< 2 Wafalme 3 >

1 Yehoramu mwana wa Ahabu akawa mfalme wa Israeli katika Samaria mwaka wa kumi na nane wa utawala wa Yehoshafati mfalme wa Yuda, naye akatawala kwa miaka kumi na miwili.
Basi katika mwaka wa kumi na nane wa Yehoshefati mfalme wa Yuda, Yoramu mwana wa Ahabu alianza kutawala juu ta Israeli katika Samaria; alitawala miaka kumi na miwili.
2 Akafanya maovu machoni pa Bwana, lakini sio kama baba yake na mama yake walivyokuwa wamefanya. Akaondoa nguzo ya ibada ya Baali ambayo baba yake alikuwa ameitengeneza.
Alifanya yaliyo maovo usoni kwa Yahwe, lakini si kama baba yake na mama yake; kwa kuwa aliiondoa ile nguzo ya mungu wa Baali ambayo baba yake aliitengeneza.
3 Hata hivyo akashikamana na dhambi za Yeroboamu mwana wa Nebati, ambazo alisababisha Israeli kuzitenda, wala hakuziacha.
Hata hivyo alishikilia dhambi za Yeroboamu mwana wa Nebati, ambaye alisababisha Israeli kufanya dhambi; wala hakuziacha mbali nao.
4 Basi Mesha mfalme wa Moabu akafuga kondoo, naye akawa ampatie mfalme wa Israeli wana-kondoo 100,000 pamoja na sufu ya kondoo dume 100,000.
Basi Mesha mfalme wa Moabu alifuga kondoo. Alikuwa akimpatia mfalme wa Israeli kondoo 100, 000 na manyoya ya kondoo dume 100, 000.
5 Lakini baada ya Ahabu kufa, mfalme wa Moabu aliasi dhidi ya mfalme wa Israeli.
Ila baada ya Ahabu kufa, yule mfalme wa Moabu aliasi dhidi ya mfalme wa Israeli.
6 Kwa hiyo wakati ule Mfalme Yehoramu akaondoka kutoka Samaria na kukusanya Israeli yote tayari kwenda vitani.
Hivyo Mfalme Joramu alikaondoka Samaria katika muda huo kuwahamasisha Waisraeli wote kwa ajili ya vita.
7 Akapeleka pia ujumbe ufuatao kwa Yehoshafati mfalme wa Yuda: “Mfalme wa Moabu ameasi dhidi yangu. Je, utakwenda pamoja nami kupigana dhidi ya Moabu?” Akajibu, “Nitakwenda pamoja nawe. Mimi ni kama wewe, watu wangu ni kama watu wako, farasi wangu ni kama farasi wako.”
Akatuma mjumbe kwa Yehoshafati mfalme wa Yuda, akisema, “Mfalme wa Moabu ameasi dhidi yangu. Je mtakwenda pamoja nami kupigana dhidi ya Moabu?” Yehoshafati akajibu, “Nitaenda. Mimi ni kama wewe, watu wangu ni kama watu wako, farasi wangu ni kama farasi wako.”
8 Akauliza, “Je, tutashambulia kupitia njia gani?” Akajibu, “Kupitia Jangwa la Edomu.”
Ndipo akasema, “Tutawashambulia kwa njia gani?” Yehoshafati akajibu, “Kwa njia ya jangwa la Edemu.
9 Hivyo mfalme wa Israeli akaondoka akiwa pamoja na mfalme wa Yuda na mfalme wa Edomu. Baada ya kuzunguka kwa siku saba, jeshi likawa limeishiwa maji kwa matumizi yao na kwa ajili ya wanyama waliokuwa nao.
Hivyo huyo mfalme wa Israeli, Yuda, na Edomu wakazunguka kwa mda wa siku saba. Hapakuwa na maji kwa ajili ya jeshi lao, wala kwa farasi au wanyama.
10 Mfalme wa Israeli akamaka, “Nini! Je, Bwana ametuita sisi wafalme watatu ili tu kututia mikononi mwa Moabu?”
Basi mfalme wa Israeli akasema, “Hii ni nini? Yahwe amewaita wafalme watatu ili kutekwa mikononi mwa Moabu?”
11 Lakini Yehoshafati akauliza, “Je, hayuko nabii wa Bwana hapa, ili tuweze kumuuliza Bwana kupitia kwake?” Afisa mmoja wa mfalme wa Israeli akajibu, “Elisha mwana wa Shafati yuko hapa. Ndiye alikuwa akimimina maji juu ya mikono ya Eliya.”
Lakini Yehoshafati akasema, “je hakuna nabii wa Yahwe, ambaye tunaweza kufanya shauri kuhusu Yahwe kupitia yeye?” Mtumishi mmoja wa wafalme wa Israeli akajibu na kusema, “Elisha mwana wa Shafati yuko hapa, ambaye alikuwa akimimina maji kwenye mikono ya Eliya.”
12 Yehoshafati akasema, “Neno la Bwana liko pamoja naye.” Kwa hiyo mfalme wa Israeli na Yehoshafati pamoja na mfalme wa Edomu wakamwendea.
Yehoshafati akasema, “Neno la Yahwe liko pamoja nami.” Hivyo mfalme wa Israeli, Yehoshaphati, na mfalme wa Edomu wakashuka chini kwenda kwake.
13 Elisha akamwambia mfalme wa Israeli, “Nina nini mimi nawe? Nenda kwa manabii wa baba yako na manabii wa mama yako.” Mfalme wa Israeli akajibu, “La hasha, kwa sababu ni Bwana ambaye ametuita pamoja sisi wafalme watatu ili atutie mikononi mwa Moabu.”
Elisha akamwambia mfalme wa Israeli, “Nifanye nini kwa ajili yako? Nenda kwa manabii wa baba na mama yako.” Ndipo mfalme wa Israeli akamwambia, “Hapana, kwa sababu Yahwe amewaita hawa wafalme watatu pamoja ili kuruhusu jeshi la Moabu liwateke.”
14 Elisha akasema, “Hakika, kama Bwana Mwenye Nguvu Zote aishivyo ambaye ninamtumikia, kama si kuheshimu Yehoshafati mfalme wa Yuda, nisingekutazama wala hata kukutupia jicho.
Elisha akajibu, “Kama Yawhe wa majeshi aishivo, ambaye nimesimama mbele zake, hakika kama nisingemheshimu uwepo wa Yehoshafati mfalme wa Yeda, Nisingevuta usikivu kwako, au hata kukutazama.
15 Lakini sasa, nileteeni mpiga kinubi.” Mpiga kinubi alipokuwa akipiga, mkono wa Bwana ukaja juu ya Elisha,
Lakini sasa niletee mwanamuziki.” Ndipo alipokuja mpiga muziki alipocheza, mkono wa Yahwe ukaja juu ya Elisha.
16 naye akasema, “Hivi ndivyo asemavyo Bwana, ‘Chimbeni bonde hili lijae mahandaki.’
Akasema, “'Yahwe asema hivi, 'Fanya hili bonde la mto mkavu lijae mahandaki.'
17 Kwa kuwa hivi ndivyo asemavyo Bwana: Hamtaona upepo wala mvua, lakini bonde hili litajaa maji, nanyi pamoja na ngʼombe wenu na wanyama wenu wengine mtakunywa.
Kwa kuwa Yahwe asema hivi, 'Hutaona upepo, wala hamtaona mvua, bali hili bonde la mto litajaa maji, na mtakunywa, ninyi na mifugo yenu na wanyama wenu wote.'
18 Hili ni jambo rahisi machoni pa Bwana. Pia ataitia Moabu mikononi mwenu.
Hiki ni kitu rahisi usoni mwa Yahwe. Pia atawapa ushindi juu ya hao Wamoabu.
19 Mtaushinda kila mji wenye ngome na kila mji mkubwa. Mtakata kila mti ulio mzuri, mtaziba chemchemi zote, na kuharibu kila shamba zuri kwa mawe.”
Mtaiteka kila ngome ya mji na kila mji mzuri, kukata kila mti mzuri, kusimamisha chemichemi zote za maji, na kuharibu kila sehemu nzuri ya nchi na miamba.”
20 Kesho yake asubuhi, karibu na wakati wa kutoa dhabihu ya asubuhi, tazama, maji yakawa yanatiririka kutoka upande wa Edomu! Nayo nchi ikajaa maji.
Hivyo asubuhi karibia na mda wa kutoa sadaka ya kuteketeza, yakaja maji kutoka uelekeo wa Edomu; nchi ikajaa maji.
21 Basi Wamoabu wote walikuwa wamesikia kuwa wale wafalme wamekuja kupigana dhidi yao. Hivyo kila mtu, kijana na mzee, ambaye angeweza kushika silaha akaitwa na kuwekwa mpakani.
Ndipo wakati Wamoabu wote waliposikia kwamba wafalme wamekuja kupigana dhidi yao, walikusanyika pamoja, wote waliotakiwa kubeba silaha, na wakasimama mpakani.
22 Walipoamka asubuhi na mapema, jua likawa linamulika juu ya maji. Wamoabu waliokuwa upande wa pili wakaona maji ni mekundu, kama damu.
Walitembea asubuhi na mapema na jua likang'aa kwenye maji. Wakati Wamoabu walipoyaona yale maji yaliyowaelekea, yanaonekana mekundu kama damu.
23 Wamoabu wakasema, “Ile ni damu! Lazima hao wafalme wamepigana na kuchinjana wao kwa wao. Sasa Moabu, twendeni tukateke nyara!”
Wakatamka kwa hasira, “Hii ni damu! Yamkini hao wafalme wameharibiwa, na wameuna wao kwa wao! Sasa basi, Moabu, ngoja tuende tukawateke nyara!”
24 Lakini Wamoabu walipofika kwenye kambi ya Israeli, Waisraeli wakainuka na kuwapiga mpaka wakakimbia. Nao Waisraeli wakaivamia nchi na kuwachinja Wamoabu.
Wakati walipokuja kwenye kambi ya Israeli, Waisraeli wakawashtukiza na kuwashambulia Wamoabi, ambao walikimbia mbele yao. Hilo jeshi la Israeli waliwakimbiza hao Wamoabu hadi kwao wakiwaua.
25 Wakaiharibu miji, kila mtu akatupa jiwe juu ya kila shamba zuri mpaka likafunikwa. Wakaziba chemchemi zote na kukata kila mti mzuri. Kir-Haresethi peke yake ndio uliobaki na mawe yake yakiwa mahali pake. Lakini hata hivyo watu waliokuwa na makombeo wakauzunguka na kuushambulia vilevile.
Waliiharibu miji, na kila aina ya amani ya nchi kila mtu alirusha jiwe mpaka ulipojaa. Walizuia kila chemichemi ya maji na kukata chini miti mizuri yote. Kir-haresethi tu ndiyo ilichwa na mawe yake. Lakini hao maaskari wakawashambulia na makombeo wakiwazunguka na kuishambulia.
26 Mfalme wa Moabu alipoona kuwa vita vimekuwa vikali dhidi yake, akachukua watu 700 wenye panga ili kuingia kwa mfalme wa Edomu, lakini wakashindwa.
Ndipo Mfalme Mesha wa Moabu alipoona kwamba ameshindwa, alichukua watu hodari wa upanga mia saba pamoja naye kwenda kwa mfalme wa Edomu, lakini walishindwa.
27 Ndipo akamchukua mwanawe mzaliwa wake wa kwanza, ambaye angekuwa mfalme baada yake, akamtoa kama dhabihu ya kuteketezwa juu ya ukuta wa mji. Ghadhabu ikawa kubwa dhidi ya Israeli; wakajiondoa kwake na kurudi katika nchi yao wenyewe.
Ndipo akamchukua mtoto wake wa kwanza, ambaye angetawala baada ya yeye, na akamuudhi kwa kumtoa kama sadaka ya kuteketezwa juu ya ukuta. Hivyo, kulikuwa na hasira kubwa dhidi ya Israeli, na hao Waisraeli, na Jeshi la Israeli likamuacha mfalme Mesha na kurudi kwenye nchi yao.

< 2 Wafalme 3 >