< 2 Wafalme 22 >
1 Yosia alikuwa na miaka minane alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka thelathini na mmoja. Mama yake aliitwa Yedida binti Adaya, kutoka Boskathi.
Yosia alikuwa na umri wa miaka minane wakati alipoanza kutawala; alitawala kwa mda wa miaka thelathini na moja katika Yerusalemu. Mama yake alikuwa anaitwa Yedida (Alikuwa binti wa Adaye wa Bozkathi).
2 Akafanya yaliyo mema machoni pa Bwana na kuenenda katika njia zote za Daudi baba yake. Hakugeuka upande wa kuume wala wa kushoto.
Alifanya yale yaliyo mema usoni mwa Yahwe. Alitembea kwenye njia zote za Daudi babu yake, na hakugeuka wala upande wa kulia au kushoto.
3 Katika mwaka wa kumi na nane wa utawala wake, Mfalme Yosia akamtuma mwandishi Shafani mwana wa Azalia, mwana wa Meshulamu, kwenda katika Hekalu la Bwana. Akasema:
Ikawa kwamba katika mwaka wa kumi na nane mfalme Yosia, akamtuma Shafani mwana wa Azalia mwana wa Meshulamu, mwandishi, kwenye nyumba ya Yahwe, akisema,
4 “Panda uende kwa Hilkia, kuhani mkuu, umwambie ahesabu zile fedha ambazo zimeletwa katika Hekalu la Bwana, ambazo mabawabu wamekusanya kutoka kwa watu.
“Panda juu kwa Hilkia yule kuhani mkuu na mwambie ahesabu pesa ambazo zilizokuwa zimeletwa kwenye nyumba ya Yahwe, ambazo walinzi wa hekalu wamezikusanya kutoka kwa watu.
5 Waambie waikabidhi kwa watu walioteuliwa kusimamia kazi ya Hekalu. Waamuru watu hawa wawalipe wafanyakazi ambao wanakarabati Hekalu la Bwana:
Zigawanywe kwenye mikono ya wafanyakazi ambao ni wasimamizi wa nyumba ya Yahwe, na waache wawapatie wafanya kazi ambao wako kwenye nyumba ya Yahwe, ili waweze kutengeneza pale palipoharibika.
6 wale maseremala, wajenzi na waashi. Waambie pia wanunue mbao na mawe yaliyochongwa ili kukarabati Hekalu.
Wapewe pesa maseremala, wajenzi, na waashi, na pia kununua mbao na kukata jiwe kukarabati nyumba ya Yahwe.”
7 Lakini hawahitajiki kutoa hesabu ya fedha walizokabidhiwa, kwa sababu wanafanya kwa uaminifu.”
Lakini zile pesa hazikutakiwa kuhesabiwa wakati walipokuwa wanapewa, kwa sababu waliimudu ile kazi kwa uaminifu.
8 Hilkia kuhani mkuu akamwambia Shafani mwandishi, “Nimekipata Kitabu cha Sheria ndani ya Hekalu la Bwana.” Akampa Shafani, ambaye alikisoma.
Hilkia kuhani mkuu akamwambia Shafani yule mwandishi, “Nimekipata kitabu cha sheria katika nyumba ya Yahwe.” Basi Hilkia akampatia kile kitabu Shafani, na kukisoma.
9 Kisha Shafani mwandishi akamwendea mfalme na kumpa taarifa akisema: “Maafisa wako wametoa ile fedha ambayo ilikuwa ndani ya Hekalu la Bwana na imekabidhiwa mikononi mwa wasimamizi wa marekebisho ya Hekalu.”
Shafani akaenda na kuchukua kile kitabu kwa mfalme, na pia kumjulisha, akisema, “Watumishi wako wamezitumia zile pesa ambazo zilizokuwa zimepatikana kwenye hekalu na zimegawiwa kwenye mikono ya wafanya kazi ambao husimamia kuangalia nyumba ya Yahwe.”
10 Ndipo Shafani mwandishi akampasha mfalme habari kwamba: “Hilkia kuhani amenipa kitabu hiki.” Naye Shafani akakisoma kile kitabu mbele ya mfalme.
Kisha Shafani yule mwandishi akamwambia mfalme, “Hilkia yule kuhani amenipatia kitabu.” Kisha Shafani akakisoma mbele ya mfalme.
11 Mfalme aliposikia maneno ya kile Kitabu cha Sheria, akararua mavazi yake.
Ikawa kwamba wakati mfalme aliposikia maneno ya sheria, alichana nguo zake.
12 Akatoa maagizo haya kwa Hilkia kuhani, Ahikamu mwana wa Shafani, Akbori mwana wa Mikaya, Shafani mwandishi, na Asaya mtumishi wa mfalme:
Kisha mfalme akamwamuru Hilkia yule kuhani, Ahikamu mwana wa Shafani, Akbori mwana wa Mikaya, Shafani mwandishi, na Asaya, mtumishi wake mwenyewe, akisema,
13 “Nendeni mkamuulize Bwana kwa ajili yangu, na kwa ajili ya watu na Yuda wote kuhusu yale yaliyoandikwa ndani ya kitabu hiki ambacho kimepatikana. Hasira ya Bwana ni kubwa inayowaka dhidi yetu kwa sababu baba zetu hawakuyatii maneno ya kitabu hiki. Hawajatenda kulingana na yale yote yaliyoandikwa humo kutuhusu sisi.”
Nenda na ukaongee pamoja na Yahwe kwa ajili yangu, na kwa ajili ya watu na kwa Yuda yote, kwa sababu ya maneno ya hiki kitabu ambacho kilichopatikana. Kwa hasira kubwa ya Yahwe ambayo ametukasirikia dhidi yetu kwa sababu babu zetu hawakusikiliza maneno ya hiki kitabu hivyo kama kutii yote ambayo yalikuwa yameandikwa kuhusiana na sisi.
14 Hilkia kuhani, Ahikamu, Akbori, Shafani na Asaya wakaenda kuongea na nabii mke Hulda, ambaye alikuwa mke wa Shalumu mwana wa Tikwa, mwana wa Harhasi mtunzaji wa chumba cha mavazi. Hulda aliishi Yerusalemu katika Mtaa wa Pili.
Basi Hilkia yule kuhani, Ahikamu, Akbori, Shafani, na Asaya wakaenda kwa Hulda nabii wa kike, mke wa Shalumu mwana wa Tikva mwana wa Harhasi, mtunza kabati la nguo (aliishi katika Yerusalemu katika mtaa wa pili), na wakaongea pamoja naye.
15 Akawaambia, “Hivi ndivyo asemavyo Bwana, Mungu wa Israeli: Mwambieni yule mtu aliyewatuma ninyi kwangu,
Akawaambia, “Hivi ndivyo Yahwe, Mungu wa Israeli, asemavyo: 'Mwambie huyu mtu aliyekutuma kwangu,
16 ‘Hivi ndivyo asemavyo Bwana: Nitaleta maafa juu ya mahali hapa na watu wake, kulingana na kila kitu kilichoandikwa katika kitabu hicho mfalme wa Yuda alichosoma.
“Hivi ndivyo Yahwe asemavyo: 'Tazama, nitaleta janga kwenye hii sehemu na juu ya wakaao hapa, kulingana na kila kitu kilichoandikwa kwenye kitabu ambacho mfalme wa Yuda alichokisoma.
17 Kwa sababu wameniacha mimi na kufukiza uvumba kwa miungu mingine, na kunighadhibisha kwa sanamu zote zilizotengenezwa kwa mikono yao, hasira yangu itawaka dhidi ya mahali hapa, wala haitatulizwa.’
Kwa sababu wamenitelekeza na kufukiza ubani kwa miungu mingine, hivyo basi wanaweza kunichochea hasira pamoja na matendo yote waliyoyafanya-kwa hiyo hasira yangu ilikuwa inawaka dhidi ya hii sehemu, na haitazimika.”'
18 Mwambieni mfalme wa Yuda, ambaye amewatuma kumuuliza Bwana, ‘Hivi ndivyo asemavyo Bwana, Mungu wa Israeli, kuhusu maneno uliyoyasikia:
Lakini kwa mfalme wa Yuda, aliye watuma kuuliza mapenzi ya Yahwe, hivi ndivyo mtakavyo mwambia: “Yahwe, Mungu wa Israeli asema hivi: Kuhusu yale maneno uliyoyasikia,
19 Kwa kuwa moyo wako ulikuwa msikivu na ulijinyenyekeza mbele za Bwana uliposikia kile nilichosema dhidi ya mahali hapa na watu wake, kwamba wangelaaniwa na kuachwa ukiwa, basi kwa sababu uliyararua mavazi yako na kulia mbele zangu, nimekusikia, asema Bwana.
kwa sababu moyo wako ulikuwa mlaini, na kwa sababu umejinyenyekesha mwenyewe mbele za Yahwe, wakati uliposikia nilichokisema dhidi ya hii sehemu na wenyeji wake, kwamba wanaweza kuwa wakiwa na laana, na kwasaabu ulizozirarua nguo zako na kulia mbele yangu, Nami pia nimekusikia-hivi ndivyo Yahwe asemavyo.
20 Kwa hiyo nitakukusanya kwa baba zako, nawe utazikwa kwa amani. Macho yako hayataona maafa yote nitakayoleta juu ya mahali hapa.’” Basi wakapeleka jibu lake kwa mfalme.
Tazama, nitakukusanya na babu zako, nawe utawekwa kaburini kwako kwa amani. Macho yako hayataona maafa yote ambayo nitayaleta kwenye hii sehemu. “"” Hivyo watu wakachukua ujumbe huu kuurudisha kwa mfalme.