< 2 Nyakati 22 >

1 Watu wa Yerusalemu wakamfanya Ahazia, mdogo wa wote wa wana wa Yerohamu, kuwa mfalme mahali pa baba yake, kwa sababu washambuliaji wa ghafula waliokuwa wameingia kambini pamoja na Waarabu, walikuwa wamewaua wana wakubwa wote wa Yehoramu. Kwa hiyo Ahazia mwana wa Yehoramu mfalme wa Yuda akaanza kutawala.
Wakaaji wa Yersusalemu wakamfanya Ahazia, mwana mdodgo wa Yehoramu, mfalme katika nafasi yake, kwa maana kundi la watu ambalo lilikuja na Waarabu katika ngome lilikuwa limewauwa wanaye wakubwa wote. Kwa hiyo Ahazia mwana wa Yehoramu, mfalme wa Yuda, akawa mfalme.
2 Ahazia alikuwa na umri wa miaka ishirini na miwili alipoanza kutawala, naye akatawala katika Yerusalemu kwa mwaka mmoja. Mama yake aliitwa Athalia, mjukuu wa Omri.
Ahazia alikuwa na umri wa mika arobaini na mbili alipoanza kutawala; alitawala kwa mwaka mmoja katika Yerusalemu. Jina la mama yake aliitwa Athalia; alikuwa binti Omri.
3 Ahazia naye akaenenda katika njia za nyumba ya Ahabu, kwa sababu mama yake alimshawishi katika kutenda maovu.
Pia Ahazia alitembea katika njia za nyumba ya Ahabu kwa maana mama yake alikuwa mshauri katika kufanya mamabo maovu.
4 Akafanya yaliyo maovu machoni pa Bwana kama walivyokuwa wamefanya nyumba ya Ahabu, kwa kuwa baada ya kufa kwa baba yake nyumba ya Ahabu ndio waliokuwa washauri wake, kwa uangamivu wake.
Ahazia alifanya yaliyokuwa maovu katika macho ya Yahwe, kama nyumba ya Ahabu walivyokuwa wakifanya, kwa maana walikuwa washauri wake baada ya kifo cha baba yake, hadi kuangamia kwake.
5 Pia akafuata shauri lao alipokwenda pamoja na Yoramu mwana wa Ahabu mfalme wa Israeli kupigana na Hazaeli mfalme wa Aramu huko Ramoth-Gileadi. Waaramu wakamjeruhi Yoramu.
Pia aliufuata ushauri wao; akaenda pamoja na Yoramu mwana wa Ahabu, mfalme wa Israeli, kwa ajili ya kupigana dhidi ya Hazaeli, mfalme wa Aramu, huko Ramothi-gileadi. Waaramu wakamjeruhi Yoramu.
6 Hivyo akarudi Yezreeli ili apate kuuguza majeraha aliyojeruhiwa huko Ramothi alipopigana na Hazaeli mfalme wa Aramu. Ndipo Ahazia mwana wa Yehoramu, mfalme wa Yuda, akashuka kwenda Yezreeli kumtazama Yoramu mwana wa Ahabu, kwa sababu alikuwa amejeruhiwa.
Yoramu akaraudi Yezreeli kwa ajili ya kuponywa majeraha ambayo walipa huko Rama, alipopigana dhidi ya Hazaeli, mfalme wa Aramu. Kwa hiyo Ahazia mwana wa Yehoramu, mfalme wa Yuda, akaenda chini Yezreeli ili kumuona Yoramu mwana wa Ahabu, kwa sababu Yoramu alikuwa amejeruhiwa.
7 Mungu alikuwa ameamuru kwamba kuanguka kwa Ahazia kungetokea atakapokwenda kumwona Yoramu. Ahazia alipowasili, wakatoka pamoja na Yoramu ili kwenda kukutana na Yehu mwana wa Nimshi, ambaye Bwana alikuwa amemtia mafuta kuangamiza nyumba ya Ahabu.
Sasa uharibifu wa Ahazia ulikuwa umeletwa na Mungu kupitia kutembelewa na Yoramu. Alipokuwa amewasiri, alienda pamoja na Yeharamu ili kumvamia Yehu mwana wa Nimshi, ambaye Yahwe alikuwa amemchagua kwa ajili ya kuingamiza nyumba ya Ahabu.
8 Yehu alipokuwa anatekeleza hukumu juu ya nyumba ya Ahabu, akawakuta wakuu wa Yuda na wana wa jamaa ya Ahazia waliokuwa wanamhudumia Ahazia, naye akawaua.
Ikawa kwamba, Yehu alikuwa akichukua hukumu ya Mungu juu ya nyumba ya Ahabu, kwamba aliwakuta viongozi wa Yuda na wana wa ndugu zake Ahazia wakimtumikia Ahazia. Yehu akawauwa.
9 Ndipo akaenda kumsaka Ahazia, nao watu wake wakamkamata alipokuwa amejificha huko Samaria. Akaletwa kwa Yehu, naye Yehu akamuua. Wakamzika kwani walisema, “Alikuwa mwana wa Yehoshafati, ambaye alimtafuta Bwana kwa moyo wake wote.” Hivyo hapakuwa na mtu mwenye uwezo katika nyumba ya Ahazia aliyeweza kushika ufalme.
Yehu akamtafuta Ahazia; Wakamkamata akiwa amejificha katika Samaraia, wakamleta kwa Yehu, na wakamuuwa. Kisha wakamzika, kwa maana walisema, “Ni mwana wa Yehoshafati, ambaye alimtafuta Yahwe kwa moyo wake wote.” Kwa hiyo nyumba ya Ahazia haikuwa na nguvu zaidi kwa ajili ya kuutawala ule ufalme.
10 Wakati Athalia mamaye Ahazia alipoona kuwa mwanawe amekufa, akainuka na kuiangamiza jamaa yote ya mfalme ya nyumba ya Yuda.
Sasa Athalia, mama wa Ahazia, akaoana kwamba mwanaye alikuwa amekufa, akaianuka na kuwauwa watoto wote wa kifalme katika nyumba ya Yehu.
11 Lakini Yehosheba, binti wa Mfalme Yehoramu, akamtwaa Yoashi mwana wa Ahazia kwa siri kutoka miongoni mwa wana wa mfalme waliokuwa karibu kuuawa. Akamweka Yoashi pamoja na yaya wake ndani ya chumba cha kulala. Kwa kuwa Yehosheba, aliyekuwa binti wa Mfalme Yehoramu, na pia alikuwa mke wa kuhani Yehoyada, alikuwa dada yake Ahazia, akamficha huyo mtoto ili Athalia asimuue.
Lakini Yehoshaba, binti wa mfalme, akamchukua Yoashi, mwana wa Ahazia, na akamvutia mbali kutoka miongoni mwa wana wa mfalme ambao waliuawa. Akamuweka yeye na mlezi wake katika chumba cha kulala. Kwa hiyo Yehoshaba, binti wa mfalme Yehoramu, mke wa Yehoiada kuhani (kwa maana alikuwa dada yake Ahazia), akamficha asimuone Athalia, kwa hiyo Athalia hakumuuwa.
12 Alibaki amefichwa pamoja nao katika Hekalu la Mungu kwa muda wa miaka sita wakati Athalia alikuwa akitawala nchi.
Alikuwa pamoja nao, wakiwa wamejificha katika nyumba ya Mungu kwa miaka sita, Athalia alipotawala juu ya Yuda.

< 2 Nyakati 22 >