< 2 Nyakati 35 >
1 Yosia akaadhimisha Pasaka kwa Bwana katika Yerusalemu, mwana-kondoo wa Pasaka akachinjwa siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza.
Moreouer Iosiah kept a Passeouer vnto the Lord in Ierusalem, and they slewe the Passeouer in the fourtenth day of the first moneth.
2 Akawaweka makuhani kwenye wajibu wao na kuwatia moyo katika utumishi wa Hekalu la Bwana.
And he appointed the Priestes to their charges, and incouraged them to the seruice of the house of the Lord,
3 Akawaambia Walawi, waliowafundisha Waisraeli wote na waliokuwa wamejiweka wakfu kwa ajili ya kazi ya Bwana, “Liwekeni hilo Sanduku takatifu katika Hekalu lile alilojenga Solomoni mwana wa Daudi mfalme wa Israeli. Halipaswi kubebwa huku na huko mabegani mwenu. Sasa mtumikieni Bwana Mungu wenu na watu wake Israeli.
And he sayd vnto the Leuites that taught all Israel and were sanctified vnto the Lord, Put the holy Arke in the house which Salomon the sonne of Dauid King of Israel did build: it shalbe no more a burden vpon your shoulders: serue now the Lord your God and his people Israel,
4 Jiandaeni kwa kufuata jamaa zenu katika migawanyo yenu, kufuatana na maelezo yaliyoandikwa na Daudi mfalme wa Israeli na mwanawe Solomoni.
And prepare your selues by the houses of your fathers according to your courses, as Dauid the King of Israel hath written, and according to the writing of Salomon his sonne,
5 “Simameni mahali patakatifu kwa kufuata migawanyo ya jamaa za baba zenu kulingana na koo zenu na pawepo Walawi kwa ajili ya kila mgawanyo wa nyumba ya baba zenu.
And stande in the Sanctuarie according to the deuision of the families of your brethren the children of the people, and after the deuision of the familie of the Leuites:
6 Chinjeni mwana-kondoo wa Pasaka, jitakaseni, nanyi kwa niaba ya koo zenu fanyeni maandalizi, mkitenda sawasawa na neno la Bwana kwa mkono wa Mose.”
So kill the Passeouer and sanctifie your selues, and prepare your brethren that they may doe according to the worde of the Lord by the hand of Moses.
7 Ndipo Yosia akawapa watu wote wana-mbuzi waliokuwepo jumla ya kondoo wapatao 30,000 kwa ajili ya sadaka ya Pasaka, pia na ngʼombe 10,000, vyote hivi kutoka mali binafsi ya mfalme.
Iosiah also gaue to the people sheepe, lambs and kiddes, all for the Passeouer, euen to all that were present, to the nomber of thirtie thousand, and three thousande bullocks: these were of the Kings substance.
8 Pia maafisa wake, wakatoa kwa hiari yao wakawapa watu, makuhani na Walawi. Hilkia, Zekaria na Yehieli, waliokuwa maafisa wakuu wa Hekalu la Mungu, wakawapa makuhani sadaka za Pasaka wana-kondoo na wana-mbuzi 2,600 na mafahali 300.
And his princes offred willingly vnto the people, to the Priests and to the Leuites: Hilkiah, and Zechariah, and Iehiel, rulers of the house of God, gaue vnto the Priests for the Passeouer, euen two thousand and sixe hundreth sheepe, and three hundreth bullockes.
9 Konania na nduguze wawili, Shemaya na Nethaneli, pamoja na Hashabia, Yeieli na Yozabadi waliokuwa viongozi wa Walawi, nao pia wakawapa Walawi wana-kondoo na wana-mbuzi 5,000 na mafahali 500, kwa ajili ya sadaka za Pasaka.
Conaniah also and Shemaiah and Nethaneel his brethren, and Hashabiah and Ieiel, and Iozabad, chiefe of the Leuites gaue vnto the Leuites for the Passeouer, fiue thousand sheepe, and fiue hundreth bullockes.
10 Huduma ilipomalizika kuandaliwa makuhani wakasimama mahali pao na Walawi katika migawanyo yao kama mfalme alivyokuwa ameamuru.
Thus the seruice was prepared, and the Priests stoode in their places, also the Leuites in their orders, according to the Kings commandement:
11 Wana-kondoo wa Pasaka wakachinjwa, nao makuhani wakanyunyiza ile damu waliyokabidhiwa, wakati Walawi wakiwa wanawachuna wale wanyama ngozi.
And they slewe the Passeouer, and the Priests sprinkled the blood with their handes, and the Leuites flayed them.
12 Wakatenga sadaka za kuteketezwa ili waweze kugawia ili migawanyo kwa kufuata jamaa za baba zao ili watoe sadaka kwa Bwana kama ilivyoandikwa katika Kitabu cha Mose. Wakafanya vivyo hivyo kwa wale mafahali.
And they tooke away from the burnt offering to giue it according to the deuisions of the families of the children of the people, to offer vnto the Lord, as it is written in the booke of Moses, and so of the bullockes.
13 Wakawaoka wale wanyama wa Pasaka kwenye moto kama ilivyoamriwa, wakachemsha zile sadaka takatifu kwenye vyungu, masufuria makubwa na vikaango na kuwagawia watu wote upesi.
And they rosted the Passeouer with fire, according to ye custome, but the sanctified things they sod in pots, pannes, and cauldrons, and distributed them quickely to all the people.
14 Hatimaye wakafanya maandalizi kwa ajili yao wenyewe na kwa ajili ya makuhani, kwa sababu wale makuhani, yaani, wazao wa Aroni, walikuwa wanatoa sadaka za kuteketezwa pamoja na zile sehemu zilizonona mpaka usiku. Hivyo Walawi wakafanya maandalizi kwa ajili yao wenyewe na kwa ajili ya makuhani wa uzao wa Aroni.
Afterwarde also they prepared for them selues and for the Priestes: for the Priestes the sonnes of Aaron were occupied in offering of burnt offrings, and the fat vntill night: therefore the Leuites prepared for them selues, and for the Priests the sonnes of Aaron.
15 Waimbaji, wazao wa Asafu, walikuwa katika nafasi zao, kama ilivyoagizwa na Mfalme Daudi, Asafu, Hemani na Yeduthuni mwonaji wa Mfalme. Mabawabu katika kila lango hawakuhitaji kuacha nafasi zao kwa sababu Walawi wenzao walifanya maandalizi kwa ajili yao.
And the singers the sonnes of Asaph stoode in their standing according to the commandement of Dauid, and Asaph, and Heman, and Ieduthun the Kings Seer: and the porters at euery gate, who might not depart from their seruice: therefore their brethren the Leuites prepared for them.
16 Kwa hiyo wakati ule huduma yote ya Bwana ilifanyika katika kuadhimisha Pasaka, kutoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu ya Bwana kama alivyoamuru Mfalme Yosia.
So all the seruice of the Lord was prepared the same day, to keepe the Passeouer, and to offer burnt offerings vpon the altar of the Lord, according to the commandement of King Iosiah.
17 Waisraeli waliokuwepo wakaadhimisha Pasaka wakati huo na Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu kwa siku saba.
And the children of Israel that were present, kept the Passeouer the same time, and the feast of the vnleauened bread seuen dayes.
18 Kulikuwa hakujafanyika Pasaka kama hii katika Israeli tangu siku za nabii Samweli wala hakukuwa na mfalme yeyote wa Israeli ambaye kamwe alishaadhimisha Pasaka kama ile aliyofanya Mfalme Yosia, akiwa na makuhani, Walawi na watu wote wa Yuda na watu wa Israeli waliokuwepo huko, pamoja na watu wa Yerusalemu.
And there was no Passeouer kept like that, in Israel, from the dayes of Samuel the Prophet: neyther did all the Kings of Israel keepe such a Passeouer as Iosiah kept, and the Priestes and the Leuites, and all Iudah, and Israel that were present, and the inhabitants of Ierusalem.
19 Pasaka iliadhimishwa katika mwaka wa kumi na nane wa utawala wa Mfalme Yosia.
This Passeouer was kept in the eighteenth yeere of the reigne of Iosiah.
20 Baada ya haya yote, Yosia alipomaliza kulitengeneza vizuri Hekalu, Neko mfalme wa Misri, akapanda ili kupigana huko Karkemishi katika Mto Frati, naye Yosia akatoka kwenda kupigana naye.
After all this, when Iosiah had prepared the Temple, Necho King of Egypt came vp to fight against Carchemish by Perath, and Iosiah went out against him.
21 Lakini Neko akamtumia wajumbe kusema, “Kuna ugomvi gani kati yangu mimi na wewe, Ee Mfalme wa Yuda? Si wewe ninayekushambulia wakati huu, bali ile nyumba ambayo nina vita nayo, Mungu ameniambia niharakishe, kwa hivyo acha kumpinga Mungu, ambaye yuko pamoja nami, la sivyo atakuangamiza.”
But he sent messengers to him, saying, What haue I to doe with thee, thou King of Iudah? I come not against thee this day, but against the house of mine enemie, and God commanded me to make haste: leaue of to come against God, which is with me, least he destroy thee.
22 Lakini hata hivyo, Yosia hakukubali kumwacha, bali alijibadilisha ili kupigana naye vita. Hakusikiliza yale Neko aliyokuwa amemwambia kwa agizo la Mungu bali alikwenda kupigana naye katika tambarare ya Megido.
But Iosiah would not turne his face from him, but changed his apparel to fight with him, and hearkened not vnto the wordes of Necho, which were of the mouth of God, but came to fight in the valley of Megiddo.
23 Wapiga upinde wakampiga Mfalme Yosia, naye akawaambia maafisa wake, “Niondoeni, nimejeruhiwa vibaya sana.”
And the shooters shot at king Iosiah: then the King saide to his seruants, Cary me away, for I am very sicke.
24 Kwa hiyo wakamshusha kutoka kwenye gari lake la farasi, wakamweka kwenye gari lingine alilokuwa nalo na kumleta Yerusalemu, ambako alifia. Akazikwa katika makaburi ya baba zake, nayo Yuda yote na Yerusalemu wakamwombolezea Yosia.
So his seruants tooke him out of that charet, and put him in the seconde charet which he had, and when they had brought him to Ierusalem, he dyed, and was buryed in the sepulchres of his fathers: and all Iudah and Ierusalem mourned for Iosiah.
25 Nabii Yeremia akatunga maombolezo kwa ajili ya kifo chake, nao waimbaji wote, wanaume kwa wanawake, hufanya ukumbusho wa Yosia katika maombolezo hadi leo. Haya yakafanywa desturi katika Israeli, nayo yameandikwa katika Maombolezo.
And Ieremiah lamented Iosiah, and al singing men and singing women mourned for Iosiah in their lamentations to this day, and made the same for an ordinance vnto Israel: and beholde, they be written in the lamentations.
26 Matukio mengine ya utawala wa Yosia na matendo yake mema, kulingana na yale yaliyoandikwa katika sheria ya Bwana:
Concerning the rest of the actes of Iosiah and his goodnesse, doing as it was written in the Lawe of the Lord,
27 matukio yote, kuanzia mwanzo hadi mwisho, yameandikwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli na Yuda.
And his deedes, first and last, behold, they are written in the booke of the Kings of Israel and Iudah.