< 2 Nyakati 4 >

1 Mfalme Solomoni akatengeneza madhabahu ya shaba yenye urefu wa dhiraa ishirini, upana wa dhiraa ishirini na kimo chake dhiraa kumi.
Vivile akatengeneza madhabahu ya shaba; urefu wake ulikuwa mikono ishirini, na upana wake ulikuwa mikono ishirini.
2 Akatengeneza Bahari ya kusubu, yenye umbo la mviringo, ya dhiraa kumi kutoka ukingo hadi ukingo na kimo cha dhiraa tano. Kamba ya urefu wa dhiraa thelathini ingeweza kuizunguka.
Pia akatengeneza bahari ya mduara ya chuma cha kuyeyushwa, mikono kumi kutoka ukingo hadi ukingo. Urefu wake kwenda juu ulikuwa mikono mitano, na bahari ilikuwa na mzunguko wa mikono thelatinini.
3 Chini ya huo ukingo, kulikuwa na mafahali kuizunguka, yaani mafahali kumi katika kila dhiraa moja. Hayo mafahali waliyasubu katika safu mbili yakiwa ya kitu kimoja na hiyo Bahari.
Chini ya kingo kuzunguka bahari kulikuwapo ng'ombe dume, kumi kila mkono,
4 Bahari hiyo ilikaa juu ya mafahali kumi na wawili, mafahali watatu walielekeza nyuso zao kaskazini, watatu magharibi, watatu kusini na watatu mashariki. Bahari hiyo ilikaa juu ya hao mafahali, nazo sehemu zao za nyuma zilielekeana.
Bahari ilisimama juu ya ng'ombe wa kulima kumi na wawili, watatu wakiangalia kaskazini, watatu wakiangalia magharibi, na watatu wakiangalia kusini, na watatu wakiangalia mashariki. Bahari iliwekwa juu yao, na robo ya sehemu zao za nyuma zote zilikuwa ndani.
5 Unene wake ulikuwa nyanda nne, na ukingo wake ulifanana na ukingo wa kikombe, kama ua la yungiyungi iliyochanua. Iliweza kuchukua bathi 3,000.
Bahari ilikuwa nene kama upana wa mkono, na ukingo wake ulikuwa kama ukingo wa kikombe, kama ua la yungi. Bahari ilikuwa na mabafu elfu tatu ya maji.
6 Kisha akatengeneza masinia kumi kwa ajili ya kuoshea vifaa, naye akayaweka matano upande wa kusini na matano upande wa kaskazini. Ndani yake ndimo walioshea vifaa vya kutumika katika sadaka za kuteketezwa, lakini ile Bahari ilikuwa ni kwa ajili ya makuhani kunawia.
Pia akatengeneza birika kumi kwa ajili ya kuoshea vitu; tano akaziweka mkono wa kulia, na tano akaziweka kushoto; vifaa vilivyotumika katika kufanayia sadaka za kuteketezwa zilipaswa kuoshwa ndani ya hizo birika. Bahari, vilevile ilikuwa kwa ajili ya makauhani kuoga humo.
7 Akatengeneza vinara vya taa kumi vya dhahabu kama ilivyoainishwa kwao na kuviweka hekaluni, vinara vitano upande wa kusini na vitano upande wa kaskazini.
Akatengeza vinara vya taa kumi vya dhahabu ambavyo vilitengenezwa kutokana na maelekezo ya jinsi vilivyopaswa kuwa; akaviweka hekaluni, vitanao mkno wa kulia, na vitano mkono wa kushoto.
8 Akatengeneza meza kumi na kuziweka hekaluni, tano upande wa kusini na tano upande wa kaskazini. Pia akatengeneza mabakuli 100 ya dhahabu ya kunyunyizia.
Akatengeneza meza kumi na kuziweka hekaluni, tano upande wa kulia, na tano upande wa kushoto. Akatengeneza birika mia moja za dhahabu.
9 Akatengeneza ukumbi wa makuhani na ukumbi mwingine mkubwa na milango yake, naye akaifunika hiyo milango kwa shaba.
Zaidi ya hayo akatengeneza mahakama ya makuhani na mahakama kuu, na milangu kwa ajili ya mahakama, akaifunika milango yake kwa shaba.
10 Akaweka ile Bahari upande wa kusini, kwenye pembe ya kusini mashariki ya nyumba.
Akaiweka bahari upande wa kulia wa nyumba, masharika, ikielekea upande wa kusini.
11 Pia akatengeneza masufuria, masepetu na mabakuli ya kunyunyizia. Kwa hiyo Huramu akakamilisha kazi katika Hekalu la Mungu kama vile Mfalme Solomoni alikuwa amemwagiza, yaani:
Huramu akayatengeza masufuria, majembe, na mabakuli ya kunyunyizia. Hivyo Huramu akamaliza kazi aliyofanya kwa ajili ya mfalme Selemani katika nyumba ya Mungu:
12 zile nguzo mbili; yale mataji mawili yaliyokuwa juu ya hizo nguzo, zile nyavu mbili za kupamba hayo mataji mawili yenye umbo la bakuli yaliyowekwa juu ya zile nguzo;
zile nguzo mbili, taji mfano wa upinde zilizo kuwa juu ya zile nguzo mbili, na nyavu mbili za za mapambo zilizofunika zile taji mbili mfano wa upinde zilizokuwa juu ya zile nguzo.
13 yale makomamanga 400 kwa ajili ya hizo nyavu mbili (safu mbili za makomamanga kwa kila wavu yakipamba hayo mataji mawili yenye umbo la bakuli juu ya hizo nguzo);
Alikuwa ametengeneza makomamanga mia nne kwa ajili ya zile nyavu za mapambo: safu mbili za makomamanga kwa kila wavu ili kufunika vimbe mbili zilizo kuwa juu ya nguzo.
14 vishikio pamoja na masinia yake;
Pia akavitengeneza vitako na mabirika juu ya kitako,
15 hiyo Bahari na hao mafahali kumi na wawili chini yake;
bahari moja na wale ng'ombe kumi na wawili chini yake,
16 pia hayo masufuria, masepetu, uma za nyama na vyombo vingine vyote vilivyohusiana. Vitu vyote ambavyo Huramu-Abi alimtengenezea Mfalme Solomoni kwa ajili ya Hekalu la Bwana vilikuwa vya shaba iliyosuguliwa.
pia masufuria, majembe, nyuma za nyama, na vyombo vingine vyote. Huramu mtaalamu akavifanya kwa ajili ya Mfalme Selemani, kwa ajili ya nyumba ya Yahwe, vya shaba iliyong'arishwa.
17 Mfalme aliagiza wavisubu vitu hivi kwenye kalibu za udongo wa mfinyanzi katika uwanda wa Yordani kati ya Sukothi na Sereda.
Mfalme alikuwa amevisubu katika uwanda wa Yordani, katika udongo wa mfinyanzi kati kati ya Sukothi na Sereda.
18 Vitu hivi vyote Mfalme Solomoni alivyotengeneza vilikuwa vingi sana hivi kwamba uzito wa shaba haungekadirika.
Hivyo ndivyo Selemani alivyovitengeneza vyombo vyote kwa wingi; kwa kweli, uzito wa shaba haukuweza kujulikana.
19 Solomoni pia akatengeneza samani zote zilizokuwa ndani ya Hekalu la Mungu: madhabahu ya dhahabu; meza za kuweka mikate ya Wonyesho;
Selemani akazitengeza samani zote ambazo zilikuwa kwenye nyumba ya Mungu, pia madhabahu ya dhahabu, na meza ambazo juu yake mkate wa uwepo ulipaswa kuwekwa;
20 vinara vya taa vya dhahabu safi pamoja na taa zake ili ziwake mbele ya sehemu takatifu ya ndani kama ilivyoelekezwa;
vinara pamoja na taa zake, ambazo zilitengezwa ili kumulika mbele ya chumba cha ndani—hivi vilitengenezwa kwa dhahabu halisi;
21 maua ya dhahabu yaliyofanyizwa, taa na makoleo (vilikuwa vya dhahabu bora kabisa);
na maua, taa, na makoleo, ya dhahabu, dhahabu safi.
22 mikasi ya dhahabu safi, mabakuli ya kunyunyizia, masinia na vyetezo; milango ya dhahabu ya Hekalu: yaani milango ya ndani ya Patakatifu pa Patakatifu, na milango ya ukumbi mkuu.
Pia mikasi ya taa, na mabakuli, vijiko, na vikaango vya sadaka za kuteketezwa vyote vilitengenezwa kwa dhahabu safi. Kuhusu mlanago wa kuingilia kwenye nyumba, milango yake ya ndani kwenye patakatifu pa patakatifu na milango ya nyumba, ambayo ni, ya hekalu, ilitengenezwa kwa dhahabu.

< 2 Nyakati 4 >