daudi hakuwatayari tena kulichukua sanduku la Yahwe katika mji wa Daudi. Badala yake, akaliweka kando katika nyumba ya Obedi Edomu Mgiti.
11 Sanduku la Bwana likabaki katika nyumba ya Obed-Edomu, Mgiti, kwa miezi mitatu, naye Bwana akambariki pamoja na nyumba yake yote.
Sanduku la Yahwe likakaa katika nyumba ya Obedi Edomu Mgiti kwa miezi mitatu. Kwa hiyo Yahwe akambariki yeye na nyumba yake yote.
12 Kisha Mfalme Daudi akaambiwa, “Bwana ameibariki nyumba ya Obed-Edomu pamoja na kila alicho nacho, kwa sababu ya Sanduku la Mungu.” Basi Daudi akateremka na kulipandisha Sanduku la Mungu kutoka nyumba ya Obed-Edomu hadi Mji wa Daudi kwa shangwe.
Kisha mfalme Daudi akaambiwa, “Yahwe ameibariki nyumba ya Obedi Edomu na kila kitu alichonacho kwa sababu ya sanduku la Mungu.” Hivyo Daudi akaenda na kulipandisha sanduku la Mungu kutoka katika nyumba ya Obedi Edomu hadi mji wa Daudi kwa furaha.
13 Wale waliokuwa wamebeba Sanduku la Bwana walipokuwa wametembea hatua sita, Daudi alitoa dhabihu fahali na ndama aliyenoneshwa.
Ikawa waliolibeba sanduku la Yahwe walipochukua hatua sita, akatoa sadaka ng'ombe na ndama aliyenona.
14 Daudi, akiwa amevaa kisibau cha kitani, alicheza mbele za Bwana kwa nguvu zake zote,
Daudi akacheza mbele ya Yahwe kwa nguvu zake zote; alikuwa amevaa naivera ya kitani pekee.
15 wakati yeye na nyumba yote ya Israeli walipopandisha Sanduku la Bwana kwa shangwe na sauti za tarumbeta.
Hivyo Daudi na nyumba yote ya Israeli wakalipandisha sanduku la Yahwe kwa vifijo na sauti za tarumbeta.
16 Ikawa Sanduku la Bwana lilipokuwa linaingia katika Mji wa Daudi, Mikali binti Sauli akachungulia dirishani. Naye alipomwona Mfalme Daudi akirukaruka na kucheza mbele za Bwana, akamdharau moyoni mwake.
Hata ikawa sanduku la Yahwe lilipofika mjini mwa Daudi, Mikali, binti Sauli, alichungulia dirishani. Akamwona mfalme Daudi akiruka na kucheza mbele ya Yahwe. Akamdharau moyoni mwake.
17 Wakaleta Sanduku la Bwana na kuliweka mahali pake ndani ya hema ambalo Daudi alikuwa amelisimamisha kwa ajili yake, naye Daudi akatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani mbele za Bwana.
Wakaliingiza sanduku la Yahwe na kuliweka mahali pake, katikati ya hema ambayo Daudi alikuwa ameliwekea. Kisha Daudi akatoa sadaka ya kuteketezwa na matoleo ya amani mbele za Yahwe.
18 Baada ya kumaliza kutoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani, Daudi akawabariki watu katika jina la Bwana Mwenye Nguvu Zote.
Ikawa Daudi alipomaliza kutoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani, akawabariki watu kwa jina la Yahwe wa majeshi.
19 Kisha akatoa mkate, andazi la tende na andazi la zabibu kavu kwa kila mtu katika mkutano wote wa Waisraeli, wanaume kwa wanawake. Nao watu wote wakaenda nyumbani kwao.
Kisha akawagawia watu wote, umati wote wa Israeli, wanaume kwa wanawake, kipande cha mkate, nyama na keki ya zabibu. Kisha watu wote wakaondoka; kila mmoja akarudi kwake.
20 Daudi aliporudi ili kuwabariki watu wa nyumbani mwake, Mikali binti Sauli akatoka nje kumlaki, akamwambia, “Tazama jinsi mfalme wa Israeli alivyojibainisha mwenyewe leo kwa kuvua mavazi yake machoni pa vijakazi wa watumishi wake, kama vile ambavyo mtu asiye na adabu angelifanya!”
Kisha Daudi akarudi ili aibariki familia yake. Mikali, binti Sauli, akatoka ili akutane na Daudi naye akasema, “Jinsi gani mtukufu mfalme wa Israeli alivyokuwa leo, aliyejiacha uchi mbele ya macho ya vijakazi miongoni mwa watumishi wake, kama mmoja wa wapumbavu ambaye bila aibu hujifunua yeye mwenyewe!”
21 Daudi akamwambia Mikali, “Nilifanya hivyo mbele za Bwana ambaye alinichagua mimi badala ya baba yako au mwingine yeyote kutoka nyumba yake wakati aliponiweka niwe mtawala juu ya Israeli, watu wa Bwana. Kwa hiyo nitacheza mbele za Bwana.
Daudi akamjibu Mikali, “Nilifanya hivyo mbele ya Yahwe, aliyenichagua juu ya baba yako na juu ya familia yake yote, aliyeniweka kuwa kiongozi juu ya watu wa Yahwe, juu ya Israeli. Mbele ya Yahwe nitafurahi!
22 Nitakuwa asiye na heshima zaidi kuliko sasa, nami nitajishusha machoni pangu mwenyewe. Lakini kwa hawa vijakazi uliosema habari zao nitaheshimiwa.”
Nitakuwa nisiye na heshima hata zaidi ya hapa, na nitajishusha mbele za macho yangu mwenyewe. Lakini kwa hawa vijakazi uliowasema, nitaheshimiwa.”
23 Naye Mikali binti Sauli hakuwa na watoto mpaka siku ya kufa kwake.
Hivyo Mikali, binti Sauli, hakuwa na watato hata alipokufa.

< 2 Samweli 6 >