< 2 Wafalme 24 >

1 Wakati wa utawala wa Yehoyakimu, Nebukadneza mfalme wa Babeli aliishambulia nchi, naye Yehoyakimu akawa mtumwa wake kwa miaka mitatu. Lakini hatimaye akabadili mawazo yake na kuasi dhidi ya Nebukadneza.
Katika siku za Yehoyakimu, Nebukadreza mfalme wa Babeli akaiteka Yuda; Yehoyakimu akawa mtumishi kwa muda wa miaka mitatu. Kisha Yehoyakimu akarudi na kuasi dhidi ya Nebukadreza.
2 Bwana akatuma wavamiaji wa Wakaldayo, Waaramu, Wamoabu na Waamoni ili kumshambulia. Aliwatuma kuiangamiza Yuda sawasawa na neno la Bwana lililosemwa na watumishi wake manabii.
Yahwe akatuma vikosi vya Wakaldayo dhidi ya Yehoyakimu, Washami, Wamoabu, na Waamoni; akawatuma dhidi ya Yuda kuiharibu. Hii ilikuwa ni kuthibitisha pamoja na neno la Yahwe ambalo aliloliongea kupitia watumishi wake manabii.
3 Hakika mambo haya yalitokea Yuda kulingana na agizo la Bwana, ili kuwaondoa kutoka machoni pake kwa sababu ya dhambi za Manase na yote aliyoyafanya,
Ilikuwa baada ya mda mfupi kwenye kinywa cha Yahwe kwamba hili likaja juu ya Yuda, kuwaondoa usoni mwa uso wake, kwa sabau ya dhambi za Manase, yote aliyoyafanya,
4 ikiwa ni pamoja na kumwaga damu isiyo na hatia. Kwa kuwa aliijaza Yerusalemu kwa damu isiyo na hatia, naye Bwana hakuwa radhi kusamehe.
na pia kwa sababu ya damu isiyokuwa na hatia aliyoimwaga, kwa kuijaza Yerusalemu kwa damu isiyokuwa na hatia. Yahwe hakuwa tayari kusamehe hilo.
5 Matukio mengine ya utawala wa Yehoyakimu na yote aliyoyafanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Yuda?
Kama kwa mambo mengine yanayomuhusu Yehoyakimu, na yote aliyoyafanya, je hayajaandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Yuda?
6 Yehoyakimu akalala pamoja na baba zake. Naye Yehoyakini mwanawe akawa mfalme baada yake.
Yehoyakimu akalala pamoja na wazee wake, na Yekonia mtoto wake akawa mfalme katika sehemu yake.
7 Mfalme wa Misri hakutoka tena katika nchi yake, kwa sababu mfalme wa Babeli alikuwa ameitwaa himaya yake yote, kuanzia Kijito cha Misri hadi Mto Frati.
Mfalme wa Misri hakushambulia tena nje ya nchi yake, kwa sababu mfalme wa Babeli alakuwa amezishinda nchi zote ambazo zilikuwa zikitawaliwa na mfalme wa Misri, kutoka kwenye kitabu cha Misri mpaka Mto wa Frati.
8 Yehoyakini alikuwa na miaka kumi na minane alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miezi mitatu. Jina la mama yake aliitwa Nehushta binti Elnathani kutoka Yerusalemu.
Yekonia alikuwa na umri wa miaka kumi na nane alipoanza kutawala; alitawala Yerusalemu miezi mitatu. Mama yake alikuwa anaitwa Nehushta; alikuwa binti wa Elnathani wa Yerusalemu.
9 Akafanya maovu machoni pa Bwana, kama vile baba yake alivyokuwa amefanya.
Alifanya yaliyo maovu usoni mwa Yahwe; alifanya yale yote ambayo baba yake aliyafanya.
10 Wakati huo, maafisa wa Nebukadneza mfalme wa Babeli walikuja ili kuishambulia Yerusalemu, nao wakaizunguka kwa jeshi.
Katika kipindi hicho jeshi la Nebukadreza mfalme wa Babeli liliishambulia Yerusalemu na kuuzunguka mji.
11 Nebukadneza mwenyewe akaupandia mji wakati maafisa wake walipokuwa wameuzunguka kwa jeshi.
Nebukadreza mfalme wa Babeli akaja kwenye mji wakati maaskari wake walipokuwa wameuzunguka,
12 Yehoyakini mfalme wa Yuda, mama yake, wahudumu wake, wakuu na maafisa wake wote wakajisalimisha kwa Nebukadneza. Katika mwaka wa nane wa utawala wa mfalme wa Babeli, akamchukua Yehoyakini kuwa mfungwa.
na Yekonia mfalme wa Yuda akatoka nje kwenda kwa mfalme wa Babeli, yeye, mama yake, watumishi wake, watoto wake, na maafisa wake. Mfalme wa Babeli akamteka katika mwaka wa nane wa utawala wake.
13 Kama vile Bwana alivyokuwa amesema, Nebukadneza akaondoa hazina yote kutoka Hekalu la Bwana na kutoka jumba la mfalme, akavichukua vyombo vyote vya dhahabu ambavyo Solomoni mfalme wa Israeli alikuwa amevitengeneza kwa ajili ya Hekalu la Bwana.
Nebukadreza akachukua kutoka pale vitu vyote vya thamani katika nyumba ya Yahwe, na walio katika nyumba ya kifalme. Akavikata vipande vipande vitu vyote vya dhahabu ambavyo Suleimani mfalme wa Israeli alivitengeneza katika hekalu la Yahwe, kama alivyokuwa amesema ingetokea.
14 Akawachukua watu wa Yerusalemu wote kwenda uhamishoni: yaani maafisa wote na mashujaa, watu wenye ustadi na ufundi, jumla yao watu elfu kumi. Watu maskini sana ndio tu waliobaki katika nchi.
Akawachukua wote utumwani Yerusalemu, viongozi wote, na wapiganaji wote, mateka elfu kumi, na mafundi wote, na wafua vyuma. hakuna aliyekuwa amesalia isipokuwa watu maskini katika nchi.
15 Nebukadneza akamchukua mateka Yehoyakini hadi Babeli. Pia akawachukua utumwani kutoka Yerusalemu hadi Babeli mama yake mfalme, wake zake, maafisa wake, na viongozi wote wa nchi.
Nebukadreza akamchukua Yekonia utumwani Babeli, pia na mama yake na mfalme, wake, maafisa, na wakuu wa nchi. Akawachukua kwenda utumwani kutoka Yerusalemu mpaka Babeli.
16 Mfalme wa Babeli pia akawahamishia Babeli mashujaa elfu saba, wenye nguvu na wanaofaa kupigana vita, na watu wenye ustadi na mafundi elfu moja.
Wapiganaji wote, elfu saba kwa hesabu, na mafundi elfu moja na wafua vyuma, wote wanaostahili kumpiga- mfalme wa Babeli aliwaleta hawa watu kwenye utumwa Babeli.
17 Akamfanya Matania, ndugu wa baba yake Yehoyakini, kuwa mfalme mahali pake, na akalibadilisha jina lake kuwa Sedekia.
Mfalme wa Babeli akamfanya Matania, kaka yake na baba yake na Yehokimu, mfalme katika sehemu yake, na kubadilisha jina lake kuwa Sedekia.
18 Sedekia alikuwa na umri wa miaka ishirini na mmoja alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka kumi na mmoja. Jina la mama yake aliitwa Hamutali binti Yeremia, kutoka Libna.
Sedekia alikuwa na umri wa miaka ishirini na moja wakati alipoanza kutawala; alitawala miaka kumi na moja katika Yerusalemu. Mama yake alikuwa anaitwa Hamutali; alikuwa binti wa Yeremia kutoka Libna.
19 Alifanya maovu machoni pa Bwana, kama alivyofanya Yehoyakimu.
Alifanya yaliyo maovu machoni mwa Yahwe; aliyafanya yale yote ambayo Yehokimu aliyoyafanya.
20 Ilikuwa ni kwa sababu ya hasira ya Bwana haya yote yalitokea Yerusalemu na Yuda, naye mwishoni akawaondoa mbele zake. Basi, Sedekia akaasi dhidi ya mfalme wa Babeli.
Kupitia hasira ya Yahwe, haya matukio yote yalitokea Yerusalemu na Yuda, hadi alipowaondoa kwenye uso wake. Kisha Sedekia akaasi dhidi ya mfalme wa Babeli.

< 2 Wafalme 24 >