< 2 Nyakati 28 >

1 Ahazi alikuwa na miaka ishirini alipoanza kutawala. Akatawala huko Yerusalemu kwa miaka kumi na sita. Tofauti na Daudi baba yake, hakufanya yaliyo mema machoni pa Bwana.
Ahazi alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala, na akatawala miaka kumi na sita katika Yerusalemu. Hakufanya yaliyoadili katika macho ya Yahwe, kama Daudi babu yake alivyokuwa amefanya.
2 Akaenenda katika njia za wafalme wa Israeli, na pia akasubu sanamu kwa ajili ya kuabudu Mabaali.
Badala yake, alitembea katika njia za wafalme wa Israeli; pia alitengeneza sanamu za kusubu kwa ajila ya Mabaali.
3 Akatoa sadaka za kuteketezwa katika Bonde la Ben-Hinomu, na kuwatoa wanawe kafara kwa kuwateketeza kwa moto, akifuata njia za machukizo za yale mataifa Bwana aliyoyafukuza humo mbele ya Waisraeli.
Zaidi ya hayo, akafukiza uvumba katika bonde la Beni Hinomu na akawaweka watoto wake ndani ya moto, kwa mjibu wa desturi za uzinzi za watu ambao Yahwe aliwafukuza nje ya nchi zao mbele za watu wa Israeli.
4 Akatoa sadaka na kufukiza uvumba katika mahali pa juu pa kuabudia miungu, juu ya vilima, na chini ya kila mti uliotanda.
Akatoa sadaka na kufukiza uvumba katika sehemu za juu na juu ya vilima na chini ya kila mti wenye majani mabichi.
5 Kwa hiyo Bwana Mungu wake akamtia mikononi mwa mfalme wa Aramu. Waaramu wakamshinda, wakachukua watu wake wengi mateka na kuwaleta mpaka Dameski. Tena alitiwa mikononi mwa mfalme wa Israeli, ambaye aliwaua watu wake wengi.
Kwa hiyo Yahwe Mungu wa Ahazi, akamweka katika mikono ya mfalme wa Shamu. Waaramu wakamshinda na kuchukua kutoka kwake kundi kubwa la mateka, wakawapeleka Damesiki. Ahazi pia aliwekwa katika mikono ya mfalme wa Israeli ambaye alimshinda kwa mauji makuu.
6 Kwa siku moja Peka mwana wa Remalia aliwaua askari 120,000 katika Yuda, kwa kuwa Yuda walikuwa wamemwacha Bwana, Mungu wa baba zao.
Kwa maana Peka mwana wa Remalia, aliwaua katika Yuda wanajeshi 120, 00 kwa siku moja, wote walikuwa wanaume hodari, kwa maana walikuwa wamemsahau Yahwe, Mungu wa babu zao.
7 Zikri, askari shujaa Mwefraimu, akamuua Maaseya mwana wa mfalme, Azrikamu mkuu wa jumba la kifalme na Elikana aliyekuwa wa pili kwa mfalme.
Zikri, mtu mwenye nguvu kutoka Efraimu, akawaua Maaseya mwana wa mfalme, Azrikamu, mwangalizi mkuu wa ikulu, na Elkana, ambaye alikuwa karibu na mfalme.
8 Waisraeli wakawachukua mateka kutoka ndugu zao, watu wapatao 200,000 hawa wakiwa ni wanawake, watoto wa kiume na wa kike. Wakachukua pia kiasi kikubwa cha nyara, ambazo walirudi nazo Samaria.
Jeshsi la Israeli likachukua mateka kutoka kwa ndugu zao 200, 000 wake, wana, na mabinti. Pia wakachukua nyara nyingi, ambazo walipeleka Samaria.
9 Lakini kulikuwako huko nabii wa Bwana aliyeitwa Odedi, akaondoka ili kukutana na jeshi liliporejea Samaria. Akawaambia, “Kwa kuwa Bwana, Mungu wa baba zenu, aliwakasirikia Yuda, aliwatia mikononi mwenu. Lakini mmewachinja kwa hasira ambayo imefika hadi mbinguni.
Lakini nabii wa Yahwe alikuwapo huko, jina lake aliitwa Odedi. Alikwenda nje kukutana na jeshi likiingia Samaria. Akawaambia, “Kwa sababu Yahwe, Mungu wa babu zenu, alikuwa na hasiri na Yuda, akawatia katika mikono yenu. Lakini mmewaua katika hasira inayofika juu mbinguni.
10 Nanyi sasa mnakusudia kuwafanya wanaume na wanawake wa Yuda na Yerusalemu watumwa wenu. Lakini ninyi je, hamna pia hatia ya dhambi mliyotenda dhidi ya Bwana Mungu wenu?
Sasa ninyi badala ya kuwahifadhi wanaume na wanawake wa Yuda na Yerusalemu kama watumwa wenu. Lakini je hamko na hatia ya dhambi zenu zidi ya Yahwe Mungu wenu?
11 Basi nisikilizeni! Mkawarudishe mateka mliowachukua kutoka kwa ndugu zenu, kwa kuwa hasira kali ya Bwana iko juu yenu.”
Sasa basi, nisikilizeni: warudisheni wafubgwa, ambao mmewachukua wa ndugu zenu, kwa maana ghadhabu ya Yahwe iko juu yenu.”
12 Ndipo baadhi ya viongozi katika Efraimu, yaani, Azaria mwana wa Yehohanani, Berekia mwana wa Meshilemothi, Yehizkia mwana wa Shalumu na Amasa mwana wa Hadlai, wakakubaliana na huyo nabii, hivyo wakawapinga wale waliokuwa wanawasili kutoka vitani.
Kisha baadhi ya viongozi wa watu wa Efraimu—Azaria mwana wa Yohanani, Berekia mwana wa Meshiremothi, na Yehizikia mwana wa Shalumu, na Amasa mwana wa Hadlai, wakasimama kinyume na wale waliorudi kutoka vitani.
13 Wakamwambia, “Hamna ruhusa kuwaleta hao wafungwa hapa, ama sivyo tutakuwa na hatia mbele za Bwana. Je, mnataka kuongezea dhambi yetu na hatia yetu? Kwa sababu hatia yetu tayari ni kubwa, nayo hasira kali ya Bwana iko juu ya Israeli.”
Wakasema kwao, “Lazimaa msiwaleta wafungwa hapa, kwa kuwa mlikusudia jambo ambalo litaleta juu yetu dhambi dhidi ya Yahwe, kuongeza dhambi juu yetu na makosa yetu, kwa maana makosa yetu ni makuu, na kuna hasira kali dhidi ya Israeli.”
14 Hivyo wale askari wakawaacha wale mateka pamoja na nyara mbele ya hao maafisa na kusanyiko lote.
Hivyo watu wenye silaha wakawaacha wafungwa na mateka mbele ya viongozi wa Israeli na kusanyiko lote
15 Kisha watu waliotajwa kwa majina wakawachukua wale mateka na kutoka zile nyara, wakachukua mavazi wakawavika wale wafungwa wote waliokuwa uchi. Wakawapatia nguo na viatu, chakula na cha kunywa, wakawapa matibabu, wote waliokuwa dhaifu miongoni mwao wakawapandisha juu ya punda, wakawaleta ndugu zao mpaka Yeriko, ndio Mji wa Mitende, kisha wakarudi Samaria.
Watu ambao walipangwa kwa majina wakanyanyuka na kuwachukua wafungwa, na kuwavika wote waliokuwa uchi miongoni mwa mateka. Wakawavika na kuwapa viatu. Wakawapa chakula wale na kunywa. Wakawahudumia majeraha yao na kuwaweka waliodhaifu juu ya punda. Wakawarudisha kwenye familia zao katika Yeriko, (Ulioitwa mji wa mitende). Kisha wakarudi Samaria.
16 Wakati ule, Mfalme Ahazi akatuma wajumbe kwa mfalme wa Ashuru kuomba msaada.
Wakati huo Mfalme Ahazi akatuma wajumbe kwa wafalme wa Ashuru kuwaomba wamsaidie.
17 Waedomu walikuwa wamekuja tena na kuwashambulia Yuda na kuchukua mateka.
Kwa maana Waedomu walikuwa wamekuja tena na kuvamia Yuda, wakachukua wafungwa.
18 Pia Wafilisti walikuwa wameshambulia miji iliyokuwa chini ya vilima na katika miji ya Negebu ya Yuda. Nao wakawa wametwaa Beth-Shemeshi, Aiyaloni, Gederothi, Soko pamoja na vijiji vyake, Timna pamoja na vijiji vyake, Gimzo pia pamoja na vijiji vyake na kuishi humo.
Wafilisti pia wakavamia miji ya nchi ya chini na ya Negebu ya Yuda. Waliichukua Beth-shemeshi, Ayaloni, Giderothi, SoKo pamoja na vijiji vyake, Timna pamoja na vijiji vyake. Wakaenda kuishi katika sehemu hizo.
19 Bwana aliishusha Yuda kwa sababu ya Ahazi mfalme wa Israeli, kwa kuwa alikuwa ameongeza uovu katika Yuda na kumkosea Bwana mno.
Kwa kuwa Yahwe aliishusha chini Yuda kwa sababu ya Ahazi, mfalme wa Israeli; kwa maana alikuwa ametenda maovu katika Yuda na alikuwa ametenda dhambi nzito sana dhidi ya Yahwe.
20 Hivyo Tiglath-Pileseri mfalme wa Ashuru akaja kumtesa badala ya kumsaidia.
Tiglath-pileseri, mfalme wa Ashuru, akaja kwake na akampa tabu badala ya kumpa nguvu.
21 Ahazi akachukua baadhi ya vitu kutoka Hekalu la Bwana, jumba la kifalme na kutoka kwa wakuu wake na kumpa mfalme wa Ashuru kama ushuru, lakini hilo halikumsaidia.
Kwa kuwa Ahazi aliteka nyara nyumba ya Yahwe na nyumba ya mfalme na viongozi, kwa ajili ya kuvitoa vitu vya thamani kwa mfalme wa Ashuru. Lakini kufanya hivyo hakukumfaidisha yeye.
22 Katika wakati wake wa mateso Mfalme Ahazi akazidi kukosa uaminifu kwa Bwana.
Mfalme Ahazi huyu huyu akatenda dhambi hata zaidi dhidi ya Yahwe katika muda wa mateso yake.
23 Akatoa kafara kwa miungu ya Dameski, waliokuwa wamemshinda, kwa kuwa aliwaza, “Kwa kuwa miungu ya mfalme wa Aramu imewasaidia wao, nitaitolea dhabihu ili inisaidie na mimi.” Lakini haya ndiyo yaliyokuwa maangamizi yake na Israeli wote.
Kwa maana aliwatolea dhabihu mingu wa Dameski, miungu ambao walimshinda. Akasema, “Kwa sababu miungu wa mfalme wa Aramu waliwasaidia, nitawatolea sadaka ili wanisaidie.” Lakini walikuwa watesi wake na Israeli yote.
24 Ahazi akakusanya pamoja vyombo vya nyumba ya Mungu na kuvivunja vipande vipande. Akafunga milango ya Hekalu la Bwana na kusimamisha madhabahu katika kila njia panda ya barabara za Yerusalemu.
Ahazi akazikusanya pamoja samani za nyumba ya Mungu na kuzikata vipande vipande. Akaifunga milango ya nyumba ya Yahwe na kuzitengeneza madhabahu kwa ajili yake mwenyewe katika kila kona ya Yerusalemu.
25 Katika kila mji wa Yuda akajenga mahali pa juu pa kuabudia miungu ili kutolea miungu mingine kafara za kuteketezwa na kuchochea hasira ya Bwana, Mungu wa baba zake.
Katika kila mji wa Yuda akafanya sehemu za juu kwa ajili ya kutolea sadaka za kuteketezwa kwa miungu wengine. Akamfanya Yahwe, Mungu wa babu zake, akasirike.
26 Matukio mengine ya utawala wake na njia zake nyingine zote, tangu mwanzo hadi mwisho, zimeandikwa katika kitabu cha wafalme wa Yuda na Israeli.
Sasa matendo yake yaliyobaki, na njia zake zote, mwanzo na mwisho, ona, yameandikwa katika kitabu cha wafalme wa Yuda na Israeli.
27 Ahazi akalala na baba zake na akazikwa katika Mji wa Yerusalemu, lakini hawakumleta kwenye makaburi ya wafalme wa Israeli. Naye Hezekia mwanawe akawa mfalme baada yake.
Ahazi akalala pamoja na babu zake, na wakamzika katika mji, katika Yerusalemu, lakini hawakumleta kwenye makaburi ya wafalme wa Israeli. Hezekia, mwanaye, akawa mfamle katika nafasi yake.

< 2 Nyakati 28 >