< 2 Wafalme 15 >
1 Katika mwaka wa ishirini na saba wa utawala wa Yeroboamu mfalme wa Israeli, Azaria mwana wa Amazia mfalme wa Yuda alianza kutawala.
Katika mwaka wa ishirini na saba wa Yeroboamu mfalme wa Israeli, Azaria mwana wa Amazia mfalme wa Yuda akaanza kutawala.
2 Alikuwa na umri wa miaka kumi na sita alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka hamsini na miwili. Mama yake aliitwa Yekolia wa Yerusalemu.
Azaria alikuwa na umri wa miaka kumi na sita alipoanza kutawala, na alitawala kwa mda wa miaka hamsini na mbili katika Yerusalemu. Mama yake alikuwa anaitwa Yekolia, na alikuwa anatokea Yerusalemu.
3 Akatenda yaliyo mema machoni pa Bwana, kama Amazia baba yake alivyofanya.
Alifanya yaliyo mema machoni pa Yahwe, kama baba yake Amazia alivyofanya.
4 Hata hivyo, mahali pa juu pa kuabudia hapakuondolewa. Watu waliendelea kutoa kafara na kufukiza uvumba huko.
Lakini, mahali pa juu hapakuwa pameondolewa. Watu wakaendelea kutoa sadaka na kufukiza ubani katika mahala pa juu.
5 Bwana akampiga mfalme kwa ukoma mpaka siku aliyokufa, naye aliishi katika nyumba iliyotengwa peke yake. Yothamu mwana wa mfalme akawa msimamizi wa jumba la mfalme, na akawatawala watu wa nchi.
Yhawe akampiga mfalme hivyo basi akawa na ukoma mpaka siku ya kifo chake na alikaa kwenye nyumba ya pekee. Yothamu, mtoto wa mfalme, alikuwa juu ya watu na kuwaongoza watu wa nchi.
6 Matukio mengine ya utawala wa Azaria na yote aliyoyafanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Yuda?
Kama kwa mambo mengine yanayomhusu Azaria, yote aliyoyafanya, je hayajaandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Yuda?
7 Azaria akalala pamoja na baba zake, naye akazikwa karibu nao katika Mji wa Daudi, na Yothamu mwanawe akawa mfalme baada yake.
Hivyo Azaria alilala pamoja na babu zake katika mji wa Daudi. Yothamu, mtoto wake, akawa mfalme katika mahala pake.
8 Katika mwaka wa thelathini na nane wa utawala wa Azaria mfalme wa Yuda, Zekaria mwana wa Yeroboamu akawa mfalme wa Israeli katika Samaria, naye akatawala miezi sita.
Katika mwaka wa thelathini na nane mwaka wa Azaria mfalme wa Yuda, Zekaria mwana wa Yeroboamu akatawala juu ya Israeli katika Samaria kwa miezi sita.
9 Akafanya maovu machoni pa Bwana, kama baba zake walivyofanya. Hakuziacha dhambi za Yeroboamu mwana wa Nebati ambazo alisababisha Israeli kuzitenda.
Alifanya yaliyo maovu usoni mwa Yahwe, kama baba zake waliyoyafanya. Hakuziacha dhambi za Yeroboamu mwana wa Nabeti, ambaye alisababisha Israeli kuasi
10 Shalumu mwana wa Yabeshi akafanya shauri baya dhidi ya Zekaria. Akamshambulia mbele ya watu, akamuua na kuingia mahali pake kuwa mfalme.
Shalumu mwana wa Yabeshi akafanya njama dhidi ya Zekaria, akamshambulia katika Ibleamu, na kumuua. Kisha akawa mfalme katika mahala pake.
11 Matukio mengine ya utawala wa Zekaria yameandikwa kwenye kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli.
Kama kwa mambo mengine yanayomuhusu Zekaria, yameandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli.
12 Kwa hiyo neno la Bwana lililonenwa kwa Yehu likatimia, kwamba, “Wazao wako wataketi juu ya kiti cha enzi cha Israeli hadi kizazi cha nne.”
Hili ndilo lililokuwa neno la Yahwe ambalo aliongea na Yehu, kusema, “Kizazi chako kitakaa katika kiti cha Israeli mpaka kizazi cha nne.” Hiyo ikatokea.
13 Shalumu mwana wa Yabeshi akawa mfalme katika mwaka wa thelathini na tisa wa Uzia mfalme wa Yuda, naye akatawala katika Samaria kwa mwezi mmoja.
Shalumu mwana wa Yabeshi akaanza kutawala katika mwaka wa thelathini na tisa wa Azaria mfalme wa Yuda, na kutawala kwa mwezi mmoja tu katika Samaria.
14 Kisha Menahemu mwana wa Gadi akaenda kutoka Tirsa mpaka Samaria. Akamshambulia Shalumu mwana wa Yabeshi huko Samaria, akamuua na kuingia mahali pake kuwa mfalme.
Menahemu mwana wa Gadi akapanda kutoka Tirza kwenda Samaria. Akamshambulia Shalumu mwana wa Yabeshi hapo, katika Samria. Akamuua na kuwa mfalme katika mahali pake.
15 Matukio mengine ya utawala wa Shalumu, na mauaji aliyoyafanya, yameandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli.
Kama kwa mambo mengine yanayomuhusu Shalumu na njama aliyoifanya, yameandikwa kwenye kitabu cha matukio cha wafle wa Israeli.
16 Wakati ule, akianzia Tirsa, Menahemu alishambulia Tifsa na kila mtu ndani yake, na wale waliokuwa maeneo jirani, kwa sababu walikataa kufungua malango yao. Akaiangamiza Tifsa yote, na kuwapasua matumbo wanawake wote wenye mimba.
Ndipo Menahemu akamshambulia Tifsa na wote waliokuwa pale, na mipaka yote kuzunguka Tizra, kwasababu hawakufungua kwenye mji. Hivyo akaushambulia, na akawapasua wanawake wajawazito wote katika hicho kijiji.
17 Katika mwaka wa thelathini na tisa wa utawala wa Azaria mfalme wa Yuda, Menahemu mwana wa Gadi akawa mfalme wa Israeli, akatawala huko Samaria kwa miaka kumi.
Katika mwaka wa thelathini na tisa wa Ahazia mfalme wa Yuda, Menahemu mwana wa Gadi akaanza kutawala; alitawala kwa miaka kumi katika Samaria.
18 Akatenda maovu machoni pa Bwana. Katika wakati wa utawala wake wote, hakuziacha dhambi za Yeroboamu mwana wa Nebati ambazo alisababisha Israeli kuzitenda.
Alifanya yaliyo maovu usoni mwa Yahwe. Katika maisha yake yote, hakuziacha dhambi za Yeroboamu mwana wa Nabeti, ambaye alifanya Israeli kufanya dhambi.
19 Kisha Pulu mfalme wa Ashuru akaishambulia Israeli. Menahemu mfalme wa Israeli akampa talanta elfu moja za fedha ili amsaidie na kumwezesha katika utawala wake.
Kisha Pulu mfalme wa Ashuru akaja kinyume cha nchi, na Menahemu akampatia Pulu talanta elfu moja za fedha, hivyo msaada wa Pulu ungeweza kuwa na yeye kuimarisha utawala wa Israeli katika nchi yake.
20 Menahemu akatoza fedha hizi kwa nguvu kutoka kwa Israeli. Kila mtu tajiri alilazimika kuchanga shekeli hamsini za fedha ambazo alipewa mfalme wa Ashuru. Basi mfalme wa Ashuru akajiondoa na hakuendelea kuikalia nchi.
Menahemu akatoza hii pesa kutoka Israeli kwa kumtaka kila mtu tajiri alipe shekeli hamsini za fedha kwake kumpatia mfalme wa Ashura. Hivyo mfalme wa Ashuru akarudi na hakukaa pale katika ile nchi.
21 Matukio mengine ya utawala wa Menahemu na yote aliyoyafanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli?
Kama kwa mabo mengine yanayomuhusu Menahemu, na yote aliyoyafanya, je hayajaandikwa kwenye kitabu cha matukio ya waflme wa Israeli?
22 Menahemu akalala pamoja na baba zake. Naye Pekahia mwanawe akawa mfalme baada yake.
Hivyo Menahemu akalala pamoja na babu zake, na Pekahia mtoto wake akawa mfalme katika mahala pake.
23 Katika mwaka wa hamsini wa utawala wa Azaria mfalme wa Yuda, Pekahia mwana wa Menahemu akawa mfalme wa Israeli huko Samaria, akatawala miaka miwili.
Katika mwaka wa hamsini wa Azaria mfalme wa Yuda, Pekahia mwana wa Menahemu akaanza kutawala juu ya Israeli katika Samaria; alitawala kwa muda wa miaka miwili.
24 Pekahia akafanya uovu machoni pa Bwana. Hakuziacha dhambi za Yeroboamu mwana wa Nebati, ambazo alisababisha Israeli kuzitenda.
Alifanya yaliyo maovu usoni pa Yahwe. Hakuziacha dhambi za Yeroboamu mwana wa Nabeti, ambazo kwa hizo alisababisha Israeli kufanya dhambi.
25 Mmoja wa maafisa wake wakuu, Peka mwana wa Remalia, akafanya shauri baya dhidi yake. Akachukua watu hamsini wa Gileadi pamoja naye, akamuua Pekahia, pamoja na Argobu na Aria, katika ngome ya jumba la kifalme huko Samaria. Kwa hiyo Peka akamuua Pekahia, naye akaingia mahali pake kuwa mfalme.
Pekahia alikuwa na afisa aliyekuwa anaitwa Peka mwana wa Remalia, ambaye alifanya njama dhidi yake. Pamoja na watu hamsini wa Gileadi, Peka akamuua Pekahia pamoja na Argobu na Arie katika Samaria, katika ngome ya nyumba ya mfalme. Peka akamuua alipomua Pekahia akawa mfalme katika mahala pake.
26 Matukio mengine ya utawala wa Pekahia na yote aliyoyafanya yameandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli.
Kama kwa mambo mengine yanayomuhusu Pekahia, yote aliyoyafanya, yameandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli.
27 Katika mwaka wa hamsini na mbili wa utawala wa Azaria mfalme wa Yuda, Peka mwana wa Remalia akawa mfalme wa Israeli huko Samaria, naye alitawala miaka ishirini.
Katika mwaka wa hamsini na mbili wa Azia mfalme wa Yuda, Peka mwana wa Remalia akaanza kutawala juu ya Israeli katika Samaria; alitawala miaka Ishirini.
28 Akafanya maovu machoni pa Bwana. Hakuziacha dhambi za Yeroboamu mwana wa Nebati, ambazo alisababisha Israeli kuzitenda.
Alifanya yaliyo maovu usoni mwa Yahwe. Hakuziacha dhambi za Yeroboamu mwana wa Nabati, ambaye alisababisha Israeli kufanya dhambi.
29 Wakati wa utawala wa Peka mfalme wa Israeli, Tiglath-Pileseri mfalme wa Ashuru alikuja na kuteka Iyoni, Abel-Beth-Maaka, Yanoa, Kedeshi na Hazori. Akateka miji ya Gileadi na Galilaya, pamoja na nchi yote ya Naftali, na kuwahamishia watu wote Ashuru.
Katika siku za Peka mfalme wa Israeli, Tiglath Pileseri mfalme wa Ashuru akaja na kuichukua Iyoni, Abel Beth Maaka, Yanoa, Kadeshi, Hazori, Gileadi, na nchi yote ya Naftali. Akawachukua hao watu hadi Ashuru.
30 Kisha Hoshea mwana wa Ela akafanya shauri baya dhidi ya Peka mwana wa Remalia. Akamshambulia na kumuua, kisha akaingia mahali pake kuwa mfalme katika mwaka wa ishirini wa Yothamu mwana wa Uzia.
Hivyo Hoshea mwana wa Ela akafanya njama dhidi ya Peka mwana wa Remalia. Akaishambulia na kisha kumuua. Kisha akawa mfalme katika mahali pake, katika mwaka wa ishirini wa Yothamu mwana wa Uzia.
31 Matukio mengine ya utawala wa Peka na yote aliyoyafanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli?
Kama kwa mambo mengine yanayomuhusu Peka, yote aliyoyafanya, yameandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli.
32 Katika mwaka wa pili wa utawala wa Peka mwana wa Remalia mfalme wa Israeli, Yothamu mwana wa Uzia mfalme wa Yuda alianza kutawala.
Katika mwaka wa pili wa Peka mwana wa Remalia, mfalme wa Israeli, Yothamu mwana wa Azaria, mfalme wa Yuda akaanza kutawala.
33 Alikuwa na miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka kumi na sita. Mama yake aliitwa Yerusha binti Sadoki.
Alikuwa na umri wa miaka ishirini alipoanza kutawala; alitawala kwa muda wa miaka kumi na sita katika Yerusalimu. Mama yake alikuwa anaitwa Yerusha; alikuwa binti ya Sadoki.
34 Akafanya yaliyo mema machoni pa Bwana, kama Uzia baba yake alivyokuwa amefanya.
Yotahmu alifanya yaliyo sahihi usoni pa Yahwe. Alifuata mfano wa yote baba yake Azaria aliyofanya.
35 Hata hivyo, mahali pa juu pa kuabudia hapakuondolewa. Watu waliendelea kutoa kafara na kufukiza uvumba huko. Yothamu akajenga upya Lango la Juu la Hekalu la Bwana.
Ila, mahali pa juu hapakuchukuliwa. Watu walikuwa wakitio sadaka na kufukiza ubani katika mahali pa juu. Yothamu akajenga lango la juu la nyumba ya Yahwe.
36 Matukio mengine ya utawala wa Yothamu na yale aliyoyafanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Yuda?
Kama kwa mambo mengine yanayomuhusu Yothamu, na yote aliyoyafanya, je yameandikwa katika kitabu cha matukio ya wafalme wa Yuda?
37 (Katika siku hizo, Bwana akaanza kuwatuma Resini mfalme wa Aramu na Peka mwana wa Remalia dhidi ya Yuda.)
Katika zamani hizo Yahwe akaanza kumtuma dhidi ya Yuda Rezini mfalme wa Sahmu, na Peka mwana wa Remalia.
38 Yothamu akalala na baba zake, akazikwa pamoja nao katika Mji wa Daudi, mji wa baba zake. Naye Ahazi mwanawe akawa mfalme baada yake.
Yothamu akalala pamoja na babu zake na akazikwa pamoja na babu zake katika mji wa Daudi, babu yake. Kisha Ahazi, mtoto wake, akwa mfalme katika mhali pake.