< 2 Nyakati 18 >

1 Basi, Yehoshafati alikuwa na mali nyingi sana na heshima. Naye akafanya urafiki na Ahabu kwa mwanawe kumwoa binti wa Ahabu.
Now Jehoshaphat had riches and honor in abundance; and he joined affinity with Ahab.
2 Baada ya miaka kadhaa akashuka kumtembelea Ahabu huko Samaria. Ahabu akachinja ngʼombe na kondoo wengi kwa ajili yake na watu aliokuwa amefuatana nao. Kisha Ahabu akamshawishi Yehoshafati kukwea pamoja naye ili kuishambulia Ramoth-Gileadi.
After certain years he went down to Ahab to Samaria. Ahab killed sheep and cattle for him in abundance, and for the people who were with him, and moved him to go up with him to Ramoth Gilead.
3 Ahabu mfalme wa Israeli akamuuliza Yehoshafati mfalme wa Yuda, “Je, utakwenda pamoja nami kupigana dhidi ya Ramoth-Gileadi?” Yehoshafati akamjibu mfalme wa Israeli, “Mimi ni kama wewe, watu wangu ni kama watu wako, farasi wangu ni kama farasi wako. Tutakuwa pamoja nawe vitani.”
Ahab king of Israel said to Jehoshaphat king of Judah, "Will you go with me to Ramoth Gilead?" He answered him, "I am as you are, and my people as your people. We will be with you in the war."
4 Lakini Yehoshafati pia akamwambia mfalme wa Israeli, “Kwanza tafuta shauri la Bwana.”
Jehoshaphat said to the king of Israel, "Please inquire first for the word of the LORD."
5 Kwa hiyo mfalme wa Israeli akawaleta pamoja manabii wanaume wapatao mia nne, akawauliza, “Je, twende vitani dhidi ya Ramoth-Gileadi, au niache?” Wakajibu, “Naam, nenda kwa kuwa Mungu ataiweka Ramoth-Gileadi mkononi mwa mfalme.”
Then the king of Israel gathered the prophets together, four hundred men, and said to them, "Shall we go to Ramoth Gilead to battle, or shall I refrain?" They said, "Go up; for God will deliver it into the hand of the king."
6 Lakini Yehoshafati akauliza, “Je, hayuko nabii wa Bwana hapa ambaye tunaweza kumuuliza?”
But Jehoshaphat said, "Isn't there here a prophet of the LORD besides, that we may inquire of him?"
7 Mfalme wa Israeli akamjibu Yehoshafati, “Bado yupo mtu mmoja ambaye kupitia yeye twaweza kumuuliza shauri la Bwana, lakini namchukia kwa sababu huwa hatabiri jambo lolote jema kunihusu mimi, lakini kila mara hunitabiria mabaya tu. Yeye ni Mikaya mwana wa Imla.” Yehoshafati akajibu, “Mfalme hapaswi kusema hivyo.”
The king of Israel said to Jehoshaphat, "There is yet one man by whom we may inquire of the LORD; but I hate him, for he never prophesies good concerning me, but always evil. He is Micaiah the son of Imla." Jehoshaphat said, "Do not let the king say so."
8 Kwa hiyo mfalme wa Israeli akamwita mmoja wa maafisa wake na kusema, “Mlete Mikaya mwana wa Imla mara moja.”
Then the king of Israel called an officer, and said, "Get Micaiah the son of Imla quickly."
9 Wakiwa wamevalia majoho yao ya kifalme, mfalme wa Israeli na Yehoshafati mfalme wa Yuda walikuwa wameketi juu ya viti vyao vya kifalme katika sakafu ya kupuria, kwenye ingilio la lango la Samaria, pamoja na manabii wote wakiwa wakitabiri mbele yao.
Now the king of Israel and Jehoshaphat the king of Judah sat each on his throne, arrayed in their robes, and they were sitting in an open place at the entrance of the gate of Samaria; and all the prophets were prophesying before them.
10 Wakati huu Sedekia mwana wa Kenaana alikuwa ametengeneza pembe za chuma, akatangaza, “Hivi ndivyo Bwana asemavyo, ‘Kwa hizi pembe utawapiga na kuwarudisha Waaramu nyuma mpaka wameangamizwa.’”
Zedekiah the son of Kenaanah made him horns of iron, and said, "Thus says the LORD, 'With these you shall push the Arameans, until they are consumed.'"
11 Manabii wengine wote walikuwa wanatabiri kitu hicho hicho, wakisema, “Ishambulie Ramoth-Gileadi na uwe mshindi. Kwa kuwa Bwana ataitia mkononi mwa mfalme.”
All the prophets prophesied so, saying, "Go up to Ramoth Gilead, and prosper; for the LORD will deliver it into the hand of the king."
12 Mjumbe aliyekuwa amekwenda kumwita Mikaya akamwambia, “Tazama, manabii wote kama mtu mmoja wanatabiri ushindi kwa mfalme. Neno lako na likubaliane na lao, nawe unene mema kuhusu mfalme.”
The messenger who went to call Micaiah spoke to him, saying, "Look, the words of the prophets declare good to the king with one mouth. Let your word therefore, please be like one of theirs, and speak good."
13 Lakini Mikaya akasema, “Hakika kama Bwana aishivyo, nitamwambia kile tu Bwana atakachoniambia.”
Micaiah said, "As the LORD lives, whatever my God says to me, that I will speak."
14 Alipofika, mfalme akamuuliza, “Mikaya, je, twende vitani dhidi ya Ramoth-Gileadi au niache?” Akamjibu, “Shambulia na ushinde, kwa kuwa watatiwa mkononi mwako.”
When he had come to the king, the king said to him, "Micaiah, shall we go to Ramoth Gilead to battle, or shall I refrain?" He said, "Go up, and prosper. They shall be delivered into your hand."
15 Mfalme akamwambia, “Je, ni mara ngapi nitakuapisha ili usiniambie kitu chochote ila kweli tu kwa jina la Bwana?”
The king said to him, "How many times shall I adjure you that you speak to me nothing but the truth in the name of the LORD?"
16 Ndipo Mikaya akajibu, “Niliona Israeli wote wametawanyika vilimani kama kondoo wasio na mchungaji, naye Bwana akasema, ‘Watu hawa hawana bwana. Mwache kila mmoja aende nyumbani kwa amani.’”
He said, "I saw all Israel scattered on the mountains, as sheep that have no shepherd. The LORD said, 'These have no master. Let them return every man to his house in peace.'"
17 Mfalme wa Israeli akamwambia Yehoshafati, “Sikukuambia kwamba huwa hatabiri jambo lolote jema kunihusu bali mabaya tu?”
The king of Israel said to Jehoshaphat, "Did I not tell you that he would not prophesy good concerning me, but evil?"
18 Mikaya akaendelea, “Kwa hiyo lisikie neno la Bwana: Nilimwona Bwana ameketi juu ya kiti chake cha enzi pamoja na jeshi lote la mbinguni likiwa limesimama upande wa kulia na wa kushoto.
Micaiah said, "Therefore hear the word of the LORD: I saw the LORD sitting on his throne, and all the army of heaven standing on his right hand and on his left.
19 Naye Bwana akasema, ‘Ni nani atakayemshawishi Ahabu, mfalme wa Israeli, ili aishambulie Ramoth-Gileadi na kukiendea kifo chake huko?’ “Mmoja akapendekeza hili na mwingine lile.
The LORD said, 'Who shall entice Ahab king of Israel, that he may go up and fall at Ramoth Gilead?' One spoke saying in this way, and another saying in that way.
20 Mwishoni, roho akajitokeza, akasimama mbele za Bwana na kusema, ‘Nitamshawishi.’ “Bwana akauliza, ‘Kwa njia gani?’
A spirit came out, stood before the LORD, and said, 'I will entice him.' "The LORD said to him, 'How?'
21 “Akasema, ‘Nitakwenda na kuwa roho ya uongo katika vinywa vya manabii wake wote.’ “Bwana akasema, ‘Utafanikiwa katika kumshawishi. Nenda ukafanye hivyo.’
"He said, 'I will go forth, and will be a lying spirit in the mouth of all his prophets.' "He said, 'You will entice him, and will prevail also. Go forth, and do so.'
22 “Kwa hiyo sasa Bwana ameweka roho ya kudanganya ndani ya vinywa vya hawa manabii wako wote. Bwana ameamuru maafa kwa ajili yako.”
"Now therefore, look, the LORD has put a lying spirit in the mouth of these your prophets; and the LORD has pronounced disaster concerning you."
23 Kisha Sedekia mwana wa Kenaana akatoka na kumpiga Mikaya kofi usoni. Akauliza, “Huyo Roho kutoka kwa Bwana alipita njia gani alipotoka kwangu ili kusema nawe?”
Then Zedekiah the son of Kenaanah came near, and struck Micaiah on the cheek, and said, "Which way did the Spirit of the LORD go from me to speak to you?"
24 Mikaya akajibu, “Utagundua siku hiyo utakapokwenda kujificha kwenye chumba cha ndani.”
Micaiah said, "Look, you shall see on that day, when you shall go into an inner room to hide yourself."
25 Kisha mfalme wa Israeli akaagiza, “Mchukueni na mkamrudishe kwa Amoni mtawala wa mji na kwa Yoashi mwana wa mfalme.
The king of Israel said, "Take Micaiah, and carry him back to Amon the governor of the city, and to Joash the king's son;
26 Mkaseme, ‘Hivi ndivyo asemavyo mfalme: Mwekeni mtu huyu gerezani na asipewe chochote ila mkate na maji mpaka nitakaporudi salama.’”
and say, 'Thus says the king, "Put this fellow in the prison, and feed him with bread of affliction and with water of affliction, until I return in peace."'"
27 Mikaya akasema, “Kama utarudi salama, basi Bwana hajanena kupitia kwangu.” Kisha akaongeza kusema, “Zingatieni maneno yangu, enyi watu wote!”
Micaiah said, "If you return at all in peace, the LORD has not spoken by me." He said, "Listen, you peoples, all of you."
28 Basi mfalme wa Israeli na Yehoshafati mfalme wa Yuda wakaenda Ramoth-Gileadi.
So the king of Israel and Jehoshaphat the king of Judah went up to Ramoth Gilead.
29 Mfalme wa Israeli akamwambia Yehoshafati, “Nitaingia vitani nikiwa nimejibadilisha, lakini wewe uvae majoho yako ya kifalme.” Kwa hiyo mfalme wa Israeli akajibadilisha na kwenda vitani.
The king of Israel said to Jehoshaphat, "I will disguise myself, and go into the battle; but you put on your robes." So the king of Israel disguised himself; and they went into the battle.
30 Wakati huu, mfalme wa Aramu alikuwa amewaagiza majemadari thelathini na wawili wa magari ya vita, “Msipigane na yeyote, mdogo au mkubwa, isipokuwa mfalme wa Israeli.”
Now the king of Aram had commanded the captains of his chariots, saying, "Fight neither with small nor great, except only with the king of Israel."
31 Wakati wale majemadari wa magari ya vita walipomwona Yehoshafati, wakafikiri, “Hakika huyu ndiye mfalme wa Israeli.” Kwa hiyo wakageuka ili wamshambulie, lakini Yehoshafati akapiga kelele, naye Bwana akamsaidia. Mungu akawaondoa kwake,
It happened, when the captains of the chariots saw Jehoshaphat, that they said, "It is the king of Israel." Therefore they turned around to fight against him. But Jehoshaphat cried out, and the LORD helped him; and God moved them to depart from him.
32 wale majemadari wakaona kwamba hakuwa mfalme wa Israeli nao wakaacha kumfuatilia.
It happened, when the captains of the chariots saw that it was not the king of Israel, that they turned back from pursuing him.
33 Lakini mtu fulani akavuta upinde pasipo lengo na kumpiga mfalme wa Israeli katikati ya kiungio cha mavazi yake ya chuma, mfalme akamwambia mwendesha gari lake, “Geuza gari na uniondoe mimi katika mapigano, nimejeruhiwa.”
A certain man drew his bow at random, and struck the king of Israel between the joints of the armor. Therefore he said to the driver of the chariot, "Turn your hand, and carry me out of the army; for I am severely wounded."
34 Vita vikaendelea mchana kutwa, naye mfalme wa Israeli akajitegemeza ndani ya gari lake kuwaelekea Waaramu hadi jioni. Basi jioni yake akafa.
The battle increased that day. However the king of Israel propped himself up in his chariot against the Arameans until the evening; and about the time of the going down of the sun, he died.

< 2 Nyakati 18 >