< 2 Nyakati 26 >

1 Kisha watu wote wa Yuda wakamtwaa Uzia, aliyekuwa na umri wa miaka kumi na sita, nao wakamfanya mfalme mahali pa Amazia baba yake.
Watu wote wa Yuda wakamchukua Uzia, ambaye alikuwa na aumri wa mika kumi na sita, na wakamfanya mfalme katika nafasi ya baba yake Amazia.
2 Ndiye alijenga upya Elathi kuirudisha kwa Yuda baada ya Amazia kulala pamoja na baba zake.
Ndiye aliuyeijenga tena Elathi na kuurejesha kwa Yuda. Baada ya hapo mfalme akalala pamoja na babu zake.
3 Uzia alikuwa na umri wa miaka kumi na sita alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka hamsini na miwili. Mama yake aliitwa Yekolia wa Yerusalemu.
Uzia alikuwa na umri wa miaka kumi na sita alipoanza kutawala. Akatawala miaka ishirini na mabili katika Yerusalemu. Jina la mama yake lilikuwa Yekolia; alikuwa wa Yerusalemu.
4 Akatenda yaliyo mema machoni pa Bwana, kama Amazia baba yake alivyofanya.
Akafanya yaliyokuwa sahihi katika macho ya Yahwe, akiufuata mfano wa baba yake, katika kila jamabo.
5 Akamtafuta Mungu katika siku za Zekaria, aliyemwelekeza kumcha Mungu. Wakati wote alipomtafuta Bwana, Mungu alimfanikisha.
Alijitoa kumtafuta Mungu katiaka siku za Zekaria, ambaye alimpa maelekezo kwa ajili ya kumtii Mungu. Kadri alivyomtafuta Yaahwe, Mungu alimfanikisha.
6 Alipigana vita dhidi ya Wafilisti na kubomoa kuta za Gathi, Yabne na Ashdodi. Kisha akajenga upya miji karibu na Ashdodi na mahali pengine katikati ya Wafilisti.
Uzia akaenda na kupigana zidi ya Wafilisti. Akaubomoa ukuta wa mji wa Gathi, Yabne, na Ashdodi; akajenga miji katika nchi ya Ashdodi na miongoni mwa Wafilisti.
7 Mungu akamsaidia dhidi ya Wafilisti na dhidi ya Waarabu walioishi Gur-Baali na dhidi ya Wameuni.
Mungu aakaamsaidia zidi ya Wafilist, zidi ya Waarabu waliokuwa wakiishi Gur - baali, na zidi ya Wameuni.
8 Waamoni wakamletea Uzia ushuru, umaarufu wake ukaenea hadi kwenye mpaka wa Misri, kwa sababu alikuwa amekuwa na nguvu sana.
Waamoni wakalipa kodi kwa Uzia, na umaarufu wake ukaenea, hata kufika maingilio ya Misiri, kwa sababu alikuwa ameanza kuwa maarufu.
9 Uzia akajenga minara huko Yerusalemu katika Lango la Pembeni, katika Lango la Bondeni na katika pembe, mahali kuta zikutanapo, kisha akaijengea ngome.
Zaidi ya hayo, Uzia akajenga minara katika Yerusalemu katika kona ya Lango, kwenye Lango la Bonde, na pa kwenye kona ya ukuta, na akavizungushia ngome.
10 Akajenga pia minara jangwani na kuchimba visima vingi vya maji, kwa sababu alikuwa na mifugo mingi chini ya vilimani na kwenye nchi tambarare. Alikuwa na watu wanaofanya kazi katika mashamba yake na kwenye mashamba yake ya mizabibu huko vilimani na katika ardhi zenye rutuba, kwa kuwa aliupenda udongo.
Akajenga minara ya ulinzi katika nyika na akachimba mabwawa, kwa maana alikuwa na ng'ombe wengi, katika visiwa vya chini na katika nchi tambarare. Alikuwa na wakulima na wapandaji wa zabibu katika mwinuko wa nchi na katika mashamba yenye rutuba, kwa maana alipenda kulima.
11 Zaidi ya hayo, Uzia alikuwa na jeshi lililofunzwa vizuri, lililokuwa tayari kwenda vitani kwa vikosi kufuatana na idadi yao kama walivyokusanywa na Yeieli mwandishi na Maaseya msimamizi chini ya maelekezo ya Hanania, mmojawapo wa maafisa wa mfalme.
Zaidi ya hayo, Uzia alikuwa na jeshi la wanaume wa kupigana vita ambao walienda vitani katika makundi ambayo idadi yake ilikuwa imehesabiwa na Yeieli, mwandishi. na Maaseya, afisa, chini ya mamlaka ya Hanania, mmoja wa maamri jeshi wa mfalme.
12 Idadi yote ya viongozi wa jamaa waliowaongoza hawa wapiganaji walikuwa 2,600.
Jumla ya wakuu wa nyumba za mababu, watu wa kupigana vita, walikuwa 2, 600.
13 Chini ya uongozi wao kulikuwa na jeshi la askari 307,500 watu waliofundishwa kwa ajili ya vita, jeshi lenye nguvu la kumsaidia mfalme dhidi ya adui zake.
Chini ya mkono wao kulikuwa na jeshi la watu 307, 500 ambao walifanya vita kwa nguvu ili kumsaidia mfalme idi ya maadui.
14 Uzia akalipatia jeshi lote ngao, mikuki, chapeo, dirii, pinde na mawe ya kombeo.
Uzia akaandaa kwa ajili yao—kwa ajili ya jeshi lote — ngao, mikuki, chapeo, deraya za majini, nyuta, na mawe ya kurusha.
15 Huko Yerusalemu watu wenye utaalamu mkubwa wakatengeneza mitambo iliyotumika katika minara na kwenye pembe za ulinzi ili kurusha mishale na kuvurumisha mawe makubwa. Sifa zake zikaenea mbali sana kwa sababu alisaidiwa mno mpaka akawa na nguvu sana.
Katka Yerusalemu alijenga mitambo, iliyobuniwa na watu wenye ujuzi, ili iwe juu ya minara na juu ya buruji, kwa ajili ya kurushia mishale na mawe makaubwa. Umaarufu wake ukaenea hadi nchi za mbali, kwa maana alisaidiwa sana hadi alipokuwa na ngavu sana.
16 Lakini baada ya Uzia kuwa na nguvu sana, majivuno yake yakamsababishia kuanguka. Alikosa uaminifu kwa Bwana Mungu wake, naye akaingia hekaluni mwa Bwana ili afukize uvumba kwenye madhabahu ya kufukizia uvumba.
Lakini Uzia alipokuwa amekuwa na nguvu nyingi, moyo wake ulijiinua akatenda kwa uovu; akafanya makosa zidi ya Yahwe, Mungu wake, kwa maana alienda kwenye nyumba ya Yahwe kwa ajili ya kufukiza uvumba juu ya madhabahu ya kufukizia.
17 Azaria kuhani akiwa pamoja na makuhani wengine themanini wa Bwana wenye ujasiri wakamfuata huko ndani.
Azaria, kuhani, akamfuata, na pamoja naye makuhanai themanini wa Yahwe, ambao walikuwa watu wenye ujasiri.
18 Wakamkabili na kumwambia, “Siyo sawa kwako, Uzia, kumfukizia Bwana uvumba. Hiyo ni kazi ya makuhani, wazao wa Aroni, ambao wamewekwa wakfu ili kufukiza uvumba. Ondoka mahali patakatifu, kwa kuwa umekosa uaminifu nawe hutaheshimiwa na Bwana.”
Walimzuia Uzia, mfalme, na wakasema kwake, “Siyo jukumu lako, Uzia, kumtolea Yahwe uvumba, bali ni kazi ya makuhani, wana wa Haruni, amabao wametengwa kwa ajili ya kutoa sadaka za uvumba. Toka nje ya sehemu takatifu, kwa maana huna uaminifu na hautaheshimiwa na Yahwe Mungu.”
19 Uzia, ambaye alikuwa na chetezo mkononi mwake tayari kufukiza uvumba, akakasirika. Alipokuwa anawaghadhibikia makuhani mbele ya madhabahu ya kufukizia uvumba katika Hekalu la Bwana, ukoma ukamtokea penye kipaji chake cha uso.
Kisha Uzia akakasirika. Alikuwa ameshikilia chetezo mkononi kwa ajili ya kufukiza uvumba. Wakati alipowaghadhabikia makuhani, ukoma ukatokea juu ya uso wake mbele ya makuhani katika nyumba ya Yahwe, pembeni mwa madhabahu ya uvumba.
20 Azaria kuhani mkuu pamoja na makuhani wengine wote walipomtazama wakaona kwamba alikuwa na ukoma penye kipaji chake cha uso wakaharakisha kumtoa nje. Naam, hata yeye mwenyewe alikuwa anatamani kuondoka kwa sababu Bwana alikuwa amempiga.
Azaria kuhani mkuu na makuhani wote wakamwanagalia, na, tazama, alikuwa amepatwa ukoma juu ya uso wake. Walimwondoa pale haraka. Kwa hakika, aliharakisha kwenda nje, kwa maana Yahwe alikuwa amempiga.
21 Mfalme Uzia alikuwa na ukoma mpaka siku ya kufa kwake. Akatengwa katika nyumba ya pekee akiwa mwenye ukoma, naye akawa ametengwa kutoka Hekalu la Bwana. Yothamu mwanawe akawa msimamizi wa jumba la mfalme, pia akawaongoza watu wa nchi.
Uzia, mfalme, alikuwa mwenye ukoma hadi siku ya kufa kwake na aliishi katika nyumba ya kutengwa tangu alipokuwa mwenye ukoma, kwa maan alitengwa na nyumba ya Yahwe. Yothamu, mwanaye, alikuwa mkuu wa anyumba ya mfalme na aliwatawala watu wa nchi.
22 Matukio mengine ya utawala wa Uzia, kuanzia mwanzo mpaka mwisho, yameandikwa na nabii Isaya mwana wa Amozi.
Mambo mengine kuhusu Uzia, mwanzo na mwisho, yako katika kile ambacho Isaya, mwana wa Amozi, nabii, aliandika.
23 Uzia akalala pamoja na baba zake, naye akazikwa karibu nao katika shamba la kuzikia lililokuwa mali ya wafalme, kwa kuwa watu walisema, “Alikuwa na ukoma.” Yothamu mwanawe akawa mfalme baada yake.
Kwa hiyo Uzia akalala pamoja na babu zake; walimzka pamoja na babu zake katika uwanja wa maziko wa Mfalme, kwa maana walisema, “Ni mwenye ukoma”. Yothamu, mwanaye, akawa mfalme katika nafasi yake.

< 2 Nyakati 26 >