< 2 Nyakati 12 >
1 Baada ya nafasi ya Rehoboamu kuimarika na kuwa na nguvu, yeye na Israeli yote waliiacha sheria ya Bwana Mungu.
Ikawa kwamba, Rehoboamu alipokuwa ameimarishwa na mwenye nguvu, kwamba akaikataa sheria ya Yahwe—na Waisraeli wote pamoja naye.
2 Kwa sababu hawakuwa waaminifu kwa Bwana, Shishaki mfalme wa Misri akashambulia Yerusalemu katika mwaka wa tano wa utawala wa Mfalme Rehoboamu.
Ilitokea katika mwaka wa tano wa Mfalme Rehoboamu, kwamba, Shishaki, mfalme wa Israeli, akaja kinyume na Yerusalelemu, kwa sababu watu walikuwa wameacha kuwa waaminifu kwa Yahwe.
3 Akiwa na magari ya vita 1,200 na wapanda farasi 60,000 na idadi isiyohesabika ya majeshi ya Walibia, Wasukii na Wakushi yaliyokuja pamoja naye kutoka Misri.
Akaja na magari elfu moja na mia mbili pamoja naye na wapand farasi elfu sitini. Askari wasio hesabika wakaja pamaoja naye kutoka Misri: Walubi, Wasukii, na Waethiopia.
4 Akateka miji ya Yuda yenye ngome akaendelea mpaka Yerusalemu.
Akaiteka miji yenye ngome ya Yuda na akaja Yerusalemu.
5 Ndipo nabii Shemaya akaja kwa Rehoboamu na kwa viongozi wa Yuda waliokuwa wamekusanyika huko Yerusalemu kwa ajili ya hofu ya Shishaki naye akawaambia, “Hivi ndivyo asemavyo Bwana, ‘Ninyi mmeniacha mimi, kwa hiyo, mimi nami sasa ninawaacha ninyi mkononi mwa Shishaki.’”
Sasa Shemaya nabii akaja kwa Rehoboamu na kwa viongozi wa Yuda ambao walikuwa wamekusanyika pamoja Yerusalemu kwa sababu ya Shishaki. Shemaya akasema kwao, “Hivi ndivyo anavyosema Yahwe: Mmenisahau, kwa hiyo pia nimewaweka katika mkono wa Shishaki”.
6 Viongozi wa Israeli na mfalme wakajinyenyekeza na kusema, “Bwana Mungu ni mwenye haki.”
Kisha wakuu wa Israeli na mfalme wakajinyenyekeza na kusema, “Yahwe ni mtakatifu.”
7 Bwana Mungu alipoona kwamba wamejinyenyekeza, neno hili la Bwana likamjia Shemaya: “Maadamu wamejinyenyekeza, sitawaangamiza bali hivi karibuni nitawapatia wokovu. Ghadhabu yangu haitamwagwa juu ya Yerusalemu kwa kupitia Shishaki.
Yaahwe alipoona kuwa wamejinyenyekeza, neno la Yahwe likamjia Shemaya, likisema, “Wamejinyenyekeza. Stawaadhibu; nitawaokoa kwa hataua fulani, na hasira yangu haitamiminwa juu ya Yerusalemu kwa mkono wa Shishaki.
8 Hata hivyo, watamtumikia Shishaki ili wapate kujifunza tofauti kati ya kunitumikia mimi na kuwatumikia wafalme wa nchi nyingine.”
Vile vile, watakuwa watumishi wake, ili kwamba wajue nini maana ya kunitumikia mimi na kuwatumikia watawala wa nchi zingine.”
9 Shishaki mfalme wa Misri alipoishambulia Yerusalemu, alichukua hazina za Hekalu la Bwana na hazina za jumba la kifalme. Akachukua kila kitu, pamoja na zile ngao za dhahabu ambazo Solomoni alikuwa amezitengeneza.
Kwa hiyo Shishaki, mfalme wa Misiri akaja Yerusalemu akazichukua hazina katika nyumba ya Yahwe, na hazina katika nyumba ya mfalme. akachukua kila kitu; pia akazichukua ngao za dhahabu alizokuwa amezitengeneza Selemani. Mfalme
10 Kwa hiyo Mfalme Rehoboamu akatengeneza ngao za shaba badala ya zile za dhahabu na kuzikabidhi kwa majemadari wa ulinzi wa zamu kwenye ingilio la jumba la mfalme.
Rehoboamu akatengeneza ngao za shaba katika nafasi zake na kuzikabidhi mikoni mwa maamrijeshi wa walinzi, amabao waliilinda milango ya kuelekea kwenye nyumba ya mfalme.
11 Kila wakati mfalme alipokwenda katika Hekalu la Bwana walinzi walikwenda pamoja naye wakiwa wamebeba hizo ngao na baadaye walizirudisha kwenye chumba cha ulinzi.
Ikawa kwamba mfalme kila alipoingia katika nyumba ya Yahwe, walinzi wakazibeba; kisha wakazirudisha katika nyumba ya ulinzi.
12 Kwa sababu Rehoboamu alijinyenyekeza, hasira ya Bwana ikageukia mbali naye, hakuangamizwa kabisa. Kukawa na hali nzuri katika Yuda.
Rehoboamu alipojinyenyekeza mwenyewe, ghadhabu ya Yahwe ikampisha mbali, kwa hiyo hakumwangamiza kabisa kabisa; pembeni, bado kulikuwa na baadhi ya wema wa kupatikana katika Yuda.
13 Mfalme Rehoboamu akajiweka imara katika Yerusalemu na akaendelea kuwa mfalme. Alikuwa na umri wa miaka arobaini na mmoja alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka kumi na saba, mji ambao Bwana alikuwa ameuchagua miongoni mwa makabila yote ya Israeli ili aliweke Jina lake humo. Mama yake aliitwa Naama, alikuwa Mwamoni.
Hivyo mfalme Rehoboamu akafanya ufalme wake imara katika Yerusalemu, na kwa hiyo akatawala. Rehoboamu alikuwa na umri wa miaka aroabaini na moja alipoanza kutawala, na akatawala kwa muda wa mika kumi na saba katika Yerusalemu, mji ambao Yahwe alikuwa ameuchagua kutoka kwa makabila ya Israeli ili kwamba aliweke jina lake humo. Jina lake aliitwa Naama, Mwamoni.
14 Rehoboamu akatenda maovu kwa sababu hakuuelekeza moyo wake katika kumtafuta Bwana Mungu.
Akafanya yaliyokuwa uovu, kwa sababu hakuuelekeza moyo wake kumtafuta Yahwe.
15 Kwa habari ya matukio katika utawala wa Rehoboamu, tangu mwanzo mpaka mwisho, je, hayakuandikwa katika kumbukumbu za nabii Shemaya na mwonaji Ido zinazohusiana na vizazi? Kulikuwako na vita mara kwa mara kati ya Rehoboamu na Yeroboamu.
Kwa mambo mengine kuhusu Rehoboamu, mwanzo na mwisho, hayakuandikwa katika maandishi ya Shemaya nabii na ya Ido mwonaji, ambayo pia yana kumbukumbu ya vizazi na vita kati ya Rehoboamu na Yeroboamu?
16 Rehoboamu akalala na baba zake, akazikwa katika Mji wa Daudi. Naye Abiya mwanawe akawa mfalme baada yake.
Rehoboamu akalala pamoja na babu zake na alizikwa katika mji wa Daudi; Abiya mwanye akawa mfalme katika nafasi yake.