< 2 Wakorintho 6 >
1 Kama watendakazi pamoja na Mungu, tunawasihi msipokee neema ya Mungu bure.
We then, as workers together with him, beseech you also that ye receive not the grace of God in vain.
2 Kwa maana asema: “Wakati wangu uliokubalika nilikusikia, siku ya wokovu nilikusaidia.” Tazama, wakati uliokubalika ndio huu, siku ya wokovu ndiyo sasa.
( For he saith, I have heard thee in a time accepted, and in the day of salvation have I succoured thee: behold, now is the accepted time; behold, now is the day of salvation.)
3 Hatuweki kitu cha kukwaza katika njia ya mtu yeyote, ili huduma yetu isionekane kuwa na lawama.
Giving no offence in any thing, that the ministry be not blamed:
4 Bali kama watumishi wa Mungu tuonyeshe kwa kila njia: katika saburi nyingi; katika dhiki, katika misiba, na katika shida;
But in all things approving ourselves as the ministers of God, in much patience, in afflictions, in necessities, in distresses,
5 katika kupigwa, katika kufungwa gerezani na katika ghasia; katika kazi ngumu, katika kukesha na katika kufunga;
In stripes, in imprisonments, in tumults, in labours, in watchings, in fastings;
6 katika utakatifu, katika ufahamu, katika uvumilivu, na katika utu wema; katika Roho Mtakatifu na upendo wa kweli;
By pureness, by knowledge, by longsuffering, by kindness, by the Holy Ghost, by love unfeigned,
7 katika maneno ya kweli na katika nguvu za Mungu, kwa silaha za haki za mkono wa kuume na za mkono wa kushoto;
By the word of truth, by the power of God, by the armour of righteousness on the right hand and on the left,
8 katika utukufu na katika kudharauliwa; katika sifa mbaya na katika sifa nzuri; tukiwa kama wadanganyaji, lakini tukiwa wakweli;
By honour and dishonour, by evil report and good report: as deceivers, and yet true;
9 tukiwa maarufu, lakini tukihesabiwa kama tusiojulikana; tukiwa kama wanaokufa, lakini tunaishi; tukipigwa, lakini hatuuawi;
As unknown, and yet well known; as dying, and, behold, we live; as chastened, and not killed;
10 tukiwa kama wenye huzuni, lakini siku zote tukifurahi; tukionekana maskini, lakini tukitajirisha wengi; tukiwa kama wasio na kitu, lakini tuna vitu vyote.
As sorrowful, yet alway rejoicing; as poor, yet making many rich; as having nothing, and yet possessing all things.
11 Tumesema nanyi wazi, enyi Wakorintho na kuwafungulieni mioyo yetu wazi kabisa.
O ye Corinthians, our mouth is open unto you, our heart is enlarged.
12 Sisi hatujizuii kuwapenda, bali ninyi mmeuzuia upendo wenu kwetu.
Ye are not straitened in us, but ye are straitened in your own bowels.
13 Sasa nasema, kama na watoto wangu: Ninyi pia ifungueni mioyo yenu kabisa.
Now for a recompence in the same, ( I speak as unto my children, ) be ye also enlarged.
14 Msifungiwe nira pamoja na watu wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa, kwa maana pana uhusiano gani kati ya haki na uovu? Au kuna ushirika gani kati ya nuru na giza?
Be ye not unequally yoked together with unbelievers: for what fellowship hath righteousness with unrighteousness? and what communion hath light with darkness?
15 Kuna mapatano gani kati ya Kristo na Beliari? Yeye aaminiye ana sehemu gani na yeye asiyeamini?
And what concord hath Christ with Belial? or what part hath he that believeth with an infidel?
16 Kuna mapatano gani kati ya Hekalu la Mungu na sanamu? Kwa kuwa sisi tu Hekalu la Mungu aliye hai. Kama Mungu alivyosema: “Nitakaa pamoja nao na kutembea katikati yao, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.”
And what agreement hath the temple of God with idols? for ye are the temple of the living God; as God hath said, I will dwell in them, and walk in them; and I will be their God, and they shall be my people.
17 “Kwa hiyo tokeni miongoni mwao, mkatengwe nao, asema Bwana. Msiguse kitu chochote kilicho najisi, nami nitawakaribisha.”
Wherefore come out from among them, and be ye separate, saith the Lord, and touch not the unclean thing; and I will receive you,
18 “Mimi nitakuwa Baba kwenu, nanyi mtakuwa wanangu na binti zangu, asema Bwana Mwenyezi.”
And will be a Father unto you, and ye shall be my sons and daughters, saith the Lord Almighty.