< 2 Nyakati 15 >

1 Roho wa Bwana akamjia Azaria mwana wa Odedi.
Roho ya Mungu ikaja juu ya Azaria mwana wa Odedi.
2 Akatoka ili kumlaki Asa na kumwambia, “Nisikilizeni, Asa na Yuda wote na Benyamini. Bwana yu pamoja nanyi mkiwa pamoja naye. Kama mkimtafuta, ataonekana kwenu, lakini kama mkimwacha yeye, naye atawaacha ninyi.
Akaenda nje kukutana na Asa na akamwambia, “Nisikilize, Asa, na Yuda wote na Benyamini: Yahwe yuko pamoja nanyi, pale mnapokuwa naye. Kama mtamtafuta, mtampata; lakini kama mtamsahau, atawasahau ninyi.
3 Kwa muda mrefu Israeli walikuwa hawana Mungu wa kweli, walikuwa hawana kuhani wa kuwafundisha na wala hawakuwa na sheria.
Sasa kwa muda mrefu, Israeli hawakuwa na Mungu wa kweli, bila kuhani wa kufundisha, na bila sheria.
4 Lakini katika taabu yao walimrudia Bwana, Mungu wa Israeli na kumtafuta, naye akaonekana kwao.
Lakini katika dhiki yao wakamrudia Yahwe, Mungu wa Israeli, na wakamtafuta, wakamta.
5 Katika siku hizo hapakuwa na amani kwa yeyote aliyesafiri, kutoka wala kuingia, kwa kuwa wakazi wote wa nchi walikuwa katika machafuko makubwa.
Katika nyakati hizo hapakuwa na amani kwake aliyesafiri kwend mbali, wala kwake aliyesafiri kuja hapa; badala yake shsida kubwa zilikuwa juu ya wenyeji wote wa wanchi.
6 Taifa moja lilipigana na taifa lingine na mji mmoja ukapigana na mji mwingine, kwa sababu Mungu alikuwa anawahangaisha kwa taabu za kila aina.
Waligawanyika vikundi vikundi, taifa dhidi ya taifa, na mji dhidi ya mji, kwa maana Mungu aliwapa shsida za kila aina ya kila mateso.
7 Lakini kwa habari yenu ninyi, kuweni hodari wala msikate tamaa, kwa kuwa mtapata thawabu kwa kazi yenu.”
Lakini muwe hodari, na msiuache mkono wenu kuwa dhaifu, kwa maana kazi yen itapewa thawabu.”
8 Asa aliposikia maneno haya na unabii wa Azaria mwana wa Odedi nabii, akajipa moyo. Akaziondoa sanamu zote zilizokuwa machukizo katika nchi yote ya Yuda na Benyamini na kutoka miji aliyoiteka ya vilima vya Efraimu. Akakarabati madhabahu ya Bwana iliyokuwa mbele ya ukumbi wa Hekalu la Bwana.
Asa aliposikia maneno haya, unabii wa odedi nabii, akajipa ujasiri na kuviondosha mbali vitu vya kuchukiza kutoka nchi yote ya Yuda na Benyamini, na kutoka miji yote aliyokuwa ameiteka kuanzia kilima cha nchi ya Efraimu, na akaijenga tena madhabahu ya Yahwe, ambayo ilikuwa mbele ya ukumbi wa nyumba ya Yahwe.
9 Kisha akakutanisha Yuda wote, Benyamini na watu kutoka Efraimu, watu wa Manase na Simeoni waliokuwa wanaishi miongoni mwao, kwa maana idadi kubwa walikuwa wamemjia kutoka Israeli walipoona kwamba Bwana Mungu wake alikuwa pamoja naye.
Akawakusanya Yuda wote na Benyamini, na wae waliokaa pamoja nao—watu wa kutoka Efraimu na Manase, na kutoka Simeoni. Kwa maana walikuja kwake katika hesabu kubwa kutoka Israeli, walipoona kwamba Yahwe Mungu wake alikuwa pamoja naye.
10 Basi wakakusanyika huko Yerusalemu mwezi wa tatu katika mwaka wa kumi na tano wa utawala wa Asa.
Kwa hiyo wakakusanyika katika Yerusalemu katika mwezzi wa tatu, katika mwaka wa kumi na tano wa utawala wa Asa.
11 Wakati huo wakamtolea Bwana dhabihu za ngʼombe 700, kondoo na mbuzi 7,000 kutoka zile nyara walizoteka.
Katika siku hiyo walimtolea Yahwe dhabihu baadhi ya nyara ambazo walikuwa wameleta; ng'mbe wa kulima mia saba na kondoo na mbuzi elfu saba.
12 Wakafanya agano kumtafuta Bwana, Mungu wa baba zao kwa moyo wao wote na kwa roho yao yote.
Wakaingia kataika agano kwa ajili ya kumtafuta Yahwe, Mungu wa babau zao, kwa moyo wao wote na roho yao yote.
13 Wale wote ambao hawangemtafuta Bwana, Mungu wa Israeli wangelazimika kuuawa, akiwa mdogo au mkubwa, mwanaume au mwanamke.
Wakakubaliana kwamba yeyote atakepuuzia kumtafuta Yahwe, Mungu wa Israeli, atapaswa kuuawa, iwe mdogo ama mkubwa, iwe mwanaume ama mwanamke.
14 Wakamwapia Bwana kwa sauti kuu, kwa kupiga kelele, tarumbeta na kwa mabaragumu.
Wakaapa kwa Yahwe kwa sauti kubwa, kwa kelele, na kwa sauti za tarumbeta na baragumu.
15 Yuda wote wakafurahia kile kiapo kwa sababu walikuwa wameapa kwa moyo wao wote. Wakamtafuta Mungu kwa bidii, naye akaonekana kwao. Kwa hiyo Bwana akawastarehesha pande zote.
Yuda wote wakakifurahia kile kiaapo. kwa maana walikuwa wameapa kwa moyo wao wote, na walimtafuta Mungu kwa nia yao yote, na walimuona. Yahwe akawapa amani pande zote.
16 Mfalme Asa akamwondolea Maaka mama yake wadhifa wake kama mama malkia kwa sababu alikuwa ametengeneza nguzo ya Ashera ya kuchukiza. Asa akaikata hiyo nguzo, akaivunjavunja na kuiteketeza kwa moto katika Bonde la Kidroni.
Pia akamwondoa Maaka, asiwe malikia, kwa sababu alikuwa amefanya sanamu ya kuchukiza ya Maashera. Asa akaivunja vunja sanamu ya kuchukiza, akaiweka kwenye mavumbi akaichoma moto huko kijitoni Kidroni.
17 Ijapokuwa hakuondoa mahali pa juu pa kuabudia miungu katika Israeli, moyo wa Asa ulikuwa umejiweka kwa Bwana kikamilifu maisha yake yote.
Lakini sehemu za juu hazikuwa zimeondolewa nje ya Israeli. Vile vile, Moyo wa Asa ulijitoa kikamilifu siku zake zote.
18 Akaleta ndani ya Hekalu la Mungu fedha na dhahabu na vile vyombo ambavyo yeye na baba yake walikuwa wameviweka wakfu.
Akaleta kwenye nyumba ya Mungu vitu vya baba yake na vitu vyake mwenyewe vilivyokuwa vya Yahwe: vitu vya fedha na dhahabu.
19 Hapakuwepo vita tena mpaka mwaka wa thelathini na tano wa utawala wake Asa.
Hapakuwa na vita zaidi hadi miaka thelathini na mitano ya utawala wa Asa.

< 2 Nyakati 15 >