< 2 Nyakati 21 >

1 Yehoshafati akalala na baba zake, akazikwa pamoja nao katika Mji wa Daudi. Mwanawe Yehoramu akawa mfalme baada yake.
And Jehoshaphat slept with his fathers, and was buried with his fathers in the city of David; and Jehoram his son reigned in his stead.
2 Ndugu zake Yehoramu, wana wa Yehoshafati walikuwa: Azaria, Yehieli, Zekaria, Azaria, Mikaeli na Shefatia. Hawa wote walikuwa wana wa Yehoshafati mfalme wa Israeli
And he had brethren, the sons of Jehoshaphat: Azariah and Jehiel, and Zechariah, and Azariah, and Michael, and Shephatiah: all these were sons of Jehoshaphat king of Israel.
3 Baba yao alikuwa amewapa zawadi nyingi za fedha na dhahabu na vitu vya thamani, pamoja na miji yenye ngome huko Yuda, bali ufalme akampa Yehoramu kwa sababu alikuwa mwanawe mzaliwa wa kwanza.
And their father had given them great gifts of silver and of gold and of precious things, besides fortified cities in Judah; but the kingdom he gave to Jehoram, for he was the firstborn.
4 Baada ya Yehoramu kujiimarisha katika ufalme wa baba yake, akawaua kwa upanga ndugu zake wote pamoja na baadhi ya wakuu wa Israeli.
And Jehoram established himself over the kingdom of his father, and strengthened himself; and he slew all his brethren with the sword, and [certain] also of the princes of Israel.
5 Yehoramu alikuwa na umri wa miaka thelathini na miwili alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka minane.
Jehoram was thirty-two years old when he began to reign; and he reigned eight years in Jerusalem.
6 Akaenenda katika njia za wafalme wa Israeli, kama nyumba ya Ahabu ilivyokuwa imefanya, kwa kuwa alimwoa binti wa Ahabu. Akatenda maovu machoni pa Bwana.
And he walked in the way of the kings of Israel, as did the house of Ahab, for the daughter of Ahab was his wife; and he did evil in the sight of Jehovah.
7 Hata hivyo, kwa sababu ya Agano ambalo Bwana alikuwa amefanya na Daudi, Bwana hakuwa radhi kuangamiza nyumba ya Daudi. Mungu alikuwa ameahidi kuidumisha taa kwa ajili yake na wazao wake milele.
But Jehovah would not destroy the house of David, because of the covenant that he had made with David, and as he had promised to give to him always a lamp, and to his sons.
8 Wakati wa Yehoramu, Edomu waliasi dhidi ya Yuda na kujiwekea mfalme wao wenyewe.
In his days Edom revolted from under the hand of Judah, and they set a king over themselves.
9 Basi Yehoramu akaenda huko pamoja na maafisa wake na magari yake ya vita. Waedomu wakamzunguka yeye na majemadari wake wa magari yake ya vita, lakini akaondoka, akapenya usiku na kuwashambulia Waedomu.
And Jehoram went over with his captains, and all the chariots with him; and he rose up by night, and smote the Edomites who had surrounded him, and the captains of the chariots.
10 Hadi leo Edomu wameasi dhidi ya Yuda. Libna pia wakaasi wakati huo huo kwa sababu Yehoramu alikuwa amemwacha Bwana, Mungu wa baba zake.
But the Edomites revolted from under the hand of Judah unto this day. Then Libnah revolted at the same time from under his hand, because he had forsaken Jehovah the God of his fathers.
11 Alikuwa pia ametengeneza mahali pa juu pa kuabudia miungu katika vilima vya Yuda na akawa amewasababisha watu wa Yerusalemu kufanya uzinzi na akawa amewapotosha watu wa Yuda.
Moreover he made high places on the mountains of Judah, and caused the inhabitants of Jerusalem to commit fornication, and compelled Judah [thereto].
12 Yehoramu akapokea barua kutoka kwa nabii Eliya iliyosema: “Hili ndilo Bwana, Mungu wa Daudi baba yako, asemalo: ‘Hukuenenda katika njia za Yehoshafati baba yako au za Asa mfalme wa Yuda.
And there came a writing to him from Elijah the prophet saying, Thus saith Jehovah, the God of David thy father: Because thou hast not walked in the ways of Jehoshaphat thy father, nor in the ways of Asa king of Judah,
13 Lakini umeenenda katika njia za wafalme wa Israeli, nawe umewaongoza Yuda na watu wa Yerusalemu kuzini, kama vile nyumba ya Ahabu ilivyofanya. Pia umewaua ndugu zako mwenyewe, watu wa nyumbani mwa baba yako, watu waliokuwa bora kuliko wewe.
but hast walked in the way of the kings of Israel, and hast made Judah and the inhabitants of Jerusalem to commit fornication, like the fornications of the house of Ahab, and also hast slain thy brethren, thy father's house who were better than thyself:
14 Hivyo basi Bwana yu karibu kuwapiga watu wako, wanao, wake zako na kila kitu kilicho chako, kwa pigo zito.
behold, Jehovah will smite with a great stroke thy people, and thy children, and thy wives, and all thy substance,
15 Wewe mwenyewe utaugua sana kwa ugonjwa wa tumbo kwa muda mrefu, hadi ugonjwa utakaposababisha matumbo yako kutoka nje.’”
and thyself with sore sicknesses, with a disease of thy bowels, until thy bowels fall out by reason of the sickness day by day.
16 Bwana akaamsha chuki ya Wafilisti na ya Waarabu walioishi karibu na Wakushi dhidi ya Yehoramu.
And Jehovah stirred up against Jehoram the spirit of the Philistines, and of the Arabians, who [are] near the Ethiopians;
17 Wakaishambulia Yuda, wakaivamia na kuchukua mali zote zilizopatikana katika jumba la mfalme pamoja na wanawe na wake zake. Hakubakiziwa mwana yeyote isipokuwa Ahazia aliyekuwa mdogo wa wote.
and they came up into Judah, and broke into it, and carried away all the substance that was found in the king's house, and his sons also, and his wives; so that there was no son left him, except Jehoahaz the youngest of his sons.
18 Baada ya mambo haya yote, Bwana akampiga Yehoramu kwa ugonjwa usioponyeka wa matumbo.
And after all this, Jehovah smote him in his bowels with an incurable sickness.
19 Ikawa baada ya muda, mwisho wa mwaka wa pili, matumbo yake yakatoka nje kwa sababu ya ugonjwa, naye akafa katika maumivu makali sana. Watu wake hawakuwasha moto kwa heshima yake, kama walivyokuwa wamewafanyia baba zake.
And it came to pass, from day to day, and at the time when the second year was drawing to a close, that his bowels fell out by reason of his sickness, and he died in cruel sufferings. And his people made no burning for him, like the burning of his fathers.
20 Yehoramu alikuwa na umri wa miaka thelathini na miwili alipokuwa mfalme, naye akatawala huko Yerusalemu miaka minane. Akafa, bila kusikitikiwa na mtu yeyote, naye akazikwa katika Mji wa Daudi, lakini si katika makaburi ya wafalme.
He was thirty-two years old when he began to reign, and he reigned in Jerusalem eight years, and departed without being regretted. And they buried him in the city of David, but not in the sepulchres of the kings.

< 2 Nyakati 21 >