< 2 Nyakati 7 >
1 Baada ya Solomoni kumaliza kuomba, moto ukashuka kutoka mbinguni na kuteketeza sadaka ya kuteketezwa na dhabihu, nao utukufu wa Bwana ukalijaza Hekalu.
Süleyman duasını bitirince, gökten ateş yağdı; yakmalık sunularla kurbanları yiyip bitirdi. RAB'bin görkemi tapınağı doldurdu.
2 Makuhani hawakuweza kuingia ndani ya Hekalu la Bwana kwa sababu utukufu wa Bwana ulilijaza.
RAB'bin Tapınağı O'nun görkemiyle dolunca kâhinler tapınağa giremediler.
3 Waisraeli wote walipoona moto ukishuka na utukufu wa Bwana ukiwa juu ya Hekalu, wakapiga magoti sakafuni wakasujudu nyuso zao mpaka chini, nao wakamwabudu na kumshukuru Bwana wakisema, “Yeye ni mwema; upendo wake unadumu milele.”
Gökten yağan ateşi ve tapınağın üzerindeki RAB'bin görkemini gören İsrailliler avluda yüzüstü yere kapandılar; RAB'be tapınarak O'nu övdüler: “RAB iyidir; Sevgisi sonsuza dek kalıcıdır.”
4 Ndipo mfalme na watu wote wakatoa dhabihu mbele za Bwana Mungu.
Kral ve bütün halk RAB'bin önünde kurban kestiler.
5 Naye Mfalme Solomoni akatoa dhabihu ya ngʼombe 22,000 pamoja na kondoo na mbuzi 120,000. Hivyo ndivyo mfalme na watu wote walivyoweka wakfu Hekalu la Mungu.
Kral Süleyman yirmi iki bin sığır, yüz yirmi bin davar kurban etti. Böylece kral ve halk Tanrı'nın Tapınağı'nı adamış oldular.
6 Makuhani wakasimama kwenye nafasi zao, vivyo hivyo Walawi wakiwa na vyombo vya uimbaji vya Bwana ambavyo Mfalme Daudi alikuwa ametengeneza kwa ajili ya kumsifu Bwana, navyo vilitumika wakati aliposhukuru, akisema, “Upendo wake wadumu milele.” Mkabala na Walawi, makuhani walipiga tarumbeta zao, nao Waisraeli wote walikuwa wamesimama.
Kâhinler yerlerini almışlardı. Kral Davut'un RAB'bi övmek için yaptırdığı ve “RAB'bin sevgisi sonsuza dek kalıcıdır” diyerek överken kullandığı çalgıları alan Levililer de yerlerini almıştı. Levililer'in karşısında duran kâhinler borazanlarını çalıyorlardı. Bu sırada bütün İsrailliler ayakta duruyordu.
7 Solomoni akaweka wakfu sehemu ya katikati ya ua uliokuwa mbele ya Hekalu la Bwana na hapo akatoa sadaka za kuteketezwa na mafuta ya sadaka za amani, kwa sababu madhabahu ya shaba aliyokuwa ametengeneza haikutosha kuweka sadaka hizo zote za kuteketezwa, sadaka za nafaka na za mafuta.
Süleyman RAB'bin Tapınağı'nın önündeki avlunun orta kısmını kutsadı. Yakmalık sunularla esenlik sunularının yağlı parçalarını orada sundu. Çünkü yaptırdığı tunç sunak yakmalık sunuları, tahıl sunularını ve yağlı parçaları almadı.
8 Hivyo Solomoni akaiadhimisha sikukuu wakati ule kwa muda wa siku saba, na Israeli wote pamoja naye. Walikuwa kusanyiko kubwa sana, watu kutoka Lebo-Hamathi hadi Kijito cha Misri.
Süleyman, Levo-Hamat'tan Mısır Vadisi'ne kadar her yerden gelen İsrailliler'in oluşturduğu çok büyük bir toplulukla birlikte bayramı yedi gün kutladı.
9 Katika siku ya nane walifanya kusanyiko, kwa kuwa walikuwa wanaadhimisha kuwekwa wakfu kwa madhabahu kwa muda wa siku saba na sikukuu kwa muda wa siku nyingine saba zaidi.
Sekizinci gün kutsal bir toplantı yaptılar. Sunağı adamaya yedi gün, bayramı kutlamaya da yedi gün ayırdılar.
10 Katika siku ya ishirini na tatu ya mwezi wa saba Solomoni akawaaga watu waende nyumbani mwao, wakishangilia na kufurahi mioyoni mwao, kwa wema mwingi Bwana Mungu aliomtendea Daudi na Solomoni na kwa ajili ya watu wake Israeli.
Kral yedinci ayın yirmi üçüncü günü halkı evlerine gönderdi. RAB'bin, Davut, Süleyman ve halkı İsrail için yapmış olduğu iyilikten dolayı hepsi mutluydu, sevinçle coşuyordu.
11 Solomoni alipomaliza kujenga Hekalu la Bwana na jumba la kifalme, naye akiwa amefanikiwa kutenda yale yote aliyokuwa nayo moyoni mwake kufanya katika Hekalu la Bwana na katika jumba lake mwenyewe la kifalme,
Süleyman RAB'bin Tapınağı'nı, sarayı ve RAB'bin Tapınağı'yla kendi sarayında yapmayı istediği bütün işleri başarıyla bitirince,
12 Bwana akamtokea Solomoni usiku na kumwambia: “Nimesikia maombi yako nami nimechagua mahali hapa kwa ajili yangu mwenyewe kuwa Hekalu kwa ajili ya dhabihu.
RAB geceleyin ona görünerek şöyle dedi: “Duanı duydum. Burayı kendime kurban sunulan tapınak olarak seçtim.
13 “Wakati nitakapofunga mbingu ili isiwepo mvua, au nikiamuru nzige kula mazao ya nchi au nikituma tauni miongoni mwa watu wangu,
“Yağmur yağmasın diye göğü kapadığımda, toprağın ürününü yiyip bitirmesi için çekirgelere buyruk verdiğimde ya da halkımın arasına salgın hastalık gönderdiğimde,
14 kama watu wangu, wanaoitwa kwa Jina langu, watajinyenyekesha na kuomba na kuutafuta uso wangu na kuacha njia zao mbaya, basi nitasikia toka mbinguni na kuwasamehe dhambi yao na nitaiponya nchi yao.
adımla çağrılan halkım alçakgönüllülüğü takınır, bana yönelip dua eder, kötü yollarından dönerse, gökten onları duyacağım, günahlarını bağışlayıp ülkelerini sağlığa kavuşturacağım.
15 Sasa macho yangu yatafumbuka na masikio yangu yatasikiliza kwa makini maombi yaombwayo mahali hapa.
Gözlerim burada edilen duaya açık, kulaklarım işitici olacak.
16 Kwa maana sasa nimechagua na kutakasa Hekalu hili ili kwamba Jina langu lipate kuwa huko milele. Macho yangu na moyo wangu utakuwepo huko daima.
Adım sürekli orada bulunsun diye bu tapınağı seçip kutsal kıldım. Gözlerim onun üstünde, yüreğim her zaman orada olacaktır.
17 “Kwa habari yako wewe, kama ukienenda mbele zangu kama Daudi baba yako alivyoenenda na kufanya yote nikuamuruyo, nawe ukizishika amri zangu na sheria zangu,
Sana gelince, baban Davut'un yaptığı gibi yollarımı izler, buyurduğum her şeyi yapar, kurallarıma ve ilkelerime uyarsan,
18 Nitakiimarisha kiti chako cha enzi kama nilivyoagana na Daudi baba yako niliposema, ‘Hutakosa kamwe mtu wa kutawala juu ya Israeli.’
baban Davut'la, ‘İsrail tahtından senin soyunun ardı arkası kesilmeyecektir’ diye yaptığım antlaşmaya bağlı kalıp krallığını pekiştireceğim.
19 “Lakini kama ukigeuka na kuyaacha maagizo na amri nilizowapa na kwenda kuitumikia miungu mingine na kuiabudu,
“Ama siz yollarımdan sapar, kurallarımı, buyruklarımı bırakır, gidip başka ilahlara kulluk eder, taparsanız,
20 ndipo nitakapoingʼoa Israeli kutoka nchi yangu niliyowapa, nami nitalikataa Hekalu hili nililolitakasa kwa ajili ya Jina langu. Nitalifanya kitu cha kudharauliwa na kitu cha kudhihakiwa miongoni mwa watu wote.
size verdiğim ülkeden sizi söküp atacağım, adıma kutsal kıldığım bu tapınağı terk edeceğim; burayı bütün ulusların aşağılayıp alay ettiği bir yer durumuna getireceğim.
21 Ingawa Hekalu hili linavutia sana sasa, wote watakaolipita watashangaa na kusema, ‘Kwa nini Bwana amefanya kitu kama hiki katika nchi hii na kwa Hekalu hili?’
Bu gösterişli tapınağın önünden geçenler hayretle, ‘RAB bu ülkeyi ve tapınağı neden bu duruma getirdi?’ diye soracaklar.
22 Watu watajibu, ‘Ni kwa sababu wamemwacha Bwana, Mungu wa baba zao, aliyewatoa Misri, nao wamekumbatia miungu mingine, wakaiabudu na kuitumikia, ndiyo sababu ameyaleta maafa haya yote juu yao.’”
Ve diyecekler ki, ‘İsrail halkı, atalarını Mısır'dan çıkaran Tanrıları RAB'bi terk etti; başka ilahların ardından gitti, onlara tapıp kulluk etti. RAB bu yüzden bu kötülükleri başlarına getirdi.’”