< 2 Samweli 22 >

1 Daudi alimwimbia Bwana maneno ya wimbo huu wakati Bwana alipomwokoa mikononi mwa adui zake wote, na pia mkononi mwa Sauli.
當上主救達味脫離了仇敵和撒烏耳的毒手時,達味向上主唱了詩歌說:
2 Akasema: “Bwana ni mwamba wangu, ngome yangu na mwokozi wangu,
「上主,我的盤石,我的保障,我的避難所;
3 Mungu wangu ni mwamba wangu, ambaye kwake ninakimbilia, ngao yangu na pembe ya wokovu wangu. Yeye ni ngome yangu, kimbilio langu na mwokozi wangu, huniokoa kutoka kwa watu wenye jeuri.
天主是我所倚靠的盤石,是我的盾牌,我的大救主,我的堡壘,我的藏身處。我的救主,是你救我脫離了強暴。
4 Ninamwita Bwana, anayestahili kusifiwa, nami ninaokolewa kutoka kwa adui zangu.
我一呼求應受頌揚的上主,我便獲救,脫離了我的仇敵。
5 “Mawimbi ya mauti yalinizunguka, mafuriko ya maangamizi yalinilemea.
死亡的波濤圍繞我,凶險的急流驚嚇我,
6 Kamba za kuzimu zilinizunguka, mitego ya mauti ilinikabili. (Sheol h7585)
陰府的繩索纏住中我,死亡的羅網絆住我; (Sheol h7585)
7 Katika shida yangu nalimwita Bwana, nilimlilia Mungu wangu. Kutoka Hekaluni mwake alisikia sauti yangu, kilio changu kikafika masikioni mwake.
在急難中我呼求上主,向我的天主呼號,衪由殿中聽了我的聲音,我的呼聲達入衪耳中。
8 “Dunia ilitetemeka na kutikisika, misingi ya mbingu ikatikisika, vilitetemeka kwa sababu alikuwa amekasirika.
因衪盛大作,大地震動戢慄,上主的基礎動盪搖撼,
9 Moshi ukapanda kutoka puani mwake, moto uteketezao ukatoka kinywani mwake, makaa ya moto yawakayo yakatoka ndani mwake.
由衪的鼻孔湧出濃煙,由衪的口中噴出烈火,由衪的身上射出火炭,
10 Akazipasua mbingu akashuka chini, mawingu meusi yalikuwa chini ya miguu yake.
使天低垂親自降下,在衪的腳下濃雲密佈。
11 Alipanda juu ya kerubi akaruka, akapaa juu kwa mbawa za upepo.
衪乘坐革魯賓飛騰,藉著風的翼羽翱翔。
12 Alifanya giza hema lake la kujifunika: mawingu meusi ya mvua ya angani.
衪四周以黑暗做帷幔,以豪雨濃雲為帳幕。
13 Kutokana na mwanga wa uwepo wake mawingu yalisogea, ikanyesha mvua ya mawe na umeme wa radi.
閃電在衪前閃爍,紅炭發出了火光。
14 Bwana alinguruma kutoka mbinguni, sauti ya Aliye Juu Sana ilisikika.
上主由高天興雷,至高者發出了呼聲。
15 Aliipiga mishale na kutawanya adui, umeme wa radi na kuwafukuza.
衪射出羽箭,使敵人四散,發閃電,使敵人驚擾。
16 Mabonde ya bahari yalifunuliwa, na misingi ya dunia ikawa wazi kwa kukaripia kwake Bwana, kwa uvumi wa pumzi kutoka puani mwake.
上主的呵斥一發,鼻孔的怒氣一出,蒼海的海低即出現,大地的地基也外露。
17 “Alinyoosha mkono kutoka juu na kunishika; alinitoa kutoka kilindi cha maji makuu.
衪由高處伸手將我拉住,由大水中將我提出。
18 Aliniokoa kutoka adui wangu mwenye nguvu nyingi, kutoka adui zangu waliokuwa na nguvu nyingi kuliko mimi.
救我脫離了我的勁敵,擺脫了強於我的仇人。
19 Walinikabili siku ya msiba wangu, lakini Bwana alikuwa msaada wangu.
他們在我困厄之日,襲擊了我,然而上主卻作了我的後盾;
20 Alinileta nje mahali penye nafasi tele, akaniokoa kwa kuwa alipendezwa nami.
衪引我步坦途,因喜愛我而救了我。
21 “Bwana alinitendea sawasawa na uadilifu wangu; sawasawa na usafi wa mikono yangu amenilipa.
上主照我的正義酬報了我,按我雙手的清白報答了我;
22 Kwa maana nimezishika njia za Bwana; sijatenda ubaya nikamwacha Mungu wangu.
因我遵行了上主的正道,沒有作惡離棄我的天主。
23 Sheria zake zote zi mbele yangu, wala sijayaacha maagizo yake.
衪的一切法令在我前,我未曾違過衪的誡命;
24 Nimekuwa sina hatia mbele zake, nami nimejilinda nisitende dhambi.
我衪前常保成全,自知提防各種不義。
25 Bwana amenilipa sawasawa na uadilifu wangu, sawasawa na usafi wangu machoni pake.
因此,上主照我的正義,我在衪的純潔,賞報了我。
26 “Kwa yeye aliye mwaminifu unajionyesha kuwa mwaminifu, kwa asiye na hatia unajionyesha kutokuwa na hatia,
仁慈的人,你待他仁慈;正直的人,你待他正直;
27 kwa aliye mtakatifu unajionyesha kuwa mtakatifu, lakini kwa aliyepotoka unajionyesha kuwa mkaidi.
純的人,你待他純樸;乖戾的人,你待他乖戾。
28 Wewe huwaokoa wanyenyekevu, lakini macho yako ni juu ya wenye kiburi ili uwashushe.
卑微的人,你必拯救;傲慢的人,你必睥視。
29 Wewe ni taa yangu, Ee Bwana. Bwana hulifanya giza langu kuwa mwanga.
上主,你是我的火炬,我的天主,照明我的黑暗。
30 Kwa msaada wako naweza kushinda jeshi, nikiwa pamoja na Mungu wangu nitaweza kuruka ukuta.
仗著你,我衝入了敵營;靠著我的天主,我跳過了牆垣。
31 “Kuhusu Mungu, njia yake ni kamilifu; neno la Bwana halina dosari. Yeye ni ngao kwa wote wanaokimbilia kwake.
天主的道路是完善的;上主的言語是純淨的;凡投衪的人,衪怍他們的後盾。
32 Kwa maana ni nani aliye Mungu zaidi ya Bwana? Ni nani aliye Mwamba isipokuwa Mungu wetu?
上主以外,還有誰是天主﹖除我的的天主外,還有誰的盤石﹖
33 Mungu ndiye anivikaye nguvu na kufanya njia yangu kuwa kamilifu.
是天主賜我毅力,使我一路順利,
34 Huifanya miguu yangu kama miguu ya kulungu, huniwezesha kusimama mahali palipo juu.
使我的腳快如鹿蹄,使我屹立高地,
35 Huifundisha mikono yangu kupigana vita; mikono yangu inaweza kupinda upinde wa shaba.
教導我手作戰,使臂膊能開銅弓。
36 Hunipa ngao yako ya ushindi, unajishusha chini ili kuniinua.
你你的救生盾賜了我,你的長甲作了我的掩護。
37 Huyapanua mapito yangu, ili miguu yangu isiteleze.
你為我的腳步拓寬了路,我的腳從未顛簸。
38 “Niliwafuatia adui zangu na nikawaseta, sikurudi nyuma mpaka walipoangamizwa.
我追趕仇敵,消滅他們;不滅絕他們,決不返回。
39 Niliwaseta kabisa, nao hawakuweza kuinuka tena; walianguka chini ya miguu yangu.
我將他們打得一蹶不振,盡都倒斃在我腳下
40 Ulinivika nguvu kwa ajili ya kupigana vita; uliwafanya adui zangu wasujudu miguuni pangu.
你賜我毅力勇作戰,把我的對手屈伏我下,
41 Uliwafanya adui zangu wageuke na kukimbia, nami nikawaangamiza adui zangu.
使我的敵人在 前轉背而逃,使我殲滅了一切仇恨我的人。
42 Walipiga yowe, lakini hapakuwepo na yeyote wa kuwaokoa; walimlilia Bwana, lakini hakuwajibu.
他們呼號,卻無人施救;呼號上主,也不獲應允。
43 Niliwaponda kama mavumbi ya nchi; niliwaponda na kuwakanyaga kama tope barabarani.
我搗碎他們地上的灰塵,踐踏他們像道上的泥土。
44 “Umeniokoa kutokana na mashambulizi ya watu wangu; umenihifadhi mimi kama kiongozi wa mataifa. Watu ambao sikuwajua wananitumikia,
你由百姓的叛亂中救拔了我,立我做了列國的首領;我不知道的人民竟給我服役;
45 nao wageni huja wakininyenyekea, mara wanisikiapo, hunitii.
外邦的子民諂媚奉承我,一聽到是我,即服從我;
46 Wote wanalegea, wanatoka katika ngome zao wakitetemeka.
外的子民驚惶失色,戰戰兢兢走的堡壘。
47 “Bwana yu hai! Sifa ni kwa Mwamba wangu! Atukuzwe Mungu, Mwamba, Mwokozi wangu!
上主萬歲! 願我的盤石受讚美,願救我的的天主受頌揚!
48 Yeye ndiye Mungu anilipiziaye kisasi, ayawekaye mataifa chini yangu,
天主是你為我報了仇,使萬民屈伏於我,
49 aniwekaye huru toka kwa adui zangu. Uliniinua juu ya adui zangu; uliniokoa toka kwa watu wajeuri.
是你救我脫離了我的仇敵,提拔我凌駕我的對手之上,救我脫免了強暴的人。
50 Kwa hiyo nitakusifu, Ee Bwana, katikati ya mataifa; nitaliimbia sifa jina lako.
為此,上主! 我要在異民中稱謝你,歌頌你的聖名。
51 Humpa mfalme wake ushindi mkuu; huonyesha fadhili zake kwa mpakwa mafuta wake, kwa Daudi na wazao wake milele.”
因為衪使自己的君大獲勝利,對自己的受傅者達味和他的子孫,廣施仁慈,直到永遠」。

< 2 Samweli 22 >