< 2 Nyakati 2 >

1 Solomoni akatoa amri kujenga Hekalu kwa ajili ya Jina la Bwana na jumba la kifalme kwa ajili yake mwenyewe.
Sasa Selemani akaamuru kulijengea nyumba jina la Yahwe na nyumamba kwa ajili ya ikulu ya ufalme wake.
2 Solomoni akaandika watu 70,000 kuwa wachukuzi wa mizigo, na watu 80,000 kuwa wachonga mawe vilimani, na watu 3,600 kuwa wasimamizi wao.
Selemeni akateua wanaume elfu sabini wabebe mizigo, na wanaume elfu themanini wa kukata mbao katika mlima, na wanaume 3, 600 kwa ajili ya kusimamia.
3 Solomoni akapeleka ujumbe huu kwa Mfalme Hiramu wa Tiro: “Unitumie magogo ya mierezi kama ulivyomfanyia baba yangu Daudi wakati ulipompelekea mierezi ya kujenga jumba lake la kifalme la kuishi.
Selemani akatuma ujumbe kwa Hiramu, mfalme wa Tiro, ukisema, “Kama ulivyofanya na Daudi baba yangu, ulivyomtumia magogo ya mierezi ili ajenge nyumba ya kuishi, fanya hivyo hivyo na mimi.
4 Sasa ninakaribia kujenga Hekalu kwa ajili ya Jina la Bwana Mungu wangu na kuliweka wakfu kwake kwa ajili ya kufukizia uvumba wenye harufu nzuri mbele zake, mahali pa kuweka mikate ya Wonyesho kwa kufuata utaratibu na kwa ajili ya mahali pa kutolea sadaka za kuteketezwa kila siku asubuhi na jioni, siku za Sabato na Mwezi Mwandamo pia katika sikukuu zilizoamriwa za Bwana Mungu wetu. Hili ni agizo la kudumu kwa ajili ya Waisraeli.
Tazama, niko karibu kujenga nyumba kwa ajili ya jina la Yahwe Mungu wangu, kuiweka wakifu kwake, kwa ajili ya kumtolea sadaka za kuteketezwa zenye viungo vitamu mbele zake, kwa ajili ya mkate wa uwepo, na kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa asubuhi na jioni, katika siku za Sabato na za mwezi mpya, na katika sikukuu zilizoteuliwa kwa ajili ya Yahwe Mungu wetu. Hii itakuwa milele, kwa Israeli.
5 “Hekalu nitakalolijenga litakuwa kubwa, kwa sababu Mungu wetu ni mkuu kuliko miungu mingine yote.
Nyumba nitakayoijenga itakuwa kubwa sana, maana Mungu wetu ni mkuu kuliko miungu mingine yote.
6 Lakini ni nani awezaye kumjengea Hekalu, maadamu mbingu, hata mbingu zilizo juu sana, haziwezi kumtosha? Mimi ni nani basi hata nimjengee Hekalu, isipokuwa liwe tu mahali pa kutolea dhabihu za kuteketezwa mbele zake?
Lakini ni nani anayeweza kumjengea Mungu nyumba, kama dunia yote na hata mbigu yenyewe haviwezi kumtosha? Mimi ni nani hata nimjengee nyumba, ispokuwa sadaka kwa ajili ya sadaka za kufukiza mbele zake?
7 “Hivyo basi nitumie mtu mwenye ustadi wa kufanya kazi ya kutengeneza dhahabu na fedha, shaba na chuma, nyuzi za rangi ya zambarau, nyekundu na buluu, mwenye uzoefu wa kutia nakshi, ili afanye kazi Yuda na Yerusalemu pamoja na mafundi wangu wenye ustadi, ambao baba yangu Daudi aliwaweka.
Kwa hiyo nileteeni mtu mwenye ujuzi wa kazi katika kazi ya dhahabu, fedha, shaba, na chuma, na ya dhambarau, na nyekundu, na sufu ya samawati, mtu anayejua kutengeza aina zote za mapambo ya mbao. Atakuwa na watu wenye ustadi waliopamoja nami katika Yuda na Yerusalemu, ambao Daudi baba yangu aliwaweka.
8 “Pia nitumie magogo ya mierezi, miberoshi na misandali kutoka Lebanoni kwa maana najua kwamba watu wako wanao ujuzi wa kupasua mbao huko. Watu wangu watafanya kazi pamoja na watu wako
Nitumieni pia mierezi, miberoshi, na miti ya msandali kutoka Lebanoni, maana najua ya kuwa watumishi wako wanajua jinsi ya kukata mbao katika Lebanoni. Angalia, watumishi wangu watakuwa na watumishi wako,
9 ili wanipatie mbao kwa wingi kwa sababu Hekalu nitakalojenga lazima liwe kubwa na zuri kabisa.
ili kwamba watayarishe mbao nyingi kwa ajili yangu, maana nyumba ninayotaka kuijenga itakuwa kubwa na ya ajabu.
10 Nitawapa watumishi wako, yaani, maseremala wakatao mbao, kori 20,000 za unga wa ngano, kori 20,000 za shayiri, bathi 20,000 za mvinyo, na bathi 20,000 za mafuta ya zeituni.”
Angalia, nitawapa watumishi wako, watu watakaozikata mbao, kori ishirini elfu za ngano ya aridhini, kori ishirini elfu za shayiri, bathi ishirini elfu za mvinyo, na bathi ishirini elfu za mafuta.” (Maandishsi ya kale yanasema: “kori ishirini elfu za ngano kama chakula”).
11 Ndipo Hiramu mfalme wa Tiro akamjibu Solomoni kwa barua: “Kwa sababu Bwana anawapenda watu wake, amekufanya wewe kuwa mfalme wao.”
Kisha Hiramu, mfalme wa Tiro, akajibu kwa maandishi, ambayo alimtumia Selemani: “Kwa kuwa Yahwe anawapenda watu wake, amekufanya kuwa mfalme juu yao.”
12 Naye Hiramu akaongeza kusema: “Ahimidiwe Bwana, Mungu wa Israeli aliyezifanya mbingu na nchi! Amempa Mfalme Daudi mwana mwenye hekima, aliyejaliwa maarifa na ufahamu, ambaye atajenga Hekalu kwa ajili ya Bwana, na jumba la kifalme kwa ajili yake mwenyewe.
Zaidi ya hayo, Hiramu akasema, “Abarikiwe Yahwe, Mungu wa Israeli, aliyeziumba mbingu na dunia, amempa Daudi mwana mwenye hekima, mwenye karama ya busara na uelewa, ambaye atajenga nyumba kwa aajili ya Yahwe, na nyumba kwa ajili ya ufalme wake.
13 “Mimi nitamtuma kwako Huramu-Abi, mtu mwenye ustadi mwingi,
Sasa nimemtum mtu mwenye ujuzi, mwenye karama ya uelewa, Hiramu, mtaalamu wangu.
14 ambaye mama yake alitoka Dani na baba yake alitoka Tiro. Yeye ni stadi wa kutengeneza vitu, kufanya kazi zote za dhahabu, fedha, shaba, chuma, mawe na mbao pamoja na kufuma. Ni stadi katika kutia rangi ya zambarau, buluu, nyekundu na nguo za kitani safi. Yeye ana ujuzi katika aina zote za kutia nakshi na anaweza kufuatiliza mchoro wowote wa kazi anayopewa. Atafanya kazi na mafundi wako na wale wa bwana wangu, Daudi baba yako.
Ni mwana wa mwanamke wa binti za Dani. Baba yake alikuwa mtu kutoka Tiro. Ana ujuzi katika kazi za dhahabu, fedha, shaba, chuma, mawe, na katika mbao, na katika dhambarau, samawati, na sufu yenkundu, na kitani safi. Pia ana ujuzi katika kutengeneza michoro ya aina yoyote na katika kubuni kitu chochote. Apatiwe nafsi miongoni mwa watumishi wako wenye ujuzi, na pamoja na wale wa bwana wangu, Daudi, baba yako.
15 “Sasa basi bwana wangu na awapelekee watumishi wake ngano, shayiri, mafuta ya zeituni na mvinyo kama alivyoahidi,
Sasa, ngano na shayiri, mafuta na mvinyo, ambayo bwana wangu aliisema, na apeleke sasa vitu hivi kwa watumishi wake.
16 nasi tutakata magogo yote yale unayohitaji kutoka Lebanoni nasi tutayafunga pamoja na kuyaweka yaelee baharini mpaka Yafa. Kisha utaweza kuyachukua mpaka Yerusalemu.”
Tutakata mbao kutoka Lebanoni, mbao nyingi kadri unavyohitaji. Tutazileta kwako kama mitumbwi kupitia bahari kwenda Yafa, na utazibeba hadi Yerusalemu.”
17 Ndipo Solomoni akaamuru ifanyike hesabu ya wageni wote waliokuwa katika Israeli, baada ya ile hesabu iliyofanywa na Daudi; wakapatikana watu 153,600.
Selemani akawahesabu watu wageni waliokuwa katika nchi ya Israeli, kwa kutumia njia ya Daudi, baba yake, aliyoitumia kuwahesabu. Walikutwa wako 153, 600.
18 Akawaweka watu 70,000 miongoni mwao kuwa wachukuzi wa mizigo, na 80,000 kuwa wachonga mawe vilimani, na 3,600 wakiwa wasimamizi juu yao ili wawahimize watu kufanya kazi.
Miongoni mwao aliwateua sabini elfu ili wabebe mizigo, themanini elfu kuwa wakataji wa mbao katika milima, na 3, 600 kuwa wasimamizi wa kuwasimamia watu wafanye kazi.

< 2 Nyakati 2 >