< 2 Nyakati 1 >
1 Solomoni mwana wa Daudi alijiimarisha kwenye milango yote! Katika ufalme wake, kwa kuwa Bwana Mungu wake alikuwa pamoja naye, naye akamfanya mkuu mno.
Selemani mwana wa Daudi, aliimariswa katika utawala wake, na Yahwe Mungu wake alikuwa pamoja naye na alimpa nguvu nyingi sana.
2 Ndipo Solomoni akasema na Israeli wote, majemadari wa maelfu na majemadari wa mamia, waamuzi na viongozi wote katika Israeli, pamoja na wakuu wa jamaa.
Sulemani akasema kwa Israleli wote, na maakida wa maelfu na wa mamia, na kwa waamuzi, na kwa kila mfalme kiongozi katika Israeli yote, wakuu wa kaya.
3 Naye Solomoni na kusanyiko lote wakakwea mpaka mahali pa juu pa kuabudia huko Gibeoni, kwa kuwa huko ndiko Hema la Kukutania la Mungu lilipokuwa, ambalo Mose mtumishi wa Bwana alikuwa amelitengeneza huko jangwani.
Hivyo Sulemani na kusanyiko lote wakaenda pamoja naye sehemu ya juu iliyokuwa Gibeoni, maana ndipo palikuwepo hema ya kukutania ya Mungu, ambayo Musa mtumishi wa Yahwe, alikuwa ameitengeneza jangwani.
4 Basi Daudi alikuwa amelipandisha Sanduku la Mungu kutoka Kiriath-Yearimu mpaka mahali alipokuwa amepatengeneza kwa ajili yake, kwa sababu alikuwa amesimamisha hema kwa ajili ya hilo Sanduku huko Yerusalemu.
Lakini Daudi alikuwa ameleta pale sanduku la Mungu kutoka Kiriath yeriam hadi sehemu ambayo alikuwa ametayarisha, maana alikuwa ameliandalia hema huko katika Yerusalemu.
5 Lakini yale madhabahu ya shaba ambayo Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, alikuwa ametengeneza yalikuwa huko Gibeoni mbele ya Maskani ya Bwana Mungu, hivyo Solomoni na kusanyiko lote walimtafuta Mungu huko.
Zaidi ya hayo, madhabahu ya shaba iliyotengenezwa na Bezaleli mwana wa uri mwana wa Huri ilikuwepo huko kabla ya mbele ya madhabahu ya Yahwe; Sulemani na kusanyiko wakaenda ilikokuwa. (Maandiko ya zamani yanasema
6 Solomoni akapanda huko yalikokuwa madhabahu ya shaba mbele za Bwana katika Hema la Kukutania, na kutoa dhabihu 1,000 za sadaka za kuteketezwa juu yake.
Selemani akaenda huko kwenye kwenye madhabahu ya shaba mbele za Yahwe, ambayo ilikuwepo mahali pa hema ya kukutamia, na akatoa sadaka elfu za kuteketezwa juu yake.
7 Usiku ule Mungu akamtokea Solomoni na kumwambia, “Omba lolote utakalo nikupe.”
Mungu akamtokea Selemani usiku huo na akasema kwake, “Omba! Nikupe nini?”
8 Solomoni akamjibu Mungu, “Umemwonyesha baba yangu Daudi fadhili nyingi, nawe umeniweka niwe mfalme mahali pake.
Selemani akasema kwa Mungu, “Umeonesha agano la uaminifu mkuu kwa Daudi baba yangu, na umenifanya mfalme katika nafasi yaye.
9 Sasa, Bwana Mungu, ahadi yako kwa baba yangu Daudi na ithibitike, kwa kuwa umenifanya mimi mfalme juu ya watu ambao ni wengi kama mavumbi ya nchi.
Sasa, Yahwe Mungu, ahadi yako kwa Daudi baba yangu itimie, maana umenifanya mfalme juu ya watu wengi kama mavumbi ya dunia.
10 Nakuomba unipe mimi hekima na maarifa, ili niweze kuongoza watu hawa, kwa kuwa ni nani awezaye kutawala hawa watu wako walio wengi hivi?”
Sasa nipe hekima na maarifa, ili niweze kuwaongoza watu hawa, maana ni nani anayeweza kuwaamua watu wako, ambao ni wengi sana kwa idadi?”
11 Mungu akamwambia Solomoni, “Kwa kuwa jambo hili ndilo shauku ya moyo wako na hukuomba mali, utajiri au heshima, wala kifo kwa ajili ya adui zako, nawe kwa kuwa hukuomba maisha marefu, bali umeomba hekima na maarifa ili kuongoza watu wangu ambao nimekufanya uwe mfalme juu yao,
Mungu akasema kwa Selemani, “Kwa kuwa hili lilikuwa kwenye moyo wako, na kwa kuwa hujaomba mali, utajiri, au heshima, wala maisha ya wale wanaokuchukia, wala maish marefu kwa jili yako binafsi, lakini umeomba hekima na maarifa kwa ajili yako, ili uwatawale watu wangu, ambao juu yao nimekufanya mfame, na hivi ndivyo nitafanya.
12 kwa hiyo utapewa hekima na maarifa. Tena nitakupa pia mali, utajiri na heshima, ambavyo hakuna mfalme yeyote aliyekuwepo kabla yako amewahi kuwa navyo, na hakuna yeyote baada yako atakayekuwa navyo.”
Sasa nitakupa hekima na maarifa, pia nitakupa mali na utajiri, na heshima, kuliko wafalme wote waliokuwepo kabla yako walivyokuwa, na baada yako hakuna yeyote atakayekuwa navyo.”
13 Ndipo Solomoni akaenda mpaka Yerusalemu kutoka mahali pa juu pa kuabudia huko Gibeoni, kutoka mbele ya Hema la Kukutania. Naye akatawala Israeli.
Kwa hiyo Selemani akaenda Yerusalemu kutoka sehemu ya juu iliyokuwepo Gibeoni, kutoka mbele ya hema ya kukutania; akatawala juu ya Israeli.
14 Solomoni akakusanya magari ya vita na farasi. Alikuwa na magari 1,400 na farasi 12,000, ambayo aliyaweka katika miji ya magari na mengine akawa nayo huko Yerusalemu.
Selemani akakusanya magari na wanaume waendesha farasi, naye alikuwa na magari 1, 400 na waendesha farasi kumi na mbili elfu ambao aliwaweka katika miji ya magari, pamoja naye, mfalme katika Yerusalemu.
15 Mfalme akafanya fedha na dhahabu kuwa vitu vya kawaida kama mawe huko Yerusalemu, mierezi akaifanya kuwa mingi kama mikuyu vilimani.
Mfalme akatengeneza fedha na dhahabu kuwa vitu vya kawaida kama mawe katika Yerusalemu, na mbao za mierezi kuwa kama miti ya mikuyu iliyomo katika nyanda za chini.
16 Farasi wa Solomoni waliletwa kutoka Misri na kutoka Kue. Wafanyabiashara wa mfalme waliwanunua kutoka Kue.
Selemani katika uagizaji wa farasi kutoka Misiri, wafanya biashara wake walinunua farasi kutoka Misiri kwa bei stahiki.
17 Waliagiza magari kutoka Misri kwa bei ya shekeli 600 za fedha, na farasi kwa shekeli 150. Pia waliwauza nje kwa wafalme wote wa Wahiti na wa Waaramu.
Waliagiza gari kutoka Misiri kwa shekeli mia sita za fedha, na farasi mmoja kwa shekeli 150. Pia walinunua kutoka kwa wafalme wa Wahiti na wafalme wa Washamu.