< 2 Nyakati 25 >

1 Amazia alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka ishirini na tisa. Mama yake aliitwa Yehoadani kutoka Yerusalemu.
Amaza alikuwa na umri wa amiaka ishirini na na tano alipoanza kutawala; alitawala miaka ishini na tisa katika Yerusalemu. Jina la mama yake lilikuwa Yehoadani, wa Yerusalemu.
2 Akatenda yaliyo mema machoni pa Bwana, lakini sio kwa moyo wake wote.
Alifanya yaliyokuwa sahihi katika macho ya Yahwe, lakini siyo kwa moyo uliojitoa kikamilifu.
3 Baada ya ufalme kuimarika mikononi mwake, aliwaua maafisa waliomuua mfalme baba yake.
Ikawa kwamba mapema utawala wake ulipokuwa umeimarika, aliwaua watumishi ambao walikuwa wamemuua baba yake, mfalme.
4 Hata hivyo hakuwaua watoto wao, lakini akafanya sawasawa na ilivyoandikwa katika Sheria, katika Kitabu cha Mose, ambako Bwana aliamuru: “Baba hawatauawa kwa ajili ya watoto wao, wala watoto hawatauawa kwa ajili ya baba zao. Kila mmoja atakufa kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe.”
Lakini hakuwaua watoto wa wale wauaji, bali alitenda kama kama ilivyoaandikwa katika sheria, katika kitabu cha Musa, kama Yahwe alivyokuwa ameamru. “Baba hatajuta kwa ajili ya watoto, wala watoto hawatakufa kwa ajili ya baba zao. Badala yake, kila mtu lazima afe kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe”.
5 Amazia akawaita watu wa Yuda pamoja, akawaweka chini ya majemadari wa maelfu na majemadari wa mamia kufuatana na jamaa zao katika Yuda yote na Benyamini. Kisha akawahesabu wale wenye umri wa miaka ishirini au zaidi na akakuta kwamba walikuwa wanaume 300,000 watu walio tayari kwa utumishi wa jeshi, walio na uwezo wa kutumia mkuki na ngao.
Aidha, Amazia aliwakusanya Yuda pamoja, na akawaandikisha kwa kufuata nyumba za babu zao, chini ya maakida wa maelfu na maakida wa mamia —wote wa Yuda na wa Benyamini. Akawahesabu kuanzia wa mika ishirini na kuendelea, na akawaona wako 300, 000 wanaume waliochaguliwa, wawezaoa kwenda vitani, walioweza kushika mkuki na ngao.
6 Akawaajiri pia watu 100,000 wapiganaji kutoka Israeli kwa talanta 100 za fedha.
Pia alikodi wanaume wa kupigana 100, 000 kutoka Israeli kwa fedha mia moja.
7 Lakini mtu wa Mungu akamjia na kumwambia, “Ee mfalme, haya majeshi kutoka Israeli kamwe usiyaruhusu yaende pamoja na wewe kwa kuwa Bwana hayuko pamoja na Israeli, wala hayupo pamoja na yeyote wa watu wa Efraimu.
Lakini mtu wa Mungu alikuja kwake na kusema, “Mfalme, usiliache jeshi la Istaeli kwenda nawe, kwa maana Yahwe hayupo pamoja na Israeli -wala na mtu Yeyote wa Efraimu.
8 Hata kama ukienda na kupigana kwa ujasiri katika vita, Mungu atakufanya ukimbie mbele ya adui, kwa kuwa Mungu anao uwezo wa kusaidia au wa kuangusha.”
Lakini hata kama mtaenda na mkiwa wenye ushupavu na imara katika vita, Mungu atawatupa chini mbele ya adui, kwa maana Mungu ana nguvu za kusaidia, na nguvu za kurusha chini”.
9 Amazia akamuuliza yule mtu wa Mungu, “Lakini itakuwaje kwa zile talanta 100 za fedha nilizolipa kwa ajili ya haya majeshi ya Israeli?” Yule mtu wa Mungu akajibu, “Bwana aweza kukupa zaidi sana ya hizo.”
Amazia akasema kwa mtu wa Mungu, “Lakini tutafanyaje kuhusu talanta mia moja nilizowapa jeshi la Israeli? Mtu wa Mungu akajibu, Yahwe anauwezo wa kukupa vingi zaidi kuliko hivyo.”
10 Hivyo Amazia akayaondoa yale majeshi yaliyokuwa yamekuja kutoka Efraimu na kuyarudisha nyumbani. Waliwakasirikia sana Yuda, nao wakarudi nyumbani wakiwa na hasira kali.
Kwa hiyo Amazia akalitenganisha jeshi lilokuja kwake kutoka Efraimu; akawarudisha nyumbani tena. Hivyo hasira yao iliwaka sana zidi ya Yuda, na walirudi nyumbani kwa hasara kali.
11 Ndipo Amazia akajitia nguvu na kuliongoza jeshi lake kwenye Bonde la Chumvi, ambako aliua watu 10,000 wa Seiri.
Amazia akajipa ujasiri na kuwaongoza watu wake kwenda nje kwenye bonde la chumvi, huko akawashinda wanaueme elfu kumi wa Seiri.
12 Jeshi la Yuda pia likawateka watu 10,000 wakiwa hai, likawapandisha juu ya jabali na kuwatupa chini kwa nguvu hata wote wakavunjika vipande vipande.
Jeshi la Yuda likawachukua elfu kumi wengine wakiwa hai. Wakawapeleka juu ya mwamba na kuwarushwa chini kutoka huko, hivyo wote wakavunjika vunjika katika vipande.
13 Wakati huo yale majeshi Amazia aliyoyarudisha na ambayo hakuyaruhusu kushiriki katika vita, yalivamia miji ya Yuda kuanzia Samaria hata Beth-Horoni. Yakawaua watu 3,000 na kuchukua kiasi kikubwa sana cha mateka.
Lakini watu wa jeshi ambalo Amazia alilirudisha, ili kwamba wasiende naye vitani, wakauvamia mji Yuda kuanzia Somaria hadi Beth- horoni. Wakawapiga watu elfu tatu na kuwateka wengi sana.
14 Amazia aliporudi kutoka kuwachinja Waedomu, alileta pia kutoka huko miungu ya watu wa Seiri. Akaisimamisha kama miungu yake mwenyewe, akaisujudia na kuitolea kafara za kuteketezwa.
Sasa ikawa kwamba baada ya Amazia kurudi kutoka kuwachinja Waedomu, akaileta miungu ya watu wa Seiri, na kuisimamisha iwe miungu yake. Akainama chini mbele ya hiyo miungu na kuitolea sadaka za uvumba.
15 Hasira ya Bwana ikawaka dhidi ya Amazia, naye akamtuma nabii kwake, ambaye alisema: “Kwa nini unauliza kwa miungu ya hawa watu, ambayo haikuweza kuwaokoa watu wake wenyewe kutoka mkononi mwako?”
Hivyo hasira ya Yahwe ikawaka zidi ya Amazia. Akamtuma nabii kwake, ambaye alisema, “Kwa nini umeitafuta miungu ya watu ambayo haikuwaokoa hata watu wake yenyewe zidi ya mkono wako?”
16 Wakati nabii alipokuwa angali anazungumza, mfalme akamwambia, “Je, wewe tumekuchagua kuwa mshauri wa mfalme? Nyamaza, ya nini uuawe?” Hivyo nabii akanyamaza lakini akasema, “Najua kuwa Mungu ameazimia kukuangamiza kwa sababu umefanya jambo hili na hukusikiliza shauri langu.”
Akiwa kwamaba yule nabii alipokuwa anaongea naye, mfalme akamwambia, “Je, wewe tumekufanya kuwa mshauri wa mfalme? Acha! Kwa nini ujitakie kuuawa?” Kisha nabii akaacha na kusema, ninajua kwamba Mungu ameamua kukuangaamiza kwa sababu umefanya tendo hili na hujasikilisa ushauri wangu.”
17 Baada ya Amazia mfalme wa Yuda kushauriana na washauri wake akatuma ujumbe kwa Yehoashi, mwana wa Yehoahazi mwana wa Yehu, mfalme wa Israeli kusema: “Njoo tukabiliane uso kwa uso.”
Kisha Amazia akashauriana na washauri na kutuma wajumbe kwa Yehoashi mwana wa Yehoahazi mwana wa Yehu, mfalme wa Israel. akisema, “Njoni, tukutane uso kwa uso katika vita”.
18 Lakini Yehoashi mfalme wa Israeli akamjibu Amazia mfalme wa Yuda, “Mbaruti uliokuwa Lebanoni ulituma ujumbe kwa mwerezi uliokuwa Lebanoni, ‘Mtoe binti yako aolewe na mwanangu.’ Kisha mnyama wa mwituni aliyekuwa Lebanoni akaja na kuukanyaga ule mbaruti.
Lakini Yehoashi mfalme wa Israeli akatuma wajumbe kwa Amaziahi mfalme wa Yuda, akisema, Mbaruti uliokuwa Lebanoni ulituma ujumbe kwa mwerezi ulioko Lebanoni, ukisema, Mtoe binti yako kwa mwanangu awe mke wake; lakini akapita hayawani katika Lebanoni akatembea na kuukanyaga chini mbaruti.
19 Wewe unasema moyoni mwako kwamba umemshinda Edomu, nawe sasa unajigamba na kujivuna. Lakini kaa nyumbani kwako! Kwa nini utafute matatizo na kujiletea anguko lako mwenyewe na la Yuda pia?”
Umesema, 'Ona, nimeipiga Edomu,' na moyo wako umekuinua juu. Jipe fahari katika ushindi wako, lakini ukae nyumbani, kwa maana ni kwa nini ujisababishie matatizo mwenyewe na kuanguka, wote wewe na Yuda pamoja nawe?'
20 Hata hivyo, Amazia hakutaka kusikia, kwa kuwa Mungu alifanya hivyo ili awatie mikononi mwa Yehoashi, kwa sababu waliitafuta miungu ya Edomu.
Lakini Amazia hakusikiliza, kwa sababu tukio hili lilikuwa limetoka kwa Mungu, ili awatie Waisraeli katika mkono wa adui zao, kwa sababu walikuwa wametafuta ushauri kutoka kwa miungu ya Edomu.
21 Hivyo Yehoashi mfalme wa Israeli akakwea kuwashambulia. Yeye na Amazia mfalme wa Yuda wakakabiliana uso kwa uso huko Beth-Shemeshi katika Yuda.
Kwa hiyo, Yehoashsi, mfalme wa Israeli, akavamia; yeye na Amazia, mfalme wa Yuda, wakakutana uso kwa uso huko Beth -shemishi, ulioko Yuda.
22 Yuda ikashindwa na Israeli na kila mtu akakimbilia nyumbani kwake.
Yuda akashindwa mbele za Israeli, na kila mtu akarudi nyumbani.
23 Yehoashi mfalme wa Israeli akamteka Amazia mfalme wa Yuda, mwana wa Yoashi, mwana wa Ahazia, huko Beth-Shemeshi. Kisha Yehoashi akamleta Yerusalemu na kuubomoa ukuta wa Yerusalemu kuanzia lango la Efraimu hadi Lango la Pembeni, sehemu yenye urefu wa kama dhiraa 400.
Yehoashi, mfalme wa Israeli, akamkamata Amazia mwana wa Yehoashi mana wa Ahazia, mfalme wa Yuda, huko Beth - shemeshi. Akamleta Yerusalemu na kuuangusha chini ukuta wa Yerusalemu kuanzia Lango la Efraimu hadi kona ya Lango, umbali wa mikono mia nne.
24 Akachukua dhahabu yote, fedha na vyombo vyote vilivyopatikana katika Hekalu la Mungu, ambavyo vilikuwa chini ya uangalizi wa Obed-Edomu, pamoja na hazina za jumba la mfalme na mateka, kisha akarudi Samaria.
Akachukua dhahabu na fedha zote, vitu vyote vilivyoonekana akatika nyumba aya Mungu kwa Obedi Edomu, na vitu vya thamanai katika nyumba ya mfalme, na mateka pia, na akarudi Samaria.
25 Amazia mwana wa Yoashi mfalme wa Yuda aliishi miaka kumi na mitano baada ya kifo cha Yehoashi mwana wa Yehoahazi mfalme wa Israeli.
Amazia mwana wa Yoashi, mfalme wa Yuda, aliishi miaka kumi na tano baada ya kifo cha Yehoashi, mwana wa Yehoahazi, mfalme wa Israeli.
26 Kwa habari ya matukio mengine katika utawala wa Amazia, kuanzia mwanzo hadi mwisho, je, hayakuandikwa katika kitabu cha wafalme wa Yuda na wa Israeli?
Kwa mambo mengingine kuhusu Amzia, mwanzo na mwisho, tazama, je, hayajaandikwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli?
27 Kuanzia wakati ule Amazia alipogeuka na kuacha kumfuata Bwana walifanya shauri baya dhidi yake huko Yerusalemu naye akakimbilia Lakishi, lakini wakawatuma watu wamfuatilie huko Lakishi nao wakamuulia huko.
Sasa kutoka wakati amabaoa Amazia aligeukia mbali asimfuate Yahwe, walianza kupanga njama zidi yake katika Yerusalemu. Akakimbilia Lachishi, lakini wakatuma watu nyuma yake wamfuate Lachishsi na walimuua huko.
28 Akarudishwa kwa farasi na akazikwa pamoja na baba zake katika Mji wa Yuda.
Wakamleta juu ya farasis na wakamzika pamoja na babu zake kataika Mji wa Yuda.

< 2 Nyakati 25 >